Star TV should declare their interest

Star TV should declare their interest

Dawa ni kuanzisha kampeni ya kususia continental decoders
Wewe kama unataka kususa susa peke yako sio utafute uungwaji mkono kwa jambo la kijinga kama hilo. Mbona huongelei ITV ambayo imekuwa kama UKAWA TV? kila siku kulalamika bila hata kuwa na sababu za msingi, wakati dialo anaanzisha star Tv ulimsadidia hata senti tano? Kumbuka hiki ni chombo binafsi na sio cha uma kama TBC, Ukitaka angalia hutaki yote haituhusu kabisa.
 
Dialo anatafuta pesa ya kulipa wafanyakazi mshahara maana kufanya kazi star TV inahitaji moyo Sana inaweza pita hata miezi mitatu hawapati mshahara wanaishi kwa ofa tu.
 
Halafu vipindi vya kuponda CCM hamlalamiki ila mkipondwa nyie mnalalama msituzingue hapa.
 
Nimekuwa nikiifuatilia Star TV kwa muda mrefu hata kabla mchakato wa uchaguzi haujaanza. Niliifurahia kwa sababu walikuwa wakiita wachambuzi ambao wanachambua kwa kutumia independent mind.

Toka mchakato wa uchaguzi uanze hii TV imeanza kupoteza credibility, wanaita wachambuzi huku wanawapangia nini cha kuongea, unawaona watu wazima wanaongea mambo ambayo hayapo kwenye nafsi zao. Nimejaribu kufanya utafiti kupata habari za ndani kulikoni, mtu mmoja aliyepata za ndani ni kwamba Star TV imelipwa na CCM kufanya upendeleo wa makusudi katika habari na uchambuzi wake. Mtu huyu ameenda mbali zaidi akasema wamehakikishiwa na CCM kwamba hata wakipigwa faini na TCRA kama walivyofanyiwa Magic FM na TBC CCM wako tayari kulipa faini!

Ni jambo lililo wazi kwamba Star TV inamilikiwa na kada wa CCM Diallo, hilo halina ubaya na ana uhuru wa kikatiba kufanya hivyo. Kinachosikitisha ni kujifanya wako balanced wakati sisi watazamaji tunag'amua. Katika nchi zilizoendelea baadhi ya vyombo vya habari huwa vina declare interest katika uchaguzi kwamba wanaunga mkono chama au mgombea fulani. Kwa hiyo nawashauri star TV watutangazie wazi kwamba katika mchakato huu wa uchaguzi wanaunga mkono CCM bila kificho, tutawaheshimu kwa hilo na hiyo ni sehemu ya demokrasia ya kweli.

Nawasilisha

Mkuu umesahau kuwataka ITV, gazeti la Nipashe, Mwananchi, Mtanzania na Tanzania Daima waseme hadharani kuunga mkono UKAWA
 
mumesahau DIALO ni mwenyekiti wa CCM mkoa na pia yupo kwenye ile Timu ya kampeni ya makufuli so amewekwa kule makusudi ili TV yake itumike.
 
Katika kipindi hiki cha uchaguzi hakuna ubishi kuwa vyombo vya habari vinatumiwa na wamiliki wake kunufaisha upande wanaoupendelea,kuna wanaofanya hivyo kwa masilahi binafsi na wengine kwa ushabiki.
Kwa upande wa vyama mbadala huko mbele ya safari wanapashwa kuanzisha magazeti yao redio zao na vituo vya televisheni kama kweli wanataka watu wajue nini kianachoendelea kwenye vyama vyao,inashangaza kuona hata website za vyama haziwi updated sijui hapo wanategemea nani awatangaze kwenye kipindi hiki cha utandawazi.
Vinginevyo mtaishia kulalamika kila siku kuwa hamtendewi haki na mama wa kambo.
 
Star TV na kwa ujumla wake, Star Media Group wako biased sana, hadi dah....!
 
Nyie hapa mbona mnatukana hatusemi?. Fungueni kituo chenu cha habari msituzingue...
 
Kwa utafiti wangu mdogo nimeona kuwa Vyombo vya habari karibu vyote vimeegemea upande fulani ingawa hakuna kilicho declare interest yake. Tuangalie magazeti pia!!. Nadhani hili ni eneo la kufanyiwa kazi katika siku za usoni. Vyombo hivi kama vitafanya kazi yake vizuri kwa kufanya uchambuzi makini wa sera za kila chama kinachotaka kushika dola, ingesaidia sana kujua ni Tanzania gani tunataka kuijenga siku za usoni, huo ungekuwa ndio mkataba wa mgombea na chama chake kwa watanzania.
 
Nimekuwa mfuatiliaji sana wa jinsi matukio ya kampeni hasa kwa nafasi ya wagombea urais yanavyoripotiwa ktk vyombo mbali mbali vya habari hasa kuhusu kile kinachoitwa mafuriko au nyomi kwa lugha ya mitaani.

Kumekuwepo pia na tabia ya kurushiana lawama miongoni mwa vyombo hivyo kuhusu uhalisia wa nyomi hiyo.

Kumekuwa na maoni na ubishano kwamba picha tunazorushiwa ni za kutengenezwa kwa kuunganisha vipande vya picha zinazochukuliwa kutoka kona tofauti tofauti na kuzirusha kwetu kama 'live' wakati nyomi hizo huwa ni za bandia.

Leo asubuhi ktk kipindi cha Tuambie kinachorushwa na Star Tv mwandishi mahiri Deodatus Balile ametuthibitishia kwamba mchezo huo upo na umekuwa ukifanywa na baadhi ya wagombea ili kuonyesha kwamba wanapata wananchi wengi wa kuwasililiza wakati si kweli.

Nawauliza TCRA na hata NEC kwamba udanganyifu na uongo huu tunaolishwa na vyombo vya habari wao hawauoni? na kama wanauona wameridhika wananchi tulishwe uongo huo na vyombo vya habari ambavyo wajibu wake ni kutupa habari zilizoshiba ukweli?
 
Thanks to Social Media... Mainstream Media wamenunuliwa karibu wote ... Tulibaki na ITV ambayo nayo kila kukicha wanazidi kufifisha matumaini ya Watanzania... Haieleweki ilikuwaje wakaacha kurusha matangazo live Arusha! Haieleweki inakuwaje kwenye Taarifa za Habari Magufuli anapewa Muda Mwingi huku UKAWA wakipewa some seconds only .. TBC, STAR TV siku hizi huwa hatuangalii kabisa ... Nahurumia kodi yangu yenye kutumika in favor of CCM yenye kueneza Umasikini kwa Watanzania wenye Utajiri mwingi wa asili ...
 
Magazeti ya Mtanzania na Mwananchi nayo yametiwa kati ..sahivi mie sisomi magazeti kwasababu najua they aren't independent kwasababu wamiliki mpaka waandishi wao wamejaa njaa kari na wako kimakundi makundi ..ni ajabu kwamba waandishi badala ya kuandika ukweli wao wako kubanana kuandika habari za michongo, nitaanza kusoma magazeti mwezi ujao panapo majaariwa
 
Mmiliki mwenyewe mnafahamu alivyo popoma na mtu mwenye mijisifa za kijinga. Mimi ni mwenyeji wa mkoa huu na kwa akili ya Diallo anategemea asante ya uwaziri ama ukuu wa mkoa. Shame on him.
 
Thanks to Social Media... Mainstream Media wamenunuliwa karibu wote ... Tulibaki na ITV ambayo nayo kila kukicha wanazidi kufifisha matumaini ya Watanzania... Haieleweki ilikuwaje wakaacha kurusha matangazo live Arusha! Haieleweki inakuwaje kwenye Taarifa za Habari Magufuli anapewa Muda Mwingi huku UKAWA wakipewa some seconds only .. TBC, STAR TV siku hizi huwa hatuangalii kabisa ... Nahurumia kodi yangu yenye kutumika in favor of CCM yenye kueneza Umasikini kwa Watanzania wenye Utajiri mwingi wa asili ...

yaani anko usichemshe kodi yako inasaidia TBC haihusiki na Sahara Media Group. Hata IPP group wana vimbwanga vyao. Jiheshimu-uheshimiwe
 
tuwe wakwel mbna hatuisemi itv pia coz wao kukicha n kutangaza mapungufu ya ccm na kuucfia ukawa.
 
Sijalalamika, kama umeona hapo kwenye uzi nimetaja kwamba ni kada wa CCM, ninachotaka atanabaishe wazi upande wake ili tujue na hatutamchukia kwa hilo.

Kama ilivyo kwa kwa StarTv na ITV they should also declare their interest maana nao wapo upande mwingine tofauti na StarTv na hata mmliliki wa ITV naye ni wa kaskazini . Nyoka ni mbaya anapokuuma wewe lakini kwa mchina ni kitoweo
 
Back
Top Bottom