Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

The Hidden Truth

Mtunzi Akida Siri Rambao

MSIMU 3

Tuendelee...

Sehemu 10: Wizi wa Benki

.... hilo, kikapita kimya “…kaka unapaswa kuwa na nguvu Shalon kuwa mtoto wa Samuel haimaanishi kuwa tumeshafeli, ni hatua nyingine na tunapaswa kukubaliana na ukweli uliopo” Karimu aliongea kisha akamshika bega “Kaka kila kitu kitakuwa sawa jiandae tukakutane na Ochola kwanza hata ofisini leo tusiende kwanza” Salimu mara akajikuta akishindwa kujizuia hali ya ubinadamu ikamtawala

“…Kaka haupaswi kusononeka sana tulia kisha kubali matokea alafu tupange hatua zetu tutazipitaje kwa sasa bado hatuja chelewa tuna nafasi la msingi tutazame hili balaa mbele yetu tuvae uhusika tulimalize kwanza likae pembeni tupige kazi kisha mengine yatafata” Karimu aliongea maneno machache nakumshika bega “Ni sawa mzee” kikapita kimya cha takribani dakika kumi na tano kila mmoja akiwa kajiinamia “Unataka kusema Shalon atakuwa yupo katika matatizo?” Salimu aaliuvunja ukimya nakumgeukia Karimu “Hapana kaka hata sisi pia nani anajua” Karimu akajikalisha vizuri huku akimtazama mwezake kwa macho ya utafiti na ndipo Salimu akaongea kwa upole

“Mhh…unajua kaka ndomana nikawa najiuliza kwa nini najikuta naelemea kwa Meroda wakati ukimtazama Shalon na Meroda mara zote huwezi kuwatofautisha katika urembo na maarifa kila mmoja akiwa na kile kizuri zaidi ya mwenzake unajua nimekaa nimetafakari sana hapa…namsitikia sana Shalon…kwa hiyo ndo kusema kuwa waaliokuwa wanamfatilia Shalon siku zote hizo ni walinzi wake! Mbona hakuwahi kutuambia mambo hayo au…unajua kuna kitu sielewi hapa inamaana tunafatiliwa na sisi bira kujijua sio?... haiwezekani kuwa mtu kama Samuel akamuacha binti yake atembee tu, dah tumeshaharibu bila shaka sura zetu za asili zitakuwa katika album ya Samuel hakuna pakutoka” Salimu alimaliza kwa masikitiko nakumuacha Karimu na bumbuwazi huku kengere ya hatari ikilia kichwani mwake. Kalimu kipindi akiwa kakaza macho akitazama juu huku akiwa kaikusanya midomo yake akaanza kutingisha kichwa kukubali kitu fulani “…mzee inatupasa kumfatilia vizuri Shalon pindi tu tukimaliza kazi hii iliyopo mbele yetu, tumpigie Komandoo Ochola tumpe habari za wizi wa benk kisha tutajua na hayo mengine badae”. Aliongea Karimu na kumshika mkono Salimu kumnyanyua wakakumbatiana. “Jiandae twende zetu bro” aliongea Karimu.

Furture Company, Upanga mashariki- Dar es Salam
Mlango ulifungwa wakavuta viti na kukaa “Vijana mnavyofikiri benki kuu ya Tanzania inaweza kuvamiwa kirahisi kweli?” Ochola aliongea huku akiwatazama kwa mshangao, mara mlio wa meseji katika simu yake ulisikika “Sorry..” akajiminya kuitoa na kuifungua lakini alijikuta moyo ukimdunda baada ya kuisoma meseji hiyo ‘Haiwezekani iwe hivi’ alijisemea nafsini nakuirudisha haraka haraka huku akiwa si mwenye kujiamini na kuendelea na mkutano. Nyakati hizo Salimu na Karimu wakiwa wameduwaa kwa mishangazo ya Komandoo “Mkuu mi nafikiri ungeturuhusu tukuthibitishie tukio hilo japo hatusemi tutafanikiwa kulizuia kwa asilimia ngapi ila tumaini letu tuweze kufanikiwa.” Karimu alimaliza na kumuangalia Komandoo Ochola kisha Salimu, “…ni sawa na je mngehitaji watu wa msaada?...” Komandoo aliongea na kunyanyua uso wake na kuziacha nyusi zake kupanda juu, kilipita kimya kidogo, Salimu akiwa mawazoni akitazama sakafuni akaanza kubadilika sura na kuwa na wasiwasi akatoa pumzi nzito akamtazama Karimu aliyekuwa upande wake wa kushoto kwa jicho la kuonesha kuwa anatakakusema kitu

“Mkuu, naamini jukumu hili tunalimudu…alafu…vilevile nafikiri tupo kwenye muda muafaka napenda kukufahamisha yale ambayo huyafahamu…” Karimu alishtuka baada ya kusikia hivyo na akabaki akimtazama Salimu kwa jicho la usiseme lakini Salimu hakunyanyua sura kumtazama Karimu yeye akaendelea “…nafikiri mzee wetu usitulaumu kwa sababu hatukujua kama mambo yatakuja geuka na kuwa kama yalivyo sasa” maneno hayo yalitokea kumshtua sana Komandoo Ochola lakini alijitahidi kuipooza habari hiyo na kujitahidi kujiweka sawa ili kuikabili “…ndio mnaweza nielezea kwa namna mtakavyo kuwa mmejiandaa. “Mzee wangu kwa sasa kwenye timu yetu tuna wasichana watatu ambao tunashirikiana nao katika majukumu ya kazi tumelifanyia kazi amuzi hili na baada ya kuona ni sahihi ndipo tukakubaliana kukufahamisha” Salimu akakaa vizuri kitini akiyapanga maneno vizuri muda huo wote Komandoo alikuwa akisikiliza vizuri huku akimtazama salimu kwa jicho.

Salimu akaendelea “...kama unakumbuka miaka kazaa nyuma tulipokuwa tunawafatilia wale jamaa pale kwenye mgahawa zaidi ni kuhusu wale mabinti watatu mmoja wao amejenga mahusiano na mimi ya kimapenzi mimi naamaanisha sisi tulikuwa wa kwanza kumuhusisha na wahusika wale walioikatili familia yangu kabla yao kwa kumaanisha kuwa ni moja ya timu husika.” Komandoo alionekana kutulia zaidi akimsikiliza Salimu pasina kutia neno. “… mkuu, sisemi kwa kupepesa namaanisha mapenzi yake Meroda yamejaa ukweli mtupu kwangu tena wenye mazingatio ndani yake” Salimu safari hii alionekana kukisogeza kichwa chake mbele na huku akimtaama Komandoo kwa jicho linalosema niamini.


Komandoo bado aliendelea kumtazama tu Salimu na kwa jicho la kumsihi aendelee kuongea. “…komandoo huyu binti nimeshawishika kuwa nae kwa nia ya kupata msaada wake japo kiukweli nahisi kuwa na mapenzi nae ila tu kwako naomba kupata ruhusa ya kuendelea kuwa nae ili niweze kulainisha ugumu wa kazi yangu, lakini sasa…”, Salimu akashusha pumzi nzito, “…kuna binti mwingine anaitwa Shalon binti huyu hatofautiani sana na Meroda kwa sababu yeye pia ananipenda na tulifahamiana kabla ya Meroda cha kustaaajabisha ni kweli yeye ndiye yule binti wa Samuel ambaye aliwahi kuwa rafiki wa baba yangu yani hapo ndipo mambo yanapo nichanganya na ushahidi ni nao ukitaka mkuu mpaka dakika hii bila kupepesa

Mzee Samuel na Pater wao ndio wanahusika na mauaji” Salimu alimaliza, Komandoo Ochola akajiegemeza kwenye egesho la kiti kisha akatazama kulia na kushoto akikusanya ngozi ya sura yake akifikiri mawili matatu tokana na tarifa hiyo kisha akaanza kuongea “ …ni sawa kwa sababu sio mbaya kujua na kuto kujua kubaya ni kufeli mpango, alafu kijana ni lazima utambue kuwa wakati mwengine mapenzi ni sehemu ya matatizo kwa watu wengi lakini kwa wakati mwengine ni sehemu ya kuleta faraja ok ni sawa wacha tuone itakavyokuwa…lakini kwa kuwa mmefika pahala ambapo nilikuwa nimepachelewesha basi ngoja niwajuze jambo moja

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com
Contact 0658328596

MSIMU 3

Sehemu 10C: Wizi wa Benk

Tuendelee...

“ …ni sawa kwa sababu sio mbaya kujua na kuto kujua kubaya ni kufeli mpango, alafu kijana ni lazima utambue kuwa wakati mwengine mapenzi ni sehemu ya matatizo kwa watu wengi lakini kwa wakati mwengine ni sehemu ya kuleta faraja ok ni sawa wacha tuone itakavyokuwa…lakini kwa kuwa mmefika pahala ambapo nilikuwa nimepachelewesha basi ngoja niwajuze jambo moja muheshimiwa Samuel na Peter kwa uchache ni watu ambao tunaenda kuwachunguza in and out yao kwa sababu wamebeba shina la matatizo hii ni taarifa niliyonayo siku nyingi baada ya kurudi kazini” habari hiyo ilitokea kuwashangaza sana Salimu na Karimu wakabaki kutazamana. “Na wanakambi Ngome kubwa huko Lushoto” aliongea tena Komandoo Ochola akalamba midomo yake kisha akawatazama vijana wake kwa zamu.

“Habari za Meroda na timu yake ninazo pia ni wanawake mashujaa sana ila nilichelewa kujua kuwa wasichana hao mmpo karibu nao sana kiasi hicho na kwa kazi yetu kuwa karibu na watu kama hao ni sawa na kukaribia kumshinda adui, nashauri tuendelee kupambana na muendelee kuteka hisia zao na kucheza na udhaifu wao pia ili muweze kuwashinda wote na sio Meroda tu kwa sababu ninacho kiamini ni kuwa si rahisi wao kuwaamini nyinyi kwa asilimia zote muamini kuwa wao watakuwa wanataka kuwajua vizuri nyinyi na mahusiano yenu katika kesi hii ili imani yao iwe yenye kukamilika, na zaidi ni kuwa usikae mbali na Shalon kwa sababu ni sehemu ya kazi yetu” bwana Ochola alimaliza wazi alionekaan kukonga nyoyo za kina Salimu na kuwafanya waanze kutabasamu. “Mkuu unajua sijui nisemeje ila sikutegemea kama utalichukulia jambo hili kwa staili hii niliamini utatupatia adhabu kwa hili jambo la kukuficha…” kabla haja maliza Ochola akaingilia

“No nonoo noo hapana usiseme tena hivyo, ni sahihi mlichokifanya ni sehemu ya kazi pia sio maana kila kitu mniambie mimi noo ila tu lazima kuwe na sababu haimanishi kuwa hampo huru katika majukumu yenu hapana mnao uhuru ila mbaya ni ile kukaa na jambo na kukosa sababu ya msingi huu ni ubaya sawa” Ochola aliongea kwa mfululizo pasina kuweka kituo.
“Sawa mkuu tumekuelewa vyakutosha sana” Karimu aliongea huku akitingisha kichwa.

Basi waliendelea na mazungumzo ambayo asilimia kubwa yalielemea kwa kina Meroda na shughuli zao ambapo taarifa hizo hazikupishana na zile alizokuwa nazo Ochola baada ya kuhama katika habari za kina Meroda. Baada ya hapo walilizungumzia jambo la uvamizi wa benki namna lilivyo kaa na mipango waliyoipanga juu ya kukabiliana kwa ushirikiano wa mawazo madhubuti. “Msishahu lakini nasubiri mnithibitishie tukio hilo hapo kesho kutwa” Komandoo Ochola alinyanyuka kitini kwa ishara ya kuondoka pahala hapo, “Sawa mkuu usiwe na wasiwasi tuachie siku hizi mbili tufanye yetu” Salimu alimtoa hofu huku akimsindikiza kwa macho.
Siku iliyo fuata

Benki kuu ya Tanzania (B.O.T), Kinondoni-Dar es Salam.
Milango ya gari ikafunguliwa karibu kabisa na eneo la maegesho vijana Salimu na Karimu wakashuka wakiwa ndani ya suti nyeusi na miwani zao pamoja na viatu vyao wakashuka katika gari ya kifahari kila mmoja akiwa na briefcase nyeusi na kuelekea kwa mwendo wa sina haraka kwenye lango lango kuu. Kwa dakika kazaa walitazama kushoto na kulia. Hao kwa hatua za taratibu mguu mbele mguu nyuma wakielekea katika lango kuu la benki hilo huku walinzi waliokaa kikakamavu na kutapakaa katika kona nyingi wakihakikisha usalama walisimama kikakamavu wakiwatolea macho wageni Salimu alitabasamu tu na kujisemea ‘Huenda mjambazi wakawa ni moja ya fidi force hawa’.

Vijana hao waliingia kama wateja wengine na kila mmoja akaingia katika jukumu lake la siku hiyo akitafuta lililompeleka asubuhi hio katika Benk hiyo. “Habari dada naweza kupata huduma ya kubadili fedha za Uero kuwa Tanzania shilingi” Salimu aliongea akiwa kasimama mbele ya kiambaza kilicho mtenganisha yeye na mtoa huduma aliyemuongelesha upande wa ndani.

Dada kwa tabasamu aliaacha kubofya bofya keybord katika meza yake na kuachia tabasamu laini “Salama tu…ndio unaweza kufanya hivyo akavuta simu yake ya mezani ya TTCL na kuandika namba Fulani na kuzipiga “Habari naomba uje hapa na pana mteja umuhudumie” alimaliza dada huyo kisha punde alionekana kuja binti mwengine aliyevalia sale mfano wa huyo aliyekuwa pahala hapo. “Habari unaweza nifata huku” dada shapu alitoa salamu na kumchukua Salimu. Karimu kwa upande wake tayari alikuwa yumo ndani ya eneo la ndani akiwa na mavazi ya fundi umeme akipita na kofia yake ya cape iliyo na nembo ya shirika la TANESCO na overall lake akipita akiingia huku na kule pasina wasiwasi wowote ule.

Kawe, Kinondoni-Dar es Salam
Laptop zao zilikuwa mezani Salimu alikuwa bize akiangaika na kubofya huku aakitafuta vitu flani Karimu akiwa pembeni yake, jasho lilimtoka Karimu alitoka na kurudi na kahawa na kumpatia huku wakiendelea kushauriana mambo. “Bingoooo” Salimu aliongea kwa sauti akakusanya viganja vyake nyuma ya kichwa chake na kuanza kunesesha mwili wake akitabasamu “Well done bro CCTV kamera zote umezihack, hakuna chenga wala mchele”

Karimu aliongea kwa furaha “Nina wazo la kupindua wazo la kwanza, kwa kuwa muda tunao tufatilie CCTV kamera maana kama ramani ya jengo tumeshaidadavua mipango yetu ya namna tutakavyolicheza sebene tumelimaliza mapema asubuhi hili la CCTV kamera ndio lililobaki tuweke nguvu pamoja kabla mizuka haijachuja” aliongea Karimu Salimu akatingisha kichwa kukubari wote wakaungana kufatailia kamera kumi na tano zilizounganishwa katika laptop yao kutumia kifaa maalumu. Masaa yakakata haraka haraka macho kodo wakizoom picha na kusikiliza maongezi kwa kila video iliyowapa mashaka “Mzee wa kazi muda umeenda naona umetulia unajambo unalolifikiria” Karimu aliuliza.

“Yea ninayo, kwanza nawazia hawa walinzi waliongia sasa hivi na watakao pokea lindo saa kumi na mbili asubuhi watakuwa ni watu wakawaida au laaa pili namna walivyoingia kuingia katika mjengo inanipa sintofahamu” aliongea Salimu “…ni kweli haijulikani lakini tusisahau kesho kuna ratiba ya kusafirisha pesa kwenda mikoani huenda hiyo ndiyo trick watakayotumia” aliongea Karimu na Salimu akadakia “…na kwa mantiki hiyo sisi hatupaswi kulala hapa tutoke twende tukakomae huko huko alimradi mazingira ya benki tumeshayajua sisi hatuna budi kujiandaa kwa kazi asubuhi itukute huko huko” “…sahihi kabisa” Karimu akampa tano Salimu.

Itaendeleaa...
IMG-20220103-WA0024.jpg
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)

Nani Anahusika???

Mtui Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com
Contact : 0658328596

MSIMU 3

Sehemu 10D: Wizi wa Benk.

Tuendelee...

.....Mzee wa kazi muda umeenda naona umetulia unajambo unalolifikiria” Karimu aliuliza. “Yea ninayo, kwanza nawazia hawa walinzi waliongia sasa hivi na watakao pokea lindo saa kumi na mbili asubuhi watakuwa ni watu wakawaida au laaa pili namna walivyoingia kuingia katika mjengo inanipa sintofahamu” aliongea Salimu “…ni kweli haijulikani lakini tusisahau kesho kuna ratiba ya kusafirisha pesa kwenda mikoani huenda hiyo ndiyo trick watakayotumia” aliongea Karimu na Salimu akadakia “…na kwa mantiki hiyo sisi hatupaswi kulala hapa tutoke twende tukakomae huko huko alimradi mazingira ya benki tumeshayajua sisi hatuna budi kujiandaa kwa kazi asubuhi itukute huko huko” “…sahihi kabisa” Karimu akampa tano Salimu.

Benki kuu ya Tanzania (B.O.T), Kinondoni-Dar es Salam
“Ni saa moja na nusu tayari Kalimu” Salimu aliongea baada ya kuitazama saa katika mkono wake wa kuume ndani ya gari kisha akachukua kinyago cha sura toka begini begi akapaka mafuta usoni kisha akavaa “Naonekanaje boss” aliongea na kumtazama Karimu ambaye teyari alikuwa na sura mpya usoni mwake “Uko poa mzee” wakapeana tano na kutoka garini. Dakika moja mbele teyari walikuwa upande wa mbele pembeni ya bustani karibu na eneo la maegesho wakizuga na ubize wa simu zao bunduki ndogo zikiwa katika viuno vyao tayari kwa kulicheza sebene.

Saa moja kamiri ilionekana gari ya kusafirisha pesa ikiingia kwa maringo na wanaume wawili maaskari maalumu wakafungua mlango wa nyuma wakashuka wakiwa wamebeba sanduku na kuingia nalo ndani ya benki wengine wawili wakiwa wamesimama kikakamavu wamevalia magwanda na mikononi wameshika siraha kali. Salimu na Karimu wakiwa na sura zao za kigeni usoni walitazamana na kuendelea kusikilizia mchezo.

Dakika tano tu pekee tayari walionekana wakirudi wakiwa na sanduku kubwa wazi lilionekana kuwaelemea walitoka na kurudi tena ndani tena na tena wakibeba mzobe mzobe wakiyumba kwa uzito. Wote waliingia garini na kuondoka kwa kasi ya haja huku king’ora cha polisi kikilia kupisha njia. Salimu na Karimu hao wakachapuka na kuingia katika gari yao kuifatilia nyuma nyuma huku wakitazama saa zao “Kaka mpango sasa unaoonekana ni kuvamiwa kwa hili gari au pia inawezekana hawa sio wahusika ndio majambazi wenyewe” “Yote yanawezekana ngoja tuone” aliongea Salimu.

Ali Hassan Mwinyi Road, Kinondoni-Dar es Salam
wakiwa wanaendelea kuleta zogo huku wakiifatilia gari mbayo ilionesha wazi inatoka hapo na kuelekea mkoani walipo kuja kuzitazama saa zao ilikuwa saa mbili kasoro tano katikati ya jiji macho yakiwa tayari kwa kuona litakalo jili walitupia macho mkoba wa siraha katika siti ya nyuma ile kufumba na kufumbua umbali wa mita sabini toka katika gari lililobeba fedha mlipuko mkubwa ulilindima na kupelekea tafran kwa watu waliokuwa karibu na eneo hilo mguu wa Karimu kwataharuki ulikanyaga break. Haraka walizivua nguo za juu Karimu akabonyeza kitu pembeni ya msakani na namba za gari zilijibadili.

Waligeuka nyuma na kuchukua siraha mara moja na kuziseti bunduki zao tayari kwa mashambulizi “one minutes left” Salimu aliongea mara kwa nje bunduki zilianza kulia hovyo kutokea upande wa mashariki huku mpigaji huyo akiwa binti mmoja aliyevalia jaketi na trak yake nyeusi juu ya pikipiki aina ya Kawasaki KLX250 Camo mkono mmoja akielekezea angani bunduki yake ya aina ya AK47 mbio akielekea katika gari la fedha nyakati hizo tayari gari moja aina ya Nissan GT-R ilipita spidi na kuwasili katika gari lililopata ajari wanaume wa tano wakashuka wakiwa na siraha kali wamevalia mavazi meusi na viziba uso,

wawili wao wakasogea karibu na gari haraka na mmoja akapachika kitu Fulani kwenye mlango wa nyuma na hata sekunde nne hazikufika mlipuko mwengine ukasikika wakazama ndani na mara zikasikika milio ya risasi tatu kisha wakatoka wakiwa tayari wame beba moja ya box la fedha wakisogelea gari lilokuwa limeshasogezwa tayari kwa kufaulisha mahela wengine wakachapuka kufata box lengine ile chap chap. Sauti tu za wananchi zilisikika huku na kule huku watu wakitapakaa hovyo hovyo wasijue wanapo kwenda hali ikiwa ni kuziokoa roho zao. Bira kusubiri Salimu na Karimu wakajibu mapigo hayo huku Salimu akimlenga mwanadada huyo na Karimu akiwa ameelekeza shabaha zake upande wa gari ambako shababi mmoja alikuwa akiwalinda wenzake na kuhimiza kuwahi Salimu alibaki na mwana dada aliyekuwa katika pikipiki wote kwa pamoja waliziachia risasi na matukio mawili yalitoke kwa mkupuo amabpo Jambazi la kike juu ya pikipiki aliyumba baada ya piki piki yake kutobolewa tairi alijitahidi kuruka na kumfanya atue katika rami akiwa salama kisha akwageukia maadui zake na kuzitupia risasi mfulululizo kwenye gari jirani waliyokuwa wamejificha kina Salimu.

Upande wa shabaha ya Karimu ilikuwa sahihi maana alimpiga vizuri jambazi yule kwenye goti la mguu wa kulia akapiga yowe la maaumivu na kumfanya kuchutama ndipo alipo tuma risasi nyingine ya kumlegeza iliyokutana na bega la upande wa mguu wenye jeraha na kupeleka kuangusha bunduki yake huku akigugumia maumivu. Tukio zima lilionwa na wenzao na kupelekea mmoja ya wale wawili kuanza kumlinda wakielekekezea risasi upande wa kina Salimu mfululizo kuwatuliza huku akijitahidi kumvutia sehemu salama kwa jili ya kumpakiza kwenye gari na kutimka, jambo ambalo halikukubaliwa na mipango ya kina Salimu ambao mapigo yao yalikuwa ni ya akili kila mmoja na lengo lake Karimu akamtupia risasi jamaa mmoja aliyekuwa na jitihada za kutaka kutoroka na mahela akifaurisha box kwenda kwenye gari akilindwa na wenzake aliyekuwa akifyatua risasi mfululizo na Karimu aliendelea kumsoma na kipiga kuwa lenga akiwasihi waache mabox ya hela na kweli ikawa hivyo wakayaachia na kujificha kwa hofu mawazo yakiwa ni kutimka.


Mapambano hayakuwa ya mchezo mchezo wote walikuwa wakipiga risasi kwa kutumia akili sana maana walionekana ni watu waliopitia mafunzo maalumu hakuna aliyepata fulsa ya kukaa waziwazi na kuitumia siraha yake atakavyo maana ukionesha sura tu unakoswa koswa na risasi ukipania kumuwinda yule na mwengine nyuma anakuwinda wewe kwa kifupi majambazi walikuwa na umoja wa kulindana kwa kuwashambulia kina Salimu ili wenzao wasiweze kudhibitiwa.

Kwa upande wa yule binti aliendelea kurusha risasi huku akisogea karibu na gari kwa ajili ya kuungana na wenzake waliokuwa wakimlinda kwa mara nyingine Salimu akaipata nafasi na akaitumia vema alifyatua risasi na kukutana na mguu wa mwana dada shupavu kikasikika kilio cha mshtuko wa uchungu “aaaah” kwa sauti yake ya kike na kuaanguka kama mzigo wa kuni uliotupwa na mbebaji aliyechoka na safari. Tukio hilo liliwazidishia hofu wanaume wa kazi walioshirikiana nae na kuwafanya wakose uwezo wa kujisimamia vema na kuanza kupiga risasi mfululizo.

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)

Nani Anahusika!!

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 10 E: WIZI WA BENK

Tuendelee...


...Upande wa shabaha ya Karimu ilikuwa sahihi maana alimpiga vizuri jambazi yule kwenye goti la mguu wa kulia akapiga yowe la maaumivu na kumfanya kuchutama ndipo alipo tuma risasi nyingine ya kumlegeza iliyokutana na bega la upande wa mguu wenye jeraha na kupeleka kuangusha bunduki yake huku akigugumia maumivu.

Tukio zima lilionwa na wenzao na kupelekea mmoja ya wale wawili kuanza kumlinda wakielekekezea risasi upande wa kina Salimu mfululizo kuwatuliza huku akijitahidi kumvutia sehemu salama kwa jili ya kumpakiza kwenye gari na kutimka, jambo ambalo halikukubaliwa na mipango ya kina Salimu ambao mapigo yao yalikuwa ni ya akili kila mmoja na lengo lake Karimu akamtupia risasi jamaa mmoja aliyekuwa na jitihada za kutaka kutoroka na mahela akifaurisha box kwenda kwenye gari akilindwa na wenzake aliyekuwa akifyatua risasi mfululizo na Karimu aliendelea kumsoma na kipiga kuwa lenga akiwasihi waache mabox ya hela na kweli ikawa hivyo wakayaachia na kujificha kwa hofu mawazo yakiwa ni kutimka.

Mapambano hayakuwa ya mchezo mchezo wote walikuwa wakipiga risasi kwa kutumia akili sana maana walionekana ni watu waliopitia mafunzo maalumu hakuna aliyepata fulsa ya kukaa waziwazi na kuitumia siraha yake atakavyo maana ukionesha sura tu unakoswa koswa na risasi ukipania kumuwinda yule na mwengine nyuma anakuwinda wewe kwa kifupi majambazi walikuwa na umoja wa kulindana kwa kuwashambulia kina Salimu ili wenzao wasiweze kudhibitiwa. Kwa upande wa yule binti aliendelea kurusha risasi huku akisogea karibu na gari kwa ajili ya kuungana na wenzake waliokuwa wakimlinda kwa mara nyingine Salimu akaipata nafasi na akaitumia vema alifyatua risasi na kukutana na mguu wa mwana dada shupavu kikasikika kilio cha mshtuko wa uchungu “aaaah” kwa sauti yake ya kike na kuaanguka kama mzigo wa kuni uliotupwa na mbebaji aliyechoka na safari.

Tukio hilo liliwazidishia hofu wanaume wa kazi walioshirikiana nae na kuwafanya wakose uwezo wa kujisimamia vema na kuanza kupiga risasi mfululizo. Mwana dada akaanza kujisotesha kwa tabau tabu kulikaribia gari ndipo aliyekuwa dereva alijitoa garini akiwa na kitu Fulani cha duara akakirushia upande wa kina Salimu na akatoka mbio kumfata binti aliyekuwa chini akigaaga gaaa kwa maumivu “Karimu boooom”

Salimu alihamaki na kunyanyuka akitoka eneo hilo la gari lao lililo kuwa limechafuka kwa risasi Karimu alielewa alichokifanya ni kunyanyuka shapu na kupiga hatua kubwa tatu na kujirusha mbele zaidi kikomandoo na kweli mlipuko ukatokea gari zilizo kuwa karibu na gari yao ziliripuka kwa mkupuo. Lakini haikuwafanya wakate tamaa waliigeuza miili yao wakaziokota bunduki zao na kuelekeza upande wa maadui wakizifyatua bila mpangilio kwa ajili ya kuwahimiza waaziache pesa za wananchi. Hali haikuwa shwari majambazi hao saba tu walikuwa kama wapo ishirini walijikuta wakiacha mabox matatu ya fedha na wakajitahidi kuwavuta wenzao waliojeruhuliwa na mashambulizi hayo ikiwemo kumvuta yule jamaa aliyejeruhuliwa mguu na bega lakini Salimu hakukubaliana nao wakajikuta wakimuacha baada ya jitihada zao kugonga mwamba wakaingia kwenye gari na kuingia katika barabara na kuondoka spidi ya kimbunga lakini bado walisindikizwa na risaisi nyuma zilizokuwa zikigonga vioo na kudunda tu hazikuingia. Vijana walionekana kukasirika lakini haikuwa mbaya walichangamka na kumsogelea jamaa aliyekuwa amebakizwa katika kona ya gari Salimu akamtia pingu wakakusanya mabox ya hela pahala hapo kisha Salimu akapiga simu pahala haraka watoka na kuingia katika gari lingine na kutimka zao.

Pindi wanaondoka tu alionekana bwana mmoja mtumzima kutoka katika tax na kuelekea eneo la tukio akiwa na ghadhabu kubwaa alifika hadi alipokuwa ameegemezwa bwana yule aliyetiwa pingu hakuuliza maswali akaanza kumtia mateke ya mbavu na kumpiga ngumi mfululizo kiasi cha kuwafanya raia wengine washangae na kujiuliza nini na ujasiri gani aliokuwa nao bwana huyo kulifanya tukio hilo eneo hilo “Nijibu Mtoto Pius yuko wapi wewe shwaaini” aliongeana kumsindikiza na ngumi za uso “Unaongea kuhusu nini we kikongwe” aliongea bwana yule domo likiwa limemlegea madamu yakimchuruzika huku akiwa kashikiliwa kifuani “Nitazame huni kumbuki yani juzi tu huni kumbuki itazame sura yangu weweee nitazame” aliongea Mzee huyo akimkwida vizuri “Mmenifanya niishi maisha ya shida sana nyinyi niambie haraka” aliongea kwa ghadhabu kubwa.

Mara akajikuta ameshikwa na polisi wakimtoa katika patashika akiwa bado kakaaidi akiwayumbisha polisi huku na kule alikuwa na ubavu kweli, Polisi wakamtia pingu mzee huyo na kumfunga katika gari wengine wakikusanya mabox ya hela yaliyosalia na baadhi yao wakichukua baadhi ya maelezo ya tukio hilo toka kwa wananchi waliyoshuhudia Jambazi alikuwa tayari amezimia kwa kipigo na sumu ya risasi katika mwili wake hajitambui hajijui akabebwa mzobe mzobe hadi katika gari na kutimka wakiacha baadhi wakifanya ulinzi eneo hilo lililo haribiwa vibaya.

Wananchi waliofanikiwa kuchukua moja ya picha na video wakazituma katika mitandao ya kijamii wakiwasifu wanaume hao waliokuwa wamevaa vazi lilo na neno moja tu polisi mbele na nyuma ya migongo yao watu hao ndio wale wale waliokuwa wakiweka mambo sawa mitaani. Wanahabari walishaweka habari hewani wakionesha namna majibizano yalivyokuwa yakiendelea kati ya vijana waliokuwa wamevalia mavazi ya kipolisi na majambazi. Swali likabaki midomoni mwa watu je watu hao ni kina nani ambao kila uchwao wananyafua mambo mabaya na hawajurikani ni kina nani. Swali hilo lilitawala hata katika vichwa vya mapolisi na viongozi wao juu ya vijana hao ambao walikuwa na sura bandia kila kukicha na hata wakiondoka hakuna ushahidi wa kuwafanya kutambulika hiyo ndiyo ilikuwa desturi yao.

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact 0658328596

MSIMU 3

Sehemu 10F: Wizi wa BENK.

....Karimu na Salimu akatingisha kichwa kukubali.

Tuendelee...

Central Polis Station, Dar es Salam
Wana habari walikuwa wamejazana nje ya kituo wakipiga zogo wakiwa na kamera zao na vinasa sauti wakiwa katika makundi makundi wakitaka, kwa mbali kidogo Salimu na Karimu wakiwa katika gari wakila karanga walimuona taxi dreva akitoka kituoni na mara Wanahabari kwa haraka wakamvamia na vinasa sauti juu juu kila mmoja akiongea la kwake akitakuwa wa kwaza zaidi ya mwengine Askali wa wili waliendelea kuwapangua na kuwapangua wakimpitisha tax dreva mpaka alipo ingizwa garini “…Sasa tunafanyaje” Karimu alivunja ukimya nakumtizama Salimu

“Jambo la msingi ni kumchunguza, tumfatilie kwanza tuyajue maisha yake ili hata tukiona hakuna cha manufaa tutaachana naye juu kwa juu pasina yeye kututambua ila akiwa na manufaa na sisi tukajiridhisha usalama wetu tutajitambulisha kama askali wakawaida ili atupe mawili matatu” aliongea Salimu “Alafu vipi kuhusu kumuuliza Meroda juu ya wale waliokimbia” aliuliza Karimu “Tena umenikumbusha asubuhi nilimtafuta lakini alikuwa bize ngoja Salimu akachukua simu yake na kupiga na kuiweka simu sikioni “Mambo…Vipi mommy…vipi…umepata taarifa yoyote kuhusu wale jamaa” aliongea Salimu kisha akaweka Loud Speaker “…ohh hapana taarifa niliozipata bado wamo jijini hapo namna ya kutoka na siku husika bado sijapata maana licha ya kuwa wote ni wamoja lakini kupata taarifa ni mpaka uhusike na au uusishwe nje ya hapo huwezi jua kitu ”

alisikika Meroda akiongea “… ahaa sawa sawa Salimu aliitika” “Ndio mpenzi yaani sisi kwa sisi tumefunzwa tusiaminiae ipo hivyo lakini msijali nyinyi endeleeni na majukumu mengine chochote nitawajulisha muwe tu tayari bye” Salimu akamtazama Karimu “…nafkiri sasa tusubiri taarifa hii lakini lazima tumjulishe Ochola mapema kama kuna jambo la kushare nasi aweze kufanya” “Yap fanya sasa hivi mwambie sasa hivi tutaenda tukitoka tunapoenda” aliongea Karimu wakapeana tano “Bro…naona gari inaanza kutoka” aliongea Karimu nakuitazama Gari ya polisi ikiwa na Taxi dreva ikashika barabara na kutimka “Haya twende zetu mzee” aliongea Salimu huku akiandika kitu katika simu yake.

Muhimbili National Hospital, Kinondoni- Dar es Salam
Polisi walionekana kuzagaa zagaa kila mahala, gari ilisimama na polisi wakatoka wakiwa pamoja na tax drever wakiongozana kuelekea ndani ya Hospitali. “Mhh kaka hii sio hali ya kawaida huyu bwana ni nani mbona sielewi hebu tugawane wacha nimfatilie huyu tax dreva wewe utabaki nje ukiangalia usalama” aliongea Salimu na kutoka garini “Hebu nipatie ule mfuko wetu” aliongea Salimu na kupokea mfuko ulionesha chupa ndogo ya chai, hot pot sahani, chupa ndogo ya maji na kikombe

“Safii” alijisemea huyo akatoka na kuelekea getini ambako kulikuwa na ulinzi mkubwa. Salimu kwa macho ya kuvizia alisogea hadi katika hodi ya watu mahututi ambapo Dereva wa taxi pamoja na maaskali walikuwa wameshakwisha ingia, “Aisee si zani kama huyu mtu kuwepo humu ni salama imekuwaje kwani hakuna chumba maalumu cha kuwekwa mtu huyu?” Taxi Drever aliulizwa swali hilo kwa maaskali waliokuwa wakiweka ulinzi kwa jambazi ambaye alionekana yupo chwee kwa usingizi “Sasa nitafanyaje na askari wamejaa tele” alijionge Tax dreva kwa sauti ya chini akiwa na wasiwasi, Salimu akiwa amejibanza akisikiliza maongezi kwa aina yake “Hapana mzee wangu kimekosekana”

Dereva akiwa na wasiwasi akitazama huku na huku akiwakagua kwa macho ya wizi wagonjwa wengine waliokuwa taabani wakibembelezwa na ndugu zao. Alipokuja tupia macho mlango wa kuingilia wodini humo alikutana na sura ya Salimu ambaye alimpa ishara ya kumfata. Dereva alishangazwa na uhitaji aliouona na akatazama kulia na kushoto kuona kama anaepewa ishara hiyo ni nani na kugundua kuwa ni yeye akajishauri shauri kisha akaongea “…aisee nisubirini nakuja” “Sawa mzee” Dereva alitoka eneo hilo na kumfata Salimu alipokuwepo wakakaa upande wa ukutani “Mzee mimi ni afisa upelelezi nimepewa hii kesi kuifatilia hapa sio sehemu salama akakitoa kitambulisha feki anachokitumia mitaani kikionesha jina tofauti na mambo mengine lakini sura ikiwa ni yake. Dereva akamtazama kwa makini “…kwa hiyo unasemaje” aliongea Tax dreva “Shika namba zangu hizi ukitoka hapa tu nitafute usiwasiliane na mtu mwengine yoyote hata hao askali wambie wakupeleke nyumbani kisha tuonane mara moja” Salimu aliongea na kumpatia business card ya biashara....

Itaendeleaa....
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Nani Anahusika???!!!

Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 10G: Wizi wa BENK

Tuendelee...


akaongea “…aisee nisubirini nakuja” “Sawa mzee” Dereva alitoka eneo hilo na kumfata Salimu alipokuwepo wakakaa upande wa ukutani “Mzee mimi ni afisa upelelezi nimepewa hii kesi kuifatilia hapa sio sehemu salama akakitoa kitambulisha feki anachokitumia mitaani kikionesha jina tofauti na mambo mengine lakini sura ikiwa ni yake.

Dereva akamtazama kwa makini “…kwa hiyo unasemaje” aliongea Tax dreva “Shika namba zangu hizi ukitoka hapa tu nitafute usiwasiliane na mtu mwengine yoyote hata hao askali wambie wakupeleke nyumbani kisha tuonane mara moja” Salimu aliongea na kumpatia business card ya biashara “Mambo ya biashara yasikuchanganye mzee” “Sawa” mara moja Salimu akachepuka na kuondoka eneo hilo na kujibanza sehemu kwa tahadhari. “Hii kazi mbona inaanza kuwa ngumu teyali kuna watu nyuma yangu pia aidha niwapoteze au niwatumie” aliongea Taxi dreva kwa sauti ya chini, Haukupita muda mrefu akiwa kakishikilia kikaratasi askali nao wakamfikia.

Taxi dreva alionekana kugutuka akaingiza mkono mfukoni na kutoka na simu akaiweka sikioni. Lakini akaishusha na kuibadili sura kuwa ya ghadhabu “Shenzi sana mbona hapokei simu” kisha akanyusa. “Mzee vipi?” mmoja ya askali alihoji “Safi jamani mi naona sasa mniache nikashughulikie familia yangu maana sijui inaendeleaje huko ilipo naomba mnipeleke lakini tu nawasihi ni gheri mlale hapa huyu jamaa sio mtu wa kawaida” alisistiza dereva wa taxi “Sasa mzee tumeambiwa na mkuu tusikuache pahala kulinda usalama wako itakuwaje sasa kwetu ikitokea ukapata madhara?” dareva akakumbuka maneno ya Karimu na kuwaza la kufanya “…nipelekeni kwanza nyumbani alafu gari yangu si ipo sehemu salama” “Ndio mzee usiwe na shaka nalo” alijibiwa na kijana yule yule. Taxi drever akaingia kwenye gari ya Polisi na safari ikaanza, Salimu na Karimu nao wakaingia garini kuwafata kwa nyuma.

Ikonga, Kinondoni-Dar es Salam
Katika chumba cha mipango timu ilikuwa imekamilika “…kwakweli sikutegemea kama tukio lile la leo linge tokea kwa namna ile mnisamee sana vijana wangu” aliongea Ochola uso ukiwa umesawajika “Hakuna shida mkuu ni kama ajali tu, jambo la msingi hapa ambalo tunatakiwa kujiandaa nalo ni namna ya kumteka yule jambazi na kumtorosha mzima mzima kumuweka mafichoni kabla jamaa zake hawajamuwahi na taratibu zipo za namna mbili aina ya kwanza ni kifo yeye mwenyewe kujiua au kuuliwa na wenzake pili kutoroshwa na wenzake haya yote yanawezekana na hapa tunapo ongea huwenda na wao wapo safarini au wameshafika sembuse wameshaanza taratibu za kumtoa hospitalini” aliongea Salimu “Correct” Ochola alidokeza kuunga mkono.

Kikapita kimya kwa muda. Komandoo Ochola akasimama hadi katika white board akachukua maker pen nyeusi akaanza kuchora michoro Fulani ya mishale kisha akaanza kuongea “Plan A ni kumtorosha jambazi na B ni kumchunguza Dereva wa Taxi ni kwa maelezo yako Karimu una maanisha na yeye ni mtu ambaye kuna anayo yajua kuhusu majambazi hawa kwa namna moja au nyingine hivyo ni lazima afanyiwe mahojiano ya kirafiki” aliongea Ochola. Baada ya hapo mazungumzo yakaanza kuhusu namna ya kumtorosha jambazi lile.

“Mkuu sasa mpango wa kumtorosha tutambue utajenga taswira kuwa ametoroshwa na wenzake je itakuwa sawa?” alihoji Karimu macho yakiwa kwa Ochola “Hapa ni lazima nitoe taarifa makao makuu juu ya kupata ridhaa ya kumuhoji….ahh au itatubidi tutumie siraha bandia zenye baruti tufanye mlipuko salama kuonesha kuwa anatoroshwa?...lakini hii italeta shida kwa wagonjwa tunaweza kusababisha vifo kwa watu wengi mnasemaje vijana” aliuliza Ochola. Mpango ulionekana kuwa mzito kidogo. Kipindi ikiwa kila mmoja akiwaza lakwake simu ya Salimu ikaingia meseji na Salimu akaifungua na kuisoma “…yes tumesharahisishiwa kazi wanandugu” Salimu katabasamu na wenzake wakamtazama kumsikiliza. “Ni hivi nimepokea ujumbe hapa toka kwa Meroda kuwa kesho kutwa asubuhi waatakuwepo ndani ya Muhimbili kufanikisha tukio la mauaji ya jambazi hivyo tuna leo na kesho tu.” Salimu aliongea lakini bado macho ya wasikilizaji yalikuwa yametumbuka yakimuangalia na masikio yakiwa juu juu “…sasa basi sisi inatupasa tufanye mpango wa mahojiano alfajiri ya kesho kutwa hiyo hiyo tena inafaida kwetu kwa sababu atakuwa ameshapata walau nafuu na kuzinduka ili kesho mimi na Karimu tuambatane kumfatilia dereva mnasemaje?” aliongea Salimu “Mhh Salimu hapa kama tunacheza kamali vile vile unajua wazo lako sio baya lakini unauhakika gani kama kweli tutapata kitu kwa dereva mfano tukapata stoli tofauti tukarudi huku yule bwana naye akawa ameshakufa” Karimu aliongea na kupelekea kuleta ugumu wa kazi kutokana kila mmoja kuonesha kutokuwa na lakusema.

Baaada ya dakika kazaa kupita “Vijana imani ndiyo inayotakiwa kuchukua nafasi yake hapa anzeni na Dereva ili atutoe mashakani kuliko kuja kumtegemea na akawa hana chochote nitasimamia usalama wake leo kutwa nzima na kesho pia nyinyi muitumie vizuri” aliongea Ochola Salimu akatabasamu “Nikweli Mkuu…nyongeza hapo lile jambazi tulipeleke kwenye chumba chochote cha siri ambacho hakitumiki, tena ikiwezekana asubuhi sana, sisi tutamuhoji vizuri kisha atarudishwa wodini hata akifa sisi tutakuwa hatuna hasara na hata tukio zima litakuwa halijajulikana na watu na pande zote kutakuwa salama si kwa mapolisi wala sio sisi maana mtuhumiwa atakuwa amekufa kifo cha kusababishwa na majeraha yake tu.” Aliongea Salimu. Mawazo yalionekana kuwa mazuri wote wakaanza kupiga makofi kumpongeza Salimu.

Itaendeleaa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom