Star Tv Na Futuhi

BadoNipo

Senior Member
Jul 4, 2008
170
28
Jamani kweli The Commedy ilikuwa inatamaniwa na watu wengi sana. nimeshangaa sana jana kuona Star TV nao wameanzisha kipindi kinaitwa FUTUHI ni cha kichekesho kama cha the commedy yaani wamekopi kila kitu. lakini hata hawachekeshi sana zaidi na kuboa tu.

Wameniboa sana imeonyesha ni jinsi gani tusivyokuwa wabunifu
 
BN
kweli vichekesho vya jana viliboa lakini vya last week walichekesha sana hasa ile ya ule ushirikina aliofanya chenge bungeni na ile show ya mbanano kwenye treni somehow wanajitahidi tuwape muda
 
Nafikiri katika zama hizi za uwazi na uhuria wamelamba dume kuingia sokoni kwani watatengeneza jina.Jana hawakunifurahisha sana.Vilevile udhaifu wao ni kwenye ubunifu.

Wangetumia fursa hii ya ze comedy kutokuwepo kutangaza jina kusudi wateke watazamaji.Wazingatie kwanza kubuni siyo kuchekesha.Si unajua kuchekesha hakusomewi wala kulazimisha, ni 'inborn'.

Wangefuatilia kipindi cha "John stewart show" CNN.Jamaa anatoa vitu vya wakubwa live lakini katika sura ya kisanii.Habadili lafudhi wala kuvaa vibaya lakini ujumbe wake na jinsi anavyokejeli yale mabaya ya wakubwa ni kichekesho na somo tosha.
 
Kwanza hili neno futuhi! nikiswahili au kijaluo? nadhani hawa vijana wanaweza kuwa wazuri iwapo watapata mhariri mzuri. Tofauti yao na ze comedy wao wanaongelea matatizo ya msingi ya wananchi kuliko hao akinajoti walikuwa busy kudhihaki watu na kutumwagia mitusi!

unajua watz wanapenda kweli mambo ya kipuuzi! au ndo umasikini wenyewe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom