Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

The Hidden Truth ( Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 4

Sehemu 12 D: Ahadi ILIYOTIMIA

Ilipoishia...

“Ohh karibu sana kijana karibu nyumbani nilipata habari zako siku nyingi sana toka kwa binti yangu kipenzi Shalon lakini sikupata fulsa ya kukutana nawe…vipi mmeshapata kifungua kinywa?” Mzee Samuel aliongea na kukaa katika sofa la jirani “Asante sana baba nimeshapata nilipotoka, nimefurahi kukutana nawe pia, najiona ni mtu mwenye bahati sana” aliongea Salimu huku akijikaza

“ …ahhh hapana ni mambo ya kawaida tu utazoea” Binti mrembo aliingia katikati ya mazungumzo akiwa kavalia sare chupa ya mvinyo ikiwa sahanini pamoja na glass akaweka karibu na alipo kaa Mzee Samuel akafungua na kumimina “Karibu baba” aliongea na kuondoka

Tuendelee...

“Asante mwanangu…ndio kijana nimeambiwa na binti yangu kuwa unampenda sana umeshampatia pete ya uchumba na uko mbioni kumuoa ni kweli jambo hili?” Samuel aliongea na kuchukua glass ya mvinyo na kumtazama kwa makini sana kijana Salimu “Ni kweli baba nampenda sana Shalon na nimekuja rasmi kujitambulisha kwako” Salimu aliongea kwa kujiamini.

“Vizuri haina haja ya kujua unafanya nini au ni nani katika shughuli gani na una kaa wapi kwa ngu hilo si muhimu la msingi tu ni kuhakikisha kuwa utampa furaha ya maisha mwanangu wa pekee sawa?” Salimu alimeza mate na kufumba macho na kuhisi maumivu ya maneno aliyoyasikia yakipita katika mishipa yake ya damu ‘Vizuri haina haja ya kujua unafanya nini au ni nani katika shughuli gani na una kaa wapi kwa ngu hilo si muhimu la msingi tu ni kuhakikisha kuwa utampa furaha ya maisha mwanangu wa pekee sawa?’

mawazoni sauti ya Muheshimiwa Samuel ilijirudia tena na kufumbua macho yake “Hicho ndicho ninachokitarajia toka katika moyo wangu baba nitafanya hivyo daima” aliongea Salimu “ Safi sana” Mzee Samuel aliongea na kumrushia macho yake binti yake aliyeonekana wazi kujawa na furaha na aibu tele machoni mwake. “Kijana wangu kama utanithibitishia hilo hakika utanifanya uwe mrithi wangu pia binafsi nimejiskia furaha sana kwa muda mrefu sana tangu nimeona mwanangu kipenzi akicheka na meno yake meupe mazuri yakionekana”

Mzee Samuel alionekana kulengwa lengwa na machozi kiasi cha kumshangaza sana Salimu ambaye alibaki kuwatazama baba na mwana kwa macho ya kipelelezi. Shalon alibaki kajiinamia tu akitazama chini kwa muda. “…asante sana kijana kwa kumfanya mwanangu awe na furaha ya kipekee utakuwa umechukua nafasi ya mama yake kipenzi masikini mke wangu”

Mzee Samuel alitoa kitambaa na kuanza kujifuta machozi na kuendelea kumshangaza sana Salimu “Baba, usihuzunike nipo kwa ajili ya Shalon hakika sitamtupa kamwe lake langu langu lake” Salimu alijikuta akiongea bila kujali Shalon alipatwa na mshtuko na kunyanyua sura yake kumtazama Salimu machoni mwake macho yakiuliza unasema kweli Salimu? kwa upande wake Salimu kama alielewa hisia za Shalon aliishia kutikisa kichwa chake kukubali tu.

“Wanangu endeleeni ngoja niwaache nikapumzike, Salimu kuwa huru baba tutaongea mengi sana nataka umuoe binti yangu haraka iwezekanavyo ndoa itakayovunja rekodi zote za maisha yaliyopita ndoa zaidi ya yule Richard” alinyanyuka na kuondoka zake akijikongoja huku akijichekesha chekesha. “Salimu hebu tutoke nje nikuoneshe mazingira mpenzi” aliongea Shalon huku akimshika mkono kusisitiza.

“Salimu ningependa kuuuliza jambo moja kabla hujaniuliza maswali mengine mengi kunihusu mimi”, Shalon aliongea huku akiwa ameushika mkono wa Salimu wakiwa nje karibu na fukwe ya bahari nyakati hizo za jioni. “Bira shaka endelea tu nakusikiliza”, Shalon akasimama na kumtazama kwa mbele kwa sekunde kazaa kisha akatabasamu na kuongea “…ulimwambia baba kuwa hutonitupa upo kwa ajili yangu langu lako lako langu si ndio au lilikutoka tu neno hilo kumridhisha baba angu” Salimu alitafakari kidogo na kutabasamu “Kweli tupu Shalon je unamashaka juu ya hilo naonekana nadanganya sivyo?”

Salimu akamkazia macho Shalon “ No no no si maanishi hivyo bali namaanisha ulikuwa una maanisha ulichokuwa unakisema maana naona ulisema tu” “ Tafadhari niamini mpenzi naongea ukweli” Salimu hivi sasa alijiweka sawa na kutodhihirisha hisia zake zilizoelemewa na matatizo yanayoushambulia moyo wake “Usinidanganye Salimu najua kuzisoma hisia pindi nimtazamapo mtu kwa dakika chache tangu jana nakuona kunakipindi una loss katika uwasilishaji wa body language kuna kitu hakipo sawa lazima unithibitishie hilo tafadhari kabla hatuja fika mbali” Salimu alimtazama Shalon kwa muda akionekana kutafakari kitu macho yakiwa machoni mwa Shalon kisha akashusha pumzi nzito

“…ni kweli Shalon nina hofu na baba yako mzazi maana nimemuona ni mtu wa kawaida lakini si kama aoekanavyo pia sikuwahi tegemea kuwa Muheshimiwa Samuel ni baba yako mzazi kabisa sijawahi ona utambulisho wako huo hata katika social media hivyo lazima niwe na wasiwasi kuna siri gani eneo hili” Shalon akamtazama vizuri Salimu “Unahakika mpenzi?” “Ndio Shalon, na nategemea kupata mengi nisiyo yajua toka kwako” “Unanipenda Salimu” “Ndio nakupenda Shalon” aliongea Salimu, Shalon kwa haraka akamvuta karibu zaidi na kugunsanisha mdomo wake na Salimu, wakakisi na kukisi tena huku Shalon machozi yakimtoka kisha akaacha na kumkumbatia,

Salimu akiwa mekutwa na bumbuwazi macho yamemtoka kalewa na tukio hisia imemjaa mpaka sehemu zake za siri zika sisimka Shalon aligundua, “Salimu nitakwambia kila kitu bila kusita na naomba ukijua ukweli huo ubaki upande wangu tafadhari na ndio maana nilitaka unipende mimi kama mimi na sio utajiri unaonizungunguka” Salimu alisikia na kutolewa katika hisia alizokwemo, akayatafakari maneno hayo kisha akatabasamu “Nipo tayari kwa hilo hata ikiwa leo hii Shalon tafadhari nitakusikiliza” Salimu “Naomba nikwambie kitu Salimu lakini nakwambia kwa sababu ndio mwanaume pekee ninaye kupenda najua sijakujua vizuri wewe wala familia yako iliyobakia lakini tangu siku ya kwanza imani yangu ipo kwako hata sijui kwanini hivyo japo kunakipindi nahisi kuna kitu kingine zaidi ya kukupenda kinachonisukuma juu yako lakini sikijui nashindwa uelewa moyo wangu lakini wacha nikwambie”

Shalon akaanza kujifuta machozi Salimu na yeye alinyanyua kiganja chake na kuanza kumpoza hisia kwa kumfuta na vidole vyake “Shalon kama huwezi usijilazimishe bado kuna siku nyingi mbele yetu maelefu ya siku” aliongea Salimu “No no lakini hakuna anaejua ni siku ngapi zimebakia kabla ya kufa usiongee hivyo wacha nikwambie sasa hivi nitajikaza tu” Shalon taratibu akaanza kuchuchumaa na kukaa mchangani Salimu naye akafuata. “Salimu ni hivi Samuel sio baba yangu mzazi kabisa...” Salimu moyo ukamlipuka paaa! “Unasemaje unaweza kurudia tafadhari?” Salimu aliongea kwa taharuki, Shalon sasa machozi yakimtoka haswa “Samuel sio baba yangu wa kunizaaa ni stori ndefu sana Salimu baba yangu mzazi aliuwawa na Samuel pamoja na mshirika wake Peter tena kwa makusudi kabisa” Salimu kwa makini huku sura akiwa kaikunja kiasi hasira zikijichimbia ndani kwa ndani na maswali kibao alibaki kumtazama tu Shalon

“…nilivyokuwa mdogo…sijasahau kitu na nina uwakika huyu baba ndiye aliyemuua mama yangu baada ya kumtambua alihusika kumuuwa baba yangu” “…baba yako? Inamaana Samuel sio baba yako?” aliongea Salimu “Ndio mpenzi baba yangu sio Samuel” aliongea Shalon kwa masikitiko sana na kutilia huruma “Pole sana mpenzi pole sana....

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 4

Sehemu 12E: Ahadi ILIYOTIMIA

Ilipoishia...

...nilivyokuwa mdogo…sijasahau kitu na nina uwakika huyu baba ndiye aliyemuua mama yangu baada ya kumtambua alihusika kumuuwa baba yangu” “…baba yako? Inamaana Samuel sio baba yako?” aliongea Salimu “Ndio mpenzi baba yangu sio Samuel” aliongea Shalon kwa masikitiko sana na kutilia huruma “Pole sana mpenzi pole sana, baba yako alikuwa nani kwani na…au mama yako alikimbia kwa baba yako nakukimbilia kwa Samuel?” Shalon aligeuka na kumtazama Salimu “…sina majibu ya maswali yako ninachokumbuka sikuwahi kumuona mama akiwa nafuraha na hata siku Moja....
.

Tuendelee
..... anakufa nilikuwa nimeshikilia simu yake kwa nia ya kumpiga picha tulikuwa tuna cheza lakini wakati wanazozana mama akaniambia niondoke niliposikia kelele zimezidi nilirudi nikiwa nimeshikilia simu kwa mtindo wa kupiga picha nilipofungua mlango ndipo mama yangu alikuwa anaongea kwa uchungu akimlaumu Samuel alivunja ahadi walioiweka kwanini alimuua akamshambulia huku akimuita mama Malaya akijisifu na kumkaba huku akimgongesha ukutani kisha akamtupa na kuondoka alipokuja mlangoni nikajificha alipotoka nikamfata mama nikilia simu nikiwa bado nimeshikilia ndipo alipo niambia kuwa Samuel sio baba yangu mzazi bali baba yangu ni Richard Edward kisha akafariki mbele yangu”

aliongea Shalon kwa uchungu wakati huo Salimu alikuwa kajishika kichwa machozi yakimtoka “Na wewe ni Richard Edward…haiwezekani iwe hivi Nooo” aliongea kwa uchungu kiasi cha kumshangaza Shalon ambaye alibaki akimshangaa “Mbona Au huamini au wewe umeelewa nini mpenzi” Shalon aliongea “Hebu nambie mbona unanichanganya Shalon inawezekana vipi hilo lakini” aliongea Salimu huku akimshika mabega akimtikisa hadi Shalon kuogopa “Salimu kwanini isiwezekane inamaana ulikuwa unanidanganya sio hunipendi au vipi unaelewa ninachoongelea lakini mbona na wewe sikuelewi? Sijafika pakunisaidia hata sijakwambia umeanza kunikwepa kumbe hunipendi”

Sahlon aliongea huku akiitoa mikono ya Salimu mabegani mwake. Kila mmoja alibaki kumshangaa mwezie. “Sikia Salimu ningekuwa na uwezo basi ningemtafuta kaka yangu Pius na kushirikiana nae katika hili kumbe wewe ni wale wale” Shalon aliongea kwa uchungu na sauti ya kilio. Salimu alijikuta akiishiwa pozi machozi yakimlenga lenga “Ina maana wewe ni dada yangu” Salimu bila kujielewa alijikuta ameyasema maneno hayo na kumshitua Shalon “Dada yako hivi sijakusikia au Eehhh hebu sema kitu hebu rudia” Shalon alimvamia Salimu na kumkwida akimtingisha tingisha Salimu hakuwa na lingine bali kutokwa na machozi pekee mwisho akajikuta akimkumbatia Shalon kumbatio zito.

Walibembelezana na kuongelea mambo baadhi yaliyopita. “…nimeshafika kwa bibi yupo hai na nimeshaonana na shangazi zangu na hivi ninavyo kwambia tunawasiliana kila wakati nimeyafanya mengi tutaongea kaka” aliongea Shalon “ Unajua nini dada Shalon kiukweli mungu ni mkubwa katika siku zote hizi nilihisi kitu tofauti kabisa juu yako sikuwa na hisia za mapenzi kabisa juu yako na sikujua kwanini kumbe nilikutanishwa na dada yangu siku ile ohh mungu wangu asante sana” aliongea Salimu na kutabasamu “Mi pia kaka lakini sikutafakari zaidi hayo, lakini nashukuru kwakuwa ni kaka yangu basi inatosha sina nafasi ya mtu mwengine wewe tu kaka”

aliongea Shalon “Ni sawa na muda umeenda sana naomba uniache niende nikapange mambo vizuri naomba usije kumuonesha hisia zozote za mashaka bwana Samuel badae nitakupigia simu nitakuelekeza pahala tukutane hatuna muda kabisa” Salimu aliongea na Shalon akatingisha kichwa kukubali wakashikana mikono na kutoka eneo hilo.

HOT spot club, Ubungo -Dar es Salam
Mziki wa taratibu ulisikika kwa mbali, katika meza ya peke “Aisee ni jambo la kushtukiza na kushangaza sana kwa kweli nimefurahia sana na tumshukuru mungu kwa kusimama upande wetu, maana nilikuwa muoga” Meroda aliongea na kutabasamu. “Jambo la msingi ni kujikaza tu Shalon kwa sababu timu yetu ipo makini na tumejipanga hatukufanyi chambo lakini najua kwa upande wako ni sehemu ya ndoto zako katika maisha ambazo unaenda kuzikamilisha” Salimu aliongea,

“Jamani kaka,wala msijali kuhusu hilo hamjui tu namna ninavyofurahi kufahamiana na nyinyi nyote nina amani sana” Shalon aliongea “… nitajitahidi kufata maelekezo na mazoezi mliyo nipa bila makosa” aliongea Shalon kwa furahs “…Vizuri dada Shalon kila kitu kitaenda sawa, kuna watu maalumu watakaoshughulikia usalama wako bila wasiwasi, maaskali watakuja kwa wakati na hata pia taarifa ya kukamatwa itakuwa tayari katika mitandao ya kijamii pindi tu tukipata signal toka kwako kwa kukibonyeza kifaa maalumu utakachokiwasha ukiwa tayari tu na si vinginivyo baada ya kuanza majibizano na Samuel ambaye kwa muda huo atakuwa ni mtu mwenye jazba hatoweza kukaa kimya akikusikiliza pindi tu ukipita mule tulipo kwambia na hapo mchezo utakuwa umekwisha maskari wataingia na kumuweka chini ya ulinzi na kumchukua”

Salimu aliongea na kumfanya Shalon kutabasamu na kutingisha kichwa “Nipo tayari kwa kazi kaka natamani siku iishe haraka haraka naamini nitafanya” “Vipi kuhusu Karimu mliwasiliana” Meroda alidakia “Yeah japo mtandao unasumbua sana lakini anaendelea vizuri na mchakato nafikiri mpaka leo jioni kesho atakuwa amefanikisha upelelezi kwa kiwango kikubwa”, Salimu aliongea na kumuacha Meroda akitabasamu “Inaonekana nyinyi wawili mlijuana muda mrefu eeh” Shalon aliongea na kutabasamu Salimu na Meroda wakatazamana “Sijui ingekuaje kama isingekuwa udugu?”

Shalon aliongea tena “Huenda tusingefahamiana, Waislamu dunia nzima wanaamini kuwa hakuna jambo linalofanywa bila idhini ya Allah Subhanahu wataala tofauti na hapo haiwezekani, na kila jambo hutokea kwa sababu na wala sio bahati mbaya” aliongea Salimu Shalon akanyanyua uso kumtazama kaka yake na kutabasamu “Ahh tuache hii mada tafadhari” aliongea Meroda” wote wakatabasamu. “Basi tufanye umpeleke mapema dada ako siunajua kesho sio mbali na jioni hii anahitaji muda wa mazoezi” meroda aliongea “Nikweli Kwa ajili ya familia na mafanikio” wote wakagongeshana glass zao.

Ndugu msomaji najua mengi unajifunza kupitia Riwaya hi ya the Hidden Truth, bila Shaka tunaendelea kuamini Mambo mengi nakuyawekea kipaumbele, usisite kumkaribisha jiran, rafiki ndugu yako kizuri kula na nduguyo.

Tumeona Siri nyingi zinazo shabiiyana na maisha halisi ya yeyote yule kokote kule duniani Kama yalivyoweza wakuta wahusika pendwa hawa

Salimu (Pius) kuzaliwa kwake mpaka leo
Karimu ( ndugu wa hiyali)
Meroda na timu yake ( ualifu mpaka kutetea haki)
Shalon ( Mpenzi wa Salimu mpaka Kaka)
Samuel na Peter (Marafiki mpaka Uadui dhidi ya Richard

Na ukaweza waelezea uwezavyo

Lakini Kuna Hawa tusiowaelewa

Komando Ochola na jopo lake
Swai na jopo lake
Richard
Mzee Habib
Jumaa
Familia ya Mchungaji Johnson
Waziri wa Mambo ya nje ( Kurasa za mwanzo)
Mh Rais wa zamani
Mh Rais wa Sasa

Hawa wote wanasiri zinazounda Hidden Truth hatujui itakuwaje japo mzunguko unaonekana kwenda kuisha Hatujui itakuwaje

Endelea kufatilia na usisite kushauri na kutoa mawazo

Asante Sana kwa muda wako

Ni Mimi mtunzi wako chipukizi

Akida Siri Rambao.
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 4

Sehemu 12 F: Ahadi ILIYOTIMIA

Ilipoishia

ala sio bahati mbaya” aliongea Salimu Shalon akanyanyua uso kumtazama kaka yake na kutabasamu “Ahh tuache hii mada tafadhari” aliongea Meroda” wote wakatabasamu. “Basi tufanye umpeleke mapema dada ako siunajua kesho sio mbali na jioni hii anahitaji muda wa mazoezi” meroda aliongea “Nikweli Kwa ajili ya familia na mafanikio” wote wakagongeshana glass zao.

Tuendelee...
Central Polis Station, Kinondoni- Dar es Salam
“Jambo mkuu” Salamu hiyo ilitolewa baada ya Saluti kupigwa kikakamavu na kijana mtanashati aliyevalia mavazi ya kiraia ndani ya ofisi dakika chache baada ya kuruhisiwa kuingia, “Jambo”, IGP Lugole aliitika na kuacha kuandika kile alichokuwa akiindika katika kitabu kidogo cha kumbukumbu.“Ndio lete riport” aliongea “Kila kitu kimeenda kama ulivyotuelekeza na Muheshimiwa yupo katika chumba maalumu hapa kituoni, lakini kuna jambo moja waandishi wahabari wamejaaa wanahitaji kukutana na wewe nasubiri ruhusa yako Kamanda” aliongea kwa utii “Hebu nisubiri nje mara moja nitakuita” Kijana kwa heshima akageuka akapiga saluti na kutoka Inspekta Jenerali akachukua simu binafsi toka mezani akatafuta namba na kupiga kisha akasikilizia sikioni “…Habari…ndio Ochola teyari yupo chini ya ulinzi….ndio…haya sawa haina shida nitawaita ofisini kwangu…asante” alikata simu na kupiga simu ya mezani.

“…tafadhari naomba umwambie afande Chonya awakaribishe waandishi wa Habari ofisini kwangu tafadhari”. Waandishi wa Habari waliingia na kuweka sawa mitambo yao tayari kwa mahujiano na Kamanda Mkuu wa jeshi la polisi “ Kwanza kabisa bila kupoteza muda napenda kutoa taarifa rasmi kwa kukamatwa na Muheshimiwa Samuel asubuhi ya leo nyumbani kwake maeneo ya Bunju kwa tuhuma za Mauaji ya familia ya Muheshimiwa Richard yaliyotokea takribani miaka ishirini na ushee iliyopita.” Inspekta Jenerali Lugole aliongea kisha akaweka vizuri miwani yake na kuwatazama waandishi wa habari ambao walikuwa wapo kimya wakifatilia taarifa hiyo huku wakiwa bize kunukuu na kushikilia vinasa sauti vyao walivyovielekeza mbele ya Kamanda Mkuu.

“…nitukio la kushtusha sana na kutetemesha hisia za kila mmoja wetu hapa na jamii nzima lakini naomba wananchi wote mlichukulie kuwa ni tukio la kawaida tu maana mtu yoyote pahala kokote bila kujali hadhi ya mtu na muda unaweza kutiwa kizuizini kutokana na kosa au makosa ya jinai yanayokuandama kama tu ukionekana ni mtuhumiwa.” Lugole akatulia kidogo akiwatazama waandishi wa habari akameza mate na kuendelea “Pia haimanishi kuwa Muheshimiwa ni mtu mbaya sana au mzuri sana hapana tunapaswa kukumbuka ni binadamu kama sisi anamatamanio ana maono na mambo mengi ila madai yake utetezi na ushahidi ndio utakao muweka huru na kumuweka mbali na tuhuma ambazo kwa sasa zina mkabiri yeye kama yeye, nimemaliza na siruhusu maswali kwa sasa” alimaliza kuongea na kufunga mjadala kwa kutaka waandishi wa habari kuondoka ofisini kwake.

Haikuwa rahisi sana kwa waandisi wa habari kuridhika kuondoka ofisini humo bila kuridhika ilikuwa ni mtafutane wakiuliza maswali mfululizo tena yenye uzito mkubwa sana, lakini Kamanda alisimamia amuzi lake, ni kwa msaada tu wa polisi kuwaondoa na kuwazuia waandishi wa Habari ofisini humo kuendelea kuwa wabishi baada ya takribani nusu saa ambazo waligoma kabisa kutoka kwa hiyari yao ndipo nguvu na vitisho zilitumika na kuwatawanya bila kuwajeruhi ndipo wakaondoka kwa vinyongo. Akiwa bado yupo ofisini akijiwazia…simu yake ikaita akatupia macho “Namba ngeni! nani tena?” akachukua na kupokea “Hallow…Ndio Muheshimiwa…ni maelekezo tu niliyoyapata na mimi nikatekeleza…ndio Binti mwenyewe alikuja ofisini nakutoa malalamiko…hapana muheshimiwa nisamee sikulifikiria hilo nilifanya wajibu wangu kwanza…walimuacha nyumbani ndio yupokizuizini…okay”

akaitoa simu sikioni “Mbona hapa kama kuna kitu sikielewi inakuwaje Muheshimiwa ananikaripia kama mtoto kiasi hiki tangu lini mtoa malalamiko akawekwa kizuizini sheria ya wapi hii” alijiongelea mara simu ikaita tena “Ndio Muheshimiwa…hapana mimi nafanya kazi yangu hivyo mnapo nihoji maswali ambayo kwa sasa sina majibu nayo mnakuwa kama mnanionea kwani sheria si ipo na ina kanuni zake” Simu ikakatwa “Haaa hawa watu vipi…ni washirika nini” alijiongelea mwenyewe.

****
Baada ya ya nusu saa kupita, Nchi nzima ilizizima Kwa habari iliyotetemesha mioyo ya watu kutokana na tarifa ilyotolewa Live katika baadhi ya vyombo vya habari kama taarifa muhimu ya dharura na walio sikia nao wakawasimulia wengine na kusimuliana, ikawa ndio habari ya mjini. Tuhuma ya mauaji ya familia ya Richard iliyoteketezwa na moto takribani miaka ishirirni iliyopita ndiyo iliyokuwa inamkabiri Samuel wakati huo, kila aliyekuwa katika zama zile alishtuka na kuziba mdomo na kuachwa midomo wazi pia taarifa ya kuwepo hai kwa mtoto pekee wa Muheshimiwa Richard nayo kwa uzito wake iliamsha hisia mpya na zilizo lala kwa mikutano iliyojengwa na vikundi katika sehemu zote za shughiuli za kijamii.

*****

Itaendeleaa....
 
Mambo yaliingiliana Sasa tutaungana soon
 
Hii hadithi mpaka nimeshasahau mtiririko wake. Itabidi ikianza kurushwa nianzie nyuma ya ilipoishia🤔
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom