Suala la ukusanyaji kodi na mapato. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la ukusanyaji kodi na mapato.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makene, Jun 27, 2011.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanajanvi, haya ni maoni yangu kwamba Babu wa Samunge ana akili na ubunifu kuliko serikari yote ya ccm na wataalam wa uchumi.Babu alibuni kikombe na kuweka gharama ndogo ya malipo. Jambo hili limekuwa jepesi kwa kila mtu kulimudu, achilia mbali gharama zingine zinazohusika kama usafiri, chakula na malazi.Kama serikari yetu ingekuwa na akili wangepanga kodi ndogo kwa wazawa kiasi kwamba kila mtu angefanya bidii ya kulipa bila kuona uzito wa kufanya hivyo.Babu ameweza kukusanya mapato makubwa, kuiingizia serikari kodi kupitia njia za mbuga na kodi zingine. Yaani amelenga kitu kinachomvuta kila mmoja kwa gharama ndogo, akitazamia kupata faida kubwa ya baadaye.Serikari ya ccm na wataalam wetu hawana akili wanazidiwa na Babu wa Loliondo.
   
Loading...