Star TV, UKAWA wapo Millenium Tower Live

Inasemekana makubaliano yalikua seif zanzibar na dr bara ingawa kidogo lipumba akawa na interest hata hivyo wabunge wa cuf wamemuomba aondoe jina lake na wao wasaidiwe kwenye majimbo waliyoachiwa ili wapate viti .Kikubwa ile sera ya kila mtu apigane mwenyewe si nzuri CDM wanaaminiwa na wenzao basi wawasaide pale inapowezekana
 
Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA jana umeshindwa kufikia muafaka wa nani atagombea Urais kwa tiketi ya UKAWA. Kulikuwo na hali ya sintofahamu katika kikao hicho na kusababisha kikao kuisha bila makubaliano ya kumpata mgombea. Dalili zilionekana mapema ambapo mjumbe muhimu na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, Mhe. James Mbatia kutohudhuria kikao hicho muhimu.

Alohojiwa Kafulila kuhusu kutohudhuria kiongozi wake, Kafulila alisema kuwa Mbatia alikuwa mgonjwa. Hatujui hadi sasa huyo Mheshimiwa anaendeleaje. Kikao hicho kiliahirishwa hadi Jumanne wiki ijayo. Je wananchi hawa viongozi wetu watafikia muafaka ili tupate mtu wa kupambana na Mhe. Magufuli endapo atapitishwa leo na CCM. Kila la kheri UKAWA katika kikao chenu hapo Jumanne.

Wana JF mnakaribishwa kusoma uzi huu na kuchangia itakapobidi.
 
Hayo ndo matatizo ya kugawana vyeo,unapogawana vyeo sawa na kugawana maslahi lazima tu muafaka uwe mgumu ikiwa kama mna mchango tofauti katika kifuta jasho hicho ,ingekua kama utaifa umewekwa mbele katika kulikomboa kutoka kwa mkoloni mweusi bila kujali hayo maslahi ingekua rahisi .Na ndo maana ZZK haachi kupiga dongo kuwa ni umoja wa vyeo
 
Hao akina mbatia ndio kikwazo kutaka nafasi kubwa hata kama share yao ktk umoja wao ni ndogo. ...hao wameitwa ili kupata synergy
 
Na Magufuli hamumuwezi!
Mlitegemea awekwe Lowasa mpate pa kusemea, sasa imekula kwenu!

Ila nilikuwa naongea na Mbunge mmoja wa CDM anamlaumu wazi wazi Lipumba eti kwann amejitokeza kugombea Uraisi!
CDM wanasema wamewaachia CUF Uraisi Zanzibar nao waachiwe Uraisi wa JMT! Hapo hapo CUF wanaogopa wasiposimamisha mgombea Uraisi JMT watapotea huku bara!
Kazi mnayo
 
Hayo ndo matatizo ya kugawana vyeo,unapogawana vyeo sawa na kugawana maslahi lazima tu muafaka uwe mgumu ikiwa kama mna mchango tofauti katika kifuta jasho hicho ,ingekua kama utaifa umewekwa mbele katika kulikomboa kutoka kwa mkoloni mweusi bila kujali hayo maslahi ingekua rahisi .Na ndo maana ZZK haachi kupiga dongo kuwa ni umoja wa vyeo

mkuu bavicha hawaelewi hili....!!!!
 
Na Magufuli hamumuwezi!
Mlitegemea awekwe Lowasa mpate pa kusemea, sasa imekula kwenu!

Ila nilikuwa naongea na Mbunge mmoja wa CDM anamlaumu wazi wazi Lipumba eti kwann amejitokeza kugombea Uraisi!
CDM wanasema wamewaachia CUF Uraisi Zanzibar nao waachiwe Uraisi wa JMT! Hapo hapo CUF wanaogopa wasiposimamisha mgombea Uraisi JMT watapotea huku bara!
Kazi mnayo

Dr. Magufuli mwepesi sana. Si ndiye aliyeshiriki kuiba nyumba .za serikali?
 
Ukawa n nn??unaposema umoja ni muunganiko wa vyama kuwa chamakimoja..sijaelewa mnakaaje mkutano huyu chadema huyu tlp..nccr nakujiita muungano
 
Ukawa n nn??unaposema umoja ni muunganiko wa vyama kuwa chamakimoja..sijaelewa mnakaaje mkutano huyu chadema huyu tlp..nccr nakujiita muungano

Wanaigiza mpaka wanajiigiza wenyewe. . ., .kwenye hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom