Star TV Jicho Ndani ya Habari: Wameenda mbali zaidi ya 'Tumethubutu,...'

...comte, nitatofautiana nawe kidogo, kuhusu elimu ya darasani kutufanya tudharau vitu vyetu. Sikumbuki mwalimu wangu hata mmoja aliyenifundisha kwamba vyetu ni dhaifu na vya nje ni bora zaidi. Nakumbuka viongozi wetu wanavyoshabikia manunuzi ya vitu vya nje na kuua uzalishaji wa vyetu wenyewe.

...Ni kweli elimu yetu ina mapungufu fulani. Enzi ya mwalimu tulikuwa na masomo na vipindi vya kujenga uwezo wa kujitegemea, lakini vililenga zaidi kwenye masuala ya kilimo na labda ufugaji. Kulikuwa na masuala ya ufundi pia. Ambacho hakikutiliwa maanani sana kilikuwa ni uongozi wa biashara na uzalishaji, lakini pia uongozi bora wa nguvukazi. Bila kusahau research and development

...Pamoja na mapungufu uliyoyabainisha, tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwenye hiyo elimu, kwani kwa ufahamu wangu, ilichokuwa ikikipima ni uelewa na si uwezo wa kukariri ambao pengine husaidia wanafunzi kufaulu lakini wakiwa hawana ufahamu wa mambo ya msingi kabisa.
inawezekana uko sahihi lakini hebu tutafakari kidogo pamoja. viongozi wetu wamesoma elimu ya darasani matokeo yake wanataka kuagiza kila kitu kutoka nje hata kuku. uongo kweli. nenda mlimani pale kama utakuta ugali wa mtama unaopikiwa na kupakuliwa kwenye chungu kama unauzwa na kuliwa.
kama kuna mechi ya ashati na azamu chamazi na man u na arsenal wakati momoja watu wataenda wapi? bado unaamini tunapenda vitu vyetu?
 
inawezekana uko sahihi lakini hebu tutafakari kidogo pamoja. viongozi wetu wamesoma elimu ya darasani matokeo yake wanataka kuagiza kila kitu kutoka nje hata kuku. uongo kweli. nenda mlimani pale kama utakuta ugali wa mtama unaopikiwa na kupakuliwa kwenye chungu kama unauzwa na kuliwa. kama kuna mechi ya ashati na azamu chamazi na man u na arsenal wakati momoja watu wataenda wapi? bado unaamini tunapenda vitu vyetu?
...Kuna mambo mawili yanayotufanya tuonekane au na tusipende vya kwetu.

...Kwanza ni kasumba iyotujaa ya kulimbukia vya wenzetu tukidhani wamevita ghafla, tukasahau, kazi ndio msingi mkuu wa maendeleo na hivyo kufanikiwa. Hatutafanikiwa kimichezo bila kuongeza juhudi katika mafunzo yake, malipo na maadili.

...Pili ni ubinafsi au na ufisadi wa kutaka kupata maslahi binafsi makubwa na si ya taifa katika manunuzi ya bidhaa toka nje. Hao kuku hawaagizi wao, hata hivyo hawajali nini kinaendelea, as long as wao na watoto wameshiba.
 
Back
Top Bottom