Stuka: Mapenzi ya 'kishirikina' ndio habari ya mujini

Stuka: Mapenzi ya 'kishirikina' ndio habari ya mujini

Kuna Ticha wangu wa martial art alikuwa anafanya meditation sana akawa hatumii kabisa nyama yoyote ile. Alipata binti ili aoe maisha yalienda sasa jamaa akawa yule binti akija kumpikia anamuuliza kuhusu nyama jamaa akamwambia situmii kabisa ila ukipendelea mi nitakuwa nanunua kwa ajili yako. Yule binti alitamani kujua sana japo kwa kipindi hicho jamaa alimwongopea nina allergy.

Baada ya mambo kuelekea kuiva yani ndoa yule binti alianza kuja na nyama choma kwenye mfuko mbaya zaidi anamfosi Ticha kula.

Jamaa hakuwahi kula na dem alikuja kuumbuka vibaya Meditation siyo mchezo.
Meditation husaidia mambo mengi ndo mana hushauriwa MTU kutafta mda wako ili usimalize energy. Sasa huyo Dada anapendwa hzo libwata lilikuwa la ninj
 
yaani domo ameshuka thamani balaa hata watu siku hizi wanamuona boya
Ndo gundu hivo sema tu watu tunafikiriaga umalaya ni starehe kumbe tunakaribisha mikosi kwenye maisha yetu bila kujua. Sasa domo ndo mvuto umeisha hamisa ana negative energy mbaya mana naye kwa waganga hajambo.
 
funguka more mkuu
Yani mkuu iko hivi yule sista kumbe jamaa aliingia chaka bovu inasadikika mzazi wake wa kike ndiye aliyempa ushauri akitahidi amkamate jamaa ili asimfatilie sanaa kama mkewe na amtawale. Hayo yalijulikana baada ya ishu kusanuka.

Yule Dada alianza kuja na dawa anaweka chini ya mto sasa jamaa akawa kabla ya kulala anashawishika kutandika kitanda anakuta viunga unga muda huo akiwa kamtuma kitu makusudi.

Yule binti alianza mchezo kulala upande mmoja tu jamaa akitaka kuhama binti anasala. Hataki kabisaa

Siku hiyo wanaenda kulala jamaa kabla hajalala kila akitaka kukaa kitandani akasema moyo ukagoma kabisa akamwambia yule bi dada shuka niweke shuka akagoma akatumia ukali sasa dem kushuka jamaa kufunua shuka HIRIZI usawa wa kichwa anapolala chini ya mto.

Jamaa hakuongea alichomwambia nakukata masikio humu humu nieleze kila kitu hii ni yako usikatae na ninahitaji kitu kimoja tu ya nini? Kutokana kwamba dem anajua jamaa ni mwana martial art pia siyo mtata bali shughuli yake si kidogo.

AKAFUNGUKA KILA KITU KUWA MAMA KATOA ADVICE NIWEZE KUKUTAWALA NA KUKUONGOZA NITAKAVYO.

Jamaa akamwambia asubuhiii nenda kayaeleze kwa baba yako kama ulivyonieleza. Jamaa hata ukweni HAKWENDA wakajiongeza.
 
Mi nipo Facebook kwenye ma group ya wanawake sasa wasiojielewa ndo huelekezana waganga na kutumia dawa za kunasa wanaume bora hata kwa single kwa waume za watu ndo usiseme ili unase, eeeh niliyoyaona nikawahurumia wanaume sana maana mwahtaji maombi, pia wanawake wanapenda kwa waganga, waganga wake huwaingizia dawa huko ukeni, imagine mganga ka si mgonjwa hali inakuwa vipi.

Tena vyuma vilivyokaza ndo kwa waganga wanajaa sana, wanaume kuweni makini na mnao date nao.

Hatari Sana bora niendelee kuwa SINGO maana nazidi kutishika,uzuri nipo porini hakuna mademu huku.
 
Wakuu,
Nipo mahali napata fanta ya baridi...na kiyepe yai...naona udenda ushakushuka...

Tuache hayo njoo kwenye mada.

Mbele yangu kuna meza imejaa wadada wa mjini wametupia pamba kali hatari.

Nasikia mmoja anasema mh! Yani yule kaka nimempa mara moja tu kachanganyikiwa..

Wakacheka wote...aliyekuwa anawapa story wenzake akageuka nyuma...kama anawasiwasi mtu asimsikie...

Nikajikausha kama nakata chipsu yai...mara nakunywa soda...akaendelea kuongea...

Unajua bana mjini bila kuwa na akili huwezi kumlata mwanaume wa kukuoa wala kukupa pesa...

Hivyo unatakiwa utumie 'dawa ya mvuto'...yani kila mwanaume akikuona anavutika...

Nilishanga kimoyomoyo...ghafla kisimu kikaita mume wangu kaja kunichukua....

Mpaka sasa najiuliza...

Wanaume mnakazi kubwa...

Doncute
Kumbe ndivyo ilivyo ,mmmh
Wanaume kazi wanayo ila wadada wana kazi zaidi ya kutuwangia
 
inabidi wanawake waliolewa kuwaombea sana waume zao na kuishi nao kwa upole na unyenyekevu kwakuwa kila mwanaume mwenye ndoa anatafutwa na wanawake saba.
  • ofisini wawili kwa ajili lunch na mizinga ya dharura.
  • mtaani watatu
    • mmoja kumkomoa mkeo kwa kuwa analinga na huko vizuri.
    • mmoja uchumi (mwanafunzi wa chuo, single mama nk)
    • mke wa mtu asiyetoshelezwa
  • skuli mate
  • mchepuko wa hiyari.
😱
 
Wakuu,
Nipo mahali napata fanta ya baridi...na kiyepe yai...naona udenda ushakushuka...

Tuache hayo njoo kwenye mada.

Mbele yangu kuna meza imejaa wadada wa mjini wametupia pamba kali hatari.

Nasikia mmoja anasema mh! Yani yule kaka nimempa mara moja tu kachanganyikiwa..

Wakacheka wote...aliyekuwa anawapa story wenzake akageuka nyuma...kama anawasiwasi mtu asimsikie...

Nikajikausha kama nakata chipsu yai...mara nakunywa soda...akaendelea kuongea...

Unajua bana mjini bila kuwa na akili huwezi kumlata mwanaume wa kukuoa wala kukupa pesa...

Hivyo unatakiwa utumie 'dawa ya mvuto'...yani kila mwanaume akikuona anavutika...

Nilishanga kimoyomoyo...ghafla kisimu kikaita mume wangu kaja kunichukua....

Mpaka sasa najiuliza...

Wanaume mnakazi kubwa...

Doncute
Halafu kweli wanawake wengi sana ni washirikina

Yaani unamkuta dada mzuri lakini ana chale sababu ya Kwa waganga eti apendwe

Nyoooo
 
Back
Top Bottom