Sports analysis 'box to box '

mukishinda ndio munakuwa wachambuzi sana. Siku ya 4:0 na 1:0 haya maneno hatukuyasikia!
Mkuu kama wewe ni shabiki wa Chelsea kwenye "Chelsea special thread ile mechi ya 1-0 hii post naimani ulikutana nayo ...

"Imagine Chelsea without ng'olo or Kante".... Wale waliobuni lile tangazo la super sport sijui waliwaza nini nimewaza hapa kutokana na kazi wanayotoa wale super sport na Yule ng'olo kante wao.....

Chelsea anatembelea kichwa, miguu, akili, moyo, mapafu na macho ya Claudio Kantelele........ Kuna wakati unahisi wapo kante watatu uwanjani.... Mmoja ana analinda, wa pili anachezesha timu na mwingine anashambulia...... Mungu kamuumba kante mfupi, mweusi lakini anawazwa sana kuliko watu mweupe na warefu.....

Marcos Rojo kwanza ndio afuate Dave save(de Gea).... Mabeki Wengi Wakizungu wanakosa roho mbaya miguuni na umafia.... Wao wamejaaliwa umafia pekee Bila roho mbaya miguuni. Washambuliaji wa kaliba ya Diego Costa wanahitaji kukabwa na mabeki kaliba ya Marcos Rojo...... Beki bora kabisa wa kati katika mchezo huu maana kumficha Diego costa huyu sio kazi rahisi.

Bado Conte anahitaji ku install mbinu za ku unlock padlock kama zile zilizowekwa na Manchester united.......

Kadi ya kwanza laini kabisa na kadi ya pili ndio nyepesi kabisa hapa ndipo kila mtu anaukimbia uamuzi...... Waswahili wanasema kila shetani na Mbuyu wake na Oliver ni mbuyu wa shetani mwekundu tu......

Hakukua na jinsi ilikuwa ni lazima mmoja w afungwe na atoke...... FA cup robo fainali kushney..... Tukutane nusu fainal.

Mwenye bei halisi ya Kante jamani kabla ya dirisha la usajili kufika ?

Chelsea 1-0 Manchester united.

Karibu mkuu
 
Wakuu Kwema

Achilia mbali kupanda na kushuka na zile mbio za ubingwa kwa wale wawili juu ,top four bado kizungumkuti ..


.
87c6eb52ad02b1ccf51cabe3ecceb6e5.jpg


Alexis Sanchez akitaka mshahara mnono ni haki yake ..... Ila pia akitaka kuondoka kwenda kutafuta mikono juu ni halali yake pia.... Mesut Ozil akitaka kuondoka ni halali kwake, ila pia akigoma kusaini kandarasi mpya ni haki yake pia..... Mzee Wenger akiomba mkataba mpya ni halali yake, ila pia akibebewa mabango ni haki yake pia. Watu wanataka mataji, wachezaji wanataka mataji ila mabosi wanamtaka mzee Wenger.

Kuna wakati akili zetu zinajidanganya kweli ila ukweli ni kwamba Arsenal ni Arsen wewe kubali wewe kataa. Mabosi wameshakubali Arsenal iwe halali yake na mashabiki hawamtaki wakiamini Arsen sio haki ya Arsenal.....

Endelea kujiuliza kwanini wazungu wamemjumuisha Alexis katika PFA player of the year list..... Alafu unalala wakati unajua uhalisia na ugumu wa michezo ya jumatatu.....

Vita ya top four sio mchezo.... Wacha tulaumiane maana huu Msimu ni wa lawama tu.

Tukutane baadae make hii wiki ya kulaumiana ...
 
Diego Simeone: "Griezmann works like a central midfielder, assists like a number 10 & finishes like a number 9." The perfect striker.



3450a65d51276357c2fb7738154bd0b1.jpg



Ila wakùu tukumbuke Mtaji wa goli moja nyumbani ni mtaji mdogo sana kwa Atletico Madrid na pia kuwabakisha mchezoni Leicester city..... Namna Leicester walivyocheza first leg sina shaka ni miongoni mwa timu ngumu iliyokutana na timu nzuri ya Atletico. Aina yao ya mchezo wa ugenini ni dhahiri shahiri wanamatarajio makubwa leo katika mchezo wa nyumbani King Power stadium.

Kiukweli bado maamuzi ya waamuzi yamendelea kuwa tatizo katika michezo mingi ulimwenguni...... Aina ya penalt aliyotoa Mwamuzi wa mchezo huo yalikinzana sana na macho yetu sambamba na screen zetu.....japo mimi nilijua labda kwa kuwa natumia Hitachi kichogo lakini nilivoangalia tena kwa jirani nilijiridhisha..

Mpira ni mchezo wa makosa na katika Zama hizi ukikosea kidogo refa anakosea sana...... Greizman alichezewa faulu nje ya box pembeni kidogo ya mstari wa box lakini kwakua mpira ni mchezo wa makosa basi refa akafunika mkono na kinaliwa tuta lililofanya wawakilishi pekee wa lawama ligi kuu ya Uingereza kulala kwa goli moja Bila.....

Sasa shughuli inahamia pale king power stadium leo na hii inaweza kuwa sehemu ngumu sana kuamua mchezo huu...... Best team loss.... kuna wakùu mbakunbuka Leicester walikuwa wazuri sana katika pressing ila pia Atletico walikuwa bora zaidi kimbinu.

First leg ..Atletico Madrid 1-0 Leicester city...

Second leg ...Leicester ....-. ..Atletico Madrid
 
4c2b5a1217ec780334f3945d2befdd41.jpg


Walioichezea Leicester city Leo na walioishuhudia Leicester city Leo watakuja kuadisia wajukuu na watoto wao kesho...... Inawezekana Atletico Madrid ndio timu nzuri kabisa na sahihi kwa Leicester na historia yao katika michuano hii na katika hatua hii.... Matokeo fair kabisa maana kwa Leicester city na historia yao hawajabebeshwa kapu... Ila ni matokeo ya kawaida sana kwa timu yenye kaliba ya Atletico Madrid. 1-1 hapa king power stadium na 1-0 kule Vicente Calderon ni matokeo ya kuadisia kwa Leicester city ya kesho.

Nendeni sasa nadhani hapo mtakuwa mmeshaonja utamu wa EPL na raha ya UCL....... Najua vita ya top four nyinyi hamuiwezi pambaneni muwe angalau mnacheza Europa league maana jezi zenu ni nguo za kushindia huku kwetu.

Leicester city 1-1 Atletico Madrid (aggr 1-2).
 
Wakuu kwema...??

7dcdfeec0614c66fc0c5cf93b58975c5.jpg


Possession ni kitu ambacho hakiwasumbui fc Barcelona, ila kuitumia hiyo possession katika kuleta matokeo mazuri nacho sio kitu cha kuwasumbua fc Barcelona, ona possession haijawasumbua Barcelona wala kuzitumia possession haikuwa tatizo kwa fc Barcelona, tatizo lilikuwa ni Juventus kukaa kwenye mianya/ njia zote za mipira ya fc Barcelona katika eneo lao la chini na katika eneo ambalo fc Barcelona walitakiwa kuitumia possession kupata matokeo mazuri......

21c575cc235f0838de8cd137a5f4a3f6.jpg


Juventus walikuwa wazuri sana katika defensive na offensive kwa wakati....... Tuliwaona Juventus wakiwa na mipango mingi wakati wanazuia ila pia tuliwaona walikuwa na mipango finyu wakati wanashambulia...... Juventus walikuwa bize na kukaba wote kasoro dybala tu.... Pia tuliwaona Barcelona wakiwa bize na kushambulia kama kawaida yao ila pia walikuwa na tatizo katika kuzuia mashambulizi kama kawaida yao...

8af76f246b885baf59010d6b06c9a6ef.jpg


Mungu wa fc Barcelona ndio Mungu wa Juventus turin.......
0b0342512bea755fa1084eb214a89648.jpg


Miujiza haitokeagi mara mbili kwa wakati mfuatano, 1 attempt on target, possession 64% ya Barcelona dhide ya 36% na 4 attempt on target za Juventus na bado ilikuwa ni dhambi kwa Juventus kutoka Bila kupata goli kwa nafasi walizozitengeneza, hapa ndipo pale waswahili walisema upele humuota asiye na kucha...

..
412e0ec32e222232e18f15ccf6be1662.jpg


Fc Barcelona wanahitaji mbinu mpya, wachezaji wapya, mipango mipya, benchi la ufundi jipya na Iniesta , Xavi na Messi mwapya pia.....
a3691e0f95d6a0f7c519df3b75d5f67c.jpg

Fc Barcelona 0-0 Juventus (aggr 3-0).
 
d0cb560d0732fbd48476769e4112dcce.jpg

ea5b81f9e2bbd3eef3f6fbbb1cf43311.jpg

Borussia Dortmund hakukuwa na namna ya kuwazuia AS Monaco.... Kwa maana Borussia Dortmund hawajarudi katika ubora wake wanakutana na Monaco iliyokatika ubora wake...... Sikuwahi kuwaonea Borussia Dortmund huruma ila kupangiwa Monaco tu niliwaonea huruma kiukweli kabisa.
1f53668322cdbf56ea90217dd23a9105.jpg


Monaco ni timu nyingine ngumu kisirisiri katika timu ngumu zilizoingia nusu fainal..... Sipendi Atletico Madrid apewe hawa jamaa maana kuna kitu kitawasikitisha watu..... Over.

Wakuu ila Mimi nina maswali 1k k ichwani na yenyewe nahisi bado machache ...mwenye kujua tofauti ya huyu bwana mkubwa tusaidianee
bab93024a4e85584c78310d1f53bb1aa.jpg


f4a826ffd1fddbba8ca7e0594fcba476.jpg
3dad83a8f6d86aac8d5298297eb41c1f.jpg


Na huyu apa ....
4922e5e1673fc122b95ddac4249edb3b.jpg


Make kazi zake simuelewii kabisa
69f1438710b904cd274557a613127f6c.jpg


Monaco 3-1 Borussia Dortmund (aggr 6-3).
 
heshima kwako lee empire unajua juventus baada ya kupoteza ile final dhidi ya barcelona mwaka juzi kwa mtazamo wangu wao ndio timu pekee barani ulaya ambayo imeamua kufanyia marekebisho kikosi chake, tulizoea kuona juventus wakicheza zaidi mfumo wa aina moja tu mechi zote wa 3+5+2 ila kwa sasa juventus wana uwezo wa kuchea style yoyote ile na ndio maana wamekuwa tishio kutokana na uimarishaji timu walioufanya.
heshima iwe juu yake Beppe marotta kwa kazi nzuri anayoifanya. namuomba mungu nusu final iwe kati ya madrid na juventus halafu gemu ianze bernabeu,
natamani
nishuhudie timbwili la mchezaji bora wa dunia wa mwaka huu Marcelo 12 na dani alves.
 
heshima kwako lee empire unajua juventus baada ya kupoteza ile final dhidi ya barcelona mwaka juzi kwa mtazamo wangu wao ndio timu pekee barani ulaya ambayo imeamua kufanyia marekebisho kikosi chake, tulizoea kuona juventus wakicheza zaidi mfumo wa aina moja tu mechi zote wa 3+5+2 ila kwa sasa juventus wana uwezo wa kuchea style yoyote ile na ndio maana wamekuwa tishio kutokana na uimarishaji timu walioufanya.
heshima iwe juu yake Beppe marotta kwa kazi nzuri anayoifanya. namuomba mungu nusu final iwe kati ya madrid na juventus halafu gemu ianze bernabeu,
natamani
nishuhudie timbwili la mchezaji bora wa dunia wa mwaka huu Marcelo 12 na dani alves.
Umenena vyema ...acha tuone kesho droo inakuwaje ...
 
Umenena vyema ...acha tuone kesho droo inakuwaje ...
Madrid wanajitambua.
Sifikiri ilikua kazi rahisi kuwazimisha bayern kwani na wao walikua na mpango wa kulipa kisasi.

Watazamaji tuliona game rahisi kwa Madrid lkn hesabu za kufanya iwe hivyo si za nchi hii.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Jiunge na group la whatsap la betting lenye members zaidi ya watu 130 upate mikeka ya uhakika na ushauri mzuri kuhusu mechi na company za betting. Kujiunga ni bure na ushauri na mikeka yote ni bure. Linki iyo hapo chini.<br /><br /><br /><br />Betting only
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Baada ya heka heka na pilika pilika za champions league now bundesliga is back!!!!!
Tuweke kando homa za uefa maana imebaki story, wale wa kubebwa wamebebwa na kubebeka now lets focus kwenye michezo ya weekend hii ambapo upande wa BL sherehe zinaanza leo saa 3:30 (tatu na nusu) usiku huu ambapo fc cologne (koln) ikiongozwa na striker wao Anthony modeste itakua kibaruani dhidi ya Hoffenheim.

Hoffenheim wenyewe wakiongozwa na kocha wao mdogo kabisa kuwahi kutokea katika ligi kuu ya ujerumani Nagelsman (miaka 28) wanahitaji droo tu ili waweza kujihakikishia kucheza michuano ya ulaya mwakani (either uefa au europa) kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hyo.

Isitoshe endapo Hertha berlin itamfunga wolfsburg hapo kesho na hoffeinhem ikashinda leo basi vijana wa Nagelsmann watakua wamejihakikishia kucheza uefa hapo mwakani. Yatakua ni mafanikio makubwa sana kwa kocha wao Nagelsmann maarufu kama "baby mourinho" mwenye umri mdogo kuliko baadhi ya wachezaji wake.

Anthony modeste ye atakua anacheza na timu yake ya zamani, ambapo hadi sasa ana magoli 23 kwenye ligi kazidiwa na PEA na Lewa pekee.


star times mechi itakua live WORLD FOOTBALL
 
mbali na mechi ya leo, mechi zingine weekend hii ni Hamburg SV wenyewe watawakaribisha vibonde Darmstadt hapo jumamosi, vibonde wengine kwa msimu huu the wolves wakiongozwa na mchezaji mwenye jina kubwa kuliko uwezo wake mario gomez watasafiri hadi mji mkuu wa ujeruman kukutana na wahuni wa mjini Hertha berlin, wakati Ingolstadt wenyewe watawakaribisha Werder bremen.

Mainz 04 baada ya wiki iliyopita kuchukua point tatu na goli moja toka kwa hertha berlin wenyewe watajaribu kurusha ndoano kama watapata bahati ya kubebwa kama wale wengine dhidi ya bayern munich isiyo na Neur.

Augsburg wenyewe watakutana na Frankfurt waliopigwa weekend iliyopita goli tatu na vijana wa black & yellow (Bvb), Augsburg watawakosa washambuliaji wao wawili Ja-cheol koo na Finnbogason baada ya kulimwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Berlin.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom