Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Story: The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)

Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Ilipoishia...

Sauti hizo zilipelekea kuupamba usiku huo uliokosa mbalamwezi na kuwa na giza totoro kuwatoa upweke na wasiwasi na kuwa fanya wasichana hao kuendelea kupamba moto na tumaini la kutoka salama.

Tuendelee...
Makomandoo hao wakike kwa haraka bila maongezi wakatokomoea na kutokomoea zaidi mbali kabisa wakiacha eneo la makao makuu likiwa nyuma mbali huku mioyo yao ikiwa na furaha ya kuondokana na utumwa wa maasi.

Mabegi yakijeshi yakiwa mgongoni, viatu miguuni vyenye soli ngumu visivyoingiza aina yoyote ya ncha kali pamoja na suruali zao ngumu nyeusi vifuani wakiwana mashati magumu ya mikono mirefu kuzuia mikwaruzo ya hapa na pale ndivyo viwalo vilivyo hefadhi miili yao usiku huo. Safari iliwachukua muda mrefu baada ya heka khamsini kwisha walikutana na chaka kubwa lisilojulikana ukubwa wake hivyo matembezi ya mchaka mchaka chinja yaliwachukua karibu saa moja na nusu baada ya yale mawili waliyoyapoteza wakivuka mashamba ya bhangi wakiwabado ndani ya milki ya kambi. Hatimaye wakakutana na ukuta mrefu sana, wote wakatabasamu na kuona mwanga wa tumaini la kutokomea kabisa pasina kujulikana kabisa.

Haraka haraka bila kulemba kila mmoja akatoa kamba ngumu ya manira spesho kabisa ianayotumiwa na wanajeshi maalumu katika kupandia na kuvuka sehemu za hatari. Kila mmoja alichukua nanga ndogo ya kupandia milima na sehemu zingine za juu na kuifunga vizuri tayari kwa matumizi. Kila mmoja akarudi hatua kazaa nyuma na kuirusha kwa ustadi kamba yenye kichwa cha nanga upande wa pili wa ukuta kisha wakazivuta kuweka kikwazo na kuona zimeshakamana sawa sawa haraka wakaaanza kukwea kwenda juu pasina kuongea kitu na walipo fika juu ya ukuta wenye upana wa futi mbili sasa wakaanza kuandaaa namna ya kushuka ambapo zoezi halikuwa refu wakafanikiwa.

Wakaanza kukusanaya vitu na kutia katika mabegi na mchaka mchaka wa kukimbia hatua fupi fupi ukaanza. Safari iliwachukua tena masaa mawili mengine na nusu hivi bado wakiwa katikapoli wakipanda na kushuka milima kwa tabu lakini hawakujari. Bado dalili ya kukutana na nyumba za watu hazikuonekana lakini hawakujari hilo wawo mbele kwa mbele. Ilikuwa teyari ishafika saa tisa za usiku wasichana sasa wakiwa vichakani bila mazungumzo.

Hatimaye baada ya mwendo mwengine wa lisaa limoja wakakutana na barabara ya rami ambayo walionekana kuitambua maana hakuna aliyeonesha uso wa mshangao zaidi ya kurudi tena vichakani wakielekea upande wa magharibi.

Baada ya dakika ishirini tu za matembezi ya kawaida kwa mbali ulionekana mji mdogo, walichokifanya kwanza ni kubadirisha nguo na kuvaa mavazi ya kawaida kisha wakachukua vitu vya msingi ikiwemo fedha za kutosha na kisha mabegi wakayatelekeza yakiwa na zana zile kichakani hao wakajitokeza katika changanyikeni bila kujulikana na mtu yeyote yule. “Habari kaka tunahitaji usafiri wa kutufikisha Mombo”, Monica aliongea huku akiliegemea gari hilo la rangi ya kijivu mojawapo ya magari yaliyokuwa yameegeshwa pembeni ya mgahawa mkubwa wa mmachame mmoja aliyefahamika kwa jina la Mushi “ohh mtaiweza bei mabinti?...”

bwana huyo aliyekuwa amesimama akiligonga gonga gari lake kwa vidole aliwajibu hukua akiwatazama kwa macho ya matamanio, kabla hajajibiwa akaedelea “usiku huu mtanipa elfu khamsini kila mmoja la sivo msubiri magari asubuhi” alimaliza kuongea safari hii jicho la tama ya ngono lili ganda katika kifua cha Monica kilichokuwa kikionesha matiti yake yaliyo jaa. Monica wala hakujali akavuta mkoba wake uliokuwa kwapani na kuufungua. Kwa macho ya wizi dereva wa taxi aliona maburungutu ya pesa yaliyomfanya ashtuke, monica akatoa kiasi na kumpatia. Dereva akazipokea na kuzihesabu laki moja na nusu keshi na kutabasamu hukua kiwaonesha kwa ishara kupanda garini.

Itaendeleaa...
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com

MSIMU 3

Ilipoishia....
Dereva akazipokea na kuzihesabu laki moja na nusu keshi na kutabasamu hukua kiwaonesha kwa ishara kupanda garini.


Tuendelee....
Baada ya mwendo wa dakika tano tu dereva akaitoa simu yake ya mkononi na kumtazama Meroda aliyeonekana hana mpango naye, mwendo wa gari ulibadilika na kuwa wa kawaida baada ya mtu wa pili kupokea simu. Mazungumzo yao yaliegemea zaidi katika lugha ya kibantu aliongea huku akigeuka kuwatazama abiria wake.

Baada ya kumaliza tu aliirudisha simu yake mfukoni kabla hajarudisha mkono katika usukani Meroda akamvaa dereva na kumgongesha kichwa katika usukani “….mpumbavu sisi sio wanawake wa mchezo?” Meroda aliongea na kuwahi usukani maana gari lilishaanza kupoteza muelekeo na kuyumba yumba katika mteremko juu ya mlima ikifata njia ya kuelekea Mombo usiku huo na hatimaye akafanikiwa kuipaki pembeni. “Wajinga sana, wanaume wengine wajinga sana wanawachukulia wanawake ni dhaifu sana, kama wengine hapa teyali wangebakwa na kuibiwa eti anabadili lugha huyu mshenzi eehh”.

Meroda huku akihema aliongea kwa tabu akiwaacha wenzake kumtazama kwa mshangao maana hawakutarajia kukutana na tukio hilo nay eye alionekana kuchukia sana. Dereva akiwa amepasuka sehemu ya juu ya paji la uso na kupelekea kuvuja damu alibebwa mzobe zobe baada ya Meroda kutoa amri huku akiwa hajijui hajitambui katikati ya safari isiyo na dalili ya gari hata moja. Safari yakei iliishia katika sehemu ya nyuma ya taxi hiyo ambapo buti la gari lilikuwa wazi akadumbukizwa ndani yake. Sasa Meroda akachukua nafasi ya dereva na kuitoa gari eneo hilo la egesho la dharura mkuku mkuku akiongoza njia ya moro dar .

Giza sasa lilionekana kuaga maana alfajiri ilianza kuonekana na wao teyari walishaingia mjini Meroda akatafuta sehemu tulivu na kuamua kuliegesha gari huku akiwa na macho makini ya kujihami. Kwa taratibu bila haraka wala pupa walichomoka garini na kuondoka wakiliacha gari hilo pembezoni mwa barabara ya vumbi iliyopakan na nyumba za watu. Safari yao ilikuwa ni ya mguu wakipandisha barabara moja Meroda akiwa mbele wenzake nyuma wakimfata pasina kuongea. Walitembea hadi katika moja ya Hotel iliyokuwa karibu kabisa na uzio wa stand kuu ya mabasi Morogoro. Baaadaya kuhudumiwa na kuchukua chumba cha double.

Walifanya mapumziko mafupi, wakajiswafi maliwatoni. Majira ya saa moja na nusu wakatoka chumbani wakiwa wapya kabisa baada ya kujipodoa na kubadili nguo na hata kubadilisha mtindo wa nywele kwa kweli walipendeza sana.

Safari yao iliishia kwenye basi la magari yaendayo Tanga, Samira akachapuka na kumsogelea konda hakuchukua muda akaonekana akitoa kiasi cha pesa na kupatiwa tiketi tatu kwa mbali akawaoneshea ishara wenzake kuwa wamfate kisha akatangulia garini.
Mkusanyiko mkubwa wa watu uliendelea kuongezeka kulizunguka gari wakiminyana lakini wakanza kupanguka kuwapisha mapolisi waliowasili eneo hilo.

Mara asakli aliyewasili eneo hilo alionekana akiongea na redio call dakika kumi pekee polisi wengine wakawasili na kuanza kufanya taratibu za kichunguzi huku gari maalumu ya mslaaba mwekundu ilifika na kubeba mwili awa laiyefahamika kuwa ndiye dereva wa gari hilo. Na kisha taratibu za kimahojiano na baadhi ya wananchi zilifanyika.

Itaendeleaa...
 
Kesho Mungu akipenda tutaingia MSIMU 4 tunaenda maliza Riwaya yetu
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Email akidasiri@gmail.com
Contact 0658328596


MSIMU WA NNE

SEHEMU 12A: AHADI ILIYOTIMIA

Dondoo:

“Kishingo upande Meroda anakubali Salimu atoke kimapenzi na Shalon kama sehemu ya kukamilisha sehemu ya kazi ya kumkamata Samuel, kisha kuivamia ngome ya Magamba na kuisambaratisha, lakini moyoni mwa Salimu anapata uzito kuliendea zoezi hilo gumu anamvisha pete ya uchumba Shalon na kupanga kukutana na Samuel baba wa Shalon uso kwa uso kumchumbia Shalon je! Salimu ataweza kuvumilia hali hiyo na vipi kama Shalon akigundua kuwa anachezewa hisia zake itakuwaje?”

Tuanze....

Meroda muda wote alikuwa amempa mgongo Salimu akilia kimya kimya huku mikono akiwa kaikusanya kifuani, kisha akaongea “Ni sawa mi nimekubalina na wazo hilo japo linauma sana kwa upande wangu Salimu na ndomana umeniona niliamua kunyanyuka baada ya kuwa nimeshindwa kuvumilia ile hali niliyokuwa najisikia pale kwenye mazungumzo” aliongea Meroda kisha akaendelea kuongea “Imeniuma lakini nitafanyaje na nimekupenda mwenyewe” aliongea tena Meroda kwa masikitiko “Please I know my love, wacha haitachukua muda mrefu niombee hilo nakuhakikishia”

Salimu aliongea huku akimshika mabega kisha akamkumbatia Merodaa na kumkisi mashavuni, Kumbatio lilichukua dakika mbili nzima huku Meroda akilia kwa kwiki sasa akiwa amegeuka akimtazama, “Mpenzi nimekubali, naomba uwe makini sana haya tuondoke mahala hapa” aliongea Meroda kwa kujiamini huku akifuta sehemu ya machozi iliyo salia machoni
Mlango ukafunguliwa na Meroda akawa wa kwanza kuingi akifatiwa na Salimu huku akiwa na uso wa bashasha akavuta kiti na kukaa huku

“Napenda kusema kuwa nimekubali kwa moyo mmoja sina kipingamizi tena” Meroda aliongea huku akitabasamu “ Vizuri binti, na asante kwa hilo, kwa hiyo hapa ni kumtumia Shalon kama daraja la kumkamata baba yake kwanza kisha ni kuivamia kambi ya Magamba mara moja naamini Pater atakuwa amechanganyikiwa sana wakati huo hivyo atakamatwa kirahisi nafikiri tumemaliza a kuna la ziada?”

aliuliza Komandooo Ochola huku akipitisha macho ya ukaguzi kwa kila mmoja, “Kimya kinamaanisha tuko pamoja na tumeleelewana basi tutawanike” aliongea tena na kuwa wa kwanza kunyanyuka.

Sand Beach, Kunduchi –Dar es Salam
Glass ilishushwa mezani taratibu huku mkono ukiwa bado umeshikilia, macho yakiwa kwenye makuti ya mnazi kiupepo cha baridi kikimkabiri kumburudisha ‘Mbona imekuwa ngumu sana kufanya jambo hili, inakuwaje nifanye hivi lakini’ mara alionekana msichana akiweka kiti vizuri na kukaa mbele yake, “Habari mpenzi pole kwa kukuweka muda mrefu sana”, Salimu akiwa kainamisha kichwa aligutuka katika dimbwi la mawazo “Ohh Shalon umefika? Samahani sijakusikia pole sana” Shalon kwa makini alibaki kumtazama tu Salimu,

“Hivi upo sawa lakini? Unaumwaa nikupeleke Hospital?!” aliongea Shalon akiwa na wasiwasi “Ahh usijari uchovu tu wa hapa na pale mambo ya kazi lakini wala usiwe na mashaka juu ya hilo nitarecover soon” “Ohh sawa itakuwa vizuri” Shalon akatabasamu kisha kwa ishara alimuita muhudumu aliyekuwa akipita mita kazaa katika meza zingine kuulizia huduma, akafika apewa mahitaji nakuondoka “Nimefurahi kupata mlo wa mchana pamoja na wewe baada ya miaka mingi, haya nambie vipi umeniitia nini hapa leo?”

aliuliza Shalon akimkazia macho Salimu akauma meno na kutoa tabasamu hafifu, “…unanichukia sana siku hizi eehh?...najua lakini usiwe na wasiwasi nimekuja kwa ajili yako Shalon” aliongea Salimu na kumfanya Shalon atazame pembeni kwa dharau “Hivi unamaanisha nini Salimu sijapata kukuelewa mwanaume wewe unayecheza na hisia zangu kila uchwao” Shalon aliongea huku akimkazia macho Salimu akimaanisha akisemacho.

Salimu akasogeza mkono wake na kushika kiganja cha Shalon kilichokuwa kimegeshwa mezani “Nina Surprise kwa ajili yako leo” Salimu akalitoa tabasamu wakati Shalon akiwa na hasira “Sijakuelewa hebu nyoosha mambo” aliongea Shalon, Salimu aliingiza mkono katika mfuko wa koti lake la suti na kutoa kibox kidogo cha rangi nyekundu “…will you marry me” “Whaaaat” Shalon macho yalimtoka akaziba mdomo wake aliuacha wazi kwa mshangao “Shalon will you marry me?” “Ohh…I…I…I WIL…AHH… I WILL MY LOVE” Shalon aliongea macho yakitandwa na wingu lamachozi asiamini macho yake akishuhudia pete yenye kito cha almasi ikiingia katika kidole cha uchumba kiganjani mwake

“…haiwezekani haiwezekani hivi naota au ni kweli Salimu wangu?” aliongea kwa sauti ya kutetemeka na kuto jiamini huku akiziba midomo yake tena kwa mkono wa kulia machozi yakimtoka. Salimu akatabasamu “Yea ni kweli tupu Shalon nimedhamiria” ‘Dahh pole sana Shalon naingia katika maisha yako kimakosa naamini nitakuumiza zaidi ya neno kuumiza siku utakayokuja kujua ukweli wangu kuwa sijawahi kukupenda kimapenzi zaidi ya urafiki, niko kazini Shalon samahani sana’ Salimu alijiwazia kisha akalitoa tabasamu la kulazimisha huku akishuhudia furaha ya Shalon “Ni siku ambayo nilikuwa nikiiota miaka,

muda mrefu Salimu I will I will Salim nipo tayari” machozi ya furaha yaliendelea kumwagika kwa furaha kiasi cha kuwashangaza watu walio kaa meza za jirani na kubaki wakimtazama na kupiga makofi baada ya kugundua kinachoendelea.

Muhudumu alifika na vyakula na kuvisambaza mezani kisha kwa heshima akawakaribisha wateja hao. “Ni kweli nilikuwaza na hamu sana ya kula mpenzi pia nilikuwa na hasira sana juu yako lakini sasa najihisi kushiba pia sina kinyongo nawe kabisa.”

Aliongea Shalon kwa furaha Salimu akaaishia kutabasamu. “Naona muda umetutupa mkono sana naweza kukupeleka nyumbani kwa gari yangu?..” aliongea Salimu “Bira shaka kwanini usifanye…Mpenzi tumeongea sana leo na tumekaa pamoja kuliko siku zote natumaini tutakuwa karibu zaidi siku zijazo” aliongea Karimu Wakanyanyuka,

wakashikana mikono na kuondoka eneo hilo kuelekea nje baada ya kupitia sehemu ya malipo, Shalon akaegesha kichwa begani mwa Salimu hao taratibu hadi kwenye maegesho ya magari. “Sorry nitapanda gari nyingine unaweza tangulia au kukaa nyuma yetu tafadhari” Shalon aliongea “Dada vipi kuhusu usalama wako” Shalon aligeuka huku akiwa kakunja sura “Tafadhari shika maneno yangu usinikere huyu ni usalama tosha” aliongea tena Shalon Dereva akainama kwa heshima na kuridi garini

Itaendeleaa....
 
Aisee mkuu! Salim anatisha ila Meroda nae jembe kuruhusu mwiko ukatumike na Shalom duh!!

Tunafuatilia hatua kwa hatua mkuu kazi nzuri Sana
 
The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact 0658328596

MSIMU 4

Sehemu 12 B: Ahadi ILIYOTIMIA

Ilipoishia...

....Tafadhari shika maneno yangu usinikere huyu ni usalama tosha” aliongea tena Shalon Dereva akainama kwa heshima na kuridi....


Tuendelee...
Bunju, Kinondoni-Dar es Salam
Salimu alitoka na kumfungulia mlango Shalon “Ohhh asante mfalme wangu” “Karibu tena malkia” Shalon akatoka kisha akamkumbatia Salimu na kumsindikiza kwa kumpiga busu takatifu mdomoni bila kujali chochote, “Nakupenda sana Salimu” aliongea kwa sauti ya mnong’ono sikioni mwa Salimu “… nakupenda zaidi Shalon wangu…lakini…sijawahi fikiria kuwa wewe unatokea kwenye familia tajiri kiasi hikii” Salimu alimtazama Shalon na kugeuza shingo kutazama mazingira akiwa katika kumbatio “Najua, usiwe na wasi kwa kuwa umeshakuwa wangu tutaongea kila kitu ….shiiii” Shalon akamnyamazisha Salimu aliyetaka kusema kitu. “Tafadhari kama nilivyokwambia kesho itabidi uje bira kukosa ukutane na baba itakuwa surprise kwako lakini usijali mpenzi wangu,” Shalon alimaliza kuongea na kumuacha Salimu akitazama vizuri mazingira kisha akaingia katika gari iliyokuwa na dereva wake geti likafunguliwa na wao wakaingia na kumuacha Salimu nje ya Uzio naye akatimua zake.

Kawe, Kinondoni-Dar es Salam
Salimu akiwa amejikalia kitini kifua wazi bukta tu kiunoni mwenyewe tu ofisini nyusoni alionekana fika ni mtu aliyejawa wasiwasi na mashaka makubwa. Dakika tano zilipopita akanyanyuka kama mtu aliyegutuka mara akakaa tena macho yakaangukia kifaa kidogo cha ukubwa wa nusu nchi ni Mini spy hidden Camera mkono ulikisogelea na kukishika akakisugua sugua na kukiangalia mara kazaa mwishowe akanyanyuka na kukichomeka kwenye USB HD kisha baada ya kukaa vizuri akaichomeka katika Computer na kuplay, yalikuwa mazungumzo kati yake na Shalon kuanzia mwanzo wa makutano,

akiwa katika kusikiliza alijivuta kwa kutumia kiti chake chaa matairi hadi katika sehemu alipo iweka miwani aliyokuwa amevaa siku hiyo aliigeuza na kutoa memory card katika ubavu wa mkono wa miwani hiyo na kuiweka katika USB HD ndogo kisha kuchomeka katika Computer yake “ Kahawa yako hii yapa mzee” Karimu aliingia na kukiweka kikombe cha kahawa katika meza, bira kujibiwa, “Shukrani sana…Vipi maendeleo huko uliko toka” Karimu akajiegemeza katika meza akimtazama Salimu kwa mbele mkononi akiwa na kikombe cha kahawa “Acha tu mzee mtoto amefurahi sana lakini binafsi sijajiskia vizuri kabisa kwa kitendo hiki ninachoendelea kukifanya ni maumivu pekee atakayokuwa nayo siku atakapotambua kuwa namtumia bure tu sina mapenzi…naenda kumfunga baba yake” Salimu kwa uchungu, Karimu akabaki kumtazama huku akionesha uso wa huruma,

“Kaka hii ndiyo kazi tuliyoichagua mzee hatuna jinsi haina baba mama wala mpenzi kazi hii”, Salimu kwa muda akajiwazia kisha akaendelea na kile alichokuwa akikifanya, “Hizi ni picha nilizopiga kupita grass camera kama unavyoona kuna askari wa kutosha katika eneo zima jengo kama unavyoliona mfano wa kasri hawa jamaa wana hera mzee” aliongea Salimu

“Vizuri sana naona kuna kamera pia ya getini hapo au siooni vizuri?” aliongea Karimu “Yenyewe mzee” aliongea Salimu “…basi kaa ukijua kuwa habari zako zipo mikononi kwa baba mkwe Mzee Samuel muda huu” “Yea ni kweli, ngoja niwatumie kina Jeff makao makuu habari hizi wazifikishe kwa Ochola, kisha tuongelee kuhusu safari yako ya Lushoto kiundani” aliongea Salimu huku akiendelea na kazi aliyokuwa akifanya. “Lakini Uliniambia kuwa umealikwa na baba ako mkwe sio” Karimu aliongea akiwa bado kasimama mkononi kashikilia kikombe “Ohh ni kweli aisee mamabo mengi nitaanda kesho asubuhi kumtembelea hivo japo nina wasiwasi sana mzee” aliongea Salimu na kujishika kichwa “Najua lakini nikupiga moyo kunde tu na kufumba macho yatapita tu” aliongea Karimu na kumsika bega ndugu yake kisha akatoka chumbani humo.

Itaendeleaa...
IMG-20210318-WA0019.jpg
 
The Hidden Truth Ukweli Uliofichika
Mtunzi Akida Siri Rambao
Contact 658318596

MSIMU 4

Sehemu 12 C : Ahadi ILIYOTIMIA

Ilipoishia.....

Salimu na kujishika kichwa “Najua lakini nikupiga moyo kunde tu na kufumba macho yatapita tu” aliongea Karimu na kumsika bega ndugu yake kisha akatoka chumbani humo

Tuendelee...
Bunju, Kinondoni- Dar es Salam
Ndani Shalon alionekana akiwa anazunguka zunguka kama mtu aliyechanganyikiwa kila saa akitazama saa yake ya mkononi huku akiwa ameshikilia gazeti chakavu, huku Samuel akiwa anapata kifungua kinywa katika mahala maalumu kwa chakula mara kazaa akimrushia macho mwanawe na asielewe amepatwa na nini. Taratibu alinyanyuka kisha kajifuta midomo yake na kuanza kumfata mwanawe alipo “…Binti yangu kuna nini teyari kuna mtu amekukera nambie sema binti yangu” aliongea Mzee Samuel akiendelea kumsogelea “…ili ukafanye mauaji si ndio?” aliongea Shalon “Samuel ghafla akasimama kwa mshtuko wa sentensi aliyoisikia na akaongea “…umesemaje?” “…acha maaigizo yasiyo kwisha baba siamini Kama mtu kama wewe mwenye heshima yako bado hujatubu tu kwa mauaji ya watu wa familia ya Richard? Unaedelea na uchafu ukijifunika ngozi ya kondoo wakati ni chui” Shalon aliongea kwa hasira bila hofu tena bila kituo. “Hee we mtoto nani kakupa habari hizi?” aliongea Mzee Samuel kwa hamaki akitazama huku na kule kwa wasiwasi “Tatizo lako unafikiri ulifukia kila kitu ardhini ulisahau ukweli hauozi wewe na washirika wako mlisahau kuwa hata ipite miaka alfu ipo siku moja haki itasimama baada ya siri kufichuka” aliongea Shalon, Samuel akiwa amebaki mdomo wazi hasira zikampanda “Kwa hiyo leo ndio umeamua kunioneshea kiburi cha mama yako eeh unataka na wewe nikuulie mbali sio sasa kwa taarifa yako huna lolote la kunitisha nasiogopi chochote sawa? Ndio nimefanya unaushahidi gani na hakuna mtu wa kutusumbua katika hilo, yani baada ya miaka mingi unataka kuniparura na vijikucha vyako dhaifu” Samuel aliongea mfululizo kwa sauti ya juu macho yakiwa mekundu kwa hasira akatoa bunduki wakati huo wafanyakazi walikuwa wamejificha wakiogopa kadhia ya baba na mama “Sikiliza utaozea jela nakwambia” Shalon aliongea bila uwoga akilia kwa uchungu bunduki ikiwa imeelekezewa kwake “Niuue na mimi nika pumzikeee tu kama wazazi wangu”

Mzee Samuel alipatwa na bumbuazi asiamini anachokishuhudia mbele yake akiwa ameshikilia bastola aliyoitoa katika mfuko wa koti lake muda mfupi uliopita akimuelekezea Shalon ambaye alikuwa akilia kwa machungu juu ya yale yaliyouumiza nafsi yake, “Weka siraha yako chini haraka sana Muheshimiwa” Mmoja ya askali aliyevalia mavazi ya kikosi maalumu akiwa ameshikilia bunduki yake kikakamavu huku timu ikiendelea kuingia haraka haraka ndani hapo. Ilikuwa kama jambo la kufumba na kufumbua tu hivi kama ndoto machoni mwa Samuel aliikuta mikono yake ikiwa nyuma ya kiuno imeshikiliwa na pingu zilizomkabili akiwatazama watu wanaongea lakini asielewe wanamaanisha nini namna alivyoingiwa na hofu ya moyo kiasi cha masikio kuziba kwa mshtuko. Nje ya nyumba palikuwa hapatamaniki kwa idadi ya polisi waliofurika tayari huku polisi wake walinzi wakiwa chini ya ulinzi wasijue kumetokea nini. Macho yake madogo yaliweza kujionea kila kitu kwa ufasaha maana hayakuwa yamepoteza nguvu kwa mshtuko.

Waandishi wa habari walikuwa wakiingia getini wakikimbizana kama watu wanaowahi mpira wa ushindi wakizuiwa na maaskali ambao waliweka ulinzi juu ya Mzee Samuel wakielekezea maiki zao. Waandishi wa habari walijitahidi kuomba wasaa wa kuulizia juu ya mtafaruku na sababu ya kukamatwa kwa Muheshimiwa huyo akiwa nyumbani kwake lakini walikosa ushirikiano na wakaishia kutazama gari ikimchukua na kuondoka nae huku wakisindikizwa na magari yaliyo beba askari makini, ilikuwa operation ya kushtukiza.

MASAA 24 YALIYOPITA

Bunju, Kinondoni-Dar es Salam
Ndani Salimu akiwa mchangamfu aliendelea kuburudishwa na kinywaji kilichokuwa kikombeni mkononi mwake akionekana nadhifu sana akitazama huku na kule thamani zilizoipamba sebure kubwa ya aina yake “Mpenzi usijali haitachukua muda na baba atapendezwa sana na wewe na amini hilo” Shalon akiwa katika sofa moja na Salimu aliongea kwa sauti ya chini yenye hisia za mahaba ya kutosha na kujichekesha chekesha. Shalon aliongea na kutabasamu.

“Hakuna shida mpenzi wangu nitasubiri tu” aliongea Salimu “Baba huyo anakuja” Kwa sauti ya kunong’ona Shalon aliongea na kumuacha Salimu kunyanyua macho yake kumtazama Mzee Samuel akishuka ngazi toka ghorofani toka juu katika hali isiyo ya kawaida Salimu alijikuta kupatwa na hasira mwili ukaanza kumchemka na kuanza kubadirika sura kiasi cha kushuhudiwa na Shalon. “…vipi mpenzi unanini? Mbona! ” Salimu akagutuka “…hapana usijali ni wasiwasi tu wa kukutana na baba yako mpenzi” Salimu akajichekesha “Ohh karibu sana kijana karibu nyumbani nilipata habari zako siku nyingi sana toka kwa binti yangu kipenzi Shalon lakini sikupata fulsa ya kukutana nawe…vipi mmeshapata kifungua kinywa?” Mzee Samuel aliongea na kukaa katika sofa la jirani “Asante sana baba nimeshapata nilipotoka, nimefurahi kukutana nawe pia, najiona ni mtu mwenye bahati sana” aliongea Salimu huku akijikaza “ …ahhh hapana ni mambo ya kawaida tu utazoea”

Binti mrembo aliingia katikati ya mazungumzo akiwa kavalia sare chupa ya mvinyo ikiwa sahanini pamoja na glass akaweka karibu na alipo kaa Mzee Samuel akafungua na kumimina “Karibu baba” aliongea na kuondoka “Asante mwanangu…ndio kijana nimeambiwa na binti yangu kuwa unampenda sana umeshampatia pete ya uchumba na uko mbioni kumuoa ni kweli jambo hili?” Samuel aliongea na kuchukua glass ya mvinyo na kumtazama kwa makini sana kijana Salimu “Ni kweli baba nampenda sana Shalon na nimekuja rasmi kujitambulisha kwako” Salimu aliongea kwa kujiamini. “Vizuri haina haja ya kujua unafanya nini au ni nani katika shughuli gani na una kaa wapi kwa ngu hilo si
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom