Gari kununua Uingereza mil.20 kulitoa Tanzania mil.27!

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,963
20,535
media

Landrover Discovery 3 2.7 TD V6 S 5 DOORS

Kwa mujibu wa mahesabu ya kukokotoa tokea kwenye tovuti ya TRA bei ndio hio je hii ni haki kweli?

Reference Number
1516118311
Make:
LANDROVER
Model:
DISCOVERY 3
Body Type:
SUV
Year of Manufacture:
2010
Fuel Type:
DIESEL
Engine Capacity:
2001 CC & ABOVE
Customs Value CIF (USD):
20461.00
Import Duty (USD):
5115.25
Excise Duty (USD):
2557.63
Excise Duty due to Age (USD):
0.00
VAT (USD):
5064.10
Total Taxes (USD):
12737
Total Taxes (TSHS):
27397287

Napenda kufahamu sababu za ushuru wa gari hili kuwa mkubwa karibu sawa na bei ambayo imenunuliwa.
 
Hii gari nimefanya tathimini halisi ya bei yake ni hizo milioni hizo 20 yaani paundi kama 5900 hivi kwa kuwa originally ni la mwaka 2006.

Lakini kwa mahesabu ya mwaka wake ambao imetengezwa inaleta kama inavyoonyesha hapo chini.

Reference Number
1516118307
Make:
LANDROVER
Model:
DISCOVERY 3
Body Type:
SUV
Year of Manufacture:
2006
Fuel Type:
DIESEL
Engine Capacity:
2001 CC & ABOVE
Customs Value CIF (USD):
13353.68
Import Duty (USD):
3338.42
Excise Duty (USD):
1669.21
Excise Duty due to Age (USD):
2503.81
VAT (USD):
3755.72
Total Taxes (USD):
11267
Total Taxes (TSHS):
24235317


Ila nilikuwa najiuliza inakuwaje kwa lile gari ambalo ni la kama miaka mitano nyuma hivi.
 
Ndio gharama za kuingiza magari bongo zilivyo. Gari unalipia ushuru sawa na bei au zaidi ya kiasi ulichonunulia gari lenyewe

Hata ungenunua corolla ya $3000 ushuru Tz ungelipa $3000 au zaidi inategemea na mwaka wa gari lenyewe

Ukinunua gari la miaka ya karibuni gari inakuwa bei kubwa Lakini ushuru wake kuingiza nchini unapungua and vice versa
 
Ndio gharama za kuingiza magari bongo zilivyo. Gari unalipia ushuru sawa na bei au zaidi ya kiasi ulichonunulia gari lenyewe

Hata ungenunua corolla ya $3000 ushuru Tz ungelipa $3000 au zaidi inategemea na mwaka wa gari lenyewe

Ukinunua gari la miaka ya karibuni gari inakuwa bei kubwa Lakini ushuru wake kuingiza nchini unapungua and vice versa

Sio kwa tz Gari ya Miaka ya karibuni ushuru wake utakimbia Gari ya mwaka 2004 na mwaka 2014 same model ushuru Mkubwa kwa model ya 2014.
 
Rafiki zangu wa kutoka nchi kama Gambia wanaingiza sana magari yao nchini mwao na kwa gari hio wanalipia kama dola 1000 hadi 1500 tu!
 
Kwa kweli ningependa kusikia kauli kutoka kwa mtu wa TRA kuja kutetea ushuru huu.

Sio kama watu wanashindwa kuingiza magari kama haya Tanzania lakini uhalali wa ushuru mkubwa kiasi hicho ndio unatisha.

Inaonekana kama kuna chembechembe za kukomoana hivi.
 
serikali yako tukufu haina chanzo kipya cha mapato so hamna namna...na hapo kuna ushuru wa reli..tbs na kadhalika...ccm oyeee
 
Sio kwa tz Gari ya Miaka ya karibuni ushuru wake utakimbia Gari ya mwaka 2004 na mwaka 2014 same model ushuru Mkubwa kwa model ya 2014.

Tz wanazingatia vitu 3 katika ushuru wa gari; CIF, age, cc za gari husika.

Gari ikiwa ya zamani kama hii gari yako hapa ya 2006 unachajiwa excise tax due to age kubwa sababu gari Ni la zamani ila kama ingekua la 2014 basi excise fees ingekuwa chini

Lakini pia hii gari ina cc kubwa so gharama inaongezeka, Tz imeweka categories za cc so hawaendi kwa exactly engine capacity ya gari moja moja which hurts a lot of customers

Kama gari ingekua la 2014 CIF yake ingekua juu Lakini taxes due to age zingekuwa chini so mwisho wa siku unakuta Bado unalipa almost bei ile ile. Magari nje sio gharama ishu kuingiza nchini
 
Gari la starehe hilo mkuu. Aingize pick up au lori au basi inayozidi viti kumi ndo afikirie kulipa hela kidogo

Mkuu hili si gari ya anasa kwa kuwa ni 4x4 ni la kawaida kabisa hilo nataka niwe la kusafiria mikoani.

Ila du hiu ushuru! ndio utanifanya nilipe huku nikilia machozi.
 
Kama sikuwanukuu vibaya viongozi wetu walisema wameweka ushuru mkubwa ili kupunguza foleni za barabarani. Logic behind wananchi washindwe kununua magari kwa wingi Richard
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Hiyo 27m bado haujaweka other charges, ukiziweka inaenda hadi 29m....serikali ya ccm ni matapeli...

Mi hapa wanadamu ndo hua siwaelewi..hv mnadhani hata tukitoa ccm mambo haya yatabadilika?hz ni biashara na inchi zote hapa duniani serekali huchukua kodi,bila hvyo inchi haiendi,nakua naamini walipa kodi sahihi wa inchi hii ni wafanyakazi tu.hata tukaingie ikulu nje ya ccm hutaona kitu kinabadilika hapa zaidi ya yote tutaishia kubadilika tu tena na kulalamika baada ya miaka miwili tu!
 
media

Landrover Discovery 3 2.7 TD V6 S 5 DOORS

Kwa mujibu wa mahesabu ya kukokotoa tokea kwenye tovuti ya TRA bei ndio hio je hii ni haki kweli?

Reference Number
1516118311
Make:
LANDROVER
Model:
DISCOVERY 3
Body Type:
SUV
Year of Manufacture:
2010
Fuel Type:
DIESEL
Engine Capacity:
2001 CC & ABOVE
Customs Value CIF (USD):
20461.00
Import Duty (USD):
5115.25
Excise Duty (USD):
2557.63
Excise Duty due to Age (USD):
0.00
VAT (USD):
5064.10
Total Taxes (USD):
12737
Total Taxes (TSHS):
27397287

Napenda kufahamu sababu za ushuru wa gari hili kuwa mkubwa karibu sawa na bei ambayo imenunuliwa.

Kamuulize Mkapa sisi Malofa na Wapumbavu tukutane October.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom