MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Nimeona Spika Tulia akizinyanyasa hoja za wananchi zilizoletwa na Waitara kuhusu mauaji ya watu Tarime na ya Ole Sendeka kuhusu Loliondo.
Kwa kutumia ujuzi wake wa sheria ameamua kutumia kiti chake cha uspika kuwa mtetezi wa serikali na kuwagaragaza wabunge hao waliokuja na hoja zenye nguvu toka kwa wananchi.
Ndipo likanijia wazo jee kama Tundu Lissu & Co ya wale wabunge machachari wangekuwepo Bungeni Tulia angeweza kuzicheza hizi "legal acrobatics" anazocheza bila kubutuliwa na kufedheheka mbele ya jamii?
Je, Watanzania wameelewa ubaya wa kuwekewa wabunge wa serikali bungeni?
Spika aliye wageuka wananchi kwa kutumia ujuzi wake wa sheria anastahili kukutana na wabunge wa "wananchi" wabobezi wa sheria aina ya kina Lissu.