Stergomena Tax: Waliopigana vita ya Kagera kuanza kulipwa pensheni kuanzia Julai 2026

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
waziri wa ulinzi Stergomena Tax amesema kuanzia mwezi julai wale waliopigana vita vya kagera wataanza kulipwa pensheni ameyasema hayo akiwa bungeni leo June 23 katika bunge la 12 mkutano wa 19 na kikao cha 51.

“Ninayo furaha kulitaarifu bunge lako tukufu kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo ni Sikivu sana inayoongozwa na Rais Samia imesikia kilio hiki cha muda mrefu sana cha maveterani waliopigana vita vya kagera kwakutambua mchango wao mkubwa maveterani hao kuanzia julai mwaka 2026 wote watalipwa pensheni”

Aidha, “Mpaka kufikia mwakani Juni, maveterani wote ambao walikuwa hawalipwi pensheni wataanza kulipwa pesheni kwa kima cha chini cha pensheni ya kijeshi na kitakuwa kinaongezeka kadiri kiwango hicho kitakavyokuwa kinapanda"

Pia soma ~ Waziri wa Ulinzi na JKT atoa ufafanuzi kuhusu malipo ya Pensheni za Maveterani wa Vita ya Kagera
 
Mwaka 1978/1979 hao watu wako hai kweli? Maana ishapita miaka 46 asa kama walikua na 30+ inamaana wengi wao 70+,
Na bora ata wangesema wanaanza kulipwa huu mwaka, 2025 eti kumbe 2026
 
Serikali ya kihuni kabisa hii.yaani watu wamepigana miaka ya Sabini ndiyo wapate haki 2026?Samia must go.no reform no electioni
 
Serikali ya kifala sana, mnalipa almost 50 years later baada ya vita, na wanajua wengi wameshajifia na waliobakia ni wazee ambao hata kufuatilia kama wataweza maana tunajua usumbufu watakaoweka mtu kulipwa, might take another 5 years kulipwa, pumbaf sana
 
waziri wa ulinzi Stergomena Tax amesema kuanzia mwezi julai wale waliopigana vita vya kagera wataanza kulipwa pensheni ameyasema hayo akiwa bungeni leo June 23 katika bunge la 12 mkutano wa 19 na kikao cha 51.

“Ninayo furaha kulitaarifu bunge lako tukufu kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo ni Sikivu sana inayoongozwa na Rais Samia imesikia kilio hiki cha muda mrefu sana cha maveterani waliopigana vita vya kagera kwakutambua mchango wao mkubwa maveterani hao kuanzia julai mwaka 2026 wote watalipwa pensheni”

Aidha, “Mpaka kufikia mwakani Juni, maveterani wote ambao walikuwa hawalipwi pensheni wataanza kulipwa pesheni kwa kima cha chini cha pensheni ya kijeshi na kitakuwa kinaongezeka kadiri kiwango hicho kitakavyokuwa kinapanda"

Uchaguzi wa 2025 umevuruga watu kwelikweli. Kwanini wasingeanza 2025 hii
 
Mwaka 1978/1979 hao watu wako hai kweli? Maana ishapita miaka 46 asa kama walikua na 30+ inamaana wengi wao 70+,
Na bora ata wangesema wanaanza kulipwa huu mwaka, 2025 eti kumbe 2026
Kweli mkuu % 99 wameshafariki na waliobakia labda Wakuu wa Majeshi.
 
Mwaka 1978/1979 hao watu wako hai kweli? Maana ishapita miaka 46 asa kama walikua na 30+ inamaana wengi wao 70+,
Na bora ata wangesema wanaanza kulipwa huu mwaka, 2025 eti kumbe 2026
Wakwetu amefariki jana.
 
Back
Top Bottom