Madhara ya chama kutawala muda mrefu. Watu huanza kwiba na kudharau waajiri wao ambao ni wananchi. Unapoona rais wa nchi haelewi kwa majibu yake kwa wananchi, jua kunatatizo. Lapili, tabia yakuwekana madaraka na kundi la watu waliokua na lengo moja tuu, kupora rasilimali za nchi. Fikirieni, ni ndani ya uongozi wake huu, nchi imepitia matatizo makubwa ya kiuchumi. Kumbukeni, waka anaingia madarakani 2005, mzee mkapa aliacha dola moja (1$=900 hadi 1000). Leo jiulizeni tumefika wapi? Ma skendo kibao yenye kuhujumu nchi: EPA, RICHMOND, wanya pori kusafirishwa nje ya nchi, ESCROW, na mikataba mingine kibao isio na manufaa kwa nchi. Kwavile wanawekana, hata akija mwingine wa chama hikihiki, ataendeleza maovu na kufichana.