Hakuna kitu hatari sana katika siasa na mstakabali wa taifa kama nchi kuwa na wanasiasa ambao wanatumia ndimi zaidi ya moja katika kufikia malengo yao.
Mchakato wa Rasimu ya Katiba unazidi kuwaibua wanasiasa walaghai ambao kwao wanachokisema leo siyo hicho watakachokisema kesho.
Ngozi walizokuwa wamezivaa viongozi wa CUF zinazoitwa kutaka serikali ya Mkataba baadaye walivua na kuvaa ngozi nyingine ya kutaka serikali tatu lakini ndani ni simba wanaotaka kuvunja Muungano ili iwe ni rahisi katika kufanikisha nia yao ya kuhakikisha hakuna kitu kinachoitwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
CHADEMA nao kwa kukosa mwerekeo na hoja endelevu za kisiasa kwa mstakabali wa taifa kutokana na siasa zao za ubaguzi wa fikra, kabila, dini na maeneo. Wananchi waliwapa angalizo kwa kuwanyima kura kupitia chaguzi mbali mbali za taifa, kwa sasa neno CHADEMA wameanza kulifuta katika vitabu na ndimi zao ili angalau warudishe mwamko kupitia njia ya kilaghai kwa kutumia jina linaloitwa UKAWA.
Walioingia kwenye mkenge wa kudhani CUF na CHADEMA wako katika siasa kwa maslahi ya taifa endelevu haitachukua muda kufahamu kuwa wao wanatengenezwa kuwa ni daraja watakalopitia CUF na CHADEMA katika kufikia malengo yao binafsi ya kutaka kupata madaraka na kuligawa taifa.
There's a general rule in Tanzania politics. Huwezi kuuvunja Muungano bila kupambana na hoja za Mwl. Nyerere na Abeid Amani Karume zilizosababisha Muungano kuwepo na kuimarika. Baada ya kujaribu kila njia bila mafanikio ili kuvunja Muungano huku wakiogopa kupambana na nguvu za hoja za kiunganishi kikuu cha Muungano ambacho ni Waasisi wetu wa Taifa na Muungano. Kwa sasa wameamua kuvua ngozi waliyokuwa wameivaa.
Kabla ya kuanza kwa bunge Maalum, Viongozi wakuu wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walikuwa wanaonekana kwa nje wako mbele kukienzi kile Waasisi wetu wa Taifa walikisimamia kwa nguvu zao zote (Muungano), lakini haikufahamika vizuri kama dhamira yao kwa ndani ilikuwa ni kuvunja Muungano kwa njia ya kilaghai.
Baada ya kugundua hili, ndiyo maana tuliwaona na kuwasikia baadhi ya viongozi kama Tundu Lissu wakianza kuwatukana waasisi wa Muungano wetu na kuwasema kuwa ni waongo na matapeli wa kisiasa in order to manipulate, deceive, and destroy Mwl. Julius Nyerere and Amani Karume reputations as the founding fathers of our Nation.
Hawawezi kufanikiwa katika satanic political mission.