AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,190
- 18,080
- Thread starter
- #61
Well kuna kitu kimenijia kichwani baada ya kusoma analysis ya AshaDii (Sweetie) na mchango wa The Boss na NN.
Kuna suala zima la utamaduni...ambao niseme unabeba kila kitu chetu kama jamii..kuanzia malezi, kazi, tabia...kila kitu kinafanyika kwa utamaduni wetu ulivyo
Ndiyo maana tunapozungumzia malezi ya watoto na kupendana hatuwezi kukwepa utamaduni wetu ulivyo (msingi wa hija ya The Boss) na jinsi ambavyo tungependa iwe (labda kutokana na tamaduni za wengine)
Kwanza, wazazi wetu enzi hizo (na hata sasa) walikuwa na ndoa za mitala, kama walivyosema wengine. Katika hali hii, ni vigumu sana kuwapata watoto wote ndani ya nyumba moja. Kinachotokea mara nyingi ni watoto kuelelewa tofauti kwenye nyumba tofauti na wote tunajua kuwa kila nyumba ina namna na aina yake ya malezi. hawa watoto wa waliolelewa kwenye nyumba tofauti lakini wakiwa na baba/mama mmoja, inaweza kuathiri sana upendo wao baadaye...kwa vile wanajisikia kama wageni miongoni mwao zaidi (kuliko kati yao). La kustaajabisha, unweza pia kukuta mzazi mmoja anampenda zaidi mtoto wa mke mwingine kuliko mke fulani, hivyo kuimarisha dhana kwamba mzazi kumpenda mtoto fulani kuliko mwingine haina uhusiano wa moja kwa moja na ukaaji wa pamoja wa wazazi hao
Pili niseme kwamba kwa siku hizi, ujio wa shule hizi za binafsi ambao watoto wanatumia muda mwingi wakiwa huko, na zaidi hasa zile za kulala, kuna mchango mkubwa katika kupunguza ukaribu kati ya mtoto na mzazi. Upande mmoja, kuna haja ya watoto kupata elimu 'nzuri na ya kisasa', na upande mwingine kuna kuwekeana umbali kati ya mzazi na mtoto, ambao baada ya muda unapunguza ukaribu na huenda mapenzi yale ambayo mtoto angependa kuyaiga na kuyapata kutoka kwa wazazi.
Tatu, kama tunazungumzia suala la watoto kwa mfano kukaa nyumba moja na wazazi wao wote wawili, hili nalo pia linazidi kuwa gumu kutokana na ugumu wa maisha ambao wakati mwingine unalazimisha wazazi kutengana kwa muda kwa sababu ya kazi au masomo, hivyo kwa wakati fulani watoto wanakosa upendo wa wazazi wote wawili. Cha kusikitisha pia, pale ambapo wanakuwepo wawili, unaweza kukuta ndiyo yale watoto kuambulia baba akimpiga mama na sio kuwaona wakiwa wawili kwa upendo!
Niharakishe kusema sina suluhisho la haraka la hii migongano ninayoiona hapa...labda tunavyozidi kujadili, tutaweza kupata suluhiho au njia bora zaidi ya malezi ambayo itawawezesha wanetu kupendana miongoni mwao na kati yetu na wao zaidi.
Kaizer Dear nimependa uloandika katika hii post ukilenga kuelezea hali halisi hasa in relation na hapo nyuma kidogo... However kama ulivosema hizo two last lines kwamba kuna umuhimu wa kutafuta Suluhisho which i believe haiwezi kua Universal kwa familia zoote... Pia umetoa aspect tatu nzito ambazo naamini kabisa with such an analysis lazima kuna an idea of how to come about making stronger Love ties as well as the already existing Blood ties... at least from one of the three...
Kikubwa ni kwamba tupende tusipende ni rahis kwa maneno kuliko vitendo.... as you have said kuna mabadiliko mengi kama vile Parents kuishi mbali....