The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Nani Anahusika???
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email
akidasiri@gmail.com
MSIMU 3
Sehemu 11F: Mchafuko
Ilipoishia...
mahusiano na mtu unaempenda s” aliongea Mzee Samuel huku akitabasamu machoni machozi yakimlenga . Shalon kwa furaha alipanda ngazi haraka haraka na kukimbilia chumbani akafungua na kujitupa kitandani akipiga kelele za furaha.
Tuendelee....
Muhimbili National Hospital, Kinondoni- Dar es Salam
Karibu kabisa na saa kumi na moja asubuhi kigiza kikiwa kina randa randa Komandoo Ochola, Salimu na Karimu walikuwa wamo Hospitalini. Kwa tahadhari Komandoo Ochola akiwa na vijana wake wakaingia katika moja ya chumba na kufunga mlango. Mara taa ikawashwa macho kwa macho wote wakayakutanisha kwa Jambazi, “Haaa Mgaya imekuwaje? Kimetokea nini mbona sielewi!?” Komandoo Ochola macho yamemtoka akipiga hatua za kuchoka na kumshika bega Mgaya “Mgaya ni wewe?” Mgaya kwa tabu alijitahidi kunyanyuka baada ya kuisikia sauti anayoifahamu huku macho yakimtoka “Ocholaaa, Ochola we ni mzimaaaa hujafa Ocholaa” aliongea kwa tabu na yeye akiwa haamini macho yake
“…acha tu ndugu yangu sijui hata pakuanzi…ulipokuwa umepotea tulipata mission ya kwenda DRC yaliyotukuta huko tuliyofanyiwa ni mabaya sana na baadhi ya wenzetu tuliuana kama kuku baada ya kugawanyika makundi mawili, sababu kuu ni uchu wa madaraka kwa kweli jeshi liligawanyika na kuchafuka watu tukawa hatuaminiani tulibaki kukukumbuka tu Ochola mi nilinusurika katika msitu wa kongo nikatokea Rwanda nikiwa sina hili wala hili dahh”. Alimaliza Mgaya kwa uchungu “Aisee mi nipo na vijana hapa tuna kazi maalumu ya kusafisha nchi na kumtafuta Komandoo Swai kwa udi na uvumba najua ndiye tatizo na mtu mbaya zaidi” aliongea Ochola Mgaya akatabasamu
“Nimefurahia sana maamuzi yako Ochola mi pia nilitamani sana kuyafanya hayo lakini sikuwa na wakumuamini na tena nilipokuja kugundua nimewekwa katika watu marehemu na mafao yangu yote kuliwa nilijikuta nakuwa masikini wa kutupwa mmoja mbaya wa kukaba na kuibia watu usiku ndipo nikajikuta nikiingia katika njia hii ndugu yangu” aliongea Mgaya na kujifuta machozi yaliyokuwa yamejaa machoni mwake. Salimu na Karimu walijikuta wakijiinamia tu sura zikiwa zimewashuka “Vijana tuna weza anza kazi yetu tafadhari anzeni mhojiano” aliongea Ochola huku akirudi nyuma taratibu
“Ndio mnaweza kunihoji kuweni huru mnataka habari gani ya maboss zangu majina ya viongozi wala rushwa mafisadi, majambazi au mnataka majina ya watu wanaofanya biashara ya siraha na madawa ya kulevya mnataka nini?...” aliongea Mgaya huku akitabasamu kisha akaendelea “…nitaongea kila kitu na kutubu kwa mola wangu hata mkiniua pia nipo radhi” alimaliza na kuendelea kuwatazama kina Salimu,
“ Ni sawa naomba kujua tu majina kamili ya mabosi zako bishara wanazozifanya washirika wao ni kina nani, maskani yenu ipo wapi idadi yenu, na ni watu wanamna gani na mnafanyaje shughuli zenu zote kwa ujumla” aliongea Karimu. Maohojiano ya pande mbili yakachukua nafasi kadri walivyopanga ikawa bandika swali bandua weka lingine toa. “Ni saa kumi na mbili kamili sasa muda hauna rafiki, asante Mzee Mgaya kwa ushirikiano wako nina mambo ya nyongeza tafadhari” aliongea Salimu akimtazama Ochola kisha Karimu kwa utulivu kisha akayarudisha macho kwa Mzee Mgaya “Ndio endelea...” aliongea Mgaya “Asante, hivi unakumbuka kifo cha Muheshimiwa Richard Edward pamoja na familia yake?..unakumbuka ubaya mlio mfanyia” Machozi yakiwa yana mlenga lenga,
Hamadi Salimu akatoka kwa nguvu na kumsogelea Mgaya lakini hakuwa wahi Karimu Alisha mzuia na kumuweka kando akimpiga piga mgongoni “Tulia kaka punguza jazba kidogo” aliongea Karimu wakati huo Salimu hasira zikiwa machoni akijaribu kujizuia kifua kikipanda na kushuka kwa hasira “Bira shaka wewe utakuwa ni mtoto wa Richard…wewe ni Pius, pole kijana nimefurahi kukutana na wewe hapa ni stori ndefu kijana” aliongea Mgaya na kumfanya Salimu aliyekuwa kajiegemeza ukutani akituliza hasira kugeuka taratibu na kumtazama “ Dunia ina mambo ya ajabu sana ni hivi mimi niliye okoa maisha yako siku ile sikujua kisa cha mauaji ya familia yako mpaka sasa sikuwahi kujua sababu hasa ya kuuliwa kwa familia yako lakini ninachokihsi ni mambo ya kimapenzi,wivu,chuki,kisasi ndivyo vilivyochukua uhai wa baba yako ila kwa sasa naomba unisamee sana kwa jambo hilo”
Salimu akamtazama sana Mzee Mgaya akatizama chini akajifuta chozi kwa tabu akaongea “…ni sawa na pole kwa majeraha yako, inamaana hakuna unachokikumbuka siku hiyo?”. “Shukran kijana wangu najua sina maisha marefu tangu sasa najua nitakufa nashukuru imekuwa sababu ya kufumbuka macho leo wewe niliye okoa maisha yako umekuwa sababu ya kunirudisha kule nilipo kuwa awali asante…lakini kuna kauli aliongea siku ile baba yako ilimaanisha kuwa kuna mtu mwengine pia aliyekuwa anahitaji maisha yake tofauti na rafiki zake kwa sababu…” Mgaya akashusha pumzi kidogo na kuwatazama kisha akaongea “…sijui lakini sisi hatukumuua baba yako aliuwawa na kijana ambaye mpaka hivi leo sikumjua na wala sikupata mtu wa kunipa jawabu zaidi ya kusisitizwa ninyamaze tu”
Kila mmoja chumbani hapo alionekana kushangazwa na kutoa macho yanayosema “KIVIPI” Mgaya akaendelea “Siku ile kijana tukiwa garini kwa ajili ya mauaji nilipokea ujumbe mfupi ulio sema “Hakikisha mtoto Pius hafi” lakin niliona na wenzangu wakitazama simu zao kana kwamba wajumbe walizotumiwa kwa kweli sikujua ujumbe ule ulitoka wapi na wala sikuwa na jeuri ya kumuuliza mtu yeyote mpaka leo, lakini siku ile…” Mgaya akajiweka sawa na kuendelea “…ilikuwa tuuwawe wote na baba yako lakini alitokea mtu...
Nani alitokeaaa usikoseee kufatilia.....