Leo katika magazeti nimesoma kichekesho limoja kuwa eti moshi mweusi wamuingia Ngeleja. Nikajiuliza hivi editors wanachekesha au? Huyu Waziri ni pandikizi la RA. Katika timu hiyo walikuwa ni pamoja na Masha, Maige, Ngeleja na Bashe alitakiwa ila kwa bahati mbaya ikashindikana!!! Ngeleja anatumikia wazee na hawawezi kumwondoa. Hebu tusikilizie tuone!! Mafisadi are powerful my friend, na kwa sasa wameshikilia Bunge!!! Hakuna kitu kitapita pale bila ngumi kupigwa hadharani. Cha msingi, tujipange kwa 2015 Chadema wawe na kituo chao cha kuhesabia Kura kwa haraka ili kupata uhakika. Yaani suala la mawakala na wasimamizi wa Chadema, kikata, kiwilaya na kila mkoa ni muhimu ili matokeo yangie mtandaoni haraka sana. Kwa mbinu hii mtaweza kukaba hao wachakachuaji.