Star TV Jicho Ndani ya Habari: Wameenda mbali zaidi ya 'Tumethubutu,...'

Mkuu ni kweli lakini nadhani unaona kuwa hayo mawili ya Elimu na Viwanda hajaenda vizuri kutokana na kukosekana mtu wa kuyafikisha mahali pazuri, bado linajirudia la uongozi bora.

Nimeipenda hii!
 
Hii ya kolero ndiyo way forward.. Au vipi! Yaani tufanye overhaul ya minds zetu,uongozi wetu,na tuchomoke[maana kukimbia tutachelewa],as if ndiyo tumekabidhiwa nchi ya Tanzania Bara na Waingereza jana! Asante.
 
Nakumbuka kuna wakati kutokana na ubora wake matairi ya General mtu ukifunga kwenye gari kila mtu anakuheshimu.... Hawa jamaa mabazaz kabisa!!!!!

halafu eti tuna maendeleo.. Wanasahau, wanajifanya wamelewa kiasi kwamba hawajui, chanzo cha uchumi imara hujengwa na viwanda!
 
Nakumbuka kuna wakati kutokana na ubora wake matairi ya General mtu ukifunga kwenye gari kila mtu anakuheshimu.... Hawa jamaa mabazaz kabisa!!!!!
Watu walikuwa wanaendesha kutoka Kenya kwenda Arusha kununua matairi hayo.
 
Tumeweza kusaidia ukombozi kusini mwa afrika+uganda kwa kuchangishana hata kuku....Leo hawana hata kumbu2!
 
Watu walikuwa wanaendesha kutoka Kenya kwenda Arusha kununua matairi hayo.

Nakumbuka tu tangazo lake...'GENERAL TYRE, EAST AFRICAA.....!!!!!!!!' Na nakumbuka mwenye tairi hizo kwenye gari lake alikuwa anaheshimika sana pia,sababu sijui! Mimi naangaliaga mijadala tunayobishanaga na Wakenya nakaa kimya! Ila nachojua waTZ ni vichwa, magenius,full maarifa! Tunaponzwa na kutojiamini,kukosa uzalendo na kujidharau bila kujua tunajidharau. Tanzania,Tanzania... Nakupenda Tanzania!
 
Hivi twaweza kurudisha ama kuanzisha mapinduzi ya viwanda? Maana shida ni kuwa hatuko focussed.. Ama tuna vipaumbele vingi...hatujui tushike lipi tuache lipi!
 
maendeleo ni kipimo cha jinsi binadamu alivyoweza kutambua na kuongeza thamani katika rasilimali zinazomzunguka ili kupata mahitaji yake ya kila siku. tusichanganye maendeleo (develpment) na ukisasa au usasa (modernisation). kama tumeweza kufika hapa leo ni dhahiri tumeendelea
 
Ungetoa mfano,wa thamani iliyoongezeka,na ni katika rasilimali zipi... Vague comments hazijadiliki!
 
Hivi twaweza kurudisha ama kuanzisha mapinduzi ya viwanda? Maana shida ni kuwa hatuko focussed.. Ama tuna vipaumbele vingi...hatujui tushike lipi tuache lipi!
...Mbona umeshatoa jibu! Tunahitaji kuwa focused. Lakini hii inahitaji real leadership.
 
Mkuu ni kweli lakini nadhani unaona kuwa hayo mawili ya Elimu na Viwanda hajaenda vizuri kutokana na kukosekana mtu wa kuyafikisha mahali pazuri, bado linajirudia la uongozi bora.
...Kwenye suala la uongozi bora, hebu tuingize mjadala wa kifilosofia kidogo. Kuna post moja humu ndani nilimwelezea Suharto -mla rushwa- na Nyerere -mchukia rushwa- na kumnukuu mtu mmoja akijadili jinsi Indonesia ilivyoendelea kwa kipindi hicho ukilinganisha na Tanzania. Sasa, tunaweza kujadili kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora, ingawa kuna watakaopinga, inategemea matendo yapi ni bora kwa mtu, jamii, taifa na mataifa.

...Hoja inabaki kuwa, Suharto hawezi kuwa kiongozi bora kama utasimamia kwenye ulaji rushwa. Lakini, kwa kusimamia maendeleo ya Indonesia kiuchumi na kijamii ataonekana kuwa ni kiongozi bora. Na kwa kuikazia hoja, tatizo la nchi hizi za kusini mwa jangwa la sahara -kwa mjadala huu- si rushwa ni upungufu wa utamaduni, mifumo na uongozi unaoweka mbele maendeleo ya mtu, jamii na taifa, kwa umoja wake.
 
maendeleo ni kipimo cha jinsi binadamu alivyoweza kutambua na kuongeza thamani katika rasilimali zinazomzunguka ili kupata mahitaji yake ya kila siku. tusichanganye maendeleo (develpment) na ukisasa au usasa (modernisation). kama tumeweza kufika hapa leo ni dhahiri tumeendelea
...Maendeleo ndio huleta uki[sasa] unaousema. Utakuwaje wa kisasa, kwa mfano, bila kuwa na maendeleo ya elimu, uchumi, jamii, n.k?

...Tufahamu pia kuwa, maendeleo hupimwa kwa vigezo kadhaa. Maana yake, ili uambiwe umeendelea lazima ulinganishwe na wenzako au na wengine kwa kuangalia mmetokea wapi kimaendeleo. Nadhani kila mmoja wetu anafahamu tumeshika nafasi zipi katika vigezo mbalimbali duniani. Kudokeza kidogo tu. Hivi majuzi watoto wa shule katika afrika mashariki walipimwa uelewa wao wa kiswahili, nadhani tunafahamu Tanzania ilishika nafasi ya ngapi.
 
Dar si Lamu,huwa napenda jinsi unavyojadili masuala. Nakubaliana kabisa na wewe. Bila uongozi bora,hata muwe na dira nzuri hamfiki mbali. Mi nadhani inatakiwa iwepo sera ya kudumu ya maendeleo. Kwamba kwa bajeti yetu tutafanya haya hata kama itachukua decades tatu na zaidi!na wananchi wote wanakuwa wanajua dira hiyo. Hata akija Rais mpya analijua hilo fika. Sanasana atatueleza mbinu atakazotumia kutufanya tuyafikie mafanikio katika mambo hayo tuliyojiwekea.
 
Back
Top Bottom