Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 7A- MUUNGANO

“Kwa kisingizio cha kuitwa na Mkuu wa shule Salimu na Karimu wanatekwa na watu wasio julikana na kupelekwa Kando ya mji, wanashtuka wakiwa kizuizini katika jengo kubwa hofu na wasiwasi unawajaa anasimama mtu wasiye mjua na kuwauliza wao ni akina nani na wanafanya kazi yao ya upelelezi na nani? Je! Ni nini kitawakuata vijana hao?”

Mpiji, Kibaha –Mkoa wa Pwani

Katika nyumba ya ghrorofa iliyokaa peke katika msitu mdogo wa miti iliyoshikana na kuleta hewa nzuri na utulivu Bwana yule anaefata nyendo za kina Salimu akiwa juu ya ghorofa mkononi darubini akiwa amevalia kaptula aligeuka kusogelea meza iliyokuwa mbele yake na akazitawanya picha tano ambazo zilikuwa zimekusanywa pahala pamoja. Baada ya kuzitawanya akachukua picha mbili tu ambazo zilikuwa zikimuonesha Salimu na Karimu wakiwa katika miuonekano ya mazigira tofauti kisha akaanza kutingisha kichwa kukubariana na mawazo yake. Akiwa kazishikilia akapiga hatua fupi fupi hadi katika moja ya vyumba “Vijana nimesha amua sasa chukuaeni majina haya na muyatume kabla ya jua halijazama hawa wanatutosha na kikubwa wameshamaliza mitihani yao ya form six jana wacha tuone”. Aliongea bwana huyo mtu mzima akiwatazama vijana wawili waliokuwa bize na kompyuta zao.

Akaziweka picha mbili mezani na mmoja wao akachukua picha hizo zilizo wekwa karibu kabisa katika meza yake “Sawa mkuu” akaitika “Mziscan hizo picha na kuzituma kwa email yake binafsi ndiyo tutakayo itumia kwa sasa sawa zungu”, “Sawa mkuu” Zungu aliitika tena.

Kibaha High School, Kibaha - Mkoa wa Pwani

“Mzee, Mkuu wa shule anasemaje hapo mbona umebung’aaa mdomo wazi” Karimu alishusha pumzi na kumtazama Karimu kwa muda, “Ndugu Mkuu wa shule anahitaji kutuona nyumbani kwake ameagiza gari nje ya uzio ni dharura” aliongea Salimu “Mhh! Mbona ghafla hivyo ahh sasa…” aliongea Karimu na kukatisghwa na Salimu “Karimu ni hivi haina shida lakini lazima tulifikirie hili vema ni yale yale mambo ya siasa tena kama siku zote au ni kuhusu mambo ya shule” Walijaribu kudodosa walau kutambua ni jambo gani. Hazikupita hata dakika sita tayari walisikia majina yao yakiitwa nje ya bweni wakaitika nakupata habari ya ugeni unaowasubiri nje ya uzio. Walitazamana Salimu na Karimu mioyo iliwabadirika wasiwasi ukawapanda “Kaka mbona imekuwa harakaharaka sana leo amemaliza tu hata…mara tunauliziwa mhh!” Salimu alihoji akimtazma Karimu. “Kaka sikia mi pia nimeshangaa lakini hebu tuvae fasta twende huenda huyo mtu aliagizwa muda ila mzee alisahau hivyo amechelewa kutoa taarifa”.

Salimu akayapima maelezo ya Karimu akayapa uzito Fulani yalimuingia kiasi Fulani lakini bado hakuridhika alichofanya ni kupotezea. Haraka haraka walivaa viwaro kisha wakatoka nje kabisa Salimu alimsimamisha Karimu kisha akatoa simu yake ya smartphone na kuipiga namba ya Mkuu wa Shule na akaiweka simu sikioni akisikilizia simu ambayo ilikuwa ikiita tu bira kupokelewa wakiwa mbele ya gari moja ndogo aina ya nissan murano rangi ya kahawia. “Shit mbona hapokei simu huyu mzee” Salimu alikunja ndita kisha akaitazama gari hiyo ambapo Dereva alionekana nje akiwaoneshea ishara ya muda unaenda. “Kaka vipi?” “hivi hii gari ulishawahi iona kabla?” Karimu aliitazama akagutuka kidogo “Mhh hapana mzee” sura ikiwa yenye wasiwasi na viulizo. “Nataka kumuuliza mkuu gari gani iliyokuja kutuchukua maana hapa naiona hii tu na sio ile gari yake tuliyoizoea wee huoni ni tatizo”. Wakati huo kwa mbali ilionekana gari ikiwa imesimama ikitazama upande ambao vijana hao walikuwepo.

Dereva sasa alionekana kupiga kelele akiwataka wafanye haraka. “Basi tufanye hivi...mtumie meseji kuwa nimekupigia na wewe hukupokea kunagari hapa inaonekana ndiyo uliyoituma sisi hatujawahi iona sasa sisi tunapanda lolote likitokea utahusika”. Salimu alionekana kufurahia wazo hilo la Karimu na yeye akafanya kama alivyoshauriwa kisha akasogea hadi kwa mlinzi na kuanza mazungumzo kisha akampa simu huyo akasogea pahala alipo karimu. “Twende zetu” hao wakaondoka na kuingia katika gari na safari ikaanza. Dereva akiwa anaendesha mwendo wa kawaida alichukua simu yake ambayo ilikuwa ikiwaka na kuzima ikionesha maneno ya 1 NEW MESSAGE iliyokuwa upande wa kushoto karibu na sehemu ya chupa ndogo ya maji ya kunywa akaichukua akaifungua kuusoma ujumbe huo. “Unaweza kuanza kazi mara moja”. Bwana huyo baada ya kuusoma ujumbe huo wa maneno na yeye akaandika wake chapu chapu “Sawa Mkuu” na akautuma kwa namba ile ile iliyotumika kutuma ujumbe wa mwanzo. Kisha akaongeza kidogo spidi na kuupandisha vioo vyote vya gari hiyo


Itaendelea .....

Mambo yanazidi kuwakaa
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 7B : MUUNGANO

Tuendeleeee...

Kisha akaongeza kidogo spidi na kuupandisha vioo vyote vya gari hiyo. “Mnasikia joto ngoja niwashe air condition”. Basi kweli akawasha Air Condition na na kisha baada ya mwendo wadakika kama tano gari ikaanza kuonekana ikizima ghafla. “Mhh hii nini sasa”. Dereva alijiongelesha kisha akabofya kitufe flan kilichokuwa kinatoa harufu nzuri ya matunda na yeye akatoka chap na milngo ikajilock. Ilikuwa ni jambo la kushangaza sana hakuna Salimu wala Karimu aliyeweza kutambua kinachoendelea taratibu wakiwa pale wakajikuta wakiishiwa nguvu walilegea na kupoteza fahamu.

Mpiji, Kibaha-Mkoa wa Pwani

Fumba na kufumbua kwa shida giza likiwa totoro ghafla taa ziliwaka Salimu na Karimu wakiendelea kupambania kurudi katika hali ya kawaida wakiwa ndani ya chumba kikubwa kwa mapana na marefu wakiwa wamekalishwa vitini na kuegemezewa mezani “Vipi zimebaki dakika ngapi dozi hiyo kuisha makali?” bwana yule yule mwenye kufatilia nyendo za kina Salimu alikuwa mbele akimuhoji Dereva kwa wakati huo na yeye alikuwa kasimama kwa ukakamavu akitazama meza waliokuwa wamelazwa kina Salimu. Bwana aliye ulizwa akanyanyua mkono wake kutazama saa mkononi mwake iliynekana si saa ya kawaida tu “…bado sekunde kumi na tano” alijibu “Kaa tayari kwa mapambano”Yule Mzee aliongea tena. Bwana yule aliongea kwa tahadhari. Mara Salimu alikuwa wa kwanza kukokhoa mfululizo na Karimu na yeye akafata akili zilipo kaa sawa walitahamaki wakiangaza macho huku na kule wakikazana kufurukuta kutoka katika kizuizi kila mmoja kwa uwezo wake lakini loo haikuwa msaada kamba ziliwazuia. “Ndugu yangu hivi kuna kitu unachochokikumbuka unikumbushe” aliongea Salimu “Hapana ndugu najaribu lakini sipati kitu” waliishia kunong’ona. Karimu alijibu akihema hovyo hovyo na kuanza kupiga kelelee za msaada.

Salimu alipata ujasiri akamkanyaga Karimu kumtuliza kisha akamkazia macho ya onyo. Sauti za vishindo vya hatua vilianza kusikika na kusababisha Salimu na Karimu kunyanyua nyuso zao “Salimu na Karimu hamjambo vijana…” Ilikuwa ni ajabu kubwa mishangao ikawajaa wakatazamana “…Salimu wewe ulihasiliwa na mzee mmoja mvuvi kule Bagamoyo unaweza kutuambia wazazi wako ni kina nani?” Salimu moyo ukamfanya Paaaa. ‘Mungu wangu hawa ni kina nani na wamenijuaje mungu wangu’ alijisemea nafsini. Karimu kwa macho ya kutaka kulia alimtazama tu Salimu kama mtu anetaka kuongea kitu lakini uwoga ukiwa unamzuia mwishowe akajitutumua na kuongea “Samahani ndugu naomba ujitambulishe na kisha useme unachokitaka kwetu” “Acheni ujinga nyinyi ni wanaume acheni kulia lia hovyo”. Bwana yule aliongea kwa ghadhabu sura akiikunja huku akiwatazama kwa zamu “Okay sasa mnaweza kuniambia boss wenu ni nani? sita waumiza.” ,“Bosss?!!” wote walitaharuki wakishangaa maneno hayo. “Sisi hatuna boss mbona, sisi ni wanafunzi yani…mzee…” Karimu aliongea kwa uwoga mkubwa akitetemeka akiachia achia maneno. “Hahaaaaa” bwana yule alicheka kivivu na kuwafanya kina Salimu waendelee kushangaa. “Vijana msiwe na wasiwasi sawa…naitwa Komandoo Ochola” aliongea Ochola “Komandoo” Salimu na Karimu kwa pamoja walilitaja jina hilo, “Naam naitwa hivyo, najua mpo na maswali mengi sana msijali mtajua kila kitu Jeff hebu lete kinywaji chetu kile na kisha uwafungue kamba”. Jeff ambaye alikuwa ndiye dereva aliyewaleta kina Salimu pahala hapo akatoka alipo na kusogea upande wa pili mkono wa kulia ambako kulikuwa na chupa mbili na kusogea nazo akaziweka katika meza na kisha akawafungua kamba. Kipindi hicho Salimu na Karimu wakimtazama tu.

Itaendelea...
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 7 C: MUUNGANO


Tuendeleeee...

Kipindi hicho Salimu na Karimu wakimtazama tu. “Kunyweni msiwe na shaka na mniamini kunyweni” Komandoo aliwaangalia kwa makini kisha akaanza kutembea akipiga hatua fupi fupi mkono mmoja akiushikiza nyuma ya kiuno na kuanza kuongea “Nawajua nyinyi kuanzia mkiwa wadogo mkiwa mnasoma msingi hadi sekondar mpaka hapo mlipofikia hahahaa ni vijana wazuri sana na ni maalumu, miezi kazaa nyuma mlikuwa mkifatilia uvamizi wa supermarket mnakumbuka?” aliongea na kuwafanya Salimu na Karimu kutacha midomo yao wazi “Hakuna nisichokijua kuwahusu nyinyi kwa kweli labda yale machache tu, nimependezwa sana na ninyi vijana, nia yangu ni kuwafanya kuwa watu maalumu katika nchi hii tuifanye kazi ya kusafisha nchi iwe na amani kwa sababu mnapenda haki, mnaujasiri, kujiamini, akili na maarifa, na vipaji mbalimbali” akaivuta pua yake na kutabasamu kisha akaedelea. “…Moyo wangu uliendelea kunisukuma na kupandisha hisia za mafanikio, niliamini kuna kitu maalumu ndani yenu vijana ndio maana nikawachagua najua mna zaidi ya hayo niliyoyataja nataka tuunde timu maalumu.” Aliongea Komandoo Ochola.

Masimulizi hayo yaliyowafanya Salimu na Karimu kutabasamu taratibu wakaanza kunywa kile kinywaji na kweli wakaanza kusikia miili na akili zao zikiwa na nafuu na kupoa . Komandoo aliendelea “…kutokana na uwezo niliousikia nilianza kuwa na mashaka na nyendo zenu kuwa kuna kazi maalumu mmepewa na majambazi au kuna Afisa amewapandikiza mnamfanyia kazi za usalama ndipo nikaaingilia kati lakini nimegundua hakuna bali nyinyi mnaipenda kazi hii siyo mnapenda kuwa Intellegencia sio” Karimu alionekana kuvutiwa sasa akiwa hana wasiwasi hata chembe “Ndio hilo ndio lengo letu Komandoo” . “Haahahaa” Ochola alicheka kivivu lakini alionekana kukumbuka kitu na sura ikakunjamana akaongea “… ngoja niwape simulizi fupi kunihusu Ili kuwatoa wasiwasi zaidi” Komandoo akakokhoa kidogo kuliweka koo lake vizuri akasogea katika meza kisha akaakaa upande akaendelea “…Nilipokuwa Parkistan nilikutana na kazi ngumu sana ambayo sitoweza kuisahau katika maisha yangu nilitembea kwa utambulisho wa Uraia wa Uingereza nikikimfatilia gaidi mmoja ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu mjini Lahole Parkistan akisomea mambo ya Engeneearing and Technology nikitembea kwa kivuli cha mwandishi wa habari wa Uingereza kazi hii niliipata toka kwa bwana mkubwa mmoja anaitwa Joka.”

Komandoo mkono mmoja ukiwa mfukoni mwa suruali yake akatazama sakafu kisha akatabasamu kidogo kipindi hicho Salimu na Karimu walionekana kuvutiwa sana na simulizi hiyo ya Komandoo na kuwafanya kusahau kama dakika kazaa nyuma walikuwa ni watu wakulia hovyo katika jengo hilo. Aliendelea Komandoo kutoa masimulizi “…nikiwa namfatilia mwanafunzi yule nilikamatwa kwa kuhisiwa kuwa ni mmpelelzi wa Marekani niliikutana na watu wenye roho mbaya wanao jua kutesa baada ya kuhisiwa ni mpelelezi kitu ambacho kilinifanya niwe kimya mpaka siku nilipo pata upenyo na kukimbia katika kambi ya watu waovu hao nikiwa na ushahidi wa tape na kufikisha katika Ubalozi wangu wa Tanzania na kuwaachia wamalizie majukumu mengine” Komandoo akiendelea kutembea akienda na kurudi kwa maringo kina Salimu wakimtazama akaendelea “…kazi hiyo iliyochukua miaka mitatu ikaishia hapo na kukutana na kazi zingine, mnajisikiaje sasa”.

Karimu alishusha pumzi nzito huuu! Akatabasamu kuonesha amependezwa sana. Komandoo sasa akawasogelea akiwa amejawa na tabasamu zito “…naomba sasa tuagane tukutane tena kesho kuna mambo muhimu nataka tuyaongee kisha tuanze hatua nyingine haraka” Komandoo akampa mkono wake wa kuume Salimu na kuufatisha kwa Karimu “Sawa Komandoo tumeelewa”. Karimu aliongea akiwa bado ameushikilia mkono akimtazama machoni kuonesha anatamani masimulizi yaendelee.


Itaendelea...
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

Mtunzi AKIDA SIRI RAMBAO
Contact : 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 7 D: MUUNGANO

Tuendeleeee...

Salimu na Karimu wakachukulia hadi katika gari na kuondolewa eneo hilo. Komando Ochola akaitoa simu mfukoni nakutoa simu na kutafuta namba akagota katika jina la Zungu akabofya kitufe na kupiga. “Vipi uliwasiliana na Head Master?” aliongea hivyo baada ya upande wa pili kupokea “...sawa haya sawa mwambie ajiandae kwa uhamisho kazi yake imeisha” alitoa simu katika sikio lake na kuirudishia katika mfuko wa suruali akasimama akisindikiza kwa macho gari iliyokuwa ikiondoka pahala hapo.

Kibaha High School, Kibaha - Mkoa wa Pwani

Ndani ya bweni, Salimu na Karimu wakiwa wamekaa mmoja juu mwengine akiwa chini katika kitanda cha ghorofa. “Kaka unajua kunakitu sijakielewa hata kidogo hebu ngoja…” Salimu alianza kujipiga sachi mifukoni akitafuta kitu mara akaonekana akitoa kitu. “Haa!” Salimu alionekana kuchoka kabisa. “Duhh!” Karimu alibaki ameduaa akimshangaa Salimu ambaye muda huo alikuwa ametulia akiwaza macho kodo akitazama mbele. “Hivi Karimu unaona kuna mambo yapo sawa katika kichwa chako?” Karimu alitulia akiyawaza maneno ya Salimu aliyokuwa akiyasema wakati huo. “Kuna…hebu nieleze unahisi vipi maana mi nashindwa kujielezea sema nimekubaliana na hali tu ilivyo” Karimu usinistaajabishe unajua hivi huoni kama kuna kitu kilitokea si tulikuwa hapa chuo na mara… mhh sielewi”. “Sawa sawa kaka, mi pia nilihisi hilo lakini bado sijaelewa tulifika fikaje pale inatubidi kesho tufanye kila namna Komandoo atuelezee tulifikaje au ndo mambo ya Intellegencia” Karimu aliongea na kumtazama machoni Salimu. “Ehh hii kazi kweli sio ya mchezo mchezo haya tuyaache tusubiri hayo ya kesho”. Salimu aliongea huku akitingisha kichwa akitazama sakafu kisha akaonge tena “…Kaka sasa naona kama nimeshakuwa tayari kufanya kazi hii muda umeshafika” aliongea Karimu “Kaka ni kweli inatubidi tushukuru, yani mtu alivyotuchambua wakati ule mi nikadhani sasa tumeshagundulika nilihisi mkojo kunitoka pale lakini bwana kumbe mtu alikuwa akitufatilia kwa mazuri usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.” Alimaliza Salimu huku akitabasamu Hiyo metheli sio mchezo” alidakia Karimu.

Kitonga, Ilala -Dar es Salam

Geti lilifunguka kwa kutumia umeme ili kuruhusu gari kuingia iliyowachukua kuingia hilo lilakoma katika eneo la maegesho ya magari ambapo kulikuwa tayari kuna gari takribani tano zote zikionekana kuwa si gari za mchezo mchezo ni za gharama ya mamilioni ya hela mazingira ya nje yalikuwa yamekaa kiulinzi ulinzi tu kamera zikionekana zimewekwa katika kona maalumu ili kuweza kudaka matukio yote kwa ufasaha.

“Shukeni vijana” Jeff aliamuru, Salimu na Karimu kwa pamoja wakatoka na kumfata Jeff aliyekuwa ametangulia mbele mita kazaa huku wakishangaa mazingira yaliyofanana na Hotel ya kitalii kwa muundo wake. “Ohh vijana wangu karibuni katika familia mpya na maisha mapya”. Komandoo Ochola aliiweka glass yake ya mvinyo mezani toka Nchi ya Italii inayojulikana kwa jina la Barolo wine na kunyanyuka kitini akiwa amevalia suruali nyeusi pamoja na shati jeupe mguuni akiwa na kiatu cheusi cha mchongoko ghali sana na kuanza kumkumbatia mmoja kabla ya mwengine. “Ohh asante sana tumekwisha karibia” Karimu aliongea hivyo huku akipepesa macho kuyashangaa mazingira ya kustaajabisha ya sebure hiyo ambayo ilikuwa imesheheni vitu vya thamani vilivyo pangwa na kupangika haswa. “Haya mnaweza mkakaa” Komandoo Ochola aliongea na kuikunja miguu yake kwa kuweka nne. “Nasikia furaha kuwa na nyinyi hapa na mjisikie teyari mmpo kazini hahahaha” alicheka kivivu kisha akaendelea. “Vijana nimewaita mje kwa sababu kuna mambo nataka kuwaeleza ili kuwajenga kisaikolojia kuhusu kazi hii kwa ufupi na namna mtakavyo anza mafunzo yenu kwa ufupi” Komandoo Ochola alichukua glass yake ya mvinyo na kupiga fundo moja akalimeza. “Vijana nataka kuwaeleza nyinyi ni watu spesho sana mnabahati sana na sisi pia tunabahati kuwapata na taifa pia lina bahati kuwa nanyi najisikia na nguvu kurudi kazini na kuungana na watu nyinyi pamoja na hao vijana wangu mnao waona” Salimu na Karimu waligeuza shingo zao kuwatazama watu watatu akiwemo Jeff wakiwa wamesimama kikakamavu wakiwatazama.


Itaendelea...
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)


Mtunzi AKIDA SIRI RAMBAO
Contact 0658328596

MSIMU WA PILI

SEHEMU YA 7 E: MUUNGANO


Tuendeleeee...


Jeff wakiwa wamesimama kikakamavu wakiwatazama. Komandoo Ochola akaendelea “…kila mtu hapo licha ya kuwa ni mtu anaye husika na upelelezi lakini anajukumu lake la kikazi na yupo vizuri katika mambo mengine hasa mapigano”.

Salimu na Karimu yalionekana kuwavutia sana mazungumzo hayo walionekana kutabasamu. Komandoo akasimama “…ninapo kuwa nazungumza mambo yanayohusu sana kazi napenda kusimama…tumaini langu kwenu ni kuwafanya wapelelezi waki komandoo na sio maaskali kama wengi walivyo nataka kuwafanya muwe miamba migumu isiyovujika na muingie popote na mfanye lolote lile kwa wakati muafaka hilo ndilo dhumuni la mimi na timu yangu kuwatafuta nyinyi na muda huu kuwa hapa pamoja” Komandoo akaangua kicheko chake cha kivivu na akaendelea “Ni lazima mzijue lugha za mawasiliano zisizo pungua kumi na mbili zinazo zungumzwa duniani tena kwa ufasaha, lazima mjue mambo ya huduma za kijamii ikiwemo namna ya kutoa matibabu na mengineyo lazima muyajue mapambano ya siraha na yakutumia viungo pekee ya kimwili mapigano kama Combat,konfuu,judo, karate ni yalazima muyajue” Salimu na Karimu kwa makini sana walionekana kuzituliza akili zao juu ya hayo wanayo yasikia”.

Komandoo Ochola akaendelea “Lazima mjue kusoma saikolojia ya mtu kumshawishi kumrubuni alimradi uweze kukipata unachokitaka…hayo ni baadhi tu” Komandoo alisogea na kuchukua tena glass yake ya mvinyo aliyokuwa akinywa taratibu na kumfanya kufinya macho kila anapo iweka kinywani mkono mmoja ukiwa mfukoni akaendelea. “Hii kazi inahitaji sana akili ya kufikiria haraka na kuamua haraka lakini maamuzi yote yakiwa chini ya ushirikiano na timu uliyokuwa nayo chini ya kitu kinachoitwa siri….” Komandoo alinyamaza kidogo kisha akapiga hatua fupi fupi huku akiivua miwani yake na kuacha jicho lake moja dogo kuonekana vizuri kisha akaongea tena”…siri ndiyo maisha ya kazi zetu hata kama ni baba, mama, mke, mchumba hapaswi kuyajua au kujua hatua zako zozote zile juu ya kazi yako hii” Komandoo aliongea maneno hayo kwa utulivu sana na kuonesha sura yenye kumaanisha sana kauli yake hiyo kiasi chakuwafanya kina Salimu kupatwa na uoga huyo akaanza kusogea katika sofa waliyokuwa wamekaa kina Salimu wakimsikiliza. “Target ya kazi yetu ni miaka kazaa ijayo hii ni baada ya nyinyi kumaliza sehemu kubwa ya masomo yenu yaliyoandaliwa kisiri siku nyingi huko ughaibuni na sio hapa ambapo ni rahisi kugundulika”.

Habari hiyo ilikuwa ni ya kushtusha sana maana si Karimu wala Salimu aliyejizuia kushangaa. “…yeaah na hiyo ni kwa sababu hii ni kazi maalumu iliyopendekezwa na Waziri wa mambo ya ndani na nje wa zamani ambaye sasa ni Muheshimiwa Elibariki Fanueli Mkwasi ambaye ndiye aliyeokoa maisha yangu kule Israel na ndiye aliyenishawishi kurudi kazini toka mafichoni nilipo kuwa ili niwatafute vijana shupavu nitakao wakabizi mikoba kwa ajiri ya kupitisha fagio la kusafisha maovu yote yanayo endelea nchini na hata kuzifufua kesi mbalimbali za watu wasio kuwa na hatia, mali zilizopokonywa kwa watu na wahusika wote kuchukuliwa hatua mara moja lengo msiwe wa kawaida mtasomea General military intelligencia (GMI) kisha mengineyo”.

Maneno matamu tena yenye uzito wa hali ya juu uliwapa kina Salimu sura mpya ya maisha na kuyaona mambo yakienda kirahisi na kuamini bahati imewaangukia wao kweli kweli. “Sasa kila kitu kitaenda sawa, mtaenda nje ya nchi kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu kupitia Schooler ship ambayo nitaisimamia mwenyewe wakati huo ili kila mmoja awe na skill yake hii ni baada ya kumaliza masomo ya JKT kisha mtaenda nje mkirudi tutafata sheria ya nchi mtaaingia katika jeshi la wananchi ili mtambulike kama wanajeshi kisha mkiingia na kufikia level fulani ndipo mtaenda India kwa ajili ya mafunzo maalumu ya upelelezi wa kijeshi hivyo mpango utakao fanyika kipindi hicho mtaujua wakati ukifika” Komandoo akamaliza na kuwatazama kwa tabasamu kipindi hicho Salimu na Karimu walikuwa mawazoni wakitafakari habari hiyo nzito. “Je kuna swali lolote vijana?”

Komandoo Ochola aliongea na kurudi pahala alipo kuwa amekaa wakati ule vijana walipo ingia sebureni hapo. Salimu alikokhoa kidogo kisha akaanza kuongea “Samahani Mkuu hivi ilikuwaje jana tukawa katika lile jumba wakati kumbukumbu zetu za mwisho tulikuwa Bwenini?” “Hahahaha…” Komandoo alicheka kivivu kama kawaida yake kisha akaanza kuongea “…kuna mchanganyiko flani wa gesi kwa sasa kuujua ni mapema sana lakini inauwezo wa kupotezesha fahamu na kufuta all short memory za dakika thelathini zilizopita tu bira madhara ya kiafya na kumuacha mtu asiweze kukumbuka matukio yaliyotokea wakati huo lakini kama ni mwerevu kama nyinyi lazima atahisi kitu tofauti, safi sana nilitegemea swali kama hilo toka kwenu” Salimu na Karimu akatazamana na kustaajabu sana. “Basi hebu nyanyukeni na niwatembeze katika mazingira ya nyumba hii na mtazame baadhi ya vitu ambavyo vitawaongezea hamasa ya kazi”. Vijana hao wakanyanyuka nakuungana na Mkuu wao huyo na kuzunguka mazingira hayo ya nyumba huku kina Jeff wakiwatambulisha baadhi ya majukumu yao yaliyo waacha mdomo wazi wabaki kushangaa “Duuh nikazani I mambo ya movie kumbe vitu vipo kweli!” aliongea Karimu baada ya kushika moja ya miwani yenye uwezo wa kurecord video na kupiga picha. Baada ya kumaliza matembezi waliingia ndani ya gari na kuongea mawili matatu kisha Komandoo Ochola akaongea “Kama nilivyo waeleza nitakuwa nawapigia mara chache na kuwapa taarifa Fulani na Mzee Habib msimueleze jambo lolote lile nitakuja kuongea nae mwenyewe wakati ukifika tunafahamiana” Komandoo Ochola aliongea kwa msisitizo na kutoka garini kisha akaufunga mlango na kuwapunguia mkono wa kwaheli.



MWISHO WA MSIMU WA PILI

ENDELEA KUFUATILIA MSIMU WA TATU
IMG-20211211-WA0046.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)


MSIMU WA TATU

SEHEMU 8A: MAAMUZI MAGUMU

“Salimu amethibitisha kuwa Meroda na timu yake ni majambazi na moyoni mwake anamini Meroda ni mwanamke anayempenda zaidi kuwahi kutokea kuliko Shalon.

Anafikiria kumueleza Meroda kuhusu historia ya maisha yake mpaka hapo alipofikia kuhusu utafutaji wa haki na kulipa kisasi huku akijua wazi kuna kukubaliwa na kuungana pamoja akipata msaada wake kuwaporomosha maadui zake lakini pia kuna kukataliwa na kushambuliwa vikali bira huruma na ndoto zake kuzima kama mshumaa katika upepo mkali, ni kipi atakachokiamua?”


Furture Company, Upanga mashariki- Dar es Salam

Komandoo Ochola alikuwa mtu wa kwanza kushuka katika gari nzuri yenye muundo wa benzi akiwa kavalia suti nyeusi bila kusahu miwani yake aipendayo machoni mwake.

Milango mengine ilifunguka na Salimu alichomoza akifatiwa na Karimu wakiwa na sare ya suti nyeusi iliyofanana na ya Komandoo Ochola. Utuuzima ulikuwa umewaingia kutokana na mabadiliko mengi ya mwili yaliyoshamiri na stairi ya mavazi yao. Walionekana kuwa ni vijana wenye mvuto haswa kwa namna walivyokuwa watu kazaa kwa mbali walionekana kuvutiwa nao kiasi cha kuwafanya kuduwaa kwa sekunde kazaa kisha kuendelea na mishughulisho.

Taratibu wakiwa nyuma wakiongozwa na Komandoo Ochola walielekea upande wa ghroofa ndefu iliyonakshiwa na vioo vya rangi ya samawati wakiacha eneo la maegesho ya magari upande mwengine. Karibu kabisa na lango kubwa la kuingilia ambapo watu kazaa walikuwa wakiingia na kutoka palikuwa na bango kubwa Future Furniture Family” Karimu alitamka huku kichwa akiwa kakielekezea juu kisha katabasamu. “Ohhh Mkuuu karibu sana” bwana mmoja aliyeonekana kuwa ni kiongozi kutokana na namna alivyojiweka alimsalimu Komandoo Ochola kwa kumpa mkono huku akiwapa na kina Salimu kwa zamu “Habari zenu…” “Salama” kwa pamoja wakaitika huku wakigeuza shingo huku na huko kutazama mandhari ya jengo na mikusanyiko ya vitu vya thamani pamoja na watu waliokuwa wamesambaa wakitazama mahitaji yao. “Bwana Devi hawa ndio wale maboss wa hii kampuni” aliongea Komandoo Ochola “Ohh karibuni sana viongozi” bwana David aliongea huku akiwa ni mwenye wasiwasi kidogo maaana alionekana kuanza kutetemeka na ugeni huo mzito usio kuwa na taarifa “Thanks” Karimu aliamua kujibu baada ya kumuona Salimu akiwa bize kukagua moja ya sofa ya ngozi mkono mmoja ukiwa mfukoni akitembea kwa maringo na majivuno makubwa. “Utawaambia vijana wako kuwa patakuwa na utambulisho wa maboss siku ya kesho asubuhi hivyo wa wahi na taratibu zingine nitakujulisha kwa simu “Sawa Mkuu” yule bwana aliitikaz kwaz unyenyekevu huku macho yakiwa chini “Unaweza kwenda kuendelea na majukumu” Komandoo Ochola alimruhusu bwana yule na kuanza kuongoza njia kukagua mali zingine nyingi za thamani ndani hapo “Komandoo vipi hili jengo linaonekana ni la thamani sana na ilikuwaje yani sielewi elewi unajua”. Karimu aliongea kwa sauti ya kunong’ona karibu kabisa na sikio la Komandoo “Ndio maana niliamua kurudi kazini...

Itaendeleaa

Kazi iendelee..
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

MSIMU WA TATU

Sehemu 8B: Maamuzi Magumu

Ilipoishia...
Karimu aliongea kwa sauti ya kunong’ona karibu kabisa na sikio la Komandoo “Ndio maana niliamua kurudi kazini kwa sababu ya muheshimiwa Rais...

Tuendeleee...

...ni mtu muelewa sana na sasa lazima tufanye kazi kama CIA…hahahaaa kuna wakati unatakiwa uwe muigizaji bora” alicheka kivivu kama kawaida yake huku akiongoza njia kuelekea upande uliokusanya seti nyingi za sofa. “Mipango yote hii niliifanya kwa siri kushirikiana na muheshimiwa Raisi kipindi chote mlipo kuwa masomoni” Salimu akiwa kuliani mwa bega la Komando akisikiliza huku akihisi utamu wa kazi maana alikuwa anatabasamu tu.

Wakaendelea kuzunguka maana jengo lilikuwa kubwa tena lililokusanya vifaa vingi vya kisasa na wateja nao walikuwa ni wengi sana. “Vijana watu makini hufanya kazi makini pia” Komandoo Ochola aliongea baada ya kutoka nje kabisa ya jengo hilo akiwa ame ambatana na kina Salimu. Hao hadi katika gari ambayo walikuja nayo gari ya gharama sana iliyowatoa watu macho maana wengi hawakuacha kuikodolea kila wakati “Tafadhari ingieni” Komandoo alitoa amri na wao wakatii. Ndani ya gari hiyo bwana Ochola akaivuta bahasha moja akaikagua akampatia Salimu na nyingine akampatia Karimu “Haya zitazameni mzikague kama kuna sehemu haipo sawa mniambie” Salimu na Karimu kila mmoja akaanza kufungua kutazama.

*****

Yaliyomo ndani haikuwa shangazo la kawaida walikutana mambo ya kustaajabisha sana kiasi cha kutazamana wenyewe kwa wenyewe, kwanza walikutana na nyaraka zinazo thibitisha kuwa wao ni watoto yatima waliokuzwa katika kituo maarufu huko mbeya. Walikutana na nyaraka Fulani iliyo onesha kudhaminiwa na serikali katika mambo yote ya masomo yao toka katika ngazi za awali hadi ngazi za juu mpaka kumaliza kwao nako kwa shule nyingine kabisa na sio zile walizo soma wao sio hicho tu hata picha za passport size zilizoscaniwa humo kwenye vyeti havikuwana sura halisi walizokuwa nazo lakini zikishabihiana na za kwao.

Kituo hicho kilianzishwa na kuwa mradi maalumu ulio funguliwa na waziri mkuuu miaka ile hivyo walichomekea humo humo na ikawa inaeleweka kwa yoyote yule atakae fikishiwa kama taarifa kwa ajili ya kuhakiki. Jambo la pili lililo waacha midomo wazi ni kuhusu vyeti vyao kuwa vya mambo ya biashara mbavyo havikuwa rahisi kuona kuwa si vya kweli kutokana na saini na ubora wake. Yani walitokea kuogopa maana kila kitu kilionekana kuwa kama sawa majina yao pia yalikuwa tofauti katika ubaba ambapo lakini saini zao zilibaki kuwa za kwao. Kwa kifupi walikuwa wameshangwazwa siku hiyo wingi wa kushangazwa mno. Komandoo Ochola akiwa mbele na dereva wake wa siku nyingi akageuka na kuwaona vijana wake wakiwa wamepatwa na mshangao na uwoga mwingi. Walijiwazia vichwani sasa kama inawezekana kufanywa mambo yote hivyo tena yakaonekana kuwa ni sahihi inashindikana vipi wao kuuziwa mbuzi kwenye kiroba balaa siku moja wakabaki kukumbuka baadhi ya maneno ya baba yao kila mmoja kwa nafasi yake.

*****

“Vijana wangu najua mmpepatwa na mshtuko sana msijali kazi sasa ndo inaanza na akaunti zenu zimeshaanza kuingiziwa mishahala tangu mwezi ulio pita” aliongea Ochola Salimu moyo ukaanza kumdunda duku duku “Msiwe na wasiwasi.

Wala hela haziingii moja kwa moja toka katika mfumo wa serikali kuna njia maalumu ambayo ni salama msiogope…tupo pamoja, vijana twendeni sasa ila hamja nipa habari ya wazazi wanaendeleaje” aliongea Ochola akiwa amegeuka akiwatazama “Wame furahi kwa kweli japo hawajatosheka kwa mwezi mmoja pekee tulio kaa nao tangu tuingie nchini” Karimu alidakia huku akiuma midomo yake. “Ni sawa ndo inavyokuwa kazi huwafanya watu kukaa mbali na watu wanaowapenda na hata kuwapoteza dereva hebu washa gari tuondoke” Ochola aliongea na kuonekana kuingiwa na huzuni. Kumbukumbu zilimpeleka zaidi ya miaka ishirini alijiona kipindi akiwa kijana mwenye nguvu zake zaidi akifurahi na familia yake ya watu wa nne pekee, mawazoni alimuona mara kazaa mkewe akilia pindi akiondoka kwenda katika majukumu yake. Alijiona alikuwa mtumwa wa kazi kweli kweli alihaha zaidi ya miezi akiwa mbali na familia yake pasina kuonana. Lakini alichokuja kulipwa ni maumivu yenye kovu la maisha.

Itaendeleaa...

Mambo yameanza rasmi
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

MSIMU WA TATU

Sehemu 8C : Maamuzi Magumu

Kawe, Kinondoni-Dar es Salam
“Vijana haya ndio yatakuwa makazi yenu mapya tangu leo huku mkiwa na utambulisho wa wafanya biashara” Salimu na Karimu wakiwa tayari nje wakitazama kwa kina mandhari wakatingisha vichwa vyao kukubaliana na Komandoo “…twendeni” Komandoo akiongoza njia geti likafunguliwa na wakaingia ndani. Ilikuwa nyumba yenye mahitaji yote muhimu na mazingira ya kuvutia kwa mtu yeyote ilikuwa yakifahari sana na yenye hadhi yao hasa.

Baada ya tambulisho ya mazingira sasa wakaa kaa sebureni na kupangilia mambo ya kazi kwa utaratibu kisha wakatoka maeneo hayo wakiwa na ratiba ya kwenda kuchukua vitu vyao ambayo walivihefadhi katika hotel ambayo walifikia.

Usiku wa manane
Salimu aliendelea kupinduka pinduka akienda hivi na vile na mwisho akaitoa shuka mwilini na kukaa kitako ‘siwezi kukaa muda mrefu bila kutafuta namna ya kuongea na hawa wanawake wote, ni nani wa kuelezwa ukweli na ni nani wa kudanganywa nani wa kupendwa na ni nani wa kuachwa’ alijiongelea nafsini kijana Salimu na mara kaaanza kupapasa kitandani na akatoa simu na kaunza kuandika ujumbe wa maneno “Habari za siku nyingi nimerudi toka masomoni nipo nchini tayari nitakutafuta siku hizi chache kuwa tayari kukutana nami” kishapo akautuma ujumbe huo kwa Meroda kisha akafanya tena kwa Shalon.
Salimu kwa nafasi yake aliendelea kutafakari ‘Lazima nichambue mbivu na mbichi kuhusu haya maisha yangu ya usoni’ alijisemea nafsini, wakati huo Karimu akiwa hajijui hajijtambui kwa usingizi.

Salimu akiwa akajiegemeza katika egesho la kitanda macho yakitazama ukutani akifanya tafakuri mada zikipishana hii haija isha inaingia nyingine na nyingine tena akishauriana na nafsi yake.

Wasichana wawili na namna ya kuwamiliki bado lilikuwa likiiingia na kutoka kana kwamba bado moyo wake haukuwa na msimamo, kichovu chovu akaaanza kutafuta katika simu yake aliyokuwa kaishikilia muda mwingi macho yakakaza katika picha za msichana Meroda, picha hizo zilionesha taswira mbalimbali. ‘Kihisia we ndiye msichna pekee uliye shinda moyo wangu’ alijisemea nafsini “Nitaanzaa na wewe Meroda sina chaguo nitakueleza kinagaubaga na utachagua cha kufanya kama kupambana na mimi au kuungana na mimi” Alijiongelea mwenyewe kisha akaanza kuandika ujumbe wa maneno.
“Habari Meroda naomba tuonane kesho jioni pindi ukiupata ujumbe huu tafadhari nijurishe, nivema ukichagua sehemu ya makutano” baada ya kuupitia mara kazaa huku akibadilisha maneno na kuandika mapya hayo ndiyo aliyaona yanafaa akautuma ujumbe huo kwa Meroda taratibu akajivuta kujinyoosha na akafumba macho kutafuta usingizi.

Dreaming Pol Hotel, Ubungo- Dar es Salam
Waliendelea kucheka kwa nguvu huku meza ikiwa imechafuliwa kwa vyakula vya kutosha na vinywaji mbalimbali, “Meroda naomba tuzungumze mara moja” Salimu aliongea kwa sauti ya kunong’ona akiwa karibu na sikio la Meroda kisha akanyanyuka kitini mwake na kumtazama Meroda kwa macho ya ‘Nakuomba tafadhari’, “Dadaz nakuja endeleeni kufurahi tafadhari, msimtenge shemeji yangu” Meroda alisogeza kiti na kutoka katika mjumuiko huko akijichekesha kwa aibu na kuwapa mgongo akiacha timu yake ikiwa pamoja na Karimu wakiendelea kula na kunywa. “Ni sawa makinika” Monica pekee alijibu. Salimu akiwa mbele kama hatua tatu mikono mfukoni akionekana kuwaza ni mtu asiye jiamini akiuma midomo na kuiachia huku macho akiyafumba kwa nguvu na kuyaachia pia. Baada ya kupiga hatua tena na tena macho yakiwa chini Meroda akiwa nyuma yake mwisho aligeuka na kumtazama Meroda kwa tabasamu jembamba kisha akajikalisha katika moja ya bembea iliyo karibu na walipokuwa pia mbali kidogo na eneo la makutano walipotokea “Meroda njoo…njoo ukae karibu nami tafadhari”. Meroda akiwa na aibu ya kimaumbile ambayo haikufichika mbele ya Salimu alijisogeza kama binti kigoli ambaye hajawahi kukaa kumuona mwanaume katika maisha yake.

Salimu alishuhudia hilo akatabasamu ‘anavyoonekana kama mwanamke dhaifu asiyejua kutoa roho za watu ama kweli penzi kitovu cha uzembe’ alijiwazia kisha akakokhoa kidogo “Meroda huwenda ukawa unanijua au ulishawahi isikia stori yangu, lakini wacha nikupe ukweli wa maisha yangu pasina kuficha hata punje ya habari kisha utaaamua kuniua au kunisaidia.” Baada ya kusikia maneno hayo aibu ilimtoka Meroda akamtazama Salimu. “Umesemaje” Meroda aliongea kwa mshtuko mkubwa

Itaendelea...

Dooo salaleee mambo ni itakuwaje Meroda atafanya nini siri imewekwa kweupeee

Atachagua kazi au atachagua Penzi ili aweze timiza ndoto za Salimu??


Tukutane kipindi kijachoo
IMG-20220103-WA0024.jpg
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

MSIMU WA TATU

SEHEMU YA 8 D: MAAMUZI MAGUMU

Tuendeleeee...

....Baada ya kusikia maneno hayo aibu ilimtoka Meroda akamtazama Salimu. “Umesemaje” Meroda aliongea kwa mshtuko mkubwa na kujikuta amesimama “Hapana Meroda, tulia kwanza unisikize usipaniki hujasikia habari yenyewe” Salimu aliongea huku akisimama kumshika mikono akiwa na macho ya huruma, Meroda akajikalisha na mzungumzo yakaanza. Mazungumzo yalichukua takribani lisaa zimaa Fanani alionekana fika kuchomwa na anayoyazungumza huku akimuacha hadhira wake akiwa hoi kwa maumivu na machungu. “Pius na sasa Salimu na sasa ni askari maalumu wa upelelezi wa kijeshi ndani ya kisasi na utafutaji wa haki” Meroda aliongea maneno hayo bila mkato, kisha akakaa kimya machozi yakimteremka mashavuni Salimu alibaki kumtazama kwa wasiwasi asielewe maana ya sentensi hiyo.
Meroda akaamua kunyanyuka huku tayali macho yakiwa yamejawa machozi ya kutosha maana muda wote wanaongea Meroda alishindwa kuvumilia kumtazama Salimu na kuishia kujiinamia. “Salimu twende tukajumuike na wenzetu alafu tuagane muda umekwenda” Meroda kwa msisitizo na sauti iliyolazimishwa kutoka akasimama tayali kuondoka. Salimu alijinyanyua huku akiwa na maswali mengi yaliyo changanyika na uwoga akawa nyuma ya Meroda bila kuongea kitu.
Walipofika sehemu walipo waacha wenzao waliwakuta wapo wakiendelea kukata maji kasoro Karimu ambaye yeye alikuwa hatumii vilevi alibaki na Juisi za kopo na kula nyama choma akisherehesha mazungumzo. Kuingia kwa Meroda na Salimu kuliwafanya wote watulie tuli wakiwatazama

. Hali ya Meroda haikujificha alionekana fika kama hajatoka kulia basi anataka kuanza kulia. Salimu yeye alilowa tu kwa jasho na macho yakiwa chini kama mtu aliye fumaniwa akavuta kiti na kukaa wasiwasi usiofichika usoni ukimtawala. “Ladies time to leave please” Meroda aliongea kwa sauti ya huzuni iliyo na unyonge nyonge kiasi cha kuwafanya wasichana wenzake washangae na kumtupia macho Salimu ya kuuliza kunaniii, lakini kwa kuwa amri imesemwa hakuna aliye thubutu kusema neno wakanyanyuka na kuondoka wakiacha vyakula mezani. Salimu na Karimu wakabaki wakiwatazama tu. “Kaka vipi kulikoni Mzee! mbona sijaelewa?” Karimu macho yakiwa yamemtoka mikono kiunoni, Salimu akazitoa pumzi nzito na kujibwaga katika moja ya kiti katika pahala alipo huku macho yakiwa yame kaza katika sahani moja wapo ya vyakula. “Yaaaani matumaini toka kwa Meroda hayapo kwa sasa tusubiri na tuwe tayari kwa lolote lile” “Unajua sijakuelewa…” Karimu alieleza huku akijikalisha kitini macho kwa Salimu. “Ni kuwa Meroda hatujui kama atakuwa upande wetu au atakuwa upande wa majambazi, na kama atakuwa upande wa hao majambazi tusitegemee kufaulu aidha….dah!” kwa hali ya kujilaumu akajishika kichwa kwa mikono yote miwili akiwa kaupinda mgongo kwa mbele kama upinde. “…Duhh hii kazi sikujua kama itakuwa ngumu kiasi hichi” Salimu alidokeza tena. Kikapita kimya cha muda bira mtu kuongea jambo lolote “Aisee twende zetu tukapumzike kwanza tusubiri jibu lake tusife moyo” Salimu alijinyanyua akaelekea kaunta na kulipa kiasi cha gharama ya mahitaji yao ya siku hiyo kisha hao wakaenda zao.

Sam Nujoma Road, Ubungo- Dar es Salam.
Meroda akiwa ndani ya gari hakuongea kitu alikuwa akilia kama mtoto mdogo, si Monica wala Samira aliye jua kinachomliza Meroda zaidi ya kuamini kuwa huwenda penzi limeingia doa hicho ndicho kilicho kuwa vichwani mwao. Meroda kulia kwakwe kulimpeleka mbali sana kimawazo alikumbuka miaka mingi nyuma maisha aliyokuwa nayo. Meroda aliwahikupitia maisha magumu sana maisha ambayo hakuwahi kuyatamani kuyaishi kwa gharama yoyote ile katika pumzi iliyosalia katika maisha yake.

Itaendelea...
 
The Hidden Truth (Ukweli uliofichika)

Nani Anahusika??

MSIMU WA TATU

SEHEMU YA 8 E: MAAMUZI MAGUMU

Tuendeleeee...

Sam Nujoma Road, Ubungo- Dar es Salam.
Meroda akiwa ndani ya gari hakuongea kitu alikuwa akilia kama mtoto mdogo, si Monica wala Samira aliye jua kinachomliza Meroda zaidi ya kuamini kuwa huwenda penzi limeingia doa hicho ndicho kilicho kuwa vichwani mwao.

Meroda kulia kwakwe kulimpeleka mbali sana kimawazo alikumbuka miaka mingi nyuma maisha aliyokuwa nayo. Meroda aliwahikupitia maisha magumu sana maisha ambayo hakuwahi kuyatamani kuyaishi kwa gharama yoyote ile katika pumzi iliyosalia katika maisha yake.
Toka anazaliwa hakuwahi kumuona baba na akajivunia naye alibaki kutulia maana kila alipojaribu kumuuliza mama yake alikuwa kama anatonesha kidonda tu cha maumivu mpaka pale alipodokezewa na marehemu bibi yake kuwa alitiwa mimba na kutelekezwa kipindi walipo shindwa kumuendeleza kimasomo na mtu ambaye hawakuwahi jua utambulisho wake wengine walisema mfanya baishara na wengine mkimbizi hakuna jibu sahihi. Kwa umri ule wa miaka nane tu mara kazaa alikutana na ma baba waliojinadi kuwa ni mtoto wao lakini yeye hakujali zaidi ya maisha yake, mwisho wakahama eneo walilokuwa wanaishi na kwenda kwenye kibanda chao huko shamba baada ya babu yake kuuza eneo la shamba la migomba alilokuwa anamiliki. Alipo maliza kidato cha nne na akiwa hana uhakika wa kuendelea kimasomo kutokana na hali ngumu ya maisha na mama yake aliyekuwa akifanya biashara ya Samaki wabichi ambayo kwa mazingira yake bado haikumfanya kujitosha yeye mwanawe na wazazi wake waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara. Meroda alipata habari za kazi za ndani huko Mkoani Morogoro akiwa na miaka kumi na sita. Hivyo aliweza kuelekea Mkoani Morogoro ambapo alifika kwa mara ya kwanza hii ni baada ya kupatana na mwenyeji wake ambaye hakumjua sura bali alikuwa na namba katika kipande cha karatasi ambapo aliishia kupiga kila wakati kwa kuomba simu za watu.Wakati anashuka garini katika stand kuu ya mabasi mjini Morogoro mpaka saa nne usiku hakuna mtu yeyote aliyejitambulisha kuwa ni mwenyeji wake mbele yake licha ya kuwa alijitahidi kuomba simu za watu na kupiga mara ikiita tu na wakati mwengine kutopatikana kabisa.

Vijana waliokosa maadili hawakuacha kumsogolea wakimtania na kumchombeza kumtaka kimapenzi maana tofauti ya umri lakini umbile lake lilitosha kumuonesha kuwa yeye ni mwanamke tayali tena mwenye uzuri zaidi ya ule unaojidhihirisha endapo tu atapata matunzo. Baada ya masaa Meroda alitafuta namba zile walau aweze kujaribu tena bahati yake usiku huo lakini hakufanikiwa kuziona ikawa ndio tatizo lingine kubwaa. Kilikuwa ni kipindi kigumu asichoweza kukisahau kwa sababu alikutana na changamoto sana siku hiyo kwa kulala katika duka moja wapo katika upande wa pili wa kituo hicho cha mabasi maeneo karibu kabisa na stand ya Dodoma tena akiwa na njaa. Meroda siku moja akiwa na maisha ya kubangaiza ya hapa na pale kutafuta riziki katika vibanda vya Mama Ntilie akiosha vyombo na kuhudumia huku akipata mshahara wa chai cha kula cha mchana na mwisho kuambulia elfu moja ambayo ni sawa na sahani ya ugali. Kila usiku kujibanza katika maduka alinusurika kubakwa na wahuni kwa kuzani yeye ni mmoja ya wasichana wanao jiuza pale Itigi .Siku ambayo Meroda huikumbuka kila anapo patwa na huzuni ni siku alipokuwa kajibanza katika banda moja la chakula maeneo ya ITIGI msamvu karibu kabisa na barabara mpya ya Morogoro Dar ndipo alipofatwa na jamaa mmoja akamng’ang’ania kuondoka nae kwa kuzani kuwa ni mmoja ya wasichana wengi wanao jiuza usiku huo. Ndipo kijana mmoja alipo ona tukio hilo la unyanyasaji likiambatana na kelele zakutaka msaada akazisikia akaamua kwenda kumtetea Meroda ambaye teyali alisha chaniwa gauni lake zuri la spesheli.

Hivyo kuwepo kwake kuka mtenganisha na jamaa yule aliye kimbia kwa kujihami kizani akiikimbiza roho yake isipate maafa. Yule kijana baada ya kumnyanyua Meroda alitumia busara zake kumshawishi kuondoka naye kwa ajili ya usalama, alimkokota kwa kumbembeleza akitaka kwenda naye anapoishi kitu ambacho kutokana na hatari aliyoishuhudia wakati mfupi uliopita Meroda aliamua kukubari. Meroda alijisemea lolote na liwe na aliongozana naye mpaka pahala anapo ishi yule kijana ambapo ilikuwa ni chumba kimoja kilichowekwa bati kati ya vinne vilivyoishia katika eneo la madirisha (nyumba isiyoisha). Meroda aliingia na kukaribishwa apumzike. Siku iliyofuta ndipo alipogundua uzuri wa kijana yule aliyemtetea usiku uliyopita na kumfanya ajihisi msisimko mkubwa alitamani kubaki na akaomba kubaki maana hakuwa na pakwenda.

Itaendelea...
 
The Hidden Truth ( Ukweli uliofichika)

MSIMU WA TATU

SEHEMU YA 8 F: MAAMUZI MAGUMU

Tuendeleeee..

...a kukaribishwa apumzike. Siku iliyofuta ndipo alipogundua uzuri wa kijana yule aliyemtetea usiku uliyopita na kumfanya ajihisi msisimko mkubwa alitamani kubaki na akaomba kubaki maana hakuwa na pakwenda.

Baada ya kuhojiwa maswali machache na kuongea mawili matatu ndipo alipogundua kuwa kijana yule ni mkubwa kwake kwa miaka minne na haya yote yalijili baada kuletewa chai na vipande vya mihogo ya kukaanga iliyo patikana mtaa huo huo wa msamvu.

Kijana huyo aliamua kumkaribisha kukaa na yeye mpaka atakapo mpata mwenyeji wake na kuondoka. Hivyo Meroda akawa anatoka kwenda kule anapo fanya kazi ya kibarua kipindi hicho hicho kijana yule na yeye akitoka kuendelea na bishara yake ya chipsi inayo anza mchana mpaka usiku mzito. Maisha ya namna hiyo kama kaka na dada iliwafanya wawe karibu zaidi japo wengi walizua maswali juu yao na kutabiri mwisho wa hayo na ndipo Meroda alijikuta akimuita mume kabisa huku akitamani siku moja ampeleke kwao akachumbiwe hivyo. Hapo sasa ndipo maisha yalipoanza kunoga kwa sababu ya akili ya maisha aliyokuwa nayo ile nyumba ya urithi isiyo isha wakajikuta wakiimalizia na kupangisha ubavu na ubavu wakiishi wenyewe japo haikumaliziwa vile ipasavyo sakafu chini, bati na milango ilitosha kuitwa nyumba ya kupangisha. Wakajikuta wakifanya pamoja biashara ya chipsi kuku, yai na mishikaki ya ngo’mbe iliyowaonesha matumaini ya mafanikio.

Mwisho wa siku kweli ndoto za Meroda zikatimia akampeleka Sospeter kwao huko Bukoba na akafunga ndoa wakawa mume na mke akiwa na miaka kumi na nane tu, waliokuwa na hisia za mambo kuwa hivyo wakawa wameshinda walioamini watabaki wakichezeana na kuzalishana tu wakawa wameshindwa. Siku moja akiwa hana hili wala lile kajipiumzikia nyumbani kwake, hamadi jirani zake usiku usiku walikuja kwa mafungu maana alikuwa ni mtu wa watu kweli kweli majirani hao walikuja kumpasha habari kuwa mumewe kabebwa katika karandinga kwa kusemekana kuwa ni mfanya biashara za madawa ya kulevya. Meroda roho ilimpasuka akatoka mbio mbio lakini watu walimzuia wakimsubirisha pakuche wakafanikiwa kumtuliza. Kesi ya mumewe haikuwa na ukweli wowote maana Meroda ndiye hasa aliyekuwa anamjua mumewe zaidi ya mtu mwengine alisingiziwa masikini wa mwenyezi mungu marafiki zake walimtumia pasina kujijua kama yeye anatumika. Sospater alipata pesa nyingi sana kwa siku kwa kuuza chips na kuku lakini aliachiwa pesa nyingi na jamaa waliokuwa wanafika hapo na kufanya bishara zao masikini yeye hakujua aliona ni ujamaa na uaminifu aliokuwa nao kwao. Ukweli ulikuwa hivi siku hiyo ya uvamizi ambao ulikuwa umeshapangwa wahusika baada ya kuona mambo yamekuwa mazito wakaamua kuweka zana zao hizo katika vazi la kipishi la bwana Sospeter hivyo polisi na firimbi zao walipo vamia tu wakatawanyika yeye akiwa hana hili wala lile akadakwa na kusachiwa akakutwa na madawa hayo ndipo ikawa mwisho wake.
Kesi ya mume wa Meroda ilikosa utetezi wa kutosha licha ya kuwa Meroda akiwa na ujauzito wake alijitahidi kuwaeleza ukweli mapolisi na hata kuwashauri namna ya kuwashika wahusika lakini alipuuzwa tu hakupata msaada zaidi ya kutukanwa na kusukumwa.

Masikini mumewe akapelekwa lupango akisubiri kesi yake kusomwa, akiwa ndani na uchungu mzito na kipigo cha kumshawishi awataje mabosi zake hali ilikuwa nzito na akajikuta anafariki dunia. Habari hizi zilishuhudiwa na Meroda alipoona mwili wa mumewe akitolewa lupango kiasi kilichomfanya aanguke na kupoteza fahamu na kujikuta Hospitali drip mkononi. Aliporejewa na fahamu zake mambo yalishabadirika alikutana na misiba miwili wa mumewe na kiumbe cha tumboni. Meroda sasa akajiona ni mtupu asiye na kitu katika maisha, alizigeuza lawama kwa mola wake na kumuuliza kwa nini awe yeye kwanini, chuki zaidi ziliwageukia mapolisi ambao walionekana kuja hapo kutoa pole ambazo Meroda aliona ni za kinafki basi tangu siku hiyo alitokea kuwachukia polisi kwa kushindwa kufanyaa kazi yao vizuri na kukamata watu wasio na hatia. Baada ya hapo Meroda akabadiri namna ya kuishi akajikuta akijiingiza katika vikundi vibaya vya kiharifu huku akiwa wa kwanza kuwavamia polisi na kuwauwa bira huruma mwisho akajikuta yupo chini ya mikono ya Samuel na Pater.

Sun set Hotel, Oyster bay-Dar es Salam
Mtikisiko wa gari ukamtoa katika dimbwi la mawazo kiunyonge Meroda akatoka garini na kuongozana na wenzake dhahiri akiwa amepwekeka sana, kwa mwendo wa kujilazimisha akaingia moja ya chumba cha duble walichopangisha Hotelini. Samira na Monica walikaa kitako wakimtazama maana tangu wameingia garini mpaka wanashuka dada yao mkubwa hajatia neno lolote na wao hawakutia neno wakabaki kusubiri.

“Jamani niliyokutana nayo kwa Salimu yameniweka katika wakati mgumu sana” Meroda aliuvunja ukimya akajilaza chali, Samira na Monica wakakaa vizuri kumsikiliza. “Kwa kifupi ni kuwa Salimu yupo kwenye kisasi na utafutaji wa Haki dhidi ya maisha ya wazazi wake waliofariki sijui kama mnakumbuka ile kesi tuliyoikuta miaka ile tunajiunga ya mauaji ya Muheshimiwa Richard ambaye inasemekana alikuwa rafiki wa maboss zetu” Samira akamtazama Monica kwa mshangao, Meroda akaendelea “…sasa bora hilo tisa kumi ni kuwa yule bwana kumbe ni Afisa upelelezi wa kijeshi ni Komandoo, miaka yote ile walikuwa nje walikuwa India, Malysia na Urusi na ndugu yake hivi ninavyo waambia...

Itaendelea...
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU WA 3

Sehemu 8G: Maamuzi Magumu

Tulipoishia....

Mtikisiko wa gari ukamtoa katika dimbwi la mawazo kiunyonge Meroda akatoka garini na kuongozana na wenzake dhahiri akiwa amepwekeka sana, kwa mwendo wa kujilazimisha akaingia moja ya chumba cha duble walichopangisha Hotelini. Samira na Monica walikaa kitako wakimtazama maana tangu wameingia garini mpaka wanashuka dada yao mkubwa hajatia neno lolote na wao hawakutia neno wakabaki kusubiri. “Jamani niliyokutana nayo kwa Salimu yameniweka katika wakati mgumu sana” Meroda aliuvunja ukimya akajilaza chali, Samira na Monica wakakaa vizuri kumsikiliza.

Tuendelee...

“Kwa kifupi ni kuwa Salimu yupo kwenye kisasi na utafutaji wa Haki dhidi ya maisha ya wazazi wake waliofariki sijui kama mnakumbuka ile kesi tuliyoikuta miaka ile tunajiunga ya mauaji ya Muheshimiwa Richard ambaye inasemekana alikuwa rafiki wa maboss zetu” Samira akamtazama Monica kwa mshangao, Meroda akaendelea

“…sasa bora hilo tisa kumi ni kuwa yule bwana kumbe ni Afisa upelelezi wa kijeshi ni Komandoo, miaka yote ile walikuwa nje walikuwa India, Malysia na Urusi na ndugu yake hivi ninavyo waambia muda si mrefu wanaingia kazini rasmi mimi hoi” aliongea Meroda na kuishiwa pozi “Heee!” Monica alitaharuki kwa sauti macho yamemtoka kwa mshangao.

“Ndio hivyo… sasa yani sijui nifanyaje?” wote wakaonekana kujawa mawazo kutokana na uzito wa jambo hilo kila mmoja akatazama pembeni akitafakari kwa namna yake “Sasa dada wewe ulimwambia nini baada ya hapo?” Meroda alimtazama Samira aliyemtwanga swali hilo huku akimtazama kwa mshangao wenye wasiwasi. “Nilihisi kama nataka kufa hivi, sikumjibu kitu nikamuaga tu na wala sijamwambia tutaonana lini kama vile tulivyo ondoka ndo vile vile”

“…eehh makubwa mbona” Monica alipaza sauti kisha akayauma meno kwa hasira. “Dada kwani wewe uliwahi mwambia kazi yetu? Na amejuaje mpaka kuomba msaada wako?” Monica aliuliza huku akimkazia macho Meroda, Meroda alimtazama Monica kwa muda akamtazama na Samira kisha akatingisha kichwa kukataaa

“Sijawahi na hata kama angekuwa ni mtu wa kawaida tu nisinge thubutu kumwambia kazi yangu lakini yeye alijua tangu siku ile pale mgahawani miaka ile ya kuvamia supermarket wakiwa advance” aliongea Meroda na kuonesha kuwa changanya wenzake akaendelea

“Sikilizeni ni waambie mi nipo tayari kuisaliti kazi yangu kwa sababu ya Salimu, sipo tayari furaha yangu nyingine ipotee kama yule Sospeter wangu” teyali Meroda akaanza kulia, Samira na Monica wakatazamana huku wakiwa na sura za wasiwasi. Monica akasimama “Jamani mimi sipo tayari kuvunja kiapo cha kazi yangu sitaweza nilishindwa kupigania haki nilipokuwa peke yangu saizi lakini sasa naweza pamoja nao” aliongea Meroda na Monica akanyanyuka na kutoka zake nje kwa hasira,

“Monica Monica...unaenda wapiiiiii?” aliita Meroda Samira akanyanyuka kumfata mlangoni lakini akasimama na kumgeukia Meroda “Ameenda” aliongea Samira akirudisha mlango na kumsogelea Meroda kikapita kimya.

“Dada usilie umenifunza mambo mengi sana wacha nikuhakikishie jambo moja kuwa Nipo sambamba na wewe sasa hivi nafata oda yako” Samira aliuvunja ukimya Meroda akashtuka macho yakamtoka akiwa haamini kilichoingia masikioni mwake “Unasemaje Samira?!” alijikuta akiuliza Samira akalitoa tabasamu lenye maana ya kile alichokuwa anakisema akaongea “Nipo pamoja na wewe na kuanzia sasa nitafata oda yako”. Meroda kwa uchungu uliochanganyika na furaha akamkumbatia kwa nguvu sana Samira, “Ohh asante sana Samira asante” wakageuka na kutazama mlangoni na kukutana na macho ya Monica akiwa kashikilia Mlango dhahiri akiwaonekana kuwa dailema. Masikini Monica machozi yakaanza kumtiririka akatoka mbio hadi walipo wenzake “Dada na mimi nipo pamoja na wewe mpaka kufa kwanza nimeichoka hii kazi” aliongea Monica kwa uchungu wa waziwazi.

“Nashukuru nyinyi ni ndugu zangu basi wacha niwamalizie simuliz yake” akaanza kusimulia kadri alivyokumbuka “Dada Meroda sasa unajua cha kufanya? sio kwamba si mwamini laa tusijisahau kanuni za kazi inatupasa sisi kwa nafasi yetu kuhakiki juu ya habari hizo sisi wenyewe isije ikatumika kivuli cha Pius kuweza kuwafikia maboss” aliongea Monica “Sawa lakini lazima ufikirie sisi kujulikana sio jambo jepesi maana tukiliamaini hilo inamaana basi serikali au watu Fulani wameshatugundua nyendo zetu si ndio?” Meroda alimrudishia swali Monica ambaye alitulia kwa muda akiwaza.

“Nimekuelewa lakini tusijisahau tuendelee kuwachunguza kujua ukweli uliopo tusijiingize wazima wazima inabidi sisi wengine tuwe nje ya ulingo kukulinda” aliongea tena Monica. Samira alitabasamu kukubari wazo la Monica “Ni kweli dada, Monica anasema jambo zuri tulifanyie kazi” Meroda akawatazama wenzake kisha akameza mate na sura ikaonekana kana kwamba anatamani kuongea kitu lakini alishindwa alichokifanya ni kuvuta simu yake aliyoitelekeza muda mrefu na kuandika ujumbe mfupi wa maneno kuhusu kukubar kwake kisha akautuma na kutabasamu akajiwazia ‘nimeshakuamini Salimu wangu naomba usiniangushe tafadhari’ Meroda alisemea nafsini kisha akaongea “…nitamtafuta leo usiku na kumjulisha kuwa tumekubali kuungana naye na maelezo zaidi tutaongea vizuri tukikutana mnaonaje hiyo” Meroda kwa tabasamu aliwatazama wenzake “…sawa tu imekaa vizuri au unasemaje Monica” Samira alidakia akimtazama Monica aliyekuwa bize muda huo akisugua kucha zake ndefu” “Iko poa wadada” akatabasamu.

Itaendeleaa
 
The Hidden Truth

Nani Anahusika

MSIMU WA TATU

SEHEMU 09: VIJANA KAZINI

Dondoo

“Chini ya Uongozi wa Komandoo Ochola kwa tiketi ya Raisi Steven James Mkuchu Salimu na Karimu wanaingia mtaani kupambana na maharamia, mafisadi, majambazi, na kila mfanya bishara haramu kwa kasi kubwa na kwa siri sana. Lakini kwa bahati nzuri au mbaya wanapokea taarifa tofauti toka kwa Meroda na kwa Komando Ochola zinawashtua na kuwashangaza. Je! Ni taarifa zinazo husu nini na zitazua mambo gani?”

Ikulu, Dare es Salam
“Vijana hongereni sana, na nimefurahi sana kuianza mission hii pamoja nanyi kama tulivyopanga na bwana Ochola...” Rais Steven James Mkuchu alionekana kujawa na furaha sana maana uso wake ulijawa na tabasamu kubwa sana, “Asante sana muheshimiwa” Salimu na Karimu waliitika kwa pamoja kwa utiifu mkubwa. Katika mazungumzo Muheshimiwa Steven aliwazungumzia kwa hisia kali sana wala rushwa, mafisadi, watu wanao husika na madawa ya kulevya, watu wanaohusika na wizi aina zote maana hao ndio wanyonyaji wa nchi akiwaomba wayakubali kwa moyo mmoja majukumu hayo na wao wakayapokea majukumu kwa mikono miwili tayali kwa kazi huku wakiwa ni wenye furaha kubwa sana.

“Jamani, vijana wangu Rais aliyetangulia mambo mengi alikuwa akiyafanya bila kuzingatia sheria, kulikuwa na matumizi mabaya ya majeshi, katika siasa.

Wasaidizi wa viongozi mbalimbali walikuwa free kulitumia jeshi la polisi kiholela katika mambo yao binafsi na baadhi ya viongozi kusahau wajibu na kupelekea wengine kuuwawa na wananchi wenye hasira kali rekodi ninazo. Kipindi hicho zamani nilikuwa Waziri wa wizara ya elimu, sayansi tecknolojia na ufundi na wakati huo Fanuel Mkwasi alikuwa waziri katika wizara ya mambo ya ndani na kumbuka kipindi hicho tulikuwa mawaziri pekee wenye ushawishi na umakini katika kazi, ndipo alinishauri kuweka jina langu katika ugombeaji Uraisi baaada ya kufa Muheshimiwa Meza nami nikafanya hivyo”. Karimu na Salimu waliendelea kumsikiliza Muheshimiwa Raisi kwa makini. Nimejitahidi kwa ushirikiano na Ochola kuteua Mkuu wa jeshi la polisi IGP Lugole na nipo kwenye uteuzi kubadilisha makanda wakuu wote mikoani nahisi itakuwa nzuri kwenu” alijichekesha kidogo na kuwatazama huku akiwa na macho ya hofu kitu ambacho kilijulikana na watu wote katika chumba cha siri. “Muheshimiwa mbona kama huna raha, kuna tatizo lolote…” Ochola aliongea akimtazama kwa jicho makini.

Muheshimiwa Raisi alimuangalia kisha akakhoa kidogo “Unajua nini kuna baadhi ya mawaziri wanachukia kuhusu uteuzi wangu wakinipiga vijembe…unajua nimebadilika mimi sio kama wale maraisi wachovu waliopita nimejiwekea vijana makini wenye damu ya uzalendo katika miili yao wapo tayali kufa kwa ajili ya nchi yao hawanunuliwi” aliongea na kutabasamu “Mwanzoni sikujua mengi yaliyopo katika kiti hiki nilichokalia sikujua mambo yanayomkabili Raisi, kwa kweli kuna vitisho na lawama nyingi sana lakini…msijari karibuni vijana. Hii ni timu yangu ya siri tutafanya kazi pampoja na TISS tutawaacha waendelee na kazi zao bila kuwaangilia kwa sababu bado kuna tatizo na Mkwasi na mawaziri wengine japo lilikuwa ni wazo lake hili lakini natamani kulitumia kwa namna nyingine” aliongea Muheshimiwa Raisi, “Muheshimiwa samahani inakuwaje sasa licha kuwa TISS ipo na mambo yalivyo nitofauti shida nini hapa” Karimu alishindwa kujizuia na kuuliza “...unajua nini kijana vigogo wengi nchini ndio wenye watoto huko TISS vijana ambao wala hawana sifa na kazi hiyo wapo wapo tu wakifanya kazi watakavyo wanaingia watakapo kwa maslahi yao binafsi huku bastola zikiwa mbele mkononi wakitishia raia na wakati mwengine wakikamata watu wasiokuwa na hatia na kuwasweka ndani kwa makosa makubwa makubwa huku wale weny makosa wakiendelea kula maisha na hata kuhamia nchi jirani kwa usaidizi wao.” Salimu na Karimu wakatazamana kwa mshangao “…ni kweli si utani vijana idara ya usalama wa taifa imeshaanguka hakina maadili kabisa kwa sababu kina fanya mambo tu alimradi tena waziwazi bira siri na ndio maana katika jamii wamechukua sura mbaya na kuonekana kama wauaji na hata walewenye uzalendo hivi sasa hawapewi ushirikiano na raia bali hubaki wakitazamwa tu”. Ilikuwa ni habari ya kuvutia sana masikioni mwa vijana kila mmoja katamani isiishe, Ochola aliwatazama tu kwa makini.

Muheshimiwa Raisi akaendelea “…kwa sasa kwakweli sina imani na Tanzania Militaly Inteligence (TMI) wala TISS, yaani sijui nisemaje vijana wangu watu hawa wanaudhaifu katika mambo mengi sana hata taaluma yao nina wasiwasi nayo lakini awali ya yote sizani kama hivi sasa kuna kile kikosi cha CHEETAH” kauli hiyo iliwashtua vijana wakatazamana kwa kusikia habari hizo za kikosi cha “CHEETAH” walikuwa na machache juu ya asili ya jina hilo na hata kikosi chenyewe lakini walitulia kwa tahadhari wayajue mengi wasiyoyajua.
Ochola alikusanya mikono yake katika paji la uso kisha akakhoa kidogo na kuwafanya watu wote wamtazame “…mmoja ya washirika wa kikosi cha CHEETAH waliosalia ni mimi hapa Komandoo Ochola”.


Itaendelea...

Duuh!!!
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact : 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 9B: VIJANA KAZINI

Ilipoishia...


wakatazamana kwa kusikia habari hizo za kikosi cha “CHEETAH” walikuwa na machache juu ya asili ya jina hilo na hata kikosi chenyewe lakini walitulia kwa tahadhari wayajue mengi wasiyoyajua.
Ochola alikusanya mikono yake katika paji la uso kisha akakhoa kidogo na kuwafanya watu wote wamtazame “…mmoja ya washirika wa kikosi cha CHEETAH waliosalia ni mimi hapa Komandoo Ochola”.


Tuendelee...

Muheshimiwa Raisi alijikuta akisimama kwa mshtuko huku akimtazama Ochola bila kusema kitu, sio yeye tu hata kina Salimu nao walimtazama maana hawakujua mengi juu ya hicho kikosi cha CHEETAH “Ohh! Haiwezekani Ochola sijasikia vizuri au…CHEETAH???!!”. Muheshimiwa bwana Mkuchu alitahamaki akimtazama vizuri Komandoo Ochola, Ochola akasimama na kuvua koti lake la kahawia akaliweka mezani akavua shati na kubaki kifua wazi akamsogelea Raisi aliyekuwa ameduwaa akimtazama na kumuonesha tattoo ya CHEETAH katika mgongo wake jambo lilimfanya Muheshimiwa Raisi kutabasamu huku machozi ya kimlenga lenga. “Ohh Ochola nimefurahi sana umenipa nguvu ya kuifanya kazi hii bila mashaka yoyote na nina penda kukiita kikosi hiki kwa jina la IRON HAND…lakini tafadhari naomba msije mkamwambia bwana Mkwasi chonde chonde hata yeye hivi sasa simuamini” aliongea Muheshimiwa Raisin na kuendelea na mazungumzo mengine katika chumba cha siri.

Kawe, Kinondoni-Dar es Salam.
Ni majira ya chakula cha usiku teyali vijana walikuwa mezani wakiandaa mazingira ya kula “Unajua nini Mzee kimasighara masighara kama picha ya kizungu tumekabiziwa nchi tuinyooshe rafiki yangu, dah!” Salimu aliongea huku akipakua rosti ya mchuzi kwenye sahani “Baba we acha tu, kilichoniacha mdomo wazi ni kile kikosi cha CHEETAH Ochola ni mmoja wao nilijikuta nikiingiwa na kibaridi chembamba aisee watu wanatoka mbali” aliongea Salimu na Karimu akadakia “Kile kikosi sio mchezo mzee ohh” Karimu akacheka kidogo na kupeleka kipande cha nyama mdomoni “…haya tusubiri tuone, maana kila siku mambo mapya yanavubuka” Salimu aliongea na kukitingisha kichwa kukubali maneno yake kisha akaongea tena “Tusubiri tuone” “Ndugu yangu tumepitia shida nyingi sana kwa kweli leo nimeona umuhimu wa Ochola kututembeza nchi mbalimbali katika vipindi vifupi vya likizo.”

Aliongea Karimu “Mi nakumbuka ndungu hasa tulipokuwa Russia katika likizo” aliongea Salimu kisha akaendelea “Nakumbuka vizuri sana mzee yani kingine kinachonishangaza sikutegemea kama tungeweza tolewa katika jeshi kwa hali na mvutano wa Meja Alfani Mashu na mashabiki wa Meja Mogesha.” Alitulia Salimu na kumtazama Karimu “ We unashangazwa na hilo mzee mi kinacho nishangaza mpaka leo ni ile hali ya kutengenezewa ajali kuwa tumekufa na kutotambulika aiseee hizi kazi zingine mzee dah, alafu ndo ikawa kimoja safari ikawa India, alafu leo tuna majina kibao na vitambulisho vyake dah yani tumekuwa kama matapeli” Karimu aliongea na kutikisa kichwa tu kipindi hicho Salimu akiwa anamtazama akijizuia kucheka.

*****

Siku tatu pekee zilitosha kukabiziwa vifaa vya kisasa kabisa vitakavyo wasaaidia vijana kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana. Waliipanga ratiba yao vema na kuanza kazi mara moja. Muda ulienda Salimu na Karimu wakawa bize sana tena ile bize haswa maana utamu wa kazi ulishaanza kuzoeleka katika akili zao na mwili kiujumla. Walizitambua mali zote walizomilikishwa kikazi na wakazikalili, walikuwa ni watu wa kutoka na kukagua miradi yao. Walionekana ni wafanya bihashara vijana tena wenye mafanikio katikati ya jiji la Dar es salam tena walio zuka vuup kama mzimu mbele ya kadamnasi.

Kipindi wakiwa bize kufatilia mambo ya biashara pia waliendelea kupokea nyaraka za kesi mbalimbali na majina ya watu Fulani Fulani ambao walihusishwa na matukio ya kiharifu kwa namna tofauti. Nyaraka hizo zilihusisha wasifu wa watu hao ambao wengi walikuwa wameshinda kesi kibadhirifu wengine wakiwa hawajatiwa mikononi tangu majina yao yakiwa midomoni mwa mapolisi tena wakiwa bado mijini wakiendelea na biashara haramu. Majina hayakuishia kwa watu wa kawaida tu la hata viongozi toka katika vyama vya siasa na walio tayali serikalini ambao walikuwa wakitumia vyeo vyao kufanya biashara ambazo ni haramu. Kazi yao haikuishia hapo tu walikutana na Komandoo Ochola na kupelekwa baadhi ya mitaa, casino, clubs na kumbi za strarehe mbalimbali jijini Dar na mikoa mikoani wakioneshwa namna mambo mengi yanavyofanyika na namna ya kukabiliana nayo huku wakiendana na mazingira husika, hiyo ndio kazi waliyo ichagua.

Wala unga toka mataifa mbalimbali walionekana waziwazi wakifanya biashara katika kumbi hizo za starehe wakifanya ufuska kwenye makasino na wanawake wakiswahili kiasi cha kuona kinyaa kweli kweli. Hawakupita humo tu wakaacha laa walitembelea katika mitaa ya uswahili na kushuhudia biashara za siraha kiholela zikiuzwa kirahisi kabisa bila wasiwasi mambo yaliyowafanya waamini kuwa Muheshimiwa Raisi bwana Steven Mkuchu alikuwa na haki ya kuongea yale yote juu ya jeshi la polisi.

Itaendeleaa...
IMG-20220103-WA0024.jpg
 
The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact 0658328596
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 9 C: VIJANA KAZINI

Tuendelee...

Wala unga toka mataifa mbalimbali walionekana waziwazi wakifanya biashara katika kumbi hizo za starehe wakifanya ufuska kwenye makasino na wanawake wakiswahili kiasi cha kuona kinyaa kweli kweli. Hawakupita humo tu wakaacha laa walitembelea katika mitaa ya uswahili na kushuhudia biashara za siraha kiholela zikiuzwa kirahisi kabisa bila wasiwasi mambo yaliyowafanya waamini kuwa Muheshimiwa Raisi bwana Steven Mkuchu alikuwa na haki ya kuongea yale yote juu ya jeshi la polisi

Miezi sita haikufika hata tangu vijana hao kuingia katika kazi ngumu yenye utashi mwingi maaana wauza madawa ya kuleya kulevya kule mitaani walianza kukamaatwa kama kumbi kumbi wakiwa na vibaraka wao.

Sifa zilimiminika kwa makamanda wakuu wa jeshi la polisi katika mikoa bila kufahamu namna kazi zilivyofanywa kirahisi. Kamanda mkuu wa jeshi la polisi jijini Dar alikuwa ni mtu wakupokea oda toka ngazi za juu tu kupitia simu wavamie sehemu Fulani na yeye hufanya hivyo na kweli mambo huwa. Jeshi la polisi sasa likaaanza kupata heshima yake iliyo ibwa muda mrefu na kupelekea kukosa uwaminifu toka kwa wananchi. Ili saidia sana maana wananchi wenye kuipenda amani sasa walitoa ushirikiano mzuri na jeshi la polisi na akina Salimu walipenyea humo humo toka kwa raia wema.

Kamanda Ochola alibaki kujichekea tu kivivu kila alipoona mafanikio yakinukia aliiendelea kuwaimarisha vijana wake na kuwapa motisha kubwa wasikate tamaa.
Passion Hotel, Kigamboni- Dar es Salam
Kwa mbali watu wawili waliozungukwa na wanaume walio tuna kwa mazoezi waliendelea kupiga hatua fupi wakionekana kuongelea jambo Fulani. Wazi walionekana ni watu wenye fedha zao za kutosha kwa namna ya mavazi ya kisasa na utanashati walio nao

“Pater hapa kuna haja ya kukutana na Mogisha na Mashu watueleze jicho kwa jicho si kama wanavyotupa maelezo mengi kama vijana wamechoka kwanini wasisajili wengine na kama tatizo ni maeneo kwanini yasibadilishwe?” aliongea mmoja wao “Ni kweli Samuel mi sikuwepo nchini lakini niliyoyakuta katika mitandao nilizani utani Utawala nauona unaanguka taratibu hatupaswi kuliachia hivi hivi hata kama bado hatuja fikia muafaka na yeye lazima tuiweke nguvu pamoja mana ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji wanavyoanza kula dagaa wakiisha kesho watakula papa” aliongea Pater “Nikweli tupu Pater hatupaswi kumuamini sana maana hata mtumwa kuna siku anakuwa mfalme, askari hawawezi kuwa wale wale, Kuna haja ya kuwasiliana na Meja mapema leo” alidokeza Samuel na kuendelea “…na ikiwezekana tumtafute leoleo tufanye makutano kabla hatuja enda sikiliza changamoto za Magamba bado hapajakucha” mlango ukafunguliwa kwa Heshima na kuingia katika gari aina ya Black Hummer H2 V8 6.0 PACK LUXURY

*****

Nyakati tofauti Meroda na rafiki zake waliendelea kukaa pembeni kumchunguza Salimu na Karimu kwa wakati wa nje ya majukumu ya kikazi ili kujiridhisha na kuamua kumsaidia kama walivyo nena kwa ndimi zao au laa. Tumaini la imani juu ya vijana hao likaendelea kumea huku Meroda akiendelea kuwadhihirishia maneno yake kutokana na kufahamu kuwa wao ndio wanaofanya shughuli za kuwanyakuwa waharifu ndani ya nchi. “Sasa jamani mi nafkiri tumeshajiridhisha vya kutosha…” Meroda kwa tabasamu alipitisha macho yake yakulembua kwa rafiki zake kisha akapiga fundo moja la mvinyo na kuendelea “…na tumeona namna wanavyofanya kazi…nafkiri sasa ni wakati wetu wa kuwasaidia” Meroda aliongea mbele yao kwa kujiamini huku akiwa kashikilia glass ya mvinyo mkononi mwake na miguu yake akiwa kaikunja nne katika kiti kirefu ndani ya moja ya Hotel ya kitalii jijini.

“Ndio dada ni wakati wetu sasa” Monica aliongea huku akichanua kwa tabasamu lake lililodhihirisha madimpoz katika shavu zake zote mbili. “Basi tuanze kazi pamoja nao” Meroda alimaliza huku akinyanyua glasi ya mvinyo juu kuhashiria kugonga chears basi kila mmoja wao akakutanisha glass yake ya mvinyo pamoja na za wenzake kwa
Kawe, kinondoni-Dar es Salam
Jua lilikuwa ndo linaishia lakini bado liliendelea kuunguza, Salimu na Karimu wakiwa wamejikalia nje ya nyumba yao ya kifahali wakipunga upepo chini ya mti karibu na swimming pull karibu na bustani, mara akaanza kuskia alarm katika saa yake ya mkononi “Karimu kuna mtu anaikaribia nyumba yetu akaibonyeza saa na kuitazama, naona ni gari hebu kuwa stand by tafadhari” aliongea Salimu kwa sauti ya chini Karimu akiwa amevalia bukta akaichukua bastola yake aina ya AMT hardballer iliyokuwa pembeni yake na kuiweka vizuri huku akiwa kasimama akisogea eneo la ukuta mara simu ya kiganjani inayomilikiwa na Salimu ikaita na kumfanya atoke mawazoni alimokuwemo na kuipokea maramoja baada ya kuona jina la Meroda “Habari Meroda…ndio nipo nyumbani saizi…mhh sio kweli inawezekana kweli…?” Salimu alionekana kuwa na mshangao kidogo lakini punde

Honi za gari zilipigwa nje ya nyumba yao na kumfanya Salimu aache mdomo wazi huku simu ikiwa sikioni akamtazama Karimu ambaye alikuwa teyali yupo atika uambaa wa ukuta bastola mkononi makini, akampa ishara ya utulivu. “Akabonyeza kitu katika saa yake na geti likaafunguka kulipisha gari kuingia. Salimu akajinyanyua kitini na kuzivaa sadro zake mikono ikiwa kifuani akifunga vifungo vya shati vilivyokuwa wazi, hakuna aliyeongea tena zaidi wakajiandaa kiakili kukutana na wageni hao. Gari matata aina ya Toyota Harrier ikaingia ndani na punde mabinti wa nguvu walitoka garini kwa mbwembwe haswa wakiwa na mavazi yao ya kimjini mjini yenye utata wa wingi wa matamanio

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Nani Anahusika!!!

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 9D : VIJANA KAZINI

Tuendelee...

vya shati vilivyokuwa wazi, hakuna aliyeongea tena zaidi wakajiandaa kiakili kukutana na wageni hao. Gari matata aina ya Toyota Harrier ikaingia ndani na punde mabinti wa nguvu walitoka garini kwa mbwembwe haswa wakiwa na mavazi yao ya kimjini mjini yenye utata wa wingi wa matamanio “Ohhh karibuni sana wageni wetu naona leo mmetufanyia surprise ya aina yake kwa kweli” Salimu aliwakaribisha wageni hao huku akiwa kumbatia mmoja badala ya mwengine kama walivyozoea na Karimu naye alifanya vivyo hivyo kisha wakaingia ndani.

“Samahani kama nimevunja ratiba zenu” Meroda alikutanisha viganja vyake kwa ishara ya msamaha pindi tu walipo ingia sebureni na kukaa katika moja ya sofa “…hapana kuweni na amani tu maana mmpo na watu wanaopenda wageni” Salimu aliongea kwa sauti ya mashaka kidogo huku akitazama meza na kulilazimisha tabasamu la uongo huku macho akiyapepesa kila mara. “Salimu ni hivi mimi na wenzangu tumekubaliana kuwasaidia kwa hali na mali katika kila hatua ya nyendo zenu.” Salimu akanyanyua uso wake kwa taharuki na kumtazama Meroda kwa muda huku uso ukiwa na viulizo vingi kisha akatazama na wale wenzakake alioongozana nao nyumbani hapo kuhakiki kauli ya aliyo isikia toka kinywani mwa Meroda. “Ndio shemeji amini hivyo…msaada tunaotaka kwenu ni mmoja msituangushe tu” Monica alikazia kumtoa wasiwasi Salimu ambaye hisia za kufanyiwa mtego zilikuwa zikimpitia pitia akilini mwake. Salimu akajikuta mwili ukiingiwa na baridi na ka moyo kakaanza kuongeza spidi ya mapigo

“nashukuru sana Meroda lakini nin wasiwasi kidogo isijekuwa umepata shinikizo?” Salimu alijikuta akiongea maneno ambayo hakuyakusudia huku jicho kavu lenye kuhitaji majibu likiwa usoni mwa Meroda, Meroda alitambua hilo moyo wake uliingiwa na huruma “Salimu, moja kwa moja unapaswa kuamini kama nilivyokuwa nimekuamini yale uliyoniambia haikuwa kazi rahisi lakini imeshakuwa Salimu” Karimu alikuwa katulia akimsikiliza Meroda kwa makini huku akiwatazama marafiki zake ambao wanathibitisha kuwa wamedhamiria toka mioyoni.

“Basi sawa tunaweza kuanza kazi mara moja, ila mnapaswa kutambua ni nyinyi tu pekee mnaotambua ukweli na sisi tunaotambua ukweli wenu” Salimu alimaliza kwa msisitizo na kisha wakabadili mazungumzo huku wakipeana baadhi ya mikakati mbali mbali ambayo kina Meroda wataipitia kwa ufupi “Lakini kabla hatuja ondoka hapa ningependa kuwahabarisha jambo moja ili akili zenu ziwe macho na utayari wa mapambano mazito”Meroda aliongea maneno hayo katika kati ya mazungumzo na kumtazama Salimu na Karimu kwa zamu zamu, maneno yaliyowafanya Salimu na mwenzke wawe na hamu ya kujua habari hiyo yenye kushtusha “Ni hivi tumeona kuwa wala si mapema kujua haya bali ni wakati sahihi maana kupigana na adui ambaye humjui ni sawa kurusha ngumi gizani na hujui itampata nani” maneno hayo yaliongeza umakini wa kusikiliza. Meroda kaendelea,

“…ni hivi Muheshimiwa Samuel na Peter ndio hasa watu wanayoitetemesha nchi hii kwa matukio yote ya uharifu na sisi ni maboss zetu tunawafanyia kazi, ni watu hatari sana sio watu wakawaida na wao wana watu na mtandao wao ni mpana umeingia katika sekta mbalimbali hadi katika serikali wapo wakihujumu nchi” Salimu na Karimu kwao ilikuwa ni taarifa ya kushangza sana kwao walihisi vitu lakini hawakutegemea kuwa watu hao eti ni maboss wa kina Meroda na zaidi ndio wanahusika katika matukio karibia yote ya uharifu pasina kujulikana iliwachoshwa habari hiyo

“…na zaidi kila mtu ana mtoto Peter ana mtoto mmoja wa kiume na Samuel ana mtoto mmoja wakike anaitwa Shalon” Salimu na Karimu wakatazamana kwa muda wakiwa na nyuso za kushangaa. Ilipotimu saa tatu juu ya alama Meroda aliaaga na kuomba kuondoka na timu yake “jamani kuna haja gani ya nyinyi kuondoka wakati nafasi za kulala zipo na mahitaji mengine” Salimu alijitahidi kubembeleza lakini wanawake walikuwa na msimamo hawakuwaweza kukubaliana nao wakaondoka zao na kuwaacha na maswali lukuki katika vichwa vyao.

Baada tu ya kuhakikisha kina Meroda wameondoka mazungumzo ya dharura yalikaliwa sebureni hapo na wakaanza kuchambua moja badala la moja.

Miongoni mwa mambo yaliyowateteresha ni habari za Samuel na Pater juu ya kuwa ndio maboss wa kina Meroda na kuonekana waziwazi walihusika katika mauaji ya wazazi wa Salimu la pili ni kuhusu kukubali kwa Meroda na timu yake katika majukumu ya kuwafichua watu wote ambao ni waharifu jambo hili lilikuwa ni lenye kujenga hoja za mashaka mawazoni mwa Salimu.

Habari hiyo ilionekana kutokuaminiwa kwa asilimia zote “ndugu yangu Karimu unafikiriaje kuhusu hawa wanawake na yale waliyo yasema” Salimu alimaliza kuongea “Mimi ninacho kiuona ndugu wacha tuwaamini lakini tuingie mguu mmmoja mmija tuweke nje hawakuchukua hata ajua hawakuchukua hata muda mrefu siku ile ile waliamua kukujibu kuwa amekubali yeye na timu yake na leo amekuja tu kututhibitishia…ahh mi naona tuwape na fasi kama wao walioyotupatia. Licha ya kuridhiana Salimu alionekana kukumbuka kitu “Hivi Meroda amelitaja jina gani kuwani la mtoto wa Samuel?” “ahhhaa alisema Shalon, hahahaa kaka bwana unafikiria ni Shalon wako mzee acha hizo bwana” Karimu aka nyanyuka na kuchukua glass yake na kuingia ndani na kumuacha Salimu akimuangalia na yeye akapuuzia na kumfata.


Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Sehemu 9E: VIJANA KAZINI

Ilipoishia....


Samuel?” “ahhhaa alisema Shalon, hahahaa kaka bwana unafikiria ni Shalon wako mzee acha hizo bwana” Karimu aka nyanyuka na kuchukua glass yake na kuingia ndani na kumuacha Salimu akimuangalia na yeye akapuuzia na kumfata.

*****

Tuendelee...

Meroda akishirikiana na wenzake walianza na wao kutoa kazi zao kwa kina Salimu wakiwaeleza habari za mashamba madogo ya bhangi huko mikoani. Salimu na Karimu bila kulemba wala kulaza usingizi waka waaga walizipokea na kuzifanya bila kujali ugumu wake wakaingia mikoani na kubadili kabisa wasifu wao kwa namna mbali mbali wakijifanya wakulima na kubadili lafudhi bila kutambulika na wakatoka na fununu za mashamba makubwa ya bangi yaliyofichwa kisha hao wanatimka na kuliachia jeshi la polisi likivamia na kuyachoma na wahusika wakiswekwa ndani, kisha hao mkoa mwingine. Ushirikiano wao na kina Meroda bado hawakuwa tayari kuudhihirisha kwa mkuu wao ambaye ndiye aliyekuwa akiwa simamamia hiyo ni kutokana na kukhofu kukosea nidhamu za kazi ambazo zinaweza kuja kuwaathiri hivyo kipindi chote hicho walikuwa wakitoa taarifa kwa mkuu wao huyo na kupewa ruhusa na wao kukamilisha mipango jambo ambalo ndilo alilokuwa akilisubiria sana kuliona miaka yote. Mbinu za kujifanya wanawake, kuvaa sura bandia, Ulema, uzee viliwasaidia sana.

Mwisho wa siku mwaka ukapinduka na mabadiliko waliyo yafanya vijana hao yalibadili sura ya nchi kwa kiwango kikubwa lakini bado maswali yalibaki ni kina nani hao wanaotambua mambo mazito kama hayo? Hata mapolisi wa kawaida na wengineo waliamini hao watu watakuwa si watu wakawaida maana si kwa utendaji huo.

Licha ya kupungua kwa matukio ya kiharifu lakini bado Samuel na Pater hawakuweza kuhisiwa hiyo ni kutokana na sera nzito waliyokuwa wamejiwekea katika vikosi vyao vyote ambavyo ni kheri kufa kuliko kusema ukweli maana ukweli utasambaratisha kizazi na familia yako yote kuliko kuamua kufa tu baada ya kubanwa. Na hiyo itafanya familia yako kuishi maisha mazuri.

Hivyo wale washirika wa Samuel na Pater waliishia kufungwa wengine wakijiua na wale walio sema ukweli walikuwa ni moja ya vikundi vidogo vidogo vilivyo amua kujiingiza katika wizi na ujambazi ili kuingiza pesa kutokana na jeshi la polisi kulala usingizi wa pono
Awali ya yote kichwani mwa kijana Salimu aliendelea kumtafakari Shalon ambaye hakuonesha utambulisho wowote kimuonekano kuwa anatokea familia ya kitajiri kiasi anachohisi na huenda hakuwa na haraka ya kulijua hilo mana asingeshindwa. Alibaki akiliacha na kutolipa nafasi.

*****

Kitonga, Ilala -Dar es Salam
Komandoo Ochola akiwa nyumbani kwake aliendelea kuzunguka mbele ya ofisi yake ndogo akiwa amevalia bukta na singrend nyeupe mkononi akiwa na kikombe cha kahawa iliyokuwa ikivuka mvuke wa moto. Jioni hiyo alitembea hatua kazaa mbele na kurudi kisha akasogea kwenye meza kuikwapua simu yake ya mkononi akachagua namba na kuipiga.

“…hallow, naomba mje nyumbani nina habari muhimu ya kuwaambia leo hii” akaikata simu hiyo na kuirudishia mezani kisha akaendelea kutembea kwa mwendo ule aliokuwanao awali.
Baada ya dakika chache
Gari aina ya…iliwasili na kufunguliwa geti wakati huo Komandoo Ochola akiwa juu Ghorofani akishuhudia gari ikatulizwa katika maegesho kisha Salimu na Karimu wakashuka na kuingia ndani huku wakiwasalimu walinzi baadhi waliokuwepo mjengoni. “Niwapatie kahawa au chai…” Ochola aliongea baada ya kusalimiana huku akionesha ishara ya kutoka eneo hilo “…Ohh hapana kiongozi tupo sawa tayari” Ochola akatabasamu kidogo na kusogea hadi katika kiti chake cha ofisi ambacho kilikuwa kikitazamana uso kwa uso na sofa moja ya watu wawili. “Ahh…nimewaita hapa kuwapa taarifa moja muhimu sana kwenu na kwangu pia” Ochola akajikalisha katika kiti cha kuzunguka katika chumba kilicho onekana kuwa ni ofisi kisha akaendelea baada ya Salimu na Karimu kukaa na kumtazama

“….kabla ya kurudi katika kazi hii nilitembelewa na Muheshimiwa Waziri Mkuu wa sasa kipindi hicho alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na nje ya nchi alinifatilia kila mara nilipokuwa nimejificha baada ya kunusurika na kifo kule Israel, kila aliponifata alinitaka nirudi kazini kisiri” alipomaliza kuongea hayo alitazama juu kwa muda kisha akaongea “…lakini kumbuka pia mauji ya Joka hayakuwa yakawaida na hakuna aliyewagundua wauaji mpaka leo, unakumbuka mchango wake lakini?! Basi jaribu urudi japo kwa ajili ya Muheshimiwa Richard aliyeuwawa kikatili mengineyo ukiyafanya basi itakuwa kwa ajili ya nchi yako hakuna atakaye kuzuia” aliongea na kwatazama “…siwezi isahau hii sentensi ipo akili miaka mingi sana sentensi

itaendeleaa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom