KERO Stendi ya Daladala Makumbusho ipo kwenye hali mbaya, inazidi kuchoka, Ushuru unatozwa lakini hakuna ukarabati

KERO Stendi ya Daladala Makumbusho ipo kwenye hali mbaya, inazidi kuchoka, Ushuru unatozwa lakini hakuna ukarabati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
photo_2025-05-15_13-17-37.jpg

photo_2025-05-15_13-17-40 (3).jpg

photo_2025-05-15_13-17-41.jpg

Stendi ya makumbusho ni kati ya Stendi ambazo zimekuwa zikipokea daladala nyingi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam, lakini stendi hiyo imekuwa ikipoteza hata ubora mdogo iliyokuwanao awali, ambapo kwa sasa imechakaa na imekuwa kero kwetu madeleva wa daladala.

Licha ya daladala zinazoingia kwenye stendi hiyo kutozwa tozo ambayo kati ya matumizi yake ni pamoja na kuboresha miundombinu ndani ya Stendi, usafi na usalama, lakini kwa sasa miundombinu imekuwa chakavu na hakuna maboresho yoyote yanafanyika wala ambayo tumeshuhudia kwa kipindi cha hivi karibuni.

Stendi imejaa mashimo na hakuna mpagilio wa magari unaoeleweka, maji machafu yamejaa kwenye mashimo mpaka yanatoa harufu, stendi imekuwa kama haina wasimamizi licha ya kuingiza pesa nyingi kulingana na daladala zinazoingia.

Maeneo maalum kwa abiria kuketi wakiwa wanangojea magari nayo yamechakaa mvua ikinyesha ndio majanga kabisa, abiria wanakimbilia kwenye maduka ya watu au kwenye magari.

photo_2025-05-15_13-17-42.jpg

photo_2025-05-15_13-17-39.jpg
Stendi ipo kwenye hali mbaya hadi sisi madereva tunaangaika kukwepa mashimo na hapo ni ndani ya stendi, kuna wakati magari yanalazimika kushusha maeneo ya nje ili kuepuka kuingia stendi, lakini hata ikifanyika hivyo wahusika wanakunyapia na kutoza faini.

Sijui nani amepewa mamlaka ya kusimamia stendi hiyo ya daladala naona kama wameshindwa, lakini wito wangu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni lazima wawajibike katika hilo maana stendi hiyo ipo kwenye eneo lao la kiutawala, maana tunajiuliza tozo tunazokatwa zinaenda wapi?
 
Msamiati wa "Maintanance Plan" haupo kwenye vichwa vya watumishi wengi wa serikali
 
Sioni umuhimu wa him stendi Tena wakati Kuna stendi ya kisasa ya mwenge imekamilika na ni few mile kutoka hapo,kilichobaki hyo stend ziingie gari za root chache sana
 
Back
Top Bottom