Strategy Za Msingi ZItakazo Wezesha Mabadiliko Na Awareness Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Strategy Za Msingi ZItakazo Wezesha Mabadiliko Na Awareness Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mzungukichaa, Nov 19, 2010.

 1. m

  mzungukichaa Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Wadau. Mi naomba tujadili strategy gani na za msingi ambazo Chama Kikuu cha Upinzani Bungeni Kinatakiwa kutumia kuhakikisha 2015 nchi hii inatawaliwa na chama cha wazalendo. Tafadhari toa mawazo ambayo wewe unafikiri yataleta tija Tanzania ya leo na kesho.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  we ndo yule jaji wa BSS?
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapa najaribu kuchangia katika mada ya thread hii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Cha muhimu kuelewa ni kwamba nguvu ya kuleta mabadiliko ya mfumo; Historia ya taifa letu imetufundisha kwamba kutoka mfumo wa chama kimoja kuja mfumo wa vyama vingi imeletwa na pressure ya Internationl Community; Kuboresha mfumo wa uendeshaji wa chaguzi chini ya NEC baadaye ni kutokana na pressure ya Internationl Community;
  Kwa mtazamo wa wanaJF wengi, matatizo yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 31.10.2010, hata kupelekea wabunge wa CDM kususa presence ya Kikwete, ni matatizo ambayo nguvu ya kuweza kuleta ufumbuzi wa haraka bado ni pressure ya Internationl Community;
  Swali la msingi ni jinsi gani ya ku-engage Internationl Community kuendelea kuelewa na kukubali kushiriki kuleta mabadiliko ya haraka!!!
  Mpaka hapa tulipofika baadhi tu ya opportunities ambazo zikitumiwa kwa hekima na busara zitaweza kuzaa matunda kwa faida ya taifa letu ni hizi;-
  1) Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa letu tuna serikali ya upinzani bungeni; tukiitumia vyema itatoa msukumo wa kuweza kubadilisha mambo mengi katika mfumo usio huru na wa haki katika sheria zetu. CDM ina viongozi na wabunge mahiri waliobobea katika masuala ya siasa, sheria na uongozi-Ilani ya CDM ni kielelezo tosha.
  2) Katika mihadhara ya kempeni na matokeo pamoja na yanayoendelea ni ushahidi tosha kwamba jamii inataka mabadiliko ya sera ya dira na uongozi-jamii imekataa sera na uongozi wa chama tawala kwani kwa miaka karibu 50 hali halisi ni ya kurudi nyuma badala kwenda mbele-hata nchi tunazowazidi kwa utajiri na sera nzur kinadharia zimetoka nyuma na kutuacha-jamii haiamini kwamba huyu mkongwe sisemu ataweza ghafla kufanya maajabu!!!!!!!!!!!!;
  3) Kama ilivyo kawaida Internationl Community haiwezi kufanya lo lote kama jamii itaonekana kuridhika na hali iliyopo; ndiyo maana hatua ambazo CDM wamekuwa wakichkua tangu kabla, wakati na baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuuwa 31.10.2010, na mpaka sasa (hasa lile la jana bungeni!!!!!) ni elimu ya muhimu sana kwa International Community ili wasiendelee kuleta fedha za kuja kutuangamiza. Tuwafikishe kuelewa na kukubali ku-support jitihada za kupata haraka sana TUME HURU kwanza katika hatua za mpito, na hatimaye KATIBA MPYA kwa mfumo wa ule wa Kenya, ambao utazingatia mstakabali wa taifa letu kwa mtazamo wa jamii ya karne ya sasa na ya miaka ijayo;
  4) Kwa CDM chama ambacho kwa sasa ndiyo mwakilishi halali bungeni wa interest ya jamii inayotaka mabadiliko, kuelimisha wafuasi wao juu ya falsafa ya sera za CDM ili wakati wote wapate support yao; hili ni kundi kubwa la wafuasi wa CDM, wasomi, makundi mbalimbali ya wanaharakati, hasa jamii ya vijana; wakati wote kufanya International Community ione majority hawako tayari kutulia mpaka Tume Huru na Katikba mpya zimepatikana, na serekali ya matakwa ya wengi ndiyo inaongoza ncha, na siyo kuitawala!!!!!!!!!
  4) Kupeleka ujumbe kwa sisiemu kwamba amani ya kweli itapatikana tu pale matakwa ya wengi yatakapotawala; na kwamba nguvu ya umma, hasa pale ambapo majority ni vijana; wawe na hekima ku-support transion strategies kama walivyofanya kwa transitions za tangu 1995 hadi sasa. Wakubali kuwa sehemu ya mabadiliko, badala ya kuwa vikwazo!!!!!!!!!!

  WanaJF tuna nafasi kubwa sana kuweza kuwa instrument of change kwa mtazamo huu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tuendelee kuchangia.

   
 4. m

  mzungukichaa Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Mtu wa Mungu...Asante kwa mawazo yako yakinifu...mwana halisi wa nchi hii.
   
 5. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  mtu wa watu, nakushauri ukiandika post ndefu, usiweke bold.. watu wengi hawataisoma kwa sababu haijafuata misingi ya uandishi bora wa makala
   
 6. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MwanaJF Kanyagio nimekusoma vizuri na kuzingatia hekima hiyo kwa faida ya mchango wa wanaJF!!!!!!!!!!!!!!!!! Asante sana!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...