Stephen Wassira: CUF hawaitaki Serikali ya Mapinduzi

Stephen Wassira: CUF hawaitaki Serikali ya Mapinduzi

Kwa hiyo kama "watanganyika" wanasherehekea siku ya uhuru. serikali ya Muungano kuanzia Rais, wizara na idara za Muungano na Bunge la Muungano watakuwa kazini. Zanzibar nayo watakuwa kazini?.

Kwa nini hakutaka ziwe ni sherehe zinazotambuliwa kitaifa na nchi "washiriki wa Muungano" kuonyesha mshikamano kama taifa.

Badala ya kujenga mtazamo wa kitaifa, unachofanya ni kujenga mtazamo wa kiserikali.

"Nchi washirika wa muungano" ni wepi hao wakati Tanganyika mnasema haipo"



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Poor Wassira eti hizo ndiyo hoja za uzuri wa S2 against S3. Haishangazi watu wenye hoja hii kukimbia midahalo ya kisomi.
 
Hili sokwe mtu linasema nn? Kamaserikal 2 zimeanza kujua na kutatua haya masuala walishindwa nn miaka 50?.
Ukimuuliza swal hilo hakiyamungu huwe kupata jibu zaidi atanguruma tu kama sokwe kwl kwl.
 
Nilimsikiliza Mhemiwa Duni Haji wa CUF kwenye mdaharo ITV hoja zake ni dhahiri nia yao ni kuuvunja muungano. Anasema wanaitaka Zanzibar yenye mambo yafuatayo:-
- Pesa yake
- Pasipoti yake
- Uhamiaji yake
- Benki kuu yake
- Sheria yake ya forodha
- Vyama vyake vya siasa
- Mambo ya nje
Sasa hapo muungano uko wapi? Na kama Muungano hakuna maana yake Mapinduzi hakuna
 
Nilimsikiliza Mhemiwa Duni Haji wa CUF kwenye mdaharo ITV hoja zake ni dhahiri nia yao ni kuuvunja muungano. Anasema wanaitaka Zanzibar yenye mambo yafuatayo:-
- Pesa yake
- Pasipoti yake
- Uhamiaji yake
- Benki kuu yake
- Sheria yake ya forodha
- Vyama vyake vya siasa
- Mambo ya nje
Sasa hapo muungano uko wapi? Na kama Muungano hakuna maana yake Mapinduzi hakuna
 
Huyu si ni yule alimkimia Mwalimu enzi za uhai wake na kwenda kuibukia NCCR Mageuzi?
 
wewe unazungumzia tanganyika gani ambayo haipo?

Kufilisika hoja ni kubaya sana. Utasikia ccm wanasema Tanganyika iliishi mwaka mmoja na ushee hivi,ikiwa na maana ilikufa,ikaenda wap hawasemi,pili Tanzania ni muungano wa nchi ngapi,hawajui...

Kibaya zaidi wanasema Tanganyika ilikufa na vitu vyake vyote,sawa,unawauliza ccm ilitokana na nini,wanajibu TANU NA ASP, Sasa TANU ni chama kilikua kinawakilisha nchi gani? Kama Tanganyika ilikufa na vitu vyake hata TANU pia ilikufa,hvyo muungano wa TANU NA ASP ULIKUA BATILI MAANA ULIHUSISHA MUUNGANO WA CHAMA CHA NCHI AMBAYO HAIPO. Kwa ujumla CCM NI CHAMA BATILI,CHA KIHUNI NA KITAPELI.
 
Nilimsikiliza Mhemiwa Duni Haji wa CUF kwenye mdaharo ITV hoja zake ni dhahiri nia yao ni kuuvunja muungano. Anasema wanaitaka Zanzibar yenye mambo yafuatayo:-
- Pesa yake
- Pasipoti yake
- Uhamiaji yake
- Benki kuu yake
- Sheria yake ya forodha
- Vyama vyake vya siasa
- Mambo ya nje
Sasa hapo muungano uko wapi? Na kama Muungano hakuna maana yake Mapinduzi hakuna
Kweli?! Mbona mapinduzi yalitokea kabla ya huo muungano? Waacheni wazanzibar wapumue.
 
Hakuna kitu hatari sana katika siasa na mstakabali wa taifa kama nchi kuwa na wanasiasa ambao wanatumia ndimi zaidi ya moja katika kufikia malengo yao.

Mchakato wa Rasimu ya Katiba unazidi kuwaibua wanasiasa walaghai ambao kwao wanachokisema leo siyo hicho watakachokisema kesho.

Ngozi walizokuwa wamezivaa viongozi wa CUF zinazoitwa kutaka serikali ya Mkataba baadaye walivua na kuvaa ngozi nyingine ya kutaka serikali tatu lakini ndani ni simba wanaotaka kuvunja Muungano ili iwe ni rahisi katika kufanikisha nia yao ya kuhakikisha hakuna kitu kinachoitwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

CHADEMA nao kwa kukosa mwerekeo na hoja endelevu za kisiasa kwa mstakabali wa taifa kutokana na siasa zao za ubaguzi wa fikra, kabila, dini na maeneo. Wananchi waliwapa angalizo kwa kuwanyima kura kupitia chaguzi mbali mbali za taifa, kwa sasa neno CHADEMA wameanza kulifuta katika vitabu na ndimi zao ili angalau warudishe mwamko kupitia njia ya kilaghai kwa kutumia jina linaloitwa UKAWA.

Walioingia kwenye mkenge wa kudhani CUF na CHADEMA wako katika siasa kwa maslahi ya taifa endelevu haitachukua muda kufahamu kuwa wao wanatengenezwa kuwa ni daraja watakalopitia CUF na CHADEMA katika kufikia malengo yao binafsi ya kutaka kupata madaraka na kuligawa taifa.

There's a general rule in Tanzania politics. Huwezi kuuvunja Muungano bila kupambana na hoja za Mwl. Nyerere na Abeid Amani Karume zilizosababisha Muungano kuwepo na kuimarika. Baada ya kujaribu kila njia bila mafanikio ili kuvunja Muungano huku wakiogopa kupambana na nguvu za hoja za kiunganishi kikuu cha Muungano ambacho ni Waasisi wetu wa Taifa na Muungano. Kwa sasa wameamua kuvua ngozi waliyokuwa wameivaa.

Kabla ya kuanza kwa bunge Maalum, Viongozi wakuu wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walikuwa wanaonekana kwa nje wako mbele kukienzi kile Waasisi wetu wa Taifa walikisimamia kwa nguvu zao zote (Muungano), lakini haikufahamika vizuri kama dhamira yao kwa ndani ilikuwa ni kuvunja Muungano kwa njia ya kilaghai.

Baada ya kugundua hili, ndiyo maana tuliwaona na kuwasikia baadhi ya viongozi kama Tundu Lissu wakianza kuwatukana waasisi wa Muungano wetu na kuwasema kuwa ni waongo na matapeli wa kisiasa in order to manipulate, deceive, and destroy Mwl. Julius Nyerere and Amani Karume reputations as the founding fathers of our Nation.

Hawawezi kufanikiwa katika satanic political mission.

Ccm wacheni porojo .swala la msingi hapa nikukubali kunywa dawa ya kutibu ugonjwa wamuungano .nayo ni kujadili rasmu ya katiba iliyopo mezani .haya mengine yote umnayo lete ni umbeya .fitina,chuki .na matusi kwa wananchi wa Tanzania
 
wengi wanajua kuwa cuf wao wanayo malengo yao ya kuvunja muungano ili hatimaye warudishe utawala wa mwarabu visiwani kwakuwa wanadai kuwa waliopinduliwa walikuwa ni babu zao na bibi zao pamoja na wajomba zao.

Lakini pia cuf wanaodai serikali tatu wote ni wale wenye uraia wa oman kwa kificho hata paspoti zao za kusafiria wanamiliki za omani.

Kwa maana hiyo na wanaodai serikali mbili ni waingereza na wakatoliki, wanaogopa nguvu za kiislam
 
Kwa maana hiyo na wanaodai serikali mbili ni waingereza na wakatoliki, wanaogopa nguvu za kiislam

Umeiweka vyema kweli.Maana unachodhania mwenzio anafikiria kutenda na unayemdhania naye anafikiri nini unataka kufanya.

Hii ni sawa na ile..Usichopenda kutendewa usimtendee mwenzio.
 
Nilimsikiliza Mhemiwa Duni Haji wa CUF kwenye mdaharo ITV hoja zake ni dhahiri nia yao ni kuuvunja muungano. Anasema wanaitaka Zanzibar yenye mambo yafuatayo:-
- Pesa yake
- Pasipoti yake
- Uhamiaji yake
- Benki kuu yake
- Sheria yake ya forodha
- Vyama vyake vya siasa
- Mambo ya nje
Sasa hapo muungano uko wapi? Na kama Muungano hakuna maana yake Mapinduzi hakuna
Ndugu, Hizi ndizo hoja za kikundi kinachojiita UKAWA halafu eti wanasema wanataka Muungano. Huhitaji hata kuwa mtaalam wa uchumi na siasa kufahamu mantiki ya kile wanachokitaka.
 
Tunaposema Zanzibar ni koloni la Tanganyika, watu wanakataa lakini ndivyo ilivyo na Wasira hapa anaonesha. Kama si kweli mamlaka yake ni pamoja na mambo ya Muungano au? je mapinduzi ni jambo la Muungano???
 
Namkubali Stephen Wassira kwa hoja zenye mashiko.
 
Back
Top Bottom