Suala la Kodi TRA: Magufuli, kwa mwenendo huu utashindwa tu

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,115
2,771
Nilikuwa nasikia TRA kuna wizi ila nilikuwa sijui ni wizi uliohalalishwa na Serikali. Naona Serikali imeamua kujikosesha mapato makusudi, kwa maana, hakuna mfanyakazi hasa wa serikali ambaye siyo mwizi atakayeweza kulipa kodi kama hizi.

Rafiki yangu alinunua gari mtumba Japan kwa $4,200 lakini TRA wakampiga Uplift ya $9,000 kama inavyoonyeshwa hapo chini.

Kwa mwenendo huu lazima makusanyo lazima yatashuka. Tanzania haitengenezi magari, na dunia ya sasa, gari siyo anasa tena. Gari ni muhimu.

Naomba kujua au ufafafanuzi wa hizi gharama. Nakumbuka rafiki yangu anayeishi Marekani alinunua gari huko huko na kulipia ushuru huko wa 4%. Hii yetu nashindwa hata kujua ni asilimia ngapi inalipiwa. Kwa kiburi na majigambo ya hii serikali, siwatakii mabaya, ila hawaendi kokote na hizi gharama hapa chini;

Reference Number 1516350471
Make: TOYOTA
Model: PREMIO
Body Type: SEDAN
Year of Manufacture: 2009
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 1501 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD): 9,000.00
Import Duty (USD): 2,250.00
Excise Duty (USD): 562.50
Excise Duty due to Age (USD): 0.00
VAT (USD): 2,126.25
Custom Processing Fee (USD): 54.00
Railway Dev Levy (USD): 135.00

Total Import Taxes (USD): 5,128
Total Import Taxes (TSHS): 11,235,448.00
 
Serikali ya Tanzania ni very mechanical, siyo serikali inayoongozwa kwa weledi.

Niliwahi kuhudhuria mkutano mmoja Arusha wa wawekezaji wakubwa, mabalozi wa Ulaya na Amerika pamoja na baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Wizara. Kilichoonekana kwa Tanzania, ni kuwa Tanzania ni nchi ambayo haina fair taxes. Fisical regime yetu ni ovyo kabisa.

Na serikali inadhani kwa kuweka viwango vikubwa vya kodi ndiyo kupata pesa nyingi. Hawataki kustretch akili zao, na kuona how they can intelligently increase government collections at the same time increase exports, imports and production.

Kariakoo sasa hivi ni kituo cha kibiashara cha kimataifa. Wafanyabisahara toka Zambia, Congo, Zimbabwe, Rwanda wanakuja kununua bidhaa Kariakoo. We do not produce, we import from China, then we export to these countries and we get the difference. Hili limewezekana kwa sababu tu wengi wa wafanyabiashara wamekuwa wakilipa kodi pungufu ya ile waliyostahili kwa mujibu wa sheria.

Kwaajili ya manufaa ya kibiashara na kiuchumi, serikali ilitakiwa kushusha kodi haraka sana ili kila mfanyabiashara alipe kodi yote kisheria bila ya kuathiri biashara maana kodi ya sasa ikilipwa kama inavyotakiwa kisheria, hakuna Mzambia au Mzimbabwe atakayekuja kununua bidhaa Kariakoo. Bidhaa za Kariakoo bei zake hazitakuwa tofauti na zile zinazoweza kununuliwa Durban.

Nchi kama Dubai zimeendelea kwa haraka sana kwa sababu ya kuwa na kodi ndogo kuliko nchi yoyote Duniani. Walijichunguza, wakaigundua na kuitambua jiografia yao, wakaitumia vizuri ili kujipatia maendeleo. Sisi serikali yetu inaendeshwa kwa msuli badala ya werevu na akili. Siku zote nchi hufanikiwa kama kuna watu wenye akili kubwa, wanaotuliza akili zao, na kutafuta mbinu ambazo wapinzani wao hawawezi kuzifikia kiurahisi.
 
Hizo gharama sio halisia, hao jamaa wa customs wanakomoa raia kwa kuwa magu kawabana kupokea rushwa. Anyways, aangalie ni jinsi gani ya kuwapoza hao customs ili kodi ziwe halisia la sivyo akubali kuwaachia huo mzigo.
 
TRA ni shida..... unakuta umeagiza spea ambayo ni replacement. ... kwa sbb inafanana part no na original basi wanachukua ile bei waliyo nayo kwenye system ya original...
Mwisho wake ushuru wa replacement parts unakuwa sawa na original parts... uhalisia ni zero pale.... ubabe tu... na ndo maana watu wanatafuta mianya ya kukwepa kodi...
 
Kodizetu ni kubwa na zakukatisha tamaa ukifananisha na UG au KE... Lakini mwisho wayote total collection yetu ya kodi ni ndogo kuliko hao wenzetu. Sjui tunafanyaje?

Umeme wetu Nao ni Ghali kuliko wenzetu lakini shirika (TANESCO) letu ni dhoofu kuliko.

Tuna vyanzo viiingi vya maji lakini usambazaji wetu ni wa shida na gharama sindogo. Meru kuna mzungu kajenga hoteli kwenye chanzo cha maji lakini anawaruhusu watu wavute maji buuuure!! Miaka Sasa.

Gesi tunayo ujazo wa matrilioni cubic ms but gesi hapa kwetu iko juu, madini yetu lakini wauzaji wakuu sio sisi, ng'ombe tele lakini maziwa, bidhaa za ngozi tunaimport, ardhi kubwa yenye rutuba lakini mchele, sukari tunaimport, miti kibao but toothpick hatujaweza tengeneza...

Tuna mambo mengi sana magumu, inafaa wasomi Kama Dr. Rutengwe watushauri tuanzie wapi au tubaki kulialia ili tuonewe huruma?
 
TRA wametangaza kuwa wameacha kufanya makadirio na badala yake sasa wanachukua bei ya kwenye invoice baada ya kupata njia ya kudhibiti udanganyifu uliokuwa ukifanywa kwenye invoice.

Kuna nafasi pia ya kwenda kulalamika katika dawati la huduma kwa mteja au elimu kwa mlipa kodi na vithibitisho vyako na wakarekebisha. Milango ya uwazi inazidi kukua, tusikatishane tamaa na wala tusiwe wepesi wa kukasirika na kukata tamaa
 
tra wanatuumiza sana watz kwa kweli,itafika mahali magari itatulazimu tuvuane tu kitaa kuliko kuagizia au kuingia show room,yaani sijui vigezo vyao vya kodi wanaangalia nn,manake ukinunua gari latest,kodi juu,ya zamani,kodi juu,sasa sijui wanatutaka nini hawa tra
 
Nilikuwa nasikia TRA kuna wizi ila nilikuwa sijui ni wizi ulioalalishwa na Serikali. Naona Serikali imeamua kujikosesha mapato makusudi, kwa maana, hakuna mfanyakazi hasa wa serikali ambaye siyo mwizi atakayeweza kulipa kodi kama hizi.

Rafiki yangu Alinunua Gari mtumba Japan kwa $4,200 lakini TRA wakampiga Uplift ya $9,000 kama inavyoonyeshwa hapo chini

Kwa mwenendo huu lazima makusanyo lazima yatashuka. Tanzania haitengenezi magari, na dunia ya sasa, gari siyo anasa tena. Gari ni muhimu. Naomba kujua au ufafafanuzi wa hizi gharama. Nakumbuka rafiki yangu aliagiza Marekani na kulipia ushuru huko wa 4%. Hii yetu nashindwa hata kujua ni asilimia ngapi inalipiwa. Kwa kiburi na majigambo ya hii serikali, siwatakii mabaya, ila hawaendi kokote na hizi gharama haha chini

Reference Number 1516350471
Make: TOYOTA
Model: PREMIO
Body Type: SEDAN
Year of Manufacture: 2009
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 1501 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD): 9,000.00
Import Duty (USD): 2,250.00
Excise Duty (USD): 562.50
Excise Duty due to Age (USD): 0.00
VAT (USD): 2,126.25
Custom Processing Fee (USD): 54.00
Railway Dev Levy (USD): 135.00

Total Import Taxes (USD): 5,128
Total Import Taxes (TSHS): 11,235,448.00
Duuh, miye hujishughulisha na masuala hayo, lkn nifahamuvyo, hilo gari ni jumla ya kodi yake plus usajili 400,000/- itakuwa 9 plus million. Si hiyo ya 11m. You must make your case strong, hapo hiyo gari TRA huiona na kuihesabu km one of posh cars, lkn kwa cc hizo, wamei uplift mno, nadhani pengine wametumia year make ya 2009. Pia, yawezekana xchange rate ya dollar imechangia. Find me at ogudaedmund@gmail.com nikaangalie kwanza gari ya mfano km hiyo last year.
 

Mimi sitaki kuiamini hii makadirio, i gues there is something wrong with the system! Ila.kwankuwa humu ndani wapo pia wakubwa wa tra, watusaide kufunguka!

Hatuwezi kuendelea kwa kukwepa kodi! Wanaolipa kodi na ambao hawslalamiki ni wale waliokuwa wanalipa siku zote, therefore hao wanaojifanya kuathirika na hata kutaka kufunga biashara zao nadhani watumie busara na walipe kodi wataona faida yake! Hata psycholojically watakuwa settled!
 
Magufuli, makodi haya ndio kero kuwa ya watanzania. Au bado hujaona?
 
Kumthibiti binadamu mwenye akili kama zako au pengine anakuzidi ni ngumu sana. Ukizingatia hawa ndio watendaji wakuu washughuli za kila siku serikalini.
 
Kodizetu ni kubwa na zakukatisha tamaa ukifananisha na UG au KE... Lakini mwisho wayote total collection yetu ya kodi ni ndogo kuliko hao wenzetu. Sjui tunafanyaje?
Umeme wetu Nao ni Ghali kuliko wenzetu lakini shirika (TANESCO) letu ni dhoofu kuliko.
Tunavyanzo viiingi vya maji lakini usambazaji wetu ni washida na gharama sindogo.Meru kunamzungu kajenga hoteli kwenyechanzo chamaji lakini anawaruhusu watu wavute maji buuuure!! Miaka Sasa.
Gesi tunayo ujazo wa matrilioni cubic ms but gesi hapakwetu ikojuu,madini yetu lakini wauzaji wakuu siosisi,ngombe tele lakini maziwa,bidhaa zangozi tunaimport,ardhi kubwa yenye rutuba lakini mchele,sukari tunaimport,miti kibao but toothpick hatujaweza tengeneza...
Tunamambo mengisana magumu inafaa wasomi Kama Dr. Rutengwe watushauri tuanzie wapi au tubaki kulialia ili tuonewe huruma?
Natamani hii post yako imfikie Magu,
Lakini wakati mwingine sisi kama watanzania nao ni shidaa,umkomoe mteja kisa umekatazwa kupokea rushwa!
 
Siyo lazima ununue gari kama hauna uwez,unaweza hata ukanunua baiskeli waache wenye uwezo wanunue magari. Rais wetu tunamuamini sanaa na tunajua mnaotaka afeli mlizoea vya bure kipindi cha Mkwere na sasa mnaisoma namba.
mkuu rejea kwenye mada. hapa hatuongelei uwezo wa kununua gari ila tunaongelea USHURU wa ajabu ajabu kama alivyoonyesha mlalamikaji hapo juu. tuliza akili kwanza usome post ya mlalamikaji kabla ya kuchangia...usichangie kwa kutumia mihemko ya kisiasa. hili suala sio la kisiasa hata kidogo.
 
Nilikuwa nasikia TRA kuna wizi ila nilikuwa sijui ni wizi ulioalalishwa na Serikali. Naona Serikali imeamua kujikosesha mapato makusudi, kwa maana, hakuna mfanyakazi hasa wa serikali ambaye siyo mwizi atakayeweza kulipa kodi kama hizi.

Rafiki yangu Alinunua Gari mtumba Japan kwa $4,200 lakini TRA wakampiga Uplift ya $9,000 kama inavyoonyeshwa hapo chini

Kwa mwenendo huu lazima makusanyo lazima yatashuka. Tanzania haitengenezi magari, na dunia ya sasa, gari siyo anasa tena. Gari ni muhimu. Naomba kujua au ufafafanuzi wa hizi gharama. Nakumbuka rafiki yangu aliagiza Marekani na kulipia ushuru huko wa 4%. Hii yetu nashindwa hata kujua ni asilimia ngapi inalipiwa. Kwa kiburi na majigambo ya hii serikali, siwatakii mabaya, ila hawaendi kokote na hizi gharama haha chini

Reference Number 1516350471
Make: TOYOTA
Model: PREMIO
Body Type: SEDAN
Year of Manufacture: 2009
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 1501 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD): 9,000.00
Import Duty (USD): 2,250.00
Excise Duty (USD): 562.50
Excise Duty due to Age (USD): 0.00
VAT (USD): 2,126.25
Custom Processing Fee (USD): 54.00
Railway Dev Levy (USD): 135.00

Total Import Taxes (USD): 5,128
Total Import Taxes (TSHS): 11,235,448.00
KWani hili tatizo limeanza leo?
 
Back
Top Bottom