Spika Ndugai: Wakurugenzi wa TARURA na RUWASA wanalipwa mishahara mikubwa kuliko Ma - DED yalivyo mambo ya ajabu

Mambo ni hivi
FB_IMG_1618468429230.jpg
IMG-20210415-WA0008.jpg
 
Itafika sehemu watanzania tutachoka n ili Bunge letu. Hivi kwa akili za kawaida tu wakurugenzi wa RUWASA na TARURA ambao wana mamlaka karibia nchi nzima na wanasimamia miradi ya mabilioni wanawezaje kulipwa sawa na DED ambaye ana mamlaka katika eneo la wilaya tu na bila kuwa na utaalamu wowote?

Hivi kweli mtu mwenye cheo cha Spika hafahamu vigezo vya viwango vya mishahara?

Tatizo kubwa ni kwamba hizi taasisi tajwa zimeondolewa chini ya mamlaka za wanasiasa na ni dhahiri kabisa kuna maslahi fulani fulani baadhi ya wabunge walikuwa wanapata kwa taasisi hizi kuwa chini ya halmashauri hivyo kuna chuki fulani ya kimaslahi.

Kiukweli tangu kuundwa kwa RUWASA kumekuwa na mabadiliko makubwa katika upatikanaji w huduma za maji vijijini, lkn kumekuwa na upinzani mkubwa toka kwa wanasiasa wanaotaka idara ya maji irudi halmashauri ili waendelee kunufaika binafsi.
 
Spika Ndugai ameshangazwa na serikali kuwalipa mishahara mikubwa wakurugenzi wa mamlaka ya maji na ile ya barabara za vijijini ambayo ni zaidi ya mishahara wanayolipwa Wakurugenzi wa wilaya...
unataka mkeo apate mshahara sawa na wakurugenzi wenye profwssional zao?
 
Mbona hasemei wabunge wanavyolipwa hela nyingi?
Mbona hasemei matibabu yake yalivyowagharimu walipa kodi hela nyingi?
Yeye amekuwa katibu au waziri wa utumishi?
badala ya kuangalia vipau mbele vya bunge ana ...............ka
 
Natumai sheria zilioanzisha taasisi hizi zilipitishwa hapo hapo mjengoni, na mishahara yao haipangwi gizani kuna mamlaka zinaridhia na kupitisha. Mshangao kama huu ni wa kinafiki sana.

Acha na sie tushangae kama yeye!
spika hajui kitu yy ni bora liende maana hajui hata mchakato wa kupandisha mishahara ya watendaji wa mamlaka hizo unaanzia wapi na nani alipisha sheria za kuanzisha hizo mamlaka na yy na wabunge wake.this is shameful
 
Spika Ndugai ameshangazwa na serikali kuwalipa mishahara mikubwa wakurugenzi wa mamlaka ya maji na ile ya barabara za vijijini ambayo ni zaidi ya mishahara wanayolipwa Wakurugenzi wa wilaya.

Ndugai amesema hayo akimuunga mkono mbunge wa Gairo mh Shabiby aliyedai wakurugenzi wa Tarura na Ruwasa wamejigeuza miungu watu.
Baada ya Magufuli kuondoka nyumbani kwa Ndugai vyuma vimekaza, anataka mke wake DED aongezwe mshahara!
 
Back
Top Bottom