Story: Money Penny ni nani lakini?!

Story: Money Penny ni nani lakini?!

B. AF LELA ULELA MSHIKAJI KUWA MSELA



Asubuhi nikaamshwa na Baba, we money penny jana mlinzi kaniambia umerudi saa 6 usiku ulikuwa wapi?!

Money Penny: nilienda kwenye sendoff baba si unajua nipo kwenye kamati, nikachelewa kurudi

Baba: wewe naona hatuelewani, nilikwambia sherehe zote aga mapema saa 4 uwe ndani

Money Penny: lakini baba jana saa 4 hata msosi hatujala. . Huoni kama unanionea na mie nimechanga laki 1 ni sawa na kuitupa barabarani
Lazima uongeze masaa ya kurudi maana haya ni mambo ya jamii, nisipohudhuria yangu nitadodewa

Baba: akanyamaza kwanza, haya mwisho saa 5 usiku

Money Penny : saa 6 daddy wangu eeh

Baba: wewe ni mtoto wa kike, kwangu hauingii saa 6 usiku na mlinzi asifungue ukija saa 6 na ukilala nje usirudi kwangu milele

Money Penny: na mkesha je?! Si unajua naendaga mkesha kanisani kumwomba Mungu huko tunamaliza saa 10 asbh inabidi tulale kanisani mpaka jua lichomoze

Baba: sasa kama unataka kushindana na mimi wewe rudi saa 6, Mungu mwombee hapa ndani, nenda kasali kanisani saa 4 mwisho, saa 6 nafunga geti langu... harusi mwisho saa 5 usiku uwe hapa ndani

Kama Mungu mpaka umkeshee ndio ajibu njoo kesha hapa chumbani, galagala weee si chumba chako, ilimradi usitupigie kelele tuliolala

Money Penny: sasa baba ukinifuga namna hii nitaolewa kweli?! Wenzangu wote wanaolewa baba zao wanawaacha huru, hapa nina miaka 24, sina hata mchumba, saa inagongaaaa sasa hivi naingia 30

Baba: kwaiyo ukirudi saa 6 usiku na kulala kanisani ndio utaolewa haraka?! Nyie walokole wajinga kabisa,

Alafu wewe mtoto, usinipande kichwani kabisa, hii ni nyumba yangu, kama nilivyosema sibadiliki huyo mwanaume anaetaka kukuoa aheshimu mawazo yangu la sivyo hakufai
Na umwambie boss wako kazini mwisho wa kuingia nyumbani kwa mzazi ni saa 4 usiku kwasababu ya foleni za kutoka mjini, ukichelewa utalala na mlinzi nje

Baba akaondoa asbh asbh keshafoka balaa, hapo namsaka mlinzi nimnyang'anye elfu 10 yangu, atakoma kwanza nimempania anamzunguka mzee anatembea na house girl tukiwa hatupo... shenzi kabisa!

Nikaona hili lishakuwa gundu kurudi home saa 4 usiku, dah mbona mapema sana, ina maana mimi disco Siendi tena au?!
Nikawasha simu nakuta sms za Taajiri zipo kama 10, baby ulifika salama, nakupigia haupatikani
Baby jaman nijibu basi, hata sijamaliza kusoma sms simu yake imeshaingia

Taajiri : baby za asbh vipi jana haukuniambia kama umefika
Umeamkaje mpenzi wangu, unajua jana umenidatisha sana na rire busu ra ghafla pare, yani mpaka nikasimamisha ghafla sasa mpaka kuja kumshusha mjombaa sio kitoto

Money Penny: hongera kwaiyo nani alikushushia

Taajiri: nirikunywa pombe nikarara

Money Penny: Aisee? Ivi Unanifanya mimi bwege sio?!

Taajiri: bwege kivipi tena?!

Money penny: Yani wewe na huyo rafkiako sijui nani si mlichukua chumba mkampiga dada wa watu mpaka akazimia,

Taajiri: nani mimi? hapana asee!

Money penny: kwani nani amepiga simu labda?!

Taajiri: hamna kitu kama hicho mpenzi

Money Penny: Sasa unataka nini kwangu labda?!

Taajiri: me nakupenda sana, ni vire jana haukunierewa nataka uwe mpenzi wangu wa maisha nikuoe tuwe na famiria, ivyo tu mpenzi, alafu
Leo nataka tuonane

Money Penny: umuoe nani na uonane na nani?! Me siolewi na vibabu

Taajiri: Ai wewe acha hizo jamaaani, nakuoa wewe mpenzi wangu?!

Money Penny: jana nimechelewa sana kurudi nyumbani kwasababu ya kushuhudia mechi zenu nyie 3, mzee kafoka leo kama Busta Rhymes anavyoimba Nimeambiwa hamna kutoka ndani weekend yotee

Taajiri: dah aya bwana pore, basi nitakupigia baadae kama vipi nije hapo nje kwenu tukae tuongee... nikuretee nini mpenzi wangu

Money Penny: kwetu hajagi mtu acha ujinga unataka kuniharibia kwa mzee alafu nifukuzwe sio?!

Taajiri: basi siji nitakuona j3 lunch time

Money Penny: usinichoshe, mama ananiita kwaheri... nikakata simu
Naanza kupanga na kupangua wapi nampata Edo anipe ubuyu wa Taajiri mara simu inaita kucheki shogangu KIDAWA

Kidawa: we mama upo wapi?!

Money Penny: nyumbani

Kidawa: nakuja hapo jiandae tutoke nina shida kali, kuna mtu nataka tumfumanie

Money Penny: eh haya njoo

Baada ya Lisa 1 akajaa, makelele kibao, nikamfungia chumbani

Kidawa: Yani penny yule bwana wangu anamwanamke mwengine afu me ananidanganya atanioa atanioa, jana nikaambiwa alikuwa serena na mwanamke

Money penny: nikashtuka mmh! Enhe sasa umeamuaje?!

Kidawa: nimetonywa yupo kigamboni southern sun hotel na mwanamke, fanya fasta twende

Nikaulamba utamu na kujiweka ma makeup kwa juu juu, totoz naenda beach, kigamboni mojaaa, njiani nikamcheki Edo, naelekea southern sun kigamboni njoo basi nipo na shogangu Kidawa

Edo: poa nitakuja saa 10 jioni

Kufika eneo la tukio watu kibaooo, nikavaa sun glasses zangu na mtandio kama dada wa kiislam, chini skinny jeans na kitop na flip flops, nipo kibichi zaidi

Tukazuga na vinywaji nipo na juice ya maembe, Kidawa ana spot huku na kule haoni mwizi wake, akaenda kuongea na receptionist anamwulizia bwana wake, mimi nimekaa zangu na juice ya embe

Mara Edo ananipigia; we mama ndio unaekunywa juice ya maembe umevaa mtandio mweusi?!

Money Penny: nikashtuka, huyu dogo mwanga au?! Nikamjibu hapana we uko wapi kwani?

Edo; mimi nakuona hapa, wewe endelea kukaa hapo hapo utanielewa kauli yangu ya jana

Money Penny: nikachoka, kuna nini leo mbona nishaanza kuogopa? !

Mara naona anaingia Taajiri na demu mwengine! Nyuma ya Taajiri yupo Mshefa na demu mwengine, nikachokaaa! Like what the *** is going on?!

Mara namwona Shoga Kidawa anamfuata Taajiri kamrukia na kumkaba shingoni anampiga mangumi anamng'ata kichwani kha!

Mshefa anaamulia pale Kidawa amemkamatia shingo sio kitoto
Taajiri wa watu kama anataka kufa sio kwa kukabwa kule wakajaa watu pale wanamulia, mimi narekodi kwenye simu yangu tukio zima

Akaja sijui ndio hotel manager akawaweka sawa na ma security wa hotel wakawaachanisha wakawekwa pembeni, me nikasogea sogea lakini sitaki kuonekana

Kidawa: kumbe ndio mambo yako taajiri ee?! Unanidanganya utanioa kumbe upo na machangudoa wengine

Mimi moyoni nasema tobaaa kweli Edo hakuwa ananitania ila ngoja niuchune nione mshefa anaingiaje kwenye hii sakataa

Kidawa akafokaaaa foka na wewe, mara ampige demu wa Taajiri na kiti mara Taajiri atake kumpiga Kidawa wanaume wakamzuia,

Kidawa katukana paleee weee
Taajiri akaanza kumjibu ovyo, mwanamke gani wewe, mimi nitakuwa na mwanamke kama wewe?!
Kwanza unanuka? ! Kitandani mbovu na matusi kibao,

Hapo roho iliniuma vibaya mno, typical wanaume wa kibongo, akiona umemweza anaanza kukusingizia vitu ambavyo hauna

Kidawa: siamini nimepoteza miaka 3 na wewe mshenzi kumbe hauna lolote!
Kidawa akawa analia pale wanaume wakawa wanambembeleza mama pole usijali, mimi kimyaaa!

Kidawa akaamua kumalizia hasira na kutoa ya moyoni, ndio maana nimetembea na rafiki yako Mshefa!

Money Penny: ohooo! hii ya leo kali!

Kidawa: Na sijawahi kujuta wala kuumia moyoni kwa kutembea nae, maana ananifikisha napotaka na dyudyu yake sio kama yao kibamia, ya Mshefa kubwa kama chupa ya Safari Lager... stupid kibamia man

Taajiri: akashtuka hakuamini, huku anamwangalia Mshefa

Mshefa: anaona aibu, anaangalia chini!
watu wanashangaa mama yangu weee hii ya leo kali

Money Penny: nikashtuka nikapaliwa na juice niliokuwa nakunywa huku nimesimama nikaanza kukohoa, mbona picha la leo ni movie ya kulipia hii? !

Taajiri akamfuata Mshefa, atake kumpiga, watu wakamshikilia Taajiri

Taajiri: wewe ndio wa kunizunguka mimi reo kweri?!

Mshefa: kimyaaa, demu wa Mshefa anashangaa wakaondoka na demu wa Taajiri maana lile picha sio la nchi hii

Taajiri: Yani mimi nimekuamini maisha yangu yote nimekutoa kijijini nimekureta mjini nimekufundisha maisha, umekuwa mtu sasa hivi unatembea na demu wangu?!

Mshefa: kimyaaa,

Money Penny: Nikaona sasa ndio wakati wa mimi kuingilia hili movie, mara simu inaita kuangalia ni Edo, nikapokea ananiambia usisogee hapo mama utakufaa

Money Penny: go to hell, nikakata simu, nikajitoa sasa niende kumsaidia Kidawa, nikamkaribia namshika kidawa namkumbatia kidawa analia, huku akina Taajiri na Mshefa wanazikunja kweli kweli, nikamweka pembeni Kidawa nikavua miwani na mtandio na flip flops zangu, nikaenda kumshika Taajiri.... Tajiri akageuka nikamzaba kibaooo
Nikampiga magumi ya uso nikaanguka chini, akanishika shingoni kwa nguvu, sijawahi kubinywa kama sikuiyo maisha yangu yotee
Nikamtemea mate usoni akanikaba nitakuua wewe fisi, nitakuua usicheze na mimi
Hapo nimekabwa miguu najitahidi kumpiga mateke wapiii piga piga na wewe! Mara naona mtu kampiga kiti cha mgongoni Taajiri akaanguka chini na mie nikaanguka chini, wakaja wanaume kama 10 wakawa wanampiga, hapo nimeshikilia koo maumivu kibao, mara akaja Kidawa akanisogeza mbali na ugomvi, ngumi zikapigwaa pale hata sijui mshefa alikimbilia wapi, ghafla security wakaongezeka, wanapiga risasi juu juu watu wanakimbiaje sasa, ni balaaa!

Sie tukaamua kuingia kwenye gari haooo nduki tukaondoka

Kuvuka kivukoni tukaingia Kempinski kujipooza maana sio kwa kupigwa kule, Tukaenda chooni kujitengeneza, Mimi shingo nyekundu, kidawa ameshaumuka usoni ni balaa!

Money Penny: Kidawa twende hospital kwanza, wakatuangalie

Kidawa: analia hataki hata kusikia, nikambembeleza pale na nini mara naona simu ya Edo,

Kupokea naulizwa, mko wapi?!

Money Penny: tupo Kempinski chooni

Deo; nakuja msitoke hapo akakata simu

Baada ya dk 45 akaja, nipo parking njoeni fasta

Tukaondoka hao kufika kwenye gari namwambia Edo embu tupeleke Aghakhan akaangaliwe kwanza unaona alivyovimba?!

akamcheki kweli kidawa kavimba shavu sio kitoto, tukaingia Aghakhan tukapata na huduma!

Wakati tupo nje tunamsubiria Kidawa na Edo, Edo akaanza kuwaka,

Edo: wewe mimi nilikwambia tangu jana achana na huyo mtu haunielewi unaona sasa angekumaliza, yule mtu sio, yani sijui ungemwelezaje mzee wako na alivyo mkononi yule baba kha!

Money Penny: kimya naskiliza rapu za DJ Edo!

Edo: akawakaa weee, kama kawaida ya wanaume, mimi namsikiliza tu nikajua dogo ana mapenzi ya kweli na dadake

Mimi nilikwambia achana na huyu Tajiri nilijua na kama sio leo wewe ungefanyiwa kitu mbayaaa yule jamaa mafia shauriako.
kwanza m block kwa simu, pili ningekuwa wewe ningebadilisha namba ya simu, maana ushachukua hela zake lazima akutafute, mimi namjua yule

Money Penny: kwasababu nilitaka kumfunga kinywa Edo, Nikamjibu poa hamna noma nitabadilisha kesho, sa hivi nipo buzy na mgonjwa

Edo: kwani money penny, wewe kilichokufanya uwe na huyu jamaa ni nini?! Najua umeumizwa lakini huyu jamaa na yule mwenzake wote mishen town wapotezee

Money Penny: pain changed me Edo, ili kumsahau yule Fala lazima nipate wanaume kama 10 hivi wa kunifanya nimsahau

Edo: sio kweli na kwa spidi yako hii mimi nadhani huyu taajiri kakufanya umsahau!

Money Penny: bado, huyu taajiri lazima nile nae sahani 1; yeye pamoja na Mshefa wake nina plan kichwani kwangu kubwa sana

Edo: ohooo! Unataka ufanyaje labda we Penny?! Yani Penny haubadiliki utundu utundu wako tangu zamani ukiwa mdogo, ila ujue ukubwani huku utapigwa nakwambia, yani utapigwa kama sio kwenda jela

Money Penny: jela kitu gani bwana? Embu nambie, hauna god father yeyote unitambulishe anisaidie hili sakataa? ! Namba sihami wala nini, sana sana namblock ila nahitaji god father waukweli kama 5 ivi

Edo: mmh sasa, mimi nawatoa wapi labda

Money penny: wewe mtoto wa mjini! Lazima unao!

Edo: Money Penny sasa hizi kesi unaniletea ni za polisi, mimi sitaki kabisa kuwekwa jela

Money Penny: acha uoga dogooo nitaftie God father 5 wiki hii unitambulishe plz we kesi yako itakuwa imeishia hapo

Edo: alafu ukishawapata hao god father utafanyaje?! Hamna mtu hapa mjini anakusaidia bila kumpa asante na asante kwa watoto wa kike ni kuuza sehemu zenu za siri, we haya tu!
Wewe utawapa nini akina god father ambao washaishi maisha yote
Unataka kufa na ukimwi kisa unamfanyia ex wako revenge?!

Money Penny: sio revenge, ni smooth operation, kuondoa uchungu ndani yangu nikimaliza nao basi
Alafu ukimwi kama malaria tu, wala usinitishie ukimwi
Hapa duniani kila mtu atakufa ndivyo Mungu ametuandikia, wala usinitishie ukimwi, mimi nakufa, we utakufa hamna atakaebaki, hata kama Nitaenda wakwanza lazima niache chata nzuri ya kibabe!
Usijali kuhusu chiu, wanawake wote kwanza sie tumeumbiwa icho icho kuwapa raha wanaume, plz Edo siwezi ongea mengi, we bado mdogo sana kwangu, nitaftie god father wazee wazee wenye 60's au 65 mpaka 70 hao washachokaa hawahitaji saana papuchi plz

Edo: mimi sina god father

Money Penny: kwaiyo swala la uchungu wangu wa kuvurugwa labda unanisaidiaje? !

Edo: potezea hayo ndio maisha, mwombe Mungu atakuondolea

Money Penny: Mungu ana sehemu yake na god father wanazo zao na penny anayo yake
Unamwona shoga kidawa, atatoka na maumivu hakuna tena, atatamani alipize kisasi mimi na yeye wote kampuni moja... kwaiyo ili tusiwape shida wanaume wa mbeleni kulipia makosa ya wanaume waliopita naomba plz nitaftie god fathers

Edo: basi poa
Mara Kidawa akatoka kwa dokta tukarudishwa Kempinski Edo akaondoa zake sie tukabakia kula

Kidawa akawa na maneno mengi ya uchungu, jinsi gani amekaa na Taajiri kwenye mahusiano, wameahidiana na kufanya mambo kibao kwenye mahusiano yao ndio sio kwamba alikuwa hajui kama ana wanawake lakini hajawahi kumfumania, akaamua kuajiri mpelelezi amchekie huyu taajiri ndo kamletea ripoti kuwa jana alikuwa na mwanamke serena Wakaingia nae chumbani na mwanaume mwengine wakawa wanamla huyo demu na kupanga kuwa leo watakuwa southern sun kigamboni

Money Penny: kimoyomoyo nasema tobaaaa kumbe kumlaumua Taajiri asbh alikuwa anafanya three sum sikuwa nakosea ee?!
Nikamhurumia kidawa nikatamani kumsaidia lakini nashindwa
Nikambembeleza na kumpa stori yangu asijiskie vibaya akapoa kidogo

Money Penny: kwahiyo mami, una mpango gan na maisha yako kwa ujumla?!


Kidawa: hata sijui wangu, nahisi kufa kufa

Money Penny: my dia hamna cha kufa, hafi mtu hapa! OK?! Lazima tukomae acha, sie bado wadogo mimi nina 24 wewe una 25, bado tunawaka wasituzeeshe hapa

Kidawa nakuomba kama rafkiangu, tushikilie mioyo tujirushe maradufu tuinjoy life nauhakika tutapata wa kutupenda kama tulivyo na ukichaa na fujo zetu sawa?!

Mimi nina plan nzuri tu ila inabidi uwe ngangari sana, kama shetani mtoa roho, alafu tafuta god father kama 2... Unao?!

Kidawa: well ninae mmoja tu lakini zee lina hela balaa lilikuwa linanitakaga limenisumbua nikamtukana sa hivi ameacha kunisumbua

Money: huyo huyo ndio mzuri, nikaanza kumpa plan akashangaa, nikaendeleza plan akawa interested akachangamka, akawa anashangaa haamini kwanza kama nina akili hio, akaanza na kucheka, nikamwambia unaona maisha sio magumu kiivyo (Basi tu namcheka amsahau lofa Taajiri)?! Nilikwambia utasahau tukaishia kula na kunywa



KWA MUENDELEZO DONDOKA KWA LINK HII 👉 👉 👉 👉 https://www.moneystarstories.com/velvet/

joanah Ekuweme moneytalk Aikambee Mtoto halali na hela
 
Hehe he
Inamaana kunioa mimi ni sawa na kupata black card ya America ya benki? Sio blue ni black bruh
Bora iwe american black card watanifikiria kwenye ufilisi sio wewe 😀.. matunzo yako yanatakiwa pelekwa kikurya.
 
Back
Top Bottom