That is very true.Dr ana mtaji wa kura 2010 ikiwemo ya kwangu ....
Mkiweka tamaa pembeni dr slaa anafaa sana tu
Habari za Jumapili wakuu.
Hadi sasa UKAWA wameamua kumsimamisha Dkt. W. P. Slaa kupeperusha bendera ya umoja huo Oct. 2015.
Kwa nini asiwepo Prf. wakati CCm wamesha weka Dkt.? au ndo miungu watu CHADEMA wanajifanya wamiliki wa UKAWA?
Hata kama siwaungimkono UKAWA katika mbio hizi ila ningejiuliza Prf. si ndio pigo muwafaka kwa Dkt. na mambo mengine tutajuana wanachama wenyewe kwa wenyewe.
cuf wameamua kujimaliza huku bara
Wewe Ruta umewaona Chadema tu kuwa ndiye wanaomng'ang'ania Dr Slaa kuwa mgombea wa Ukawa, unajifanya umesahau mgombea wenu wa CCM mzee wa mamvi ambaye 'timu Lowassa' waliapa kuwa iwe isivyo lazima mgombea wao ndiye atangazwe kuwa mgombea wa Urais, hadi wajumbe watatu wa CC wakiongozwa na Nchimbi kuutangazia Umma wa watanzania kuwa hawayatambui matokeo ya CC yao yaliyomuengua mzee wa mamvi?Chadema ndio wamiliki wa UKAWA na wana lazimisha Slaa aongoze jahazi wakati wanajua Slaa ni kiongozi wa dini na watanzania wengi hawato mpigia kura!
Mkuu unajisumbua bure Chadema hawawezi kukubali bora kila mtu aingie kivyake kwenye uchaguzi wapate kura mbili mbili.
Yaani nchi iongozwe na padre? Bora nife
Hivi unadhani Wazanzibar wanafikiri kama wewe?unadhani watampa kura Dr Slaa?Nampenda sana Dr Slaa na nadhani ana sifa za kuwa rais,ila sina uhakika kama atashinda.Tundu Lissu anaweza kuwa chaguo salama.
Kwa mtindo huo huo CUF waiachie CHADEMA nafasi ya kugombea urais wa Zanzibar na kwa kuwa CUF wana nguvu huko waipigie CHADEMA kampeni kwa nguvu.nimefikiri sana, jambo ambalo ni gumu sana kukubalika na CHADEMA, BADALA YA KUMUWEKA slaa awe mgombea, muwekeni lipumba na chadema wote na cuf mpigieni kampeni lipumba, tutaweza kumshinda kabisa magufuli, ila tukigawana kura kama kiwete alivyokuwa anasema jana, lipumba atachukua zake chache chadema chache na nyingi watabaki nazo kina maccm. chukueni ushauri huu. mimi ni chadema lakini nimefikiri sana namna gani tunaweza kumvunja shingo huyo nyoka anayeitwa ccm, nikaona bora tujifanye wajinga tu tumpe profesa.
Hata mimi naamini hivyo
Magufuli ni mkristo dhabiti kuliko huyo dk. Slaa, ka taarifa yako kama ulikuwa hujui
majembe ya KIKATOLIKI SLAA VS MAGUFULI.