The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email
akidasiri@gmail.com
MSIMU 3
Tuendelee...
SEHEMU 10: UVAMIZI WA BENK
Dondoo;
“Salimu anapokea taarifa ya uvamizi wa benk kuu ya Tanzania, katika hatua za kukamilisha majukumu anatokea dereva wa tax na kumjeruhi moja ya majambazi na kuwashangaza watu yeye ni nani hasa?! Kabla ya kuamua la kufanya wanapanga mpango wa kukutana na dereva wa tax huku wakipanga mpango wa kumtorosha jambazi lillokamatwa na kufanya mahojiano. Je! mipango yao itafanikiwa?”
Ngome Msitu wa Magamba, Lushoto- Tanga.
Meroda na rafiki zake wakiwa wamejibanza katika mwisho wa jengo wakichungulia kwa tahadhari, mara kundi likaonekana kundi likikatika. Meroda na wenzake wakatoka kulifata huku wakilindana, ghafla wote wakabonyea baada ya kusikika kwa vishindo vya watu upande mwengine, lilikuwa kundi lingine wakielekea upande ule uliokwenda kundi lililotangulia.
Baada ya utulivu kukolea Meroda akajitosa kwa mwendo wa mbonyeo akiwafata nyuma nyuma hadi katika jengo moja refu akatulia akageuka na kutoa ishara kwa wenzake. Baada ya kufika wenzake Meroda kwa ustadi akabetua dirisha la mbao ukapatikana upenyo akaliweka jicho lake na kuchungulia.
Samuel na Pater wakiwa katikati ya nusu duara la kundi la watu. Upande wa nje akaonekana msichana matata ndani ya mavazi meusi ya mterezo yakiwaka waka chini akiwa na viatu virefu akiwa na haraka kubwa akiufata mlango wa jengo. “Hee Jane!” Meroda aliongea kwa mshtuko kwa sauti ya kunong’ona wazi akiwa na wasiwasi. Hofu ikiwa imempanda Meroda aliendelea kutegesha sikio kunasa habari kwa kadri alivyoweza, alipotosheka akang’atuka na kutoka zake kwa staili ile ile aliyoingilia pahala hapo ya nyatu nyatu. Meroda baada ya kuingia katika chumba ambacho wanaishi yeye na wenzake
“Jamani habari mbaya kundi B na kundi F la Jane Dume yalikuwa na kikao cha uteuzi chini ya usimamizi wa Meja Mogisha na Alfani Mashu kwaa ajili ya uvamizi wa Benk Kuu ya BOT kesho kutwa naogopa itakuwaje”
aliongea akiwatazama wenzake mikono ikiwa kiunoni akiibana midomo yake “Mhh hapo wanaenda kwenye vita au maana hao watu sio watu wa mchezo ni vichaaaa wa bunduki” Monica aliongea akiuwacha wazi mdomo wake na kuwatazama wenzake zamu zamu “Sasa tunafanyaje shemeji zangu…. ehhh mungu wangu” aliongea tena na kujishika tama akiwa bado amekaa kitandani “Sijui kwa kweli lakini naona la msingi ni kuwatumia ujumbe mfupi muda huu”
aliongea Meroda huku akichukua simu yake mezani na kuanza kuandika ujumbe na kuutuma. “Vipi umeshamtumia na imefunguliwa tayari?” Samira aliuliza “Yeah nimeshafanya” Meroda akasogeza uso kutazama kioo cha simu “Amejibu tayari…anasema asante kwa taarifa mapema kukikucha atafanya mipango ya kuzuia tukio” mara Meroda akaonekana kuwa na mawazo
“… lakini nina wasiwasi sana jamani sijajua uwezo wao sijawahi kuwaona kwa macho uwezo wao kiasi cha kuwalinganisha na kina Jane wanaofanya mazoezi magumu kila kukicha” aliongea Meroda, Samira akamuangalia Meroda huku akiwa kasimama “Dada wala usijali ni kazi yao binafsi nina imani watafanikiwa” Samira akajitupa kitandani. “Jamani sijui nimwambie na lile lingine” Meroda aliazisha mazungumzo kiasi cha kuwafanya wenzake wamtazame kwa mshangao
“Dada kwani huja mwambia? kama umeamua kumsaidia mtu basi msaidie bila kujali hainahaja ya kuwaza mambo katika negative mind siku akija jua ulijua au unajua utamuu ni taarifa anapaswa kuwa nazo ili wajipange wataanzia wapi” Monica aliongea huku akimtolea macho Meroda,
“Dada sio siri nakuona ujasiri wako umeanza kupotea kwa sababu ya mapenzi na sizani kama utafanikiwa kwa stairi hiyo acha wivu” Meroda aligeuka na kumtazama Monica akionekana kuumizwa na maneno hayo kaisi cha kuandika ujumbe mwengine na kuutuma na kuaambatanisha na picha kisha akajilaza.
Kawe, Kinondoni-Dar es Salam
Muda wote Salimu alikuwa bado kajiinamia tu huku mkono ukiwa umeshikilia simu shingo kaipinda ikitazama pembeni macho yakiwa mekundu na michirizi ya machozi yaliyo kauka kuchola ramani toka machoni hadi mashavuni akiwa sofani, huku sauti ya hodi ikifatana na mlio wa mlango unaogongwa ukiendelea kusikika chumbani humo lakini wala hakuonekana kushtuka wala kujali. Ndipo mlango ukafunguliwa na Karimu akaingia “Kaka kuna nini?”
Karimu aliduwaa kuona hali ya unyong’onyo ikiwa imemtawala ndugu yake wa hiyari hakusubiri akakurupuka hadi alipo. Kinyonge Salimu akanyanyua mkono na kumnyooshea simu. Karimu akaipokea na kutoa password alichokutana nacho kilimfanya ashtuke macho yakamtoka akamtazama Salimu na kujikalisha kitini kama mtu aliyetembea muda mrefu bila kupumzika. Simuni kulikuwa na mtiririko wa picha za Shalon akiwa na Mzee Samuel na maelezo chini yake yakithibitisha hilo, kikapita kimya “…kaka unapaswa kuwa na nguvu Shalon kuwa mtoto wa Samuel haimaanishi kuwa tumeshafeli, ni hatua nyingine na tunapaswa kukubaliana na ukweli uliopo” Karimu aliongea kisha akamshika bega “Kaka kila kitu kitakuwa sawa jiandae tukakutane na Ochola kwanza hata ofisini leo tusiende kwanza” Salimu mara akajikuta akishindwa kujizuia hali ya ubinadamu ikamtawala
Itaendeleaa....
Mambo yameiva huku