Star Time hamtutendei haki.

Eraldius

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
1,120
906
Hivi mnajiona sawa.Mpaka tv inayoendeshwa kwa kodi zetu tuilipie? Eti airtime ikiisha wanakata mpaka TBC1.Kwahiyo nayenyewe tuite chanel ya kulipia.Kweli hii ni TEKNOBANIA
 
cha ajabu ni kwamba, pale kwangu kimara mwisho haikamati, nimejaribu kuelekeza kiantena kisarawe weee haikamati, nikakirusha kabatini nikanunua kingámuzi kingine....kwasababu nilishakinunua, naomba waweke mitambo ya kusambaza network yao dsm nzima...kuna maeneo mengi tu dsm hayakamati..hasa kimara huku.
 
Hivi mnajiona sawa.Mpaka tv inayoendeshwa kwa kodi zetu tuilipie? Eti airtime ikiisha wanakata mpaka TBC1.Kwahiyo nayenyewe tuite chanel ya kulipia.Kweli hii ni TEKNOBANIA

Nakubhaliana na wewe kua hawa wanatuibia sana na technologia yao ya kichinachina.
Lakini hapo kwenye red! NO. Kwa sababu hapa kwangu siku ya tatu hii wamekata coz sijalipa lakini tbc 1 tu ndo kama kawa inaonesha.
 
cha ajabu ni kwamba, pale kwangu kimara mwisho haikamati, nimejaribu kuelekeza kiantena kisarawe weee haikamati, nikakirusha kabatini nikanunua kingámuzi kingine....kwasababu nilishakinunua, naomba waweke mitambo ya kusambaza network yao dsm nzima...kuna maeneo mengi tu dsm hayakamati..hasa kimara huku.

Umenunua decoder gani inayokamata vizuri zaidi?
 
mbona mimi sijalipia na ninangalia tbc1 hawajaikata, na ninaishi kimara stop ninapata stesheni zote kwa ile antena ya ndogo ya ndani.
 
Ingetakiwaga isinunuliwe kamwe hala tuone wangepeka wapi!

Kale kadeki chao nimeweka hapa ndani tu!
Haikamataki!
Wizi mtupu!

Nafikiri hili ni mradi wa mtu fulani fisadi
 
Bw.Hute suala la kukamata au kutokamata signal linatokana na eneo ulipo mfano Kimara kuna mabonde na milima yakutosha inategemea wapi ulipo. ama sio?
 
Inabidi tupeane maujanja jinsi ya kukichakachua uwe ulipii na unakamata stesheni zote.
 
Inakera zaidi pale unapangalia kitu / habari nzuri mara ina stuck.......utasubiri hapo na ikirudi ule uhondo umeshapita. Yaani ni balaa. Nimemulizia mtu wa hapo kwao anadai ninunue antenna ya nje coz mm natumia antenna ndogo ya ndani.
 
pia walisema sabasaba waweka geographical mbona hatuioni,ubc wameireplace na emanuel tv hu ni wizi manina zao startym
 
awa jamaa uozo kweli,tena matapeli wasiojua kusoma nyakati
 
Ukitaka mateso nunua star times! Mara imekata, mara imeganda, kama antena ya nje ndo kabisa. Utaenda kuzungusha mpaka miguu iume! Ila ukikamata free channels ndio raha tupu. Ziko clear full mamuvie halafu bure!
 
Mkuu, kusema kweli hakuna sababu ya kulipia channels za humu nchini, hata na zile za Kenya mbona DSTV tuna angalia bila kulipiaTBC1,CITIZEN,KBC,CCTV na nyingine za kidini. Kwa maoni yangu STARTIMES isilipishe Channel zote za TBC, ITV(wakikubaliana),Channel10, MlimaniTV, ATN, CCTV, CITIZEN, KBC na za Uganda.
 
Inakera zaidi pale unapangalia kitu / habari nzuri mara ina stuck.......utasubiri hapo na ikirudi ule uhondo umeshapita. Yaani ni balaa. Nimemulizia mtu wa hapo kwao anadai ninunue antenna ya nje coz mm natumia antenna ndogo ya ndani.

Hata ukinunua antenna ya nje ku-freeze mara kwa mara kwa picha na sauti kuko pale pale, uwezi kulinganisha StarTimes na DSTV. Mimi naona mambo ya kutokuwa serious na customer care kume-trickle down kutoka TBC mpaka StarTIMES!
 
Bw.Hute suala la kukamata au kutokamata signal linatokana na eneo ulipo mfano Kimara kuna mabonde na milima yakutosha inategemea wapi ulipo. ama sio?

Mkuu mbona niliwahi kuwasikia STARTIMES wanasema wana mbinu za kusambaza mawimbi kwenye mabonde na milima bila matatizo! Sasa sijuhi hizo zilikua ni mbinu za kuwachota akili raia au nini sijuhi!
 
Ukitaka mateso nunua star times! Mara imekata, mara imeganda, kama antena ya nje ndo kabisa. Utaenda kuzungusha mpaka miguu iume! Ila ukikamata free channels ndio raha tupu. Ziko clear full mamuvie halafu bure!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom