Sports analysis 'box to box '

Baada ya heka heka na pilika pilika za champions league now bundesliga is back!!!!!
Tuweke kando homa za uefa maana imebaki story, wale wa kubebwa wamebebwa na kubebeka now lets focus kwenye michezo ya weekend hii ambapo upande wa BL sherehe zinaanza leo saa 3:30 (tatu na nusu) usiku huu ambapo fc cologne (koln) ikiongozwa na striker wao Anthony modeste itakua kibaruani dhidi ya Hoffenheim.

Hoffenheim wenyewe wakiongozwa na kocha wao mdogo kabisa kuwahi kutokea katika ligi kuu ya ujerumani Nagelsman (miaka 28) wanahitaji droo tu ili waweza kujihakikishia kucheza michuano ya ulaya mwakani (either uefa au europa) kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hyo.

Isitoshe endapo Hertha berlin itamfunga wolfsburg hapo kesho na hoffeinhem ikashinda leo basi vijana wa Nagelsmann watakua wamejihakikishia kucheza uefa hapo mwakani. Yatakua ni mafanikio makubwa sana kwa kocha wao Nagelsmann maarufu kama "baby mourinho" mwenye umri mdogo kuliko baadhi ya wachezaji wake.

Anthony modeste ye atakua anacheza na timu yake ya zamani, ambapo hadi sasa ana magoli 23 kwenye ligi kazidiwa na PEA na Lewa pekee.

star times mechi itakua live WORLD FOOTBALL
Asante kiongozi ...mapendekezo yako naona yalitimia kwa Hoffenheim
e8c398ef97686f160a7678dcd42e2449.jpg

Japo walimiliki mpira haswa Hoffenheim iliwachukua mpaka dakika as lala salama kupata bao make Koln japo kuna kipindi walikuwa wanapoteana uwanjani lakin making nzuri iliwachukua daki 58 kujipatia bao Hector akimpasia vyema Bittencourt ...

Mfumo wao Hoffenheim 3-1-4-2 niliupenda na wananyumbulila haswa ...haikuwa bahati yao Koln make 93 kusawazisha na kujihakikishia nafasi ya 3 credit keep Hoffenheim
 
mbali na mechi ya leo, mechi zingine weekend hii ni Hamburg SV wenyewe watawakaribisha vibonde Darmstadt hapo jumamosi, vibonde wengine kwa msimu huu the wolves wakiongozwa na mchezaji mwenye jina kubwa kuliko uwezo wake mario gomez watasafiri hadi mji mkuu wa ujeruman kukutana na wahuni wa mjini Hertha berlin, wakati Ingolstadt wenyewe watawakaribisha Werder bremen.

Mainz 04 baada ya wiki iliyopita kuchukua point tatu na goli moja toka kwa hertha berlin wenyewe watajaribu kurusha ndoano kama watapata bahati ya kubebwa kama wale wengine dhidi ya bayern munich isiyo na Neur.

Augsburg wenyewe watakutana na Frankfurt waliopigwa weekend iliyopita goli tatu na vijana wa black & yellow (Bvb), Augsburg watawakosa washambuliaji wao wawili Ja-cheol koo na Finnbogason baada ya kulimwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Berlin.
Asante mkuu kwa updates na uchambuzi yakinifu
 
Jiunge na group la whatsap la betting lenye members zaidi ya watu 170 upate mikeka ya uhakika na ushauri mzuri kuhusu mechi na company za betting. Kujiunga ni bure na ushauri na mikeka yote ni bure bado watu wachache group lijae. Linki iyo hapo chini.<br /><br /><br /><br />Betting only
we jamaa unakera unajua???? kama watu hawataki kujiunga na group lako si unapotezea tu
 
mchezaji wa dortmund aliye kwa mkopo Freiburg Pascal stenzel anaipatia goli la pili freiburg akitokea sub dhidi ya leverkusen.

game ipo live
 
b109b0e2b0001eee7c5368b6a78078b3.jpg

Naanza kuamini Neymar atakuwa jino siku za usoni mdomoni mwa fc Barcelona, anapokosemana hakuna wakuziba panabaki nafasi na sio mwanya...... Kuna wakati Messi alionekana kummis Neymar sababu mpira ulikuwa ili ufike mbele basi inabidi Messi mwenyewe na Iniesta wahusike kwa asilimia kubwa sana......

Bado lile tatizo la Real Madrid katika kiungo litaendelea kuwa tatizo sugu...... Mondric, Kroos na Casemiro kuna wakati wanajikuta wanafanya kazi moja tu kukaba na kuchezesha timu ila kazi ya kupandisha timu imekuwa miguuni mwa Marcelo mara zote.

Madrid wamekuwa na tatizo la mipira ya mwisho.... Hili tatizo linatokana na viungo wawili wa nyuma kati ya wale watatu(Kroos na Mondric) kuwa chini sana wakati timu ina shambulia na ndio maana mara nyingi nafasi za magoli zimekuwa zilitoka pembeni mwa uwanja...... Ukiachana na Marcelo na Carvajol kama watu wanaotengeneza nafasi nyingi za magoli ila Bado Marco Asensio ndio mwanadamu katika wale watatu wa mbele aliye na final touch ambayo Madrid amekua akiikosa kutoka kwa Bale, Benzema na Ronaldo. Hili linaweza likawa tatizo sugu kwa vijana wa Zinedine Zidane.

Ter Stegen na Keylor Navas mnastahili pongezi sana kwa asilimia kubwa mmefanikiwa kuficha baadhi ya makosa ya mabeki kushindwa kuwalinda..... Fc Barcelona Bado beki haijawahi kukaa sawa ila pia Real Madrid Bado beki haipo sawa kipindi hichi.......

Deni la Gareth Bale kwa Real Madrid na ada ya Perez ni kubwa kuliko alichokifanya katika ile BBC..... match fitness pamoja na injuries za mara kwa mara zinampunguza makali na kumgongezea deni mbele ya mashabiki wa los Blanco......

Messi na Ronaldo wakiondoka tutawamisi sana..... Sijajua Mungu atatuletea wakina nani tena machoni mwetu na kwenye balloon d'Oro zao..... Leonel Messi Leo anakuwa bora mbele ya Christian Ronaldo kwa kuibeba timu katika mchezo muhimu kama huu ninawawaza sana watakao kuwa na majukumu baada ya hawa wanadamu.

Ukweli ni kwamba Barcelona wanahitaji wahitimu wa La Masia pia Madrid anahitaji Galatico wapya ili heshima yao iendelee Kudumu siku za usoni.....

Alichokifanya Sergio Roberto ni marudio ya ushujaa katika uwanja mwingine.... Maana yeye ndio kaamua mchezo uisheje kwa kumfungisha tela Marcelo.....

Real Madrid 2-3 Fc Barcelona.
 
Huu mchezo aliupoteza ZZ toka alivopanga kikosi, ameamua akomae na BBC wakati ana vijana wenye uchu na magoli kama morata, Asensio i will take also vazquez ahead of benzema, Benzema amekua mzigo mzito sana kwa attacking force ya madrid but still ZZ anamuanzisha, sipati picha morata huwa anajisikiaje anapoona benzo anakumbatiwa hivo.

Bale alikua katoka kwenye injury katrain kwa siku mbili tu, unakuja kumuanzisha kwenye mechi ngumu na ya kuamua ubingwa kama hii, mwisho wa siku anaku-cost sub. Marcelo, Ramos, Casemiro wote walikua hovyo, huwa nawashangaa sana mashabiki wa madrid wanapo msifia casemiro na kumuona Busquet wa kawaida.

Nadhani ni muda sasa wa ZZ kuachana na hyo BBC yao, awaamini vijana kama wanalengo la kupata chochote msimu huu
 
Mkuu umeongezea vyema .ana vijana wengi wa kubadirisha matokeo tatzo lake BBC sijui anawaamini nini
 
433928d4059ac92d6b0a64449aecc22c.jpg

4dfeab2c3506d0ebcf79a0c282b85607.jpg

Waliwahi kusema: HIS SINGLE PASS CAN CHANGE THE GAME.
Andrea Pirlo:

Kabla sijafahamu uzuri Andrea Pirlo akiwa na jezi ya AC Milan, kumbe alipita Inter Milan kuanzia 1998, alicheza michezo 22 tu ya Msimu mmoja wa 1998-1999 kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Reggina mwaka 1999, na Msimu wa 1999 - 2000 alitumikia tena kwa mkopo akiwa na Brescia, kabla ya mwaka 2001 kuuzwa rasmi kutoka Inter Milan kwenda AC Milan ambapo ndipo na Mimi nilianza kumfahamu na kuvutiwa naye na hatimae kuwa mshabiki wake mpaka kesho.

Fundi huyu wa pass zenye mnyooko wa rula, aliitumikia AC Milan kwa miaka 10 yenye mafanikio kwake na kwa timu pia. Kuanzia mwaka 2001 akivua jezi ya Inter Milan na kuvaa jezi ya AC Milan mpaka mwaka 2011. Kupitia miguu yake AC Milan ilivuna ilichokipanda, kupitia image yake yeye mwenyewe alijivunia alichobarikiwa, kupitia miguu yake tulimtaja kama mmoja ya waitaliano bora kabisa wenye uwezo wa kubadili mchezo kwa pasi yake moja tu...... Alibarikiwa Imani na kubebwa na nyota ya kupendwa huyu ni Andrea Pirlo.

2001-2011 babu huyu fundi wa eneo la kiungo, alifanikiwa kuchukua Serie A mara 2(2004 na 2011), kafanikiwa kuchukua Italian Cup(2004), hakuacha pia Italian Super Cup(2003), akafanikiwa zaidi kuchukua Champions League mara 2( 2003 & 2007), na baadae UEFA Super Cup mara 2(2003 & 2007), Club World Cup. Tunahesabu lakini.....

Hapa Pirlo alituvutia Wengi sana, tukawa teyari tushajenga imani na miguu yake katika kila inachokifanya katika kuugusa mpira mbele ya macho yetu. Nyakati hizo ndizo nyakati ambazo Carlo Ancelotti alikuwa amembadilisha kutoka katika possession aliyokuwa akiicheza kama kiungo mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji wa kati, na kumpatia majukumu mapya ya kushuka chini na kucheza mbele ya mabeki wa kati (deep lying playmaker)..... Tukaanza kumuona akianzisha mipira chini na kutuliza timu. Mpaka Leo hii babu huyu mwenye umri wa takribani miaka 38 anacheza katika eneo ambalo mwanadamu Carlo Ancelotti alimwona ndilo eneo lake sahihi.

Baada ya kuweka heshima ya kutosha akiwa San Siro na Giuseppe Meeza. Kuanzia mwaka 2011 mpaka mwaka 2015 Heshima yake iliendelea kubebwa na ubora wa miguu yake. Anakwenda kuvaa jezi ya ndoto zake, jezi ya kibibi kizee cha Turin Juventus. Akiwa na Juventus aliendelea kufanya vile vitu vilivyotufanya tumtaje kwenye mabishano na mijadala yetu vijiweni. Kama kawaida hakuwazidi kuniangusha katika kufufua mipira iliyokuwa imekufa, aliendelea kuwa bora sana katika mipira ya kuvusha eneo la katikati ya uwanja na kumfikia mlengwa( hapa tulimwita mgombanishi).... Okay... Akiwa na Juventus alifanikiwa kuchukua Serie A mara 4, akachukua Italian Cup na Italian Super Cup. Kule Milan walimtaja sana ila huku Turin wakamuimba zaidi na zaidi.

Kabla hajatangaza kuvua jezi ya timu ya taifa ya Italy (Azzuri)..... Alitufanya tumtaje na kumuwaza kama ni miongoni mwa viungo bora ambao wanasumbua akili za makocha wanao kutana na taifa la Italy...... Aina ya uchezaji wake Bado tuna tafuta mtu wa kumfananisha naye, nguvu kidogo ila akili mingi... Akiwa na jezi ya Italy alivutia zaidi katika aina ya uchezaji wake. Nakumbuka mambo mengi sana kuhusu Pirlo na jezi ya timu ya taifa ila Pole penenka dhidi ya Joe Hart. ...
Tangu 2002 mpaka 2015 (116 caps, 13 goals: akiwa kachukua World Cup) akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Italy. Hiyo imetosha yaliyobaki yakiobaki tutasimuliana kwa mdomo tuache maandishi yapumzike....
93720ee8c8db58f0b34637dd2f589219.jpg

New York city fc..... Ndio sehemu aliyopo hivi sasa
Na teyari ameshatangaza kuvua viatu vyenye Meno sita, baada ya kuvua jezi ya Inter Milan, AC Milan na
Juventus.... Na sasa anataka kutundika jezi yenye Etihad kifuani katika enga ya geto na kurudi kuishi kama binadamu wa kawaida... Baada ya kucheza michezo 715 ngazi ya klabu, 116 akiwa na jezi ya Italy na kufunga magoli 86 pamoja na kushinda vikombe 18.
e48466731bb46d4489f8bbac72e3aa25.jpg

Jiandae Pirlo kudondosha chozi... Miguu yako ni rafiki wa mpira ule wa duara na hautolia mwenyewe mpira nao utatoa chozi kabla ya wewe kupokea Maua kutoka Milan, Turin na New York. Najua utatumis ila nasi tutakutaja sana katika mabishano yetu vijiweni....
a17c266bb105f0757738b32159693016.jpg

Respect .....
5baf394819f6e9438b8249b87da9d7a4.jpg

HK
 
Wakuu hivi kuna mwenye maono na hii picha na kilichotokeaa katika mechi iliyochezwa haswa baada ya kusawazishaa bao??

ff532f41ae0c2e7aa57752fe7dcd058e.jpg
 
Good News; Galatasaray after hearing of Emmanuel Eboue's situation:

Offered Him U14 Assistant Coaching Role
Provided Him With Accommodation
Sufficient Salary to Re-Build His Life

Unbelievable Gesture
b68c446fbb1c288a299fad72d5b06138.jpg
 
Back
Top Bottom