Spika wa bunge (Anne Makinda) akiri posho kuongezwa!

Laiti kama ungekuwa huku chuoni, unajionea maisha ya wanafunzi ambao hawana mkopo, usingetetea posho. Tanzania ni masikini, inabidi hata hicho kidogo tulichonacho tugawane pamoja, tumeshasahau socialism.
Hivi tunashangaa nini!!! Wabunge kupata posho ya 200,000 na per diem ya 80,000 kwa siku?!!! Yaani sh 280,000 tu kwa siku ndo inatulalamisha au kuna kingine? Kwani kuna cha ajabu hapo?

Kwani sisi tulitaka wao wafanyeje... Kuna wabunge ambao hawafiki 400, lakini tuna vigogo wa wizara zaidi ya 1000. Hivi humu kuna mtu anadhani hawa vigogo wanapokea per diem ya 80,000??? Thubutuu... Akalale hoteli ya sh ngapi... ale chakula cha sh ngapi... amkarimu "mwenyeji" wake wa usiku huo kwa sh ngapi?

Kwa taarifa yenu, hakuna mkurugenzi, wala naibu wake, wala kamishna, wala mkuu wa kitengo gani sijui serikalini anayekubali kupata per diem ya 80,000, hakuna. Ila wao wana namna ya kufanya. Boss ana safari ya siku tatu, anaandikiwa siku kumi. Hapo anapata sh zake 800,000. Hebu gawanya kwa tatu uone kama huyu mtu kapata per diem ya 80,000!!! Ndio, ndo hivo wanafanya, kwani nani hajui? Kwani nayekuja ku-audit ni nani... Utouh?!!! Hivi mmesahau ule mkasa wa mwaka juzi ambapo afisa kilimo na mifugo wa wilaya moja hapa nchini alikuwa na per diems za siku 400 katika mwaka mmoja?!!! Hebu nikumbusheni ni mwaka upi uliowahi kuwa na siku zaidi ya 366...

Ndio maana nikauliza wabunge wao wafanyeje? Wao siku zao za kuwa vikaoni zinatangazwa waziwazi kwa wananchi. Hawawezi kukaa siku 10 wakaandikiwa siku 40, ni ngumu. Sasa wao kwa kuwa hawana namna ya kuchakachua siku wafanyeje... potelea mbali wakaamua kujilipua.

Ni jambo la kusikitisha tukiangalia fedha za watanzania zinavyoishia mifukoni mwa wanyonyaji wachache. Ubadhirifu ni mkubwa mno serikalini. Watu wanaandika posho za vikao na za safari nyingi kwa vikao na safari ambazo hazijawepo. Kwenye halmashauri za wilaya, kama idara ya maji kwa mfano wana field work, wakapeana field allowances, lazima mkurugenzi wa wilaya na mkuu wa idara ya maji walipwe hata kama hawahusiki na shughuli inayofanywa. Bajeti ya serikali inayosomwa bungeni na kanyaboya, na utekelezaji wake haufiki hata 15%. Zaidi ya 75% ya fedha za OC zinazopelekwa mawizarani, na kwenye taasisi za serikali zinaishia mifukoni mwa wakubwa (au zinapitia), na haziendi kwenye maendeleo. Tuliona wizara ya ujenzi ilipewa zaidi ya trillion moja bajeti ya mwaka huu... asikudanganye mtu.. zikienda milioni mia tano tushukuru Mungu.

Ni jambo la kusikitisha, na namwomba Mungu siku moja tupate raisi kama Kagame, walau uozo huu utapungua.

Shame on wabunge, shame on viongozi wa serikali, shame on us Tanzanianas...

By the way nimesahau... Hivi hamjui kuwa wabunge wengi wanajua hawatarudi bungeni 2015? Sasa hamuoni kuwa ni fursa yao kujikusanyia "kahazina" kakuwafaa "uzeeni"?
 
Ongezeko la Posho za vikao kwa wabunge ni rushwa iliyotolewa na Kikwete akiwa ndiye mkuu wa serikali kuridhia malipo hayo kwa wabunge. Hii imetolewa kama motisha kwa wabunge ili wapitishe mswada wa sheria ya kuunda katiba mpya. Rushwa ni rushwa tu hata kama ingekuwa na sura ya kondoo au simba. Mbona Ikulu imekaa kimya kama si mpango wa Ikulu kuongeza posho za kuwarubuni wabunge? Speaker Makinda ni mhanga tu, na walimweka kwa ajili hiyo na anawajibika kwa waliomweka.

Kila kukicha vituko haviishi serikali ya Kikwete na kila siku anazidi kuweka ufa na kuwafungulia wapinzani njia ya kuishika Ikulu Uchaguzi ujao. CCM inajutia na maji ukishayavulia nguo huna budi kuyaoga.

Jitihada za kujivua magamba sidhani kama zina mshiko wakati simba anayemaliza mifugo bado yuko zizini. Njia mbdala ni kuhakikisha simba anayemaliza mifugo asiwepo zizini na wanaCCM wanajua hili.

Kama mnakumbuka habari zilizovuja kwamba viongozi wa kitaifa wastaafu wasiwepo kwenye kamati kuu hii ni kutokana na wao kuendelea kumlinda mkuu wa nchi ili aendelee kuwalinda. Pale Dodoma majuzi ilipoanzishwa hoja ya magamba Mkapa alimshinikiza Kikwete kusitisha hoja hiyo na kuendelea na ajenda nyingine.

Haya makubwa, mpaka mwaka 2015 njia nyeupe kwa wapinzani kuongoza dola na CCM kuwa chama cha upinzani hali itakayowafikisha CCM kusambaratika na kubakia historia tu.
 
Hapo ndipo wasomi wengine ni lazima tuwe na mashaka sana na huo usomi wao,hivi Dr mzima unadanganya ili iweje???halafu akalaumu sana vyombo vya habari kuwa ndio vilileta habari ambayo sio ya kweli KUMBE NI KWELI.kashirila umeaibika sana uso wako umejaa aibu,kichwa chini umeumbuka.naamini hutadanganya tena acha papara na fikiri kisomi na si kimasaburisaburi.
 
Back
Top Bottom