yusufummaka
Member
- Apr 7, 2012
- 30
- 20
Nimakosa kutaka kuweka kitasa kipya kwenye mlango ulioliwa na mchwa (mbovu), kaa kitako, tafakari na amua kuchonga mlango mpya ili viendane na kitasa kipya unachotaka kuweka. Mlango umeoza kila kona kwanini unahangaika kutaka kuwekewa kitasa kipya? kitawekwa wapi?. Hata kama utagoma huwezi kupata mafanikio unayokusudia sanasana walimu mtawaumiza watoto wa kaka na dada zenu huku mitaani na vijijini, wale watoto wa wanaowapunja mishahara hawasomi shule mnazofundisha ninyi. Mgomo sahihi ni wa kuwaondoa wanaowapunja maslahi yenu, bassiii! sio kugomea kuwafundisha watoto wa walalahoi. Tabia hii itasababisha watoto wa watawala waendelee kutawala nchi hii, maana wao hawajui kama kuna mgomo wanajiandaa vema na kufanya mitihani ya NECTA. Acheni ushamba kazeni buti, wekeni akili zenu kwenye elimu ya watoto wa masikini ndio watakaolikomboa taifa hili.