MAKA Jr
JF-Expert Member
- Nov 17, 2016
- 256
- 185
Popote mlipo, vyombo vya Habari na waandishi wote wa Habari nchini hamjatumia weledi katika kuripoti Habari ya Mandonga. Hamjatusaidia na wala hamjatupa elimu ya kutosha katika hili. Mmekuwa kama kasuku. Lakini ni kawaida yenu. Imefika hatua sasa, kila mtu anataka kuwa hodari wa kuelezea jinsi ya kufanikiwa katika maisha.
Hivi ni chombo gani cha Habari kimemwambia Mandonga ajifunze kujenga misingi ya maisha, na asitegemee hizi ngekewa ambazo nyingi ni za muda mfupi? Kwa nini hammwambii kuwa hayo makampuni yatamtumia na kisha yakiona haingizi pesa yatamwacha? Media za Kitanzania sijui ni lini mtabadilika. Ndio maana watu tulishajikita kuangalia BBC na media nyingine makini kwa sababu ya huu 'utopolo' wenu.
Ngoja niwape mifano.
Hakuna asiyejua kuwa mapeperi (makampuni) yanaweza kukutumia kwa faida zao. Na wakati huna manufaa kwao, watakupa kama gunia lililooza la viazi.
Wako wapi hawa?
1. Dr. Shika (Marehemu. Alitumiwa na kuachwa)
2. Pierre Liquid (haifai tena kwao)
3. Mzee Mpili (haifai tena kwao)
4. Karim Mandonga (ana manufaa kwao leo, lakini baadae atakuwa hafai).
Sasa, mbona hamsemi kuhusu ili? Mbona hamtaki kutufundisha tuwe na misingi imara ili tusijekutumiwa na kuachwa kama wengine?
Hakika vyombo vya Habari na waandishi wa Habari hamjawa sawa katika kutoa Habari hii.
Badilikeni basi. Nyie mna nguvu. Mmshauri Mandonga na wengine watakaofuata kuwa wajenge misingi ya maisha toka chini. Msiwe kama kasuku kila siku mnamsifia.