Startimes: kweli wandugu tumekubali kushindwa?

Kwa bahati bahati mbaya sana watu humu JF hamuaminiki, kila mtu anataka kuonekana mjanja kwa wengine..


Ndio maana ukiweka maujanja hapa wengine wanayachukua na kuenda kutundika FB..

Na wengine kupiga simu kwenye kampuni usika wakitaka kuelezwa namna ya kutumia huduma zao bure..

Watu kama hawa wamefanya baadhi yetu tuwe wachoyo wakushare maujanja hapa hivyo vitu vingi tuna faidi wenyewe kwa sababu kama hizo hapo juu. Tunahitaji kubadilika jamani.

na watu wenye viblogu njaa wanaanika maujanja ya jf, matokeo yake huduma zinasitishwa, hebu imagine siku zile net ya zero facebook ilipofungwa tukapata gap lingine hata miezi miwili haijapita jamaa wakafunga, yan nikimkamata mmoja nampa life ban
 
Habari njema kwako: waweza kuangalia chaneli zote kwa sh.900(mia tisa)tu kwa siku. Ukilipia ijumaa sh.2,700/= unaburudika weekend nzima, hii inakuepusha kulipia mwezi mzima wakati matumizi yako si kila siku.

Jaribu leo uone raha yake bila ya kuchakachua!


mmmmhh acha kumuingiza chaka mwenzako

4 * 2700 =10800

300 * 30 =9000

ipi expensive
 
Kuna channel za free hawazionyeshi kama itv,star tv, chanel ten ,clouds .kulikoni tunaona tbc tu
 
watanzania kweli wezi hakuna cha mkubwa wala mdogo, wote uzalendo sifuri, yaani king'amuzi cha sh elfu tisa kwa mwezi unataka bure? hata unga wa kula watoto utataka wa bure, sasa unadai maendeleo serikali ikufanyie wakati kodi hulipi inakuwaje ndugu yangu? jiulize mko wangapi wenye tabia hiyo na katika huduma ngapi hapa nchini?
 
Mkuu ee, buku 9 sio parefu kivile. Unless kama huitaji king'amuzi. Startimes being the cheapest. Nashauri aidha uachane nayo, ama uilipie. You dont have to crack everything.
 
Ebu kaka try hiyo ya tsh 900 per day. Nadhani nzuri, kma RUKU vile
 
Duh sasa kama hata Startimes imekushinda mkuu si balaa hili! Anyway maybe kuna namna ya kuchakachua si unajua startimes yenyewe ni ya wachina ambao nao ni mabingwa wa kuchakachua!

Mi na DSTV yangu kama sina hela poa tu naenda kuangalia mpira Bar, nikipata nasherehekea home....life goes on
 
Back
Top Bottom