Star tv Live: Kukithiri kwa ufisadi, maadili yamepuuzwa?

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
Jamani kuna majadiliano yanaendelea on Star TV; CCM, CUF na NCCR wanatuwakilisha vyema.

Mada: Kukithiri kwa ufisadi, maadili yamepuuzwa?

Wageni:

Mwigulu Nchemba, Felix Mkosamali na Mnyaa
 
Mwigulu anatema pumba tu eti alishawahi kumuandikia katibu wa bunge kupeleka hoja ya ufisadi.
 
Azimio la Arusha wengi wanaliogopa,hata hao walioko studio,walio karibu waulizeni muone
 
Azimio la Arusha wengi wanaliogopa,hata hao walioko studio,walio karibu waulizeni muone
Hujakosea mkuu. Mkosamali analipwa mara 25 ya mshahara ambao angepata kama asingekuwa bungeni. Hivi kati ya mwalimu au daktari na mbunge ni yupi tunayemhitaji zaidi?
 
Mwigilu badala ya kujadili mada yeye anajitahidi kukisafisha chama ili kionekane kuwa rushwa wanazokula ni kawaida coz hata vyama vingine mbona wanakula. Tukisema tuishi hivi hii nchi itasambaratika.

Naunga mkono hoja za Mnyaa na Mkosamali we need to follow principles rather than propaganda
 
Mnyaa na Nchemba wanaogopa kutoboa jipu, wanazungukazunguka tu.

Mkosamali amekosa support ya Mdee hapo jipu lingepasuka.
 
Yahaya, ile taarifa ya CPW ilionesha kuwa moja ya suala lilowaangusha sana viongovi wa Bunge kwa wastani wa ufanisi wao ni namna walivyoshughulikia madai ya kuwepo rushwa ndani ya Bunge na miongoni mwa wabiunge.

Mfano ulotolewa ni jinsi walivyosghulikia madai ya Mh. Kafulila aliyewataja kwa majina wabunge waliodai Rushwa tangu Mei 2011. KWA HIYO VIONGOZI NA WASIMAMIZI WA MFUMO NDIO WALIOSHINDWA KUCHUKUA HATUA.

Mwigulu anaelezaje suala hili?

Mnyaa hajui kwamba kila sheria duniani ina mapungufu: muhimu ni zile nguvu za seria zinatumikaje kudhibiti hali iliyopo?? kwa hali ilivyo, hata kukiwa na sheria nzuri kiasi gani, kwakuwa viongozi hawawajibiki, haiwezi kufanya kazi. Mengine ni nyongeza.
 
Mwigulu nchemba ni mchumia tumbo hana jipya. Hoja zake hazina nia dhabiti ya kutatua matatizo sugu yanayoliangamiza hili taifa. Mara nyingi huwa anajenga hoja kuwafurahisha viongozi wa chama. Mimi ninakadi ya CCM ambayo niliichukua miaka mingi nilipokuwa chuo kikuu, lakini kwa sasa sina hamu kabisa na siasa za chama changu ambazo nyingi zina mrengo wa kulindana wao kwa wao.
 
mwigulu usitutishe kuwa tutakuja kulia,mmetuliza sana na hatuna cha kuogopa.nchi imeisha.
 
Mwigulu Nchemba anasema vyama vya upinzani wanachukuwa ruzuku halafu wanagawana, anaendelea zaidi anasema vinanuka rushwa kuzidi CCM tatizo hawajapata nafasi Watanzania watakuja kujuta.
 
Mwigulu Nchemba anasema vyama vya upinzani wanachukuwa ruzuku halafu wanagawana, anaendelea zaidi anasema vinanuka rushwa kuzidi CCM tatizo hawajapata nafasi Watanzania watakuja kujuta.
Sasa wewe ulitegemea aseme chadema itashinda?
 
Dah mkosamali anafunguka sana,mb unakopeshwa mil90 za magari,iweje ununue vogue ya mil300? Umepata wapi hela? Anasema mtu kama huyo kamata weka ndani.
 
Mwigulu hawezi kujielekeza kwenye tatizo yeye ni kujielekeza kwa chadema tu,wanairamba mnakazi sana.
 
Back
Top Bottom