Kwa kuwa Stanbic wamegoma, na Inaonekana wana baraka za wakubwa flani kutoitoa orodha, je Hakuna sheria za nchi zinazoweza kuwalazimisha kutoa hiyo list? Japo majaji wetu nao walikula cha juu lakini nahisi kutakuwa na taratibu kama sio za hapa basi hata kimataifa.
Hakuna sehemu tunaweza kuishtaki stanbic wakatoa ile list?
Heshima kwenu wanajamvi !
Heri kwa sikuuu ya Xmas na Mwaka mpya 2015
Harbinder ameonesha ni namna gani alivyo mwananaume wa shoka,watu wenye dhamana wanaogopa kufanya maamuzi ya maana juu ya ESCROW kwa kwa kulinda maslahi ya Taifa, kisa ni huyu Singa na washarika walionufaika na Issue nzima ya IPTL/ESCROW.
Kwa namna ilivyo Harbinder Seith Singa ni mtu mwenye nguvu mpaka kiasi Dola inahofia,vyombo vyote ikiwepo Mahakama ,vimewekwa mfukoni na huyu mtu, watuhumiwa walio wengi wa hii Saga hii hawajaguswa.Kwa hoja hiyo huyu bwana anastahili kupokea pongezi,naam huyu ni mwanaume wa shoka,mpaka Serikali inamtetemeka ,na kuogopa hata kutekeleza maazimio ya Bunge!!!
Naam,Tanzania tu mambo haya yanawezekana,Ingekuwa China kwa issue kama hii tayari tungekuwa tunashuhudia misiba na maombolezo ya watu kunyongwa. Ila Tz kwa vile ipo kwenye AUTO PILOT mambo haya yanaonekana kama comedy ya akina JOTI na BAMBO.
Ningekuwa na muda wa kutosha ningetunga shairi la kumsifia Harbinder Seith Singa kwa namna anavyoichezea Serikali.
Congratulation Harbinder for keeping our government in your Pocket.But I wonder how great your pocket is? Enough to keep our government in your pocket ? Keep it up Harbinder.
Nawasilisha kwa kejeli moyoni naumia.
UKANA SHILUNGO,
Likizoni Masasi.
Na akili yangu inanituma kwamba ujio wa Zuma ulikuwa na kitu flan kuhusu Escrow kwa sababu stanbic ni member wa standard bank ambao ni South Africa based.
Ebu tuchangamshe akili hapa.