Stephen Wassira: CUF hawaitaki Serikali ya Mapinduzi

Stephen Wassira: CUF hawaitaki Serikali ya Mapinduzi

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira amesema viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) hawayatambui Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Pia, amesema baadhi ya wajumbe wake, wanapinga Siku ya Mapinduzi, kutambuliwa katika kalenda za kitaifa nchini kote.

Wassira alisema hayo katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Uwanja wa Kibandamaiti mjini Zanzibar.

Alisema chama hicho hakina dhamira na nia nzuri kwa Wazanzibari katika Mapinduzi ya Januari mwaka 1964.

Akifafanua, alisema alipambana na viongozi wa CUF wakati wakijadili Katiba katika Bunge Maalumu la Katiba na kuwaeleza umuhimu wa Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ndiyo yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka katika makucha ya wakoloni.

Kwa mfano, Wassira alimtaja mmoja wa wajumbe waliokuwemo katika kamati yake, ambayo yeye alikuwa kiongozi kuwa ni Ismail Jussa, ambaye alikuwa akipinga na kutaka siku ya Mapinduzi, isitambuliwe na kufanywa kuwa siku ya mapumziko kitaifa.

Alisema Jussa anataka siku za sherehe za kitaifa, ikiwemo Mapinduzi ya Januari 1964 na Uhuru wa Tanganyika, ziondolewe na zisitambuliwe kama siku za kitaifa rasmi.

“Hawa watu ni wa ajabu sana kumbe hawayatambui Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, kwani hata katika kamati za Bunge Maalumu la Katiba nilipambana nao kikamilifu huku wakitaka Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964 isitambuliwe rasmi,” alisema.

Wassira alisema serikali zote mbili, tayari zimeanza kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za Muungano, ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi wa Zanzibar.

Hata hivyo, alisema kitendo cha wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakiongozwa na wapinzani kutoka nje ya vikao, kwa kiasi kikubwa kutaathiri na kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano.

“Nasikitishwa sana na kitendo cha wapinzani kutoka nje ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, kwa sababu kutapelekea kero za Muungano zinazoihusu Zanzibar kushindwa kupatiwa ufumbuzi wake,” alisema.
chanzo:Habarileo.
 
  • Thanks
Reactions: gsu
Hakuna kitu hatari sana katika siasa na mstakabali wa taifa kama nchi kuwa na wanasiasa ambao wanatumia ndimi zaidi ya moja katika kufikia malengo yao.

Mchakato wa Rasimu ya Katiba unazidi kuwaibua wanasiasa walaghai ambao kwao wanachokisema leo siyo hicho watakachokisema kesho.

Ngozi walizokuwa wamezivaa viongozi wa CUF zinazoitwa kutaka serikali ya Mkataba baadaye walivua na kuvaa ngozi nyingine ya kutaka serikali tatu lakini ndani ni simba wanaotaka kuvunja Muungano ili iwe ni rahisi katika kufanikisha nia yao ya kuhakikisha hakuna kitu kinachoitwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

CHADEMA nao kwa kukosa mwerekeo na hoja endelevu za kisiasa kwa mstakabali wa taifa kutokana na siasa zao za ubaguzi wa fikra, kabila, dini na maeneo. Wananchi waliwapa angalizo kwa kuwanyima kura kupitia chaguzi mbali mbali za taifa, kwa sasa neno CHADEMA wameanza kulifuta katika vitabu na ndimi zao ili angalau warudishe mwamko kupitia njia ya kilaghai kwa kutumia jina linaloitwa UKAWA.

Walioingia kwenye mkenge wa kudhani CUF na CHADEMA wako katika siasa kwa maslahi ya taifa endelevu haitachukua muda kufahamu kuwa wao wanatengenezwa kuwa ni daraja watakalopitia CUF na CHADEMA katika kufikia malengo yao binafsi ya kutaka kupata madaraka na kuligawa taifa.

There's a general rule in Tanzania politics. Huwezi kuuvunja Muungano bila kupambana na hoja za Mwl. Nyerere na Abeid Amani Karume zilizosababisha Muungano kuwepo na kuimarika. Baada ya kujaribu kila njia bila mafanikio ili kuvunja Muungano huku wakiogopa kupambana na nguvu za hoja za kiunganishi kikuu cha Muungano ambacho ni Waasisi wetu wa Taifa na Muungano. Kwa sasa wameamua kuvua ngozi waliyokuwa wameivaa.

Kabla ya kuanza kwa bunge Maalum, Viongozi wakuu wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walikuwa wanaonekana kwa nje wako mbele kukienzi kile Waasisi wetu wa Taifa walikisimamia kwa nguvu zao zote (Muungano), lakini haikufahamika vizuri kama dhamira yao kwa ndani ilikuwa ni kuvunja Muungano kwa njia ya kilaghai.

Baada ya kugundua hili, ndiyo maana tuliwaona na kuwasikia baadhi ya viongozi kama Tundu Lissu wakianza kuwatukana waasisi wa Muungano wetu na kuwasema kuwa ni waongo na matapeli wa kisiasa in order to manipulate, deceive, and destroy Mwl. Julius Nyerere and Amani Karume reputations as the founding fathers of our Nation.

Hawawezi kufanikiwa katika satanic political mission.
 
wengi wanajua kuwa cuf wao wanayo malengo yao ya kuvunja muungano ili hatimaye warudishe utawala wa mwarabu visiwani kwakuwa wanadai kuwa waliopinduliwa walikuwa ni babu zao na bibi zao pamoja na wajomba zao.

Lakini pia cuf wanaodai serikali tatu wote ni wale wenye uraia wa oman kwa kificho hata paspoti zao za kusafiria wanamiliki za omani.
 
Mbn hujaaongelea kero za muungano za tanganyika mtazitatua lini y zanzibar pekee, hv mnawaogopa nn hao watu
 
Hivi mara ya mwisho Wassira na Abdul Kindovu Katembo na team yake ya Vuvuzela kufika Zanzibar kichama na kufanya mikutano ilikuwa lini ewe mpiga picha??
 
Kwani Rasimu imewasilishwa na Ukawa?
Naona mnataka Ukawa waimbe wimbo wa serikali 2
Tunataka watu wanaosimamia maoni yetu tuliyotoa kwa Tume ya Warioba.
 
Yaani badala ya kuzungumzia kero anamlaumu Jussa?
Kama kuzungumzia kero hata Jussa ni kero.

Kama ulikuwa na maana ya kero za Muungano, Mh. Wassira alisema,
Wassira alisema serikali zote mbili, tayari zimeanza kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali za Muungano, ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi wa Zanzibar.
Ukitaka maelezo zaidi kuhusu ufafanuzi wa kile alikisema, unaweza kupata kupitia video au fuatilia kitakachojiti katika Bunge la Katiba
 
Cuf amepata mume mpya ameshamdharau wa ujana
 
spinning za kijinga, CUF wanakubali mapinduzi na serikali ya mapinduzi na ndio maana wakawa sehemu ya serikali hio.

suali la kusema isiwekwe kwenye katiba ilikua pamoja na kuondosha tarehe ya uhuru wa tanganyika, ila hili halitamki kwa kuwa linamchoma.

nchi washirika ndio washerehekee na kuweka kwenye katiba zao siku zao za uhuru na katiba ya muungano ibaki na siku ya muungano. ipo wazi na clear
 
wengi wanajua kuwa cuf wao wanayo malengo yao ya kuvunja muungano ili hatimaye warudishe utawala wa mwarabu visiwani kwakuwa wanadai kuwa waliopinduliwa walikuwa ni babu zao na bibi zao pamoja na wajomba zao.

Lakini pia cuf wanaodai serikali tatu wote ni wale wenye uraia wa oman kwa kificho hata paspoti zao za kusafiria wanamiliki za omani.
Serikali iliyoshindwa kazi utawajua mawakala wake hivi kama watu wanajulikana wana paspoti za Omani kwa nini wasishughulikiwa? Mnamiliki dola kwa udhaifu mkubwa.
 
Bora kutawaliwa na MWARABU kuliko kutawaliwa na Tanganyika.
 
Mimi toka ccm iliposhindwa kutusimamia pale Waziri wenu aliposema eti hela za EPA zilienda usalama Wa Taifa kumbe uongo mwishoe balali akafia USA kimagumashi leo mmekuaje Wazalendo?
Wacha wale waliokuwa Wazalendo Wakafichua Ufisadi Wa Epa, Meremeta na Richmond tuendelee kuwaamini.
 
Sikiliza meza ya duara ya sauti ya Ujerumani.
Nape
Mchungaji Msigwa
Mzee Salim Rashid(Katibu wa kwanza wa baraza la mapinduzi).
Na Mh.Hamad Yussuf Mshamba(Kamishna wa Tume ya Warioba)

AUDIO | DW.DE
 
Kama kuzungumzia kero hata Jussa ni kero.

Kama ulikuwa na maana ya kero za Muungano, Mh. Wassira alisema,

Ukitaka maelezo zaidi kuhusu ufafanuzi wa kile alikisema, unaweza kupata kupitia video au fuatilia kitakachojiti katika Bunge la Katiba

Ni kweli kabisa MwanaDiwani, hizi kero za Muungano zitatatuliwa na Wassira & nduguze wakiwa kaburini wamekufa kwa sababu wakiwa hai kero ndiyo zinazidi kila kukicha.
 
Last edited by a moderator:
Kama kuzungumzia kero hata Jussa ni kero.

Kama ulikuwa na maana ya kero za Muungano, Mh. Wassira alisema,

Ukitaka maelezo zaidi kuhusu ufafanuzi wa kile alikisema, unaweza kupata kupitia video au fuatilia kitakachojiti katika Bunge la Katiba

Kero za Tanganyika nani anazisimamia naona mmefanya kero za muungano ndio za Tanganyika hebu haya mambo yawekwe wazi sasa.
 
Back
Top Bottom