Statement ya Mhe. Zitto Kabwe : To the Ministers-Nothing to Celebrate, go to work

mi bado sijaona cha ajabu zidi ya Mawaziri wapya; cha msingi kama Makatibu Wakuu wa kila Wizara hawatakuwa makini na kazi zao na hawa Mawaziri wapya wataendelea kulaumiwa pia. Kiutendaji Makatibu wakuu ndio watendaji wakuu kwa kila Wizara; uozo na uvundo unaojitokeza auwezi kuisha kama Makatibu wakuu hawatawajibishwa pia.

Zitto amesema waende kazini sawa lakini kazi yao hasa wanaijua????.
 
excellent advice..nyie kafungueni vyupa tu kusheherekea...kumbukeni 2015 is around the corner
 
Sioni sababu ya kuwapa ushauri! Ni bora tu waachwe waendelee kujichimbia kaburi na hatimaye waondoke wote kabisa.

Miaka zaidi ya 50 lichama hilo hilo limoja liko madarakani. Wengine tumechoka.

I want change, a breath of fresh air.

tatizo ni kuwa inafikiriwa kwamba CCM imepata viongozi "wapya". Watu ni wale wale, chama kile kile, sera zile zile.. kwanini inafikiriwa kuwa sasa watabadilika? Kwani hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri kubadilishwa? Ingekuwa kubadili mawaziri inabadilisha trajectory of leadership tungekuwa na matumaini kidogo. Nilitegemea kauli ingekuwa hakuna matumaini na wananchi wajiandae kuing'oa CCM in 2015. Tusiwape wananchi matumaini yasiyotimilika kwa kuendelea kuangalia mawaziri na uongozi wa CCM, uongozi ambao umejithibitisha kushindwa.
 
Kwa upya huu wa mawaziri tutegemee bunge lijalo litakuwa ni la kahidi tu basi...haswa hapo nishati na fedha....kama mjuavyo ndio tumeingia ofisini tunaahidi kulifanyia kazi.....
 
Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate. Hit the ground running.

Imetolewa na:

ZZK
Dar-es-Salaam
Jumamosi Mei 5 2012

well said sir!! ila hii issue ya RELI mpaka leo hii siielewi elewi...what really happened to reli zetu na miaka yote hii serikali ya kikwete imeshindwa kuja na solutions?
 
Mheshimiwa zitto, waache wafu wazike wafu wao, sisi tuendelee na m4c watatukuta mbele ya safari, wakati huu hata waziri akiwa malaika so long ni ccm hakuna jipya, nani amekuambia kuwa mwakyembe anaweza kujenga reli chini ya akina jk na el? Nani atamruhusu ajijenge kisiasa hivyo wakati walishamkosa kosa na sumu?
 
Yah. Hili la Zitto ni kweli kabisa maana jumanne tutashuhudia jinsi maua na mashahada yatakavyajazana pale IKULU kuwapongeza hawa jamaa maana kwa maisha ya watanzania kuteukiwa kuwa waziri ni sherehe badala ya kuwaza majukumu kuwa ni mazito wanawaza ULAJI na VX/V8.

Kwa Dr. Mwakyembe, tunajua kuwa RELI inahujumiwa ili magari ya wakubwa yasafirishe mizigo toka bandarini na kuwepo kwa reli ni pigo kwa biashara yao. Hivyo kama ulivyowahi kwisha sema wewe ni muwazi na mkweli, reli iwe ni alama ya utambulisho wa jina lako kwa watanzania.

Semi-trailler za wakubwa zinatuharibia barabara kila uchao kwa maslahi ya wachache walafi wa nchi. Fufufa reli yetu uwe shujaa mioyoni mwa watanzania. Otherwise, GOSE MALI GA NYANGI.
 
Duh! Kwa hiyo Zitto ameona kuna mabadiliko yamefanyika?!

Nilifikiri angeendelea na hoja ya kutokuwa na imani na PM!! Tena kwa dharau za rais kurudisha same crooks kwenye baraza,hoja ingekuwa na nguvu zaidi.

Halafu anakuja anaanza kuwapongeza! Mh!
 
hapa mtu anaweza kujiuzulu kabla hajaapishwa

Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in changamoto nyingi sana
 
Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza Kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea Kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.

Concept ya kumpongeza Mkuchika, kwa sababu kakubali kujiuzulu halafu karudishwa siielewi.

Naelewa habari ya kutoa mfano, lakini kama mtu anajiuzulu kikweli kwa kukubali makosa yake ningemtegemea kukataa appointment.

Hizi habari za kupongeza michezo ya "danganya toto", wapinzani wanamuandama waziri, waziri anajifanya kuwa na principle na kukubali kujiuzulu (pengine kwa maelewano na rais kwamba atarudishwa), anarudishwa, anakubali kazi, anapigiwa makofi kwa kutoa mfano. Changa la macho limekamilika.

Hivi Zitto anachopongeza ni nini hapa? Au ni mambo ya diplomatic rhetoric? Kama ni diplomatic rhetoric zinaweza kutuma "mixed signals" kwa watu tunaoangalia uongozi wa nchii hii critically.

Alhaji Ally Hassan Mwinyi alivyokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani miaka ya sabini aliwahi kujiuzulu kwa sababu alishindwa kuzuia mauaji ya wazee waliouawa kwa kushukiwa kuwa wachawi huko Shinyanga.. Nyerere akamsetiri mtu wake, akamtupa ubalozini Masr, akarudi uSpika baraza la wawakilishi, yalipotokea "machafuko ya hali ya hewa Zanzibar" na Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi kulazimishwa kujiuzulu, Nyerere akamweka Mwinyi kama "rais wa muda wa Zanzibar".

Uncle mmoja kwenye system akaniambia "huyu Mwinyi ndiye anakuja kuwa rais wetu baada ya Nyerere". Nilikuwa mdogo lakini nikaona, duh, watu washajua rais kabla ya uchaguzi? Mwinyi alifanya mengi mazuri, aliboronga mengi, lakini mie najiuliza mtu aliyekwishajiuzulu kwa nini apewe nafasi tena? Ya urais?

Ukijiuliza sana utaona uongozi wa nchi yetu kamwe haujawahi kuwa serious kwenye habari ya meritocracy.

Ndiyo maana tutashangaa sana watu wanataka kujiuzulu/ wanajiuzulu, halafu wanarudishwa. Washapiga ma deal mengi pamoja, wanaona kuongeza watu wapya kutaongeza risk. Bora tuendelee na network yetu ile ile.

Ndiyo maana hata baada ya miripoti ya CAG, hata hao waliotolewa kwa scandals kibao, huwezi kusikia hata mmoja kashtakiwa.

Ni kama vile Watanzania wanafanywa watoto wadogo, wanapigwa danganya toto ya kwamba kumtoa mtu mwizi uwaziri ni adhabu tosha.

Ujumbe kwa wezi wengine ni kwamba iba fastafasta, ukishikiwa bango sanasana utatolewa kazinai, hakuna kushtakiwa.

Naangalia tu hii nchi watu wanavyozidi kukosa imani na serikali. Kuna siku zitafyatuka kwa sababu watu wataona waziwazi kwamba hakuna hata tumaini la kupata haki.

Hapo ndipo habari zote za michezo ya redio ya kisiasa zitakapoishiwa nguvu, hata hao wapinzani watashindwa kuwazuia wananchi wenye hasira wakiongozwa na jeshi la wasio na ajira (takriban graduates 650,000 kwa mwaka wakati kazi zote katika formal economy ni takriban 500,000).

This is worse than corruption, the term doesn't do justice because it implies a deviation from some norm. What we have is a kleptocracy, in a sense that the abnormal is accepted as normal. The CAG reports are ignored, culprits are not prosecuted.

Hata vinara wa upinzani nao wanawapongeza "kwa kuonyesha mfano wa kujiuzulu nusunusu"!!!

Movie lile lile.
 
Zitto, Zitto,
Mkuu wangu huoni kama JK amechukua yeye sifa asizostahili kabisa maana alichofanya ni kufunika kombe wanaharamu wapite?. Huwezi kutegemea kwamba hili ni fundisho kwa viongozi bali ni mchezo ule ule tulouona wakait wa kina Karamagi, Meghji, Diallo na wengine wakati JK kisha badilisha mara tatu na hakuna bora lililotendeka zaidi ya kutazama makosa makubwa sio mawaziri bali mfumo mzima wa uongozi ndio mbovu. Huwezi kuwa mna Waziri mkuu alochaguliwa na rais, waziri wa wizara na naibu wake waliochaguliwa na rais halafu bado Katibu mkuu wa wizara kachaguliwa na rais! Hawa wote wanawajibika kwa rais, nani atamheshimu mwenzake?.

Mfumo wa utawala ni mbovu mbovu, hii unaondoa nguvu ya utawala bora hata kama mtabadilisha mawziri kila siku kutlingana na utendaji kazi hatutafanikiwa...Accountability inatanguliwa na Responsibility na ukisha weka vichwa viwili ktk jambo moja kila mmoja atakuja na lake na ukityazama scandal zote nchini zimetokana na kutoelewana ktk ulaji baina ya Waziri, Naibu na katibu mkuu. Mfumo mzima unajenga fursa ya FITNA baina ya watendaji na viongozi. Binafsi yangu sioni sababu ya kuwa na Waziri mku ukiwa na rais ambaye sii ceremonial, sioni sababu ya kuwa na Waziri msomi wa ikiwa una katibu mkuu ndiye mtendaji.

Kifupi mkuu wangu vita bado inaendelea yasikupumbaze kabisa matokeo ya baraza hili jipya maan sii swala la mtu mmoja, Ufisadi ni Gonjwa la Kitaifa halina mwisho kwa kubalisha watu maana huyo huyo waziri alifanya Ufisadi na watu wa nje, hakuufanya pekee hivyo hao watu wapo huru na wataingia tena kupitia mlango wa mbele kama kawa.
 
So much has happened and in the next three years, we really need to pray for our Nation since the game of politics has become like a football pitch.

God heal the wounds of the Nation as we pray for change and consideration of the common Mwananchi.
 
So much has happened and in the next three years, we really need to pray for our Nation since the game of politics has become like a football pitch.

God heal the wounds of the Nation as we pray for change and consideration of the common Mwananchi.

Praying is passive, we need to be more active.

We have been praying since before Mangungo, what good has it done us?

We pray too much, we do too little. We need to do more and pray less
 
as long as msanii bado yuko mjengoni mapambano inabidi yaendelee,hili baraza haliwezi kuwa na ufanisi kuliko raisi aliyeliteua
 
Katika siasa za ushindani sioni sababu ya kumpa ushauri mshindani mwenzio.

Rais Obama asingeshinda urais kama W angefanikiwa. Rais Clinton asingeshinda urais kama H.W. Bush angefanikiwa. Rais Reagan asingeshinda urais kama Jimmy Carter angefanikiwa. Tony Blair chama chake kisingeshinda ile 1997 kama John Major na chama chake wangefanikiwa.

Miaka 50 ni mingi mno kwa chama kimoja kuwa madarakani. CCM hawana jipya. Hata wamuweke nani kwenye baraza la mawaziri...hakuna jipya. Sera ni zile zile...mirangi yao ni ile ile na matokeo ni yale yale. That's insanity.

Hivi sijui wengine hawachoki kuwa na lichama limoja madarakani kwa zaidi ya nusu karne? Mimi nimechoka na kamwe sitawapa ushauri wa nini cha kufanya. Nitawaacha waharibu ili watu wazidi kupata sababu ya kuwatoselea mbali.
Aisee Nyani Ngabu umenikuna siyo mchezo. Mimi nakubaliana nawe kabisa kwamba huu siyo muda wa kuishauri ccm. Hiki chama kipo madarakani tangu uhuru takriban miaka 50 iliyopita na hakuna cha maana kilichofanywa na ccm kinacholingana na umri huo. Leo hii unaishauri ccm ili iweje!!! Ajabu kabisa. Solution hapa ni kukirushia vilago kikaendelee na usingizi wake wa pono na wengine waingie madarakani tuwaone. Kwa jinsi hali ilivyo, ccm hata ikikaa madarakani miaka mingine 50 tusitarajie mabadiliko yoyote mengine. Lazima wang'olewe ifikapo 2015.
 
Hata Mkuchika alitakiwa kutemwa! Watu kama akina Hawa Ghasia, Maghembe, Wassira, Mwandosya (angeachwa apone maana hawezi kuwa efficient ktk hali ya ugonjwa), Gerson Lwenge, Malima, Makala (ambaye walimtema uweka hazina wa chama, sijuwi kabadilika nini?) hawamsaidii kubadilisha chochote JK! Watu wamechoka na uwezo wa kufanya changes hawana. Mbaya zaidi kuongeza ukubwa wa baraza-kumbebesha mzigo mtz!
 
Back
Top Bottom