Statement ya Mhe. Zitto Kabwe : To the Ministers-Nothing to Celebrate, go to work | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Statement ya Mhe. Zitto Kabwe : To the Ministers-Nothing to Celebrate, go to work

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TeamZitto, May 5, 2012.

 1. TeamZitto

  TeamZitto Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inapatikana URL: https://zittokabwe.wordpress.com/2012/05/05/to-the-ministers-nothing-to-celebrate-go-to-work/

  Mawaziri, hakuna sherehe, nendeni mkawajibike!


  Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo la Bunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwa kazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia.

  Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza Kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea Kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.

  Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.

  Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in a changamoto nyingi sana. Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato ya Utalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.
  Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia, siwapi pongezi Bali nawatakia kazi njema. Nawatakia uwajibikaji mwema. Uwajibikaji ndio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe.

  Kwa Waziri wa Fedha, ambaye mimi ni Waziri Kivuli wake (Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni hataniwajibisha pia), namwambia uteuzi wake ni changamoto kubwa sana katika maisha yake.
  Hivi sasa eneo lenye Bajeti kubwa kuliko zote nchini ni huduma kwa Deni la Taifa (services to national debt). Lazima kuangalia upya Deni la Taifa. Hivi sasa Deni la Taifa ukijumlisha na Dhamana za Serikali (government guarantees) limefikia tshs 22trn mpaka Desemba 2011. Nimewahi kutaka ukaguzi Maalumu katika 'account' ya Deni la Taifa. Linarejea wigo huu. Tunalipa takribani 1.9trn tshs kwa mwaka kuhudumia Deni la Taifa. Zaidi ya Bajeti ya miumbombinu, Afya, Maji, Umeme nk.

  Mfumuko wa Bei, misamaha ya kodi na kodi zinazozuia watanzania kujiajiri ni changamoto kubwa sana Wizara ya Fedha lazima ihangaike nayo.
  Usimamizi wa Mashirika ya Umma kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na hasa usimamizi wa Hisa za Serikali katika kampuni binafsi ni masuala yanayohitaji masuluhisho sasa na sio baadaye.

  Kwa Mwalimu wangu dkt. Mwakyembe, utakumbukwa kwa Jambo moja tu. RELI. 'make our Railway system work'. Hutakuwa na 'legacy' nyingine isipokuwa Reli maaana Bandari bila Reli ni sawa na Bure.
  Tunatumia zaidi ya tshs 300bn kwa mwaka kukarabati barabara wakati tunahitaji tshs 200bn kukarabati Reli iweze kusafirisha mzigo kwenda Bandarini na kutoka Bandarini.

  Ndio maana nasema hakuna Jambo la kusherehekea maana wajibu mliopewa na Rais ni mtihani mkubwa kwenu katika kulitumikia Taifa letu. Msipowajibika, mtakumbwa na fagio la chuma!

  Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate. Hit the ground running.

  Imetolewa na:

  ZZK
  Dar-es-Salaam
  Jumamosi Mei 5 2012
   
 2. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Seconded ZZK.

  Imefika wakati kila mmoja wetu ajue cheo ni dhamana. Ili kuitimiza dhamira ya dhamana aliyopewa inampasa kuwajibika kwa uadilifu katika mamlamka aliyopewa.

  Ile dhana ya kuteuliwa kwa cheo fulani ni kupewa ulaji imepitwa na wakati.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Maneno ya msingi sana, na sio kwa Mawaziri tu na Manaibu wake, hata wabunge

  Cheo ni dhamana, kila mtu awajibike kwa nafasi yake, uchama, udini na ukabila usahauliwe sasa.
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Seconded ZZK
  Asante sana kuwakumbusha kuwa hakuna la kusherehekea
  bado mwezi mmoja tuu tuanze mchakato wa kutangaziwa budget ya mwaka ujao wa fedha na bado hali ya uchumi ni mbaya
  hakuna la kusherehekea maana masuala mengi yako kama hayaendi vile
  Ni wakati wa mapambano
  Ila msimamo wako na hoja yako tunaamini itaendelea maana ndio mlilokuwa mnapigania
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sioni sababu ya kuwapa ushauri! Ni bora tu waachwe waendelee kujichimbia kaburi na hatimaye waondoke wote kabisa.

  Miaka zaidi ya 50 lichama hilo hilo limoja liko madarakani. Wengine tumechoka.

  I want change, a breath of fresh air.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  NN nimeipenda statement yako kaka
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Well said kamanda Zitto. Uwajibikaji ndio msingi wa maendeleo.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Katika siasa za ushindani sioni sababu ya kumpa ushauri mshindani mwenzio.

  Rais Obama asingeshinda urais kama W angefanikiwa. Rais Clinton asingeshinda urais kama H.W. Bush angefanikiwa. Rais Reagan asingeshinda urais kama Jimmy Carter angefanikiwa. Tony Blair chama chake kisingeshinda ile 1997 kama John Major na chama chake wangefanikiwa.

  Miaka 50 ni mingi mno kwa chama kimoja kuwa madarakani. CCM hawana jipya. Hata wamuweke nani kwenye baraza la mawaziri...hakuna jipya. Sera ni zile zile...mirangi yao ni ile ile na matokeo ni yale yale. That's insanity.

  Hivi sijui wengine hawachoki kuwa na lichama limoja madarakani kwa zaidi ya nusu karne? Mimi nimechoka na kamwe sitawapa ushauri wa nini cha kufanya. Nitawaacha waharibu ili watu wazidi kupata sababu ya kuwatoselea mbali.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwanini mumwache Pinda nyie Wabunge? Hawa mawaziri waliotakiwa kuondoka, baadhi yao bado wapo. Itakuwa vema kuendelea kula nao sambamba hadi nao waondolewe.

  Inashangaza watu kama Malima na madudu yote hayo na ufuska juu, bado anaendelea kupeta.

  Hawa jamaa wa Tamisemi, bado wanaendelea kupeta.

  Waliohusika wote hadi Mawaziri wakaondolewa kama TBS na huyu Ekerege (Tanzanians KILLER) basi lazima wapelekwe sehemu husika kwa kusababisha vifo kibao vya Watanzania kwa kuingiza bidhaa mbovu na hivyo Watanzania kufa kwa wingi kwenye ajali za magari (Matairi kupasuka), madawa feki, mioto majumbani kwa sababu ya umeme, vyakula feki.

  Mungu bariki huku mitaani na nyie mtarudi. Kama si nyinyi basi watoto wenu au ndugu watakula na kutumia hiyo Mifeki.

  SHETANI awakaribishe kwake na mkumbuke milele, hasa wee Ekerege, HUKUMU NI HAPAHAPA duniani na Dua la kuku...
   
 10. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hana lolote huyo zzk amemaliza kazi aliyotumwa asubiri ujira wake..eti mkuchika anaampongeza kwa kukubali kujiudhuru...,sasa alivyokua analiambia bunge waliowajibika akiwemo mkuchika alikua anataka tu wakubali kujiudhuru au ni upotevu wa mali ya umma ndio uliomsukuma atamke yote aliyotamka bungeni...?achalia hilo alilalama sana juu ya wizi sasa kujiudhuru tu inasaidia nn kwa mwamanchi mtanzania anayeteseka na maisha magumu sasa?au ndio alitaka kukuza umaarufu wake tu then apate ujira kwa njia nyingine...!shida tutakufanazo watanzania asijifanye anauchungu na nchi na ushauri mzuri wakati ni msanii tuu pia.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi baada ya zaidi ya miaka 50 ya utawala wa chama kimoja niko tayari kabisa kuwapa nafasi watu wengine nao tuone wanaweza kutufanyia nini.

  Kwa hiyo kwa sasa nadhani njia pekee iliyobaki ni kuiondoa kabisa CCM madarakani...wakae benchi...wajipange upya na labda nitaweza kuwafikiria tena huko baadaye.
   
 12. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wazee wakongwe tunawaitaje vile? Sijui malenga wetu kama nimekosea mtanirekebisha....wao walisema lakuvunda halina ubani.......utajaza mwenyewe
   
 13. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ZKK, sawa, ujumbe mzuri kwa wateule na watendaji wote wa govt.

  Pamoja na hayo, nawaomba Wabunge wawatie moyo na kuwapa ushirikano. Wakosoeni wanapoboronga, na kutoa mapendekezo ya kusahihisha kasoro au makosa yao. Kama ni makosa ya kukosa uaminifu.....hakuna kuvumiliana.

  Lakini pia wapongezeni wanapofanya vizuri na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kufanya vizuri zaidi.

  Isiwe ni kosa moja, pengine la kibinaadam ......anashinikizwa kuondoka. Mazuri mawili matatu....kimya, kana kwamba hakuna kilichotokea.
   
 14. M

  Mantuntunu Senior Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe Kama Mimi, am not thrilled kabisa na hawa mawaziri wapya kwani hakuna jipya watakalofana, I just want a complete change, chama kingine, am not seeing any changes kwa hawa watu.
   
 15. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Sherehe ziishie kwenye mawazo yao tunahitaji maendeleo , Nadhani wizara ya Maji ndo kabisa itakufa kifo chema
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hebu jiulize tu wewe mwenyewe....ni mabaraza mangapi ya mawaziri yameshavunjwana kuundwa upya, ever since you can remember?

  Na ni wakati gani baraza baada ya kuvunjwa na kuundwa upya ambapo matokeo yake yalikuwa neema kwa wananchi?

  Chama kipya madarakani siyo guarantee ya ujio wa neema. Lakini hakuna ubaya kujaribu. Haya ma CCM tumeshajua jinsi yalivyo. Hayawezi kuongoza.

  I'm ready for a change.
   
 17. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kuna siku wana wema wa Tanzania watasimama na kuhesabiwa na mwenye kuwahesabu atawapa thawabu.Rafiki Zitto Zuberi Kabwe, Filikunjombe,Chadema kama timu ninyi mpo katrika hao.Keep it up,the struggle continues!
   
 18. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye kodi za mishahara.......tuna sheria moja tuu ya kodi ya mapato tunaomba ifanye kazi kwa usawa bila kubagua wafanyakazi wa umma na wa sekta binafsi.
   
 19. HT

  HT JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  politicians cannot be trusted regardless of their color, faith or party. one have to be a patriot to be trusted. is he?
   
 20. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Nimelipenda hili bandiko kwa kweli, siasa ni mchezo wa ajabu sana huwezi kuuelewa ukiwa nje. Kwa kauli hii ya ZZK ni kwamba kama mawaziri wengine wote wangejiuzulu mapema bila kujitetea (bila makuu) na rais akawarudisha yeye ZZK angewapongeza kwa hilo?

  Nini maana ya uwajibikaji? Ni kujiuzulu ghafla na rais akikurudisha haina shida kwa sababu tayari ulishajiuzulu? Tafadhali Mh ZZK naomba ufafanuzi wa hii kauli au uifute kabisa.
   
Loading...