Siku zinakwenda sasa na hakuna chochote kinachosemwa kuhusu suala la mbunge wa ccm na kiongozi mnene kabisa wa ccm ambaye pia anaita mapesa ya wizi vijisenti kufanya vitendo vya uchawi bungeni.
Mheshimiwa Sitta uliahidi kufanyia uchunguzi jambo hili, je umefikia wapi? Kama mnataka kufunika aibu katika hili basi ujue kuwa litajadiliwa hapa JF kwa vile ni jambo muhimu sana kwa maendeleo ya siasa za Tanzania. Wahenga walisema kuwa mficha kidonda harufu itamuumbua. Nakuomba Mheshimiwa Sitta ulete report ya uchawi bungeni na wahusika wachukuliwe hatua haraka sana iwezekanavyo.
Nafikiri mwenye kutakiwa kutoa ripoti hapa sio Spika kwani yeye tayari alishawasilisha nyaraka na vielelezo kwa vyombo vya dola , sasa hapa adaiwe Mkemia mkuu ,na polisi pamoja na idara ya usalama wa taifa .
Ripoti ya uchawi bungeni ni muhimu ikatoka kwani kuna wabunge wengine huko bungeni ambao kwa kusema kweli kauli zao zinatia shaka.
Mimi naisubiria kwa hamu kubwa sana ili ukweli ujulikane na utendaji kazi wa mafisadi wa ccm uwe wazi zaidi
Mimi naisubiria kwa hamu kubwa sana ili ukweli ujulikane na utendaji kazi wa mafisadi wa ccm uwe wazi zaidi
Shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiih Hey watch out usije kupigwa kipapai na wewe kwa kufunua mambo ya juju la waheshimiwa ambalo nahisi spika ameitia kapuni kiaina....Sasa unakumbushia tena? Unaweza kusikia jogoo analia tumboni mwako humo..Teh! teh!tehteh!!
Kwa hali ilivyo kipapai kinaweza kuwa tayari kwani wabunge wenyewe wanalala tu huko bungeni!
kweli kabisa mushi, ukiona jinsi wanavyolala huku mafisadi wakipeta tu basi utaamini kuwa vipapai vimewazidia nguvu. Unakumbuka Dr Slaa alivyokumbusha wabunge kusema kila kinachoandikwa hadi Mkullo akabidi kubadili maandishi kwenye bajeti yake?
Waache uchawi na kufanya kazi, inatisha sasa.
Kama watu wameanza kuchinja akina mama wanatafuta makoo itakuwa hii ya unga kwenye bunge, wakubali wasikubali uchawi upo, wangetoa taarifa tu ili guessing game iishe.
Tena si ya kuisubiria kwa hamu...Bali waitoe kabla hata ya kuanza mjadala wa TAIFA!
Kwani si walisema huo "UNGA UNGA" Uko kwa mkemia mkuu?
Sasa kama kuna mbunge wetu ambaye alipata madhara na wabunge wetu ndio watunga sheria...Then inakuwa vipi waathirike ama KUTISHIWA MAISHA YAO halafu mjadala uendelee bila ya kutoa taarifa kamili za UCHUNGUZI?
Tuambiwe huo unga unga ilikuwa ni nini na huyo aliyouweka alikuwa na maana gani?
Inamaana Mkemi Mkuu nae ni mganga? Maana ninavyofahamu mimi kama sio mganga basi jibu litakalo kuja tutaambiwa sio Uganga ni VUMBI TUU MAANA SIUNAJUA DODOMA KUNA VUMBI SANA
Inamaana Mkemi Mkuu nae ni mganga? Maana ninavyofahamu mimi kama sio mganga basi jibu litakalo kuja tutaambiwa sio Uganga ni VUMBI TUU MAANA SIUNAJUA DODOMA KUNA VUMBI SANA