Spika Tulia amtembelea Profesa Jay, asema afya yake inaendelea kuimarika

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, jana Machi 14, 2022 aliwatembelea na kuwajulia hali Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay pamoja na Mama mzazi wa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Halima Mdee, Bi. Theresia Mdee ambao wamelazwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Dkt Tulia ameelezwa kuwa hali za wagonjwa hao zinaendelea kuimarika kila siku tofauti na awali ambapo, pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wahudumu wa hospitali hiyo wakiwemo madaktari ambao wamekuwa wakijitolea kwa nguvu zote katika kuokoa maisha ya watu.


Source: Dodoma Zone

Spika.jpg


Spika 22.jpg


Spika 1.jpg
 
Vizuri,lakini kutoleta picha ya mgonjwa mwingine inaleta maswali kwa baadhi ya watu.
 
Kutembelea wagonjwa ni jambo jema.
Pole sana Joseph Haule.
Ila huyo profesa uchwara anatafuta nini kwa Jay?
Maana ni kilaza hatari asije akamdhuru...
 
Back
Top Bottom