Sports analysis 'box to box '

Umasikini wa Leicester city ni katika kiungo cha kati (central midfielder) hapa Claudio Rainier anaumiliki wa viungo wanne (mendy, amartey, king na Drinkwater) ambao wanauwezo wa kupambana na viungo wa timu nyingine kwa asilimia kadhaa..... Hawa Leicester city wamewekeza (invest) sana katika sehemu tatu za timu yao.... Wamewekeza katika back line, wamewekeza katika attacking midfielders na pia wamewekeza katika strekers..... Waliridhika na viungo wa kati kwa kusahau kuwa Drinkwater na Kante walikuwa free from injury muda mwingi katika kipindi cha ubora wa Leicester city.

Leo katika mchezo dhide ya Middlesbrough... Katikati ya dimba ndipo sehemu iliyopata tabu sana kwa Leicester city. Forshaw, de roon na Clayton viungo hawa wa Aitor Karanka wameweza kumfundisha kitu Claudio Rainier.

Leicester city walianza kushindwa kuanzia katikati ya dimba alafu ndio ulloa na Okazak wakafuata. Kama sio uimara wa Morgan, Huth, Futch na Simpson basi ubao ungesomeka vibaya. Kuna wakati kuwa na sehemu imara moja kunaiokoa sehemu dhaifu mara chache kama hivi.

Ranier alifahamu kitakachotokea Msimu huu ndio maana hakutumia muda mwingi kusherekea ubingwa ila alitumia muda mwingi kuuguza mgonjwa wake..... Dah kulamba sukari Msimu uliopita na kunywa chai isiyo na sukari Msimu huu vinaweza kumtesa sana Ranier kuliko Mahrez na Vardy.

Boro anaendelea kubaki nafasi ya 16 na alama zake 19... Huku Leicester city akitanua katika nafasi ya 14 na alama zake 21.

Last game 0-0 Hk
 
Dah..... Kweli usipoenda kwenye harusi za wenzio nao hawatokuja kwenye mazishi yako.

Arsenal aliuliwa lakini hakufa moja kwa moja.... Ila Bournemouth nao wakafa robo. Vitality stadium ni kiwanja kingine kigumu sana katika EPL..... Bournemouth walikuwa vizuri sana sana kabla ya red card na hata baada ila makosa yao katika making ndio yaliyoifanya come back ya Arsenal kuwa na nguvu.

Uchovu wa kupumzika siku moja na kucheza tena hii umechangia uchovu kwa timu zote.... Ila Bado Arsenal wana mhitaji sana Cazola na Wilshire katikati au mbele ya Xhaka na coquelin kuliko iwobi.

Muulizeni Wenger vipi January atasajili ata mchezaji mmoja tu ?....

Fraser Fraser...... Nikawaza kama Yule Jack Wilpower angekuwa kauzwa kwa Bournemouth na sio mkopo ingekuwaje pale kati, uchanganye na ile Fraser....

Siku Giroud akiondoka arsenal basi ujue mwezi utakaofuata Babu Wenger naye ataondoka.... Huyu ndiye anayemweka Wenger pale Emirate stadium...... Muda wa Giroud ndio muda wa Wenger.... Magoli ya Giroud ndio mshahara wa Wenger.

Msimu wa lawama....

Bournemouth 3-3 Arsenal
 
The January 2017......

Huyu Victor Wanyama ametumwa fedha au ametumwa kazi....? Any way kazi na fedha zinapiganiana ila Wanyama anacheza utafikiri Tottenham Hotspur ipo moyoni mwake toka utoto...... Wanyama the best midfielder so far.

Wakati Chelsea akivunja na kuharibu record ya Tottenham ya kutokufungwa pale darajani, sehemu ya kiungo cha Chelsea kiliwekwa na kuwa chini ya ulinzi wa Wanyama na Dembele..... Vivyo hivyo Leo wakati Tottenham anavunja na kuharibu record ya Chelsea kutokufungwa hapa white hate Lane, kiungo cha Chelsea kiliendelea kuwa chini ya ulinzi wa Wanyama na Dembele. Ukiachia kukaba basi Dembele anakupa kitu cha pekee ambacho wanyama, kante na matic hawana... Personal skillful... Uwezo wa kudrive timu kwenda mbele na umiliki wa mpira ndicho kitu alichowazidi hawa viungo wengine wa kati.

3:4:3 against 3:4:3..... Hapa Moses na Alonso walizidiwa sana katika kukaba pia waliathiriwa sana na speed technical ya Walker na Rose kama wings back wenzao. Magoli yanatengenezewa upande wa Alonso then yamefungwa upande wa Moses.

Christian Ericksen huyu ni quite player ambaye kinachomfanya avae jezi sio kupiga chenga, sio kupiga dalizi, sio kukimbia na mpira..... Ubora wake katika final touch iwe ya dead balls au live balls ndicho kitu pekee kinachomfanya avae jezi na kuwa katika first eleven. Hazard ni tajiri wa pace, dribble, possession ila Leo haikuwa siku yake nzuri kwa matokeo maana Chelsea wanatengeneza nafasi tatu tu za hatari katika lango la Spurs.

Niliwahi kuandika kuwa anaye kimbizwa na Spurs kazi anayo ila anayemkimbiza Spurs pia ana kazi...... Spurs yupo vizuri sana labda tu mumuombee injuries. Kumbe ili umfunge Chelsea lazima upitemo(3:4:3) ahahahaha.

Timu zote zilizopo ndani top six Bado zinauwezo wa kushindania ubingwa kutokana na matokeo haya ya Leo.....

Tuendelee kulaumiana maana huu Msimu ni wa lawama.... Happy new yeah Anthony Conte happy new year best young talented player so far Delle Alli.

Tottenham Hotspur 2-0 Chelsea
 
Marefa huwa wanalaumiwa pale wanapotoa card na pale wanapoacha kutoa card kwa usahihi.... Duniani kote ipo hivyo...

FA ya uingereza ina nguvu sana ila Imefanikiwa kuzifanya Sheria 17 za soka kuwa na nguvu kuliko FA yenyewe, mashabiki wake, vilabu vyao na hata pesa na umaarufu wao vyote hivyo vimekubali kutii sheria bila shuruti.

Leo mtu anafunga kwa mkono na hakuna fujo, Leo mtu anafunga goli akiwa kaotea(offside) hakuna fujo, Leo mtu anapata red card isiyosahihi hakuna fujo, leo refa anatoa maamuzi tata hakuna fujo..... FA imefanikiwa kuwaaminisha na kuwafanya mashabiki wake waamini sana na waheshimu sana katika Sheria 17 za soka mbali na ushabiki wao.

Hakuna fujo katika ligi kuu uingereza sababu ya Waamuzi..... Hakuna vifungo virefu kwa waamuzi sababu ya makosa ya mchezo, hakuna hukumu nzito sababu ya maamuzi mabovu...... FA na mashabiki wake hawa wahukumu waamuzi sababu ya maamuzi yao ila tafsiri ya sheria 17 ndio inayowahukumu waamuzi. Ndio maana Atkinson, Dean, cluttenbuge na wengine Wengi wanaishi na kuendelea kuheshimika katika maamuzi yao japo wanakosea na kuishi katika msimamo wao.

Katika kila mchezo katika ligi ya uingereza makosa ya waamuzi yapo yakutosha ila hakuna fujo sababu FA haitoi adhabu ili kumridhisha shabiki wa mchezo husika.... FA inatoa adhabu kukosoa maamuzi ambayo Kila mtu aliamini yalikuwa sio sahihi kutokana na sheria.......

Martin Saanya na waamuzi wake wanashindia kifungo kwa kosa la kukataa goli la Ibrahim Ajibu Migomba na kukubali goli la Hamisi Tambwe pamoja na kutoa kadi nyekundu isiyo halali kwa Jonas Mouse..... Dah hapa ni nje na mbali sana ya FA ile yenye kupiga hatua nyingi mbele..... Hapa FA yetu imeshindwa kuzifanya Sheria 17 ziwe kubwa kuliko vilabu vyetu, ziwe kubwa kuliko mashabiki wote na pia kuwafanya waamuzi waheshimike na waaminiwe katika maamuzi yao. Hapa Saanya na wenziwe lazima wawe na uoga katika maamuzi, wawe na maamuzi yakusuasua na wasijiamini. Leo Martin Saanya na wenzie wakitoka kifungoni nani atawaamini wao na maamuzi yao katika michezo watakayochezesha.

Point....
FA ime clear ile card ya mwarabu Sophian Feghoul na kukubalina na utetezi wa mark Dean na line two wake juu ya goli la kuotea la Zlatan Ibrahimovic..... Nikabaki nashangaa Mark Dean na line two wake wanaendelea kutesa katika kipenga kwenye viwanja vyao na tv zetu..... Hapa wanaheshimu sana sana maamuzi ya waamuzi.

Martin Saanya ni mmoja wa waamuzi bora sana na wenye sifa kubwa nje ya taifa letu...... Kumtengeneza Mwamuzi mwingine katika kipenga ambacho hakieshimiwi kimaamuzi mpaka aje afike alipofika Saanya ni atakuwa kafungiwa mara 50 katika career yake ya uamuzi. Mrudisheni Saanya bhn na maamuzi yake yaheshimike.

Pamoja na makosa wanayofanya, maamuzi yao tata Bado cluttenbuge, Atkinson na Dean ni miongoni mwa waamuzi bora kwa sasa ndani ya 10 bora ya waamuzi..... Yote ni sababu FA imewaheshimu na kuyaheshimu maamuzi yao na dunia nzima ikawaheshimu.
Sasa hivi Kocha haruhusiwi kumzungumzia Mwamuzi vibaya, mchezaji naye haruhusiwi kulalamika kwa kumnyooshea Mwamuzi mkono. Wanafanikiwa na wanaendelea kufanikiwa.

Bila waamuzi.... Bila kutengeneza waamuzi bora wenye kuaminiwa, wenye kuheshimiwa..... Itafika mahala tutawaleta waamuzi kutoka nje na timu kutoka nje ili tufurahie mpira wa WENZETU katika viwanja vyetu.

Next touch.... Mark Dean anapewa big match na anachezesha na uwanja utajaa na mpira utaisha na ataboronga na maamuzi yake yataheshimika na waingereza watakubaliana na matokeo...... Sababu hawaendagi na matokeo yao mifuko mwao.
 
Braza... uko vizuri..
Ukiweka mapenzi pembeni na kutanguliza uhalisia ktk njia inayofaa utafika mbali.
 
The man on the penalty.... The penalty on the gloves.....

Mwenye picha ya hawa jamaa baada ya zile penalty wakiwa wanarudi home anitumie..... Kuna mtu tunabishana hapa maana huyo wa nyuma nasikia hajuagi kuendesha chombo.....

Penalty penalty penalty penalty penalty okay sio kesi wacha tukutane fainali maana nasikia man of the match wa fainal ataondoka na duka na friji kabisa Maana umeme itakuwepo muda wote.

Simba SC 0-0 Yanga SC (4-2 penalties)

Final....
Azam fc vs Simba SC.
6fbb101898d2cb3bc6c8fd59760b204c.jpg
 
Wanaompigia hesabu Nathan Ake nadhani Marcos Alonso anaendelea kuwapa jibu.... Ni ngumu kumtoa mtu katika position yake mpaka aamue mwenyewe......

Nadhani katika siku mpira ulikuwa unamfuata Alonso alipo ni jana.... Jana huyu mwanadamu hakuangaika sana kuufuata mpira katika box la Leicester city..... Ila mpira ndio ulikuwa unamtafuta wapi alipo Alonso.... Goli mbili zote mpira umemtafuta Alonso na kwa target nzuri aliyokuwa nayo mipira yote kaikwamisha wavuni...

Akikosekana Diego costa.... Magoli hayakosekani.... Leicester city waliingia na mbinu ya kutaka kumfunga Chelsea na sio mbinu ya kumzuia kwanza Chelsea then baadae wajaribu kumfunga.
Chelsea huyu inakubidi uanze na mbinu ya kumzuia alafu baadae akishazuilika ndio mbinu za kumfunga zianze....

Yule Ndindi anahitaji kuizoea ligi na mifumo na wachezaji wenziwe. Anajua sana

Leicester city 0-3 Chelsea
 
Xhaka ni mtu mwingine wa kuifikiria sana katika ile sheria mpya ya kadi..... Kama ikishindikana mtajikuta kadi za Njano nyingi nu zake na machela ni zenu.....

Kweli goli ni makosa yanayonufaisha..... Kabla ya goli la kwanza la Arsenal wale Burnley walikuwa wanawashika mwamba wawili(two man on post).... Ila wakati kona ya goli ilipopigwa golikipa alisahau kusisitiza watu wawili tena wawe katika milingoti yake.... Hapa kichwa cha Mustaph kinaenda pale pale kwenye post ambayo haikuwa na mtu..... One mistake one goal....

Clearly penalty for both sides.... Hapa nikawaza sheria mpya ya mipigo ya penalty.... Mita 25 sio karibu wala sio mbali kukimbia na mpira.... Naamini babu Wenger atakuwa kashangilia sana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.... Ushindi mzuri na mgumu kwa muda mzuri na mgumu....

Tough game by the way..... Vipi lawama ?

Arsenal 2-1 Burnley.
f9290737ae24c3d5dc88cc56e43dc72a.jpg
 
Kwa aina hii ya approaching ya mchezo kwa united, ni dhahiri shahiri kuwa united wanaweza kuondoka nafasi ya 6 mwezi may 2017..... Hii ni record nyingine kwa Jose Mourinho na pesa zake.

Hii kutokujua sub ya Paul labile Pogba ni kitu kingine kinachovutia wapinzani sana katika michezo ambayo Pogba anakuwa chini ya kiwango..... Unapokutana na timu inayoundwa kuanzia kwenye kiungo na ukawa na Pogba huyu basi ni lazima muwahi kuondoka uwanjani.

Marcos Silva sumu yake tamu inakolea taratiibu huku akiendekea kupunguza ile ratiba ngumu kwenye macho yetu..... Hull wanakuja sasa.... Moja ya njia yao kuu ya ku diffend ni ku possess.... Massive plan asee.

Hii ni mara ya 3 mfuatano ambapo hull anakutana na united na bado Mourinho kacheza na mbinu zile zile.... Katika michezo 3 mfuatano.... United kashinda 1, Hull city kashinda 1 na wametoa sare 1.... Takwimu nzuri sana kwa hull city ila pia ni takwimu za kawaida sana kwa united.

United kashindwa kupunguza gape la point 2 baina yake na city, na sasa kaongeza gape la point 4...... Hii ndio 6 namba ya kishetani kwenye timu ya shetani ...... Poor Mourinho plan so far.

Mwenye jezi ya golikipa wa Hull city anipatie maana inawezekana ina namba 6 pia.

Wacha lawama ziendelee.... Maana hata 6 nayo ni lawama.

Manchester united 0-0 Hull city.
 
The man on the penalty.... The penalty on the gloves.....

Mwenye picha ya hawa jamaa baada ya zile penalty wakiwa wanarudi home anitumie..... Kuna mtu tunabishana hapa maana huyo wa nyuma nasikia hajuagi kuendesha chombo.....

Penalty penalty penalty penalty penalty okay sio kesi wacha tukutane fainali maana nasikia man of the match wa fainal ataondoka na duka na friji kabisa Maana umeme itakuwepo muda wote.

Simba SC 0-0 Yanga SC (4-2 penalties)

Final....
Azam fc vs Simba SC.
6fbb101898d2cb3bc6c8fd59760b204c.jpg
Hahaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom