Naona wachangiaji wengi humu hamuifahamu na wala hamuijui jimbo la RORYA. Sikumbuki kuwa OWAWA alienda Rorya kwa mara ya mwisho lini na kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu 2010 OWAWA hakukanyaga Rorya. Owawa anajulikana sana Dar na kwenye vyombo vya habari lkn siyo ndani ya Rorya. Mimi namfahamu sana Kamanda Owawa na namkubali sana ktk medani za siasa na kwenye harakati zake. Ningependa kumshauri kama ana nia ya kugombea Ubunge akagombee jimbo lingine na siyo Rorya. Siasa za Rorya siyo siasa za kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii. Owawa najua ni mwanarorya, ila namkaribisha Rorya!
Kama mtu anaweza tumpe moyo na kusema ukweli,mimi nakumbuka kuwa amekuwa akienda Rorya kila mara ila alichosema kuwa bado ni mapema kwa mtu anataka kuingia kwenye siasa za Rorya lazima ajipange kwanza,ni kweli alikuwa Anasaidia kampeni mgombea Ubunge wa CHADEMA martin Ochola Ndira,nakumbuka 2010 nilikutana nao Shirati,Osiri,Busanga,Nyambori,Kirongwe,Bugire,utegi na Kinesi,kwa hiyo kusema kuwa hafiki Rorya nadhani uongo,mwaka huu mwezi wa tano alikuwa Randa,Kagwaa,Bugire na Masonga.Nadhani njia anayotumia kujipanga kwa jimbo la Rorya ni tofauti sana na njia tuliyozoea.Mwaka jana mwezi wa kumi na mbili alikuwa Rorya uku akiwasiliana na wazee wakimila ili aweze kuandika kitabu kinachohusu Rorya na Changamoto zake.
Ila inabidi ajipange sana kwa sababu tatizo la kwao Rorya ni watu kurubuniwa na pesa na kuacha wenye uwezo,labda kuamka kwa wananchi inaweza kumsaidia.Binafsi nampa big up sana kwa uwezo binafsi na ujasiri alionao,jamaa kwenye ukweli utamchoka atakwaambia bila kupindisha,atafute ngawira ili ajaribu kama ataweza.