Star TV Jicho Ndani ya Habari: Wameenda mbali zaidi ya 'Tumethubutu,...'

Wanauliza nini maana ya MAENDELEO????? Dotto muongozaji wa kipindi anasema Nchi zilizoendelea hujulikana kuwa ni Nchi za Viwanda. Sasa je,tulipoua viwanda vyetu,je huko ni kutafuta maendeleo?
 
mratibu wa kipindi anajiuliza, Mchina akija kukutembelea akiona unatumia vyombo, nguo, chanuo,n.k. vya kutoka kwao China anajisikiaje? Ama we Mtanzania ukienda nchi za nje, ukakuta kahawa,na bidhaa mbalimbali za kitanzania zinatumika katika maisha yao ya kila siku,je ungejisikia namna gani?
 
kaktika uchumi kuna view za aina mbili.

A.traditional view

B.morden view.

Tz tunatumia view ya A kupima maendeleo yetu ambacho sio kigezo sahihi. Mana kina consider kigezo cha GDP PEKEE.
 
Mratibu wa kipindi amesummarize kwa kusema, pamoja na mengi,kwamba anashangaa kuona timu ya Kilimanjaro Stars,imeshindwaje kuandika jina la nchi kwenye jezi! Rwanda,Uganda,hata Zanzibar,wameandika! Hili sikuwahi kuligundua!
 
haya masuala naona kila mtu anaongelea tu lakini tusichojua wengi wetu ni je, ni watu wangapi hapa "Tanzania Bara" (naona ndio jina jipya linalotumika sasa kuelezea nchi hii) wanaweza kuongea na kusikika!? ...unakuta ni wale wale 20%!
Angalia miradi yote iliyofanyika (hasa hii miaka ya 2000), angalia 'signposts' za project zote kuanzia barabara, maji, shule, afya nk zimefadhiliwa kwa zaidi ya 70% na fedha kutoka nje ya nchi. Na nadhani ndicho chanzo cha kuifanya nchi hii iwe ya 3 kuwa 'kuombomba' duniani!
Tulingeliweza kukumbuka haya pamoja na mengine mengi, tusingetumia (wasingetumia) muda huu kusherehekea bali wangetumia muda huu kutafakari. Hii inabatilisha kauli mbiu ya "Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele". Ni kweli hatujaweza mengi tuliyothubutu na kama tunasonga mbele basi hatujui hata tuendako!
tumeweza kuongeza chuki na gap kati ya walionacho na wasionacho.

Amedhubutu kutambulisha udini katika sehemu mbalimbali nchini mwetu.

Amesonga mbele kwa kuua uchumi kwa nguvu zake zote.

Uhuni hoyee
Tumeweza kuongeza shule,vyuo ili hali mashirika ya umma mengi yamefilisika,no creation ya vyanzo vya ajira,sijui itakuaje
Wamegusia kilimo pia,je, ilikuwaje miaka 50 iliyopita,tukathubutu vipi, tukawezaje?kulikuwa na jembe la mkono, je kutumia pawa tilla ndio kuweza?
 
nimekupata lukindo. Bora maadhimisho haya yangemalizika na mijadala ya namna hii.. Sio mtu anachekelea sarakasi za uwanjani za watoto kufunzwa na Wachina!
 
Mtu ambaye alitoa machozi katika hotuba yake ya kwanza bungeni akiwa Rais,na kutufanya hata wale ambao hatukumpigia kura,tuanze kuwa na imani naye! Akatueleza kuwa,HE MAY BE WEARING A SMILE BUT HE IS FIRM ON ISSUES! Akatutafsiria kuwa tusimwone kwa haiba yake ya kuchekacheka,kwani ana msimamo kwenye masuala ya msingi.. Nilitegemea jana alie! Tena alie zaidi ya alivyowahi kulia hapo kabla katika maisha yake! Kwa sababu jamani,hawa wanaogombea nafasi mbalimbali,inabidi kuwaangalia kama kweli wako dhati kulikomboa Taifa letu lililodumaa[maana si changa tena]. Kama hatujaweza kuwaamini,tuwaulize watuthibitishie!! Kwamba tutawaamini vipi? Ah Tanzania,nchi yangu Tanzania!
 
Na mimi najiuliza hivyohivyo nahisi hali itakuwa mbaya kama hii trend haitabadilishwa. Na wananchi wenyewe ndio wakuleta hayo mabadiliko kwa kupiga kura bila kushawishiwa na pilau.
Tumeweza kuongeza shule,vyuo ili hali mashirika ya umma mengi yamefilisika,no creation ya vyanzo vya ajira,sijui itakuaje
 
Yaani kama vyombo vyote vingekuwa na kautaratibu kama StarTV nadhani wangemulika hali halisi na WaTZ wote wangejitambua lakini baadhi ya ni upopompoo mpaka basi kama Tbc sitakagi hata kuangalia hovyo kabisa.
 
...Kuna yule bwana mmoja -nadhani ni mwalimu au kitu kama hicho- ametoa mfano wa baba anayevaa suti kali, lakini watoto dhoofu bin hali. Akasema, angekuwa yeye ange"overhaul" serikali nzima.

...Cha muhimu ni kuwa, tumeacha kufanya vya msingi ili wananchi wa kawaida wapate ajira na kuongeza kipato, tumebaki wachache kujilimbikizia mali na anasa.

...Ilibidi tuwekeze -kwa kuanzia- na tushawishi ujenzi wa viwanda ambavyo vingezalisha kutokana na malighafi tulizonazo, kuongeza thamani yake na kuwapatia wananchi ajira na kipato zaidi. Tuna misitu na tunavuna magogo, lakini tunayasafirisha nje na kununua samani zisizodumu. Hapo tumepoteza ajira na kipato cha watanzania na tumefaidisha wengine. Viwanda vya mbao na samani vingetoa ajira kwa watanzania na kukuza vipato vyao, nao wangenunua mali nyinginezo zinazozalishwa na wenzao na kukuza uchumi.

...Unawezaje kusema kilimo kwanza -kwa mkulima wa pamba-, wakati hakuna viwanda vya kufuma nyuzi, kutengeneza vitambaa, na nguo. Vilivyopo ni vichache na vinaagiza malighafi nyingi toka nje.

...Hatutaweza kuondoa tatizo la ajira na kukuza vipato vya watanzania kwa kutegemea kilimo -na kwa maana hiyo kukiita, kwanza au uti wa mgongo au ujuavyo vingine- bali kwa kujenga viwanda vitakavyotumia maghafi zetu na kuziongeza thamani, vitakavyozalisha bidhaa zisizohitaji teknologia ya hali ya juu kabisa. Vijana wengi wako mijini, wanafanya uchuuzi wa bidhaa toka nje, hali ambayo si endelevu na inadidimiza maendeleo. Hatuwezi kuwa na maendeleo kwa mfumo huu. Hawa walipaswa kufanya kazi viwandani na kuwa wateja wa bidhaa za wazee wao toka mashambani.

...Mjadala wa leo ulikuwa mzuri. Nampongeza Dotto kwa kipindi chake. Tuambiane ukweli, labda tutausikia na kuufanyia kazi hatimae. Hatutaendelea kama taifa bila viwanda, vidogo na vikubwa.
 
ukiangalia bora hata ukoloni wa mzungu ulikuwa na maendeleo kweli kuliko ukoloni wetu wa weusi kwa weusi
kweli kabisa ....hata miji wakoloni ilipangika ukiona dar au nairobi ya mkoloni ni tofauti sio rahisi wakati ule kujenga mji bila miundo mbinu yaani hata maji machafu na masafi leo hatujui tunafanyaje dar tulileta wazungu kutusaiddia bara bara wachina kibao kila macine moja ina mchina .leo nini tunafanya wenyewe nyerere alituachia kiwanda cha baiskeli leo kiko waip?

 
kweli kabisa ....hata miji wakoloni ilipangika ukiona dar au nairobi ya mkoloni ni tofauti sio rahisi wakati ule kujenga mji bila miundo mbinu yaani hata maji machafu na masafi leo hatujui tunafanyaje dar tulileta wazungu kutusaiddia bara bara wachina kibao kila macine moja ina mchina .leo nini tunafanya wenyewe nyerere alituachia kiwanda cha baiskeli leo kiko waip?


Cha General Tyre East Africa je!!
 
Ndo naangalia sisiemu wanazani maendeleo ni kua na maghorofa kibao dar si lamu.

Tunadanganywa kama watoto! Siku moja mkuu wa kaya akasema mnasema hakuna maendeleo wakati foleni za magari mnaziona! Halafu akacheka kwa kebehi!
 
Jamani nimefurahi sana, tumethubutu ndio maana hata mizinga tu ya kufungia nyuki bado tunaagiza. Ni kweli tumethubutu kumaliza madini yetu na tumeweza kubadilishana na vyandarua. tumethubutu kuwa na Rais anayelinda Mafisadi na tumeweza, tumethubutu kutaja mafisadi wakasema hatuwawezi na tukashindwa kuwafukuza. Mbona kauli mbiu Iko sashihi? Tumethubutu kuibiwa na tumeweza na tunasonga mbele kuibiwa, na kulinda wezi.

Hii sijui nani angesaidia kujibu..
 
ukiangalia bora hata ukoloni wa mzungu ulikuwa na maendeleo kweli kuliko ukoloni wetu wa weusi kwa weusi

Wataalamu wa mambo ya kisiasa,walitabiri ama kuonya kuwa ukoloni wa weusi utakuwa mgumu sana kuondoka!
 
Na mimi najiuliza hivyohivyo nahisi hali itakuwa mbaya kama hii trend haitabadilishwa. Na wananchi wenyewe ndio wakuleta hayo mabadiliko kwa kupiga kura bila kushawishiwa na pilau.

kuna uelewa na mwamko mkubwa sana..sema basi tu! Kama vyama pinzani vingesimamisha mgombea mmoja wa urais
 
Back
Top Bottom