Tena tusichoke kutenda mema!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,502
19,302
Kuna ofisi moja nilipita, ya serikali, ndugu wapokezi (receptionists) jueni kuwa Mungu amewaweka hapo ili mhudumie wananchi, acheni kiburi, fanyeni kama mnafanya huduma kwa wanadamu mliyotumwa na Mungu kwasababu kwanz amnapokea mshahara kutokana na kodi za wananchi hawahawa! acheni dharau, acheni roho mbaya, kazi hizo mlizo nazo ni neema tu Mungu anaweza kuwaachisha akawapa watu wengine wanaolia mtaani huko hawana kibarua, vilio vya wanyonge vikimfikia Mungu, huwa haachi kushuka kuwatetea.

Neno la Mungu lilinijia moyoni, kwamba wala tusichoke kutenda mema, maana tutapokea ijara tusipozimia roho. maana yake nini? ishi katika kutenda mema hadi mwisho, bila kuacha, kwasababu kama utafanya hivyo bila kuacha, at the end of the day Mungu atakupa thawabu.

Wagalatia 6:9 inasema, Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.

1. unaenda Ofisi ya uma au yeyote, unakutana na karani amenunaaa na anaamini bila yeye wewe huwezi kusaidiwa kwa lolote. kumbe boss wake ndiye anayetoa huduma. manesi pia mpo hapa, daktari ndiye anayetibu, acheni roho mbaya kwa wagonjwa.

2. unamkuta mfanyakazi wa uma badala ya kuhudumia, amekazana anapiga simu kwa shost zake, anaongea mambo ya kimbea tu, anacheka, ila upo pale unasubiri amalize kuongea mambo ya mtani huko ili akuhudumie. hii sio sawa, fanyeni mlichoajiriwa nacho,

3. unamkuta mfanyakazi wa umma au yeyote, anakuzungushaaa kutoa huduma anataka umpe rushwa. ndugu zangu, hela ni ngumu kwa kila mtu na rushwa ni dhambi, sisi wengine huwa hatutoi rushwa kwasababu tumeokoka, kuna wengine wajane, wengine wana mikopo, wengine wana shida mno, hata wakiwapa hiyo rushwa inawaumaaa, waoneeni huruma, Mungu asije kuwanyanyua kwenye ivyo vibarua vyenu awape wale wa mtaani. hesabu kwamba umepewa uwakala wa kuhudumia watu, sio wa kuchuma pesa za dhurma.

4. Ofisi za ardhi, polisi, mahakamani, TRA, jueni kuwa pesa za rushwa mnazolazimisha watu watoe, Mungu anawaona. kwani mbona nchi zingine unaenda ardhi unapewa hati chapchap tu? kwanini ninyi hadi mzungusheee? mbona nchi zingine ukikamatwa tu wanakupa haki ya dhamana? mbona nchi zingine ukijaribu kutoa rushwa hata mahakamani wanakukamatisha? Mungu anawaona na amewapa hizo kazi mhudumie watu, anao uwezo kuwanyang'anya pia. tumeshaona kwa wengi.

5. unaendesha gari, trafiki anaanza kutaftiza kosa hadi alipate. au upo kwenye daladala, unashangaa kuona konda anaomba 2000 anapokaribia kwa traffiki kumbeni makusanyo, sijui wanapeleka kwa wakubwa zao au nini, nguo mlizovaa zinanuka rushwa, viatu na nyumba zenu vinanuka rushwa, na hiyo ndiyo imewafitinisha na Mungu, okokeni, mwogopeni Mungu.

6. Mungu, nakuomba unisaidie nitende mema, nikiwa kazini nitende mema kwa watu wote bila kujali cheo, status ya pesa au elimu, nisaidie Bwana nitende mema nikiwa barabarani, nikikutana na watu wowote wale wawe watenda dhambi au wema, niwatendee wema na kuushinda ubaya kwa wema. Mungu, nisaidie kuwasamehe hata wale wanaonikosea ili na wewe unisamehe mimi makosa yangu kwani ndio agizo lako, nisaidie niichuchumilie taji ya uzima wa milele hadi pale utakaponichukua, kwa Jina la Yesu Kristo. Amen.
 
utendapo mema jua hayawezi kwenda bure, utapata thawabu yake, na mabaya pia.
 
Mtendee mtu yale unapenda utendewe 😜
hii ndio sheria ya Mungu, ubarikiwe kwamba una ufahamu wa Neno la Mungu. do what you would like others do for you. vile unavyopenda watu wakutendee na wewe watendee hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom