Staili za kulia msibani!

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Wana MMU habari,

Kwanza kabisa napenda kutoa laana zangu za dhati kwa yule member aliyesema MMU Ifungwe.

Pili, ningependa tujadili swala la kulia msibani,
Kuna watu wanalia kwa staha na kuonyesha machungu yao toka moyoni,ila kuna kundi la pili ambalo linakua kwa kasi,la waombolezaji wanaolia kwa unafiki na kebehi.
Utakuta mtu analia na kugaragara chini,kuanzia sebuleni mpaka nje ya nyumba.
Jaman huu ni ungwana?
 
We ni nani hata uamue kwamba mtu akilia kwa sauti tu na kujigaragaza anakua analia kinafiki???
Kila mtu ana namna yake ya kuonyesha furaha/masikitiko...wako ambao hata kulia hua hawalii kwasababu
sivyo wanavyodeal na machungu yao.Kwahiyo kwasababu tu wa pembeni hafanyi kama wewe
haina maana anakosea.

Hujawahi kuona watu ambao wao wakiwa na furaha sana wanaishia kulia badala ya kucheka??Tuwaite nao ni wanafiki
kwasababu wanaonyesha furaha yao tofauti na watu wengine?

Jibu...SIO UUNGWANA wewe kupangia watu namna gani waonyeshe machungu yao.
 
ukiona mtu analia kwenye msiba ujue analia na mengi hivyo sio rahisi kwa wewe uliye nje ya nafsi ya yule mtu uweze kutambua hisia zake.
 
We ni nani hata uamue kwamba mtu akilia kwa sauti tu na kujigaragaza anakua analia kinafiki???
Kila mtu ana namna yake ya kuonyesha furaha/masikitiko...wako ambao hata kulia hua hawalii kwasababu
sivyo wanavyodeal na machungu yao.Kwahiyo kwasababu tu wa pembeni hafanyi kama wewe
haina maana anakosea.

Hujawahi kuona watu ambao wao wakiwa na furaha sana wanaishia kulia badala ya kucheka??Tuwaite nao ni wanafiki
kwasababu wanaonyesha furaha yao tofauti na watu wengine?

Jibu...SIO UUNGWANA wewe kupangia watu namna gani waonyeshe machungu yao.

Elewa fact.

Elewa hoja.

Na uchangie.
 
Na wale ambao wakipata taarifa ya msiba,wako macho makavuu
halafu wanapitia bar kwanza,wanakunywaa,ndio wanaelekea msibani kutoa 'perfomance' ya kulia....
 
Labda umekutana na wale Professional Waliaji Misibani! Wale wanalia hata mzazi wa Marehemu wanamzidi!

Ukijua mahusiano HALISI ya mliaji (ktk kundi unalolalamikia kuzidisha speed na maonesho ya uchungu) ingekusaidia kuwa na nguvu kutoa hoja yako.
 
nakuna wengine staili zao za kulia ni kuwatazama watu....mtu yupo chumbani lakini
anaenda kusimama dirishani na kuliaa weeee mpaka watu mnaulizana kwani yule na marehemu walikuwaje...
unaambiwa aahh ni jirani yake tu....lol
 
Wana MMU habari,

Kwanza kabisa napenda kutoa laana zangu za dhati kwa yule member aliyesema MMU Ifungwe.

Pili, ningependa tujadili swala la kulia msibani,
Kuna watu wanalia kwa staha na kuonyesha machungu yao toka moyoni,ila kuna kundi la pili ambalo linakua kwa kasi,la waombolezaji wanaolia kwa unafiki na kebehi.
Utakuta mtu analia na kugaragara chini,kuanzia sebuleni mpaka nje ya nyumba.
Jaman huu ni ungwana?[/
QUOTE]
Labda ni mapepo.
 
Ama marehemu kaugua mwaka mzima, hajaenda hata kumuona wala kupiga simu! Siku anafika msibani analia kuliko mke wa marehemu na wauguzaji! Wonders will never cease
Na wale ambao wakipata taarifa ya msiba,wako macho makavuu
halafu wanapitia bar kwanza,wanakunywaa,ndio wanaelekea msibani kutoa 'perfomance' ya kulia....
 
Tupo tofauti, hili linatufanya tuwe na aina tofautitofauti za life style.
 
Misiba imekua ndio sehemu za biashara siku hizi, kila kitu ni show, all plastic ndugu yangu.
Utapeli na kupoteza muda tu!
Lakini wabongo utawaeleza nini?! Wao hodari wa kupotezeana muda tu!
 
misiba ya siku hizi imekuwa ni sehemu ya mauzo yaaani wauza sura tu,kuna watu wanalia msibani kwa kelele hata chozi hana,
 
Mara nyingi watu wanaopenda kufanya maonesho sio real!Ndo maana kwenye maandiko wameitwa wanafiki,so kiukweli wanakera,hata kusali Yesu alisema "ingia ndani funga mlamgo na madirisha kisha usali"kama jambo jema kama kusali linatakiwa lifanyike kwa staha sembuse kuomboleza?
 
Nilidhani unazungumzia mlio wa kitandani! ya misibani sitapenda nijadili maana kila mtu anastyle zake za kulia. hata wanaume wanalia misibani, na wengi wao wanalia moyoni kitu ambacho ni ngumu ku assess.

Kuhusu milio ya kitandani ukikuta mwanamke analia mpaka anagaragara huyo ni mfanyabiashara mkuu angalia sana!
 
We unawaza ngono tu.
 
Mkuu hiyo inategemeana na makabila,mfano waarusha wengi wao wanawake unakuta wanajigaragaza na unakuta mtu mpaka anazimia,nadhani ni maumivu na sio unafki unaosema,mtu hawezi akalia mpaka akazimia halafu useme ni unafki,kila mtu ana moyo wa aina yake,kuna wengine wakiachwa na wapenzi wao wanakunywa sumu,sasa je msiba siyo zaidi?mi nadhani ni jinsi mioyo ya watu ilivyo,mwingine anaweza kujikaza na mwingine hana huo uwezo.
 
Na wale ambao wakipata taarifa ya msiba,wako macho makavuu
halafu wanapitia bar kwanza,wanakunywaa,ndio wanaelekea msibani kutoa 'perfomance' ya kulia....
Basi ina maana wamepokea huo msiba kiasi kwamba heri akapoteze kwanza mawazo huko baa
 
Back
Top Bottom