Spika Ndugai unataka Lissu afe?

Spika Ndugai unataka Lissu afe?

Anaandika #Bollen_Ngeti

SPIKA NDUGAI ANATAKA LISSU AFE??

KITENDO cha Bunge la Ndugai kumfutia mshahara na posho zingine za kibunge Tundu Lissu ni unyama na ushahidi wa dhahiri kuwa Spika Job Ndugai akibanwa anaweza walau kusaidia kujua waliopanga kumuua kwa mabunduki Lissu September 7, 2017.

Mwanzoni nilijua ni kauli tu za kisiasa lakini kwa Ndugai kuamua kweli kumfutia mshahara Lissu ni jaribio jingine la kutaka kumuua Lissu na safari hii naona wanataka afe kwa njaa na familia yake.

Risasi 16 zilishindikana kumuua Lissu baada ya Mungu kusimamia "show". Jaribio la pili lilikuwa ni kumfutia dhamana ili akamatwe na Interpol aswekwe ndani na magongo yake na majeraha. Hakika angekufa kwa mateso na uchungu. Hili nalo Mungu akaepusha. Mahakama ikakataa. Safari hii naona njia sahihi iliyochaguliwa ni kumfutia mshahara Lissu ili afe kwa njaa, watoto wasiende shule, ndugu tegemezi waathirike. Huku ni kumuua Lissu na ni uthibitisho kuwa nguvu ya kummaliza Lissu ni kubwa mno kiasi kwamba bila Mungu Lissu si kitu!

Ndugai anadai hajui aliko Lissu na anafanya nini huko asikojua. Ndugai akumbushwe tu kwamba Lissu yuko hospitali huko Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risaso 38 na 16 kumuingia mwilini na hivi karibuni amemaliza kufanyiwa upasuaji wa 23. Anasubiri uamuzi wa madaktari kumruhusu kutoka au la!

Lissu ni Mtanzania kama wewe na mimi. Ana ndugu, jamaa na marafiki hata ndani ya Mafikizolo, Chadema, Inzile, Gweregwere, CUF, jeshini, TISS, vyuoni, Magogoni nakadhalika! Tumuombee apone ili awatumikie wananchi wake. Tofauti zetu kisiasa zisitutofautishe hadi kufikia kuuana kwa njaa. Wabunge wote unganeni kumpinga Ndugai, pigeni kelele hadi nchi za mbali kupinga uamuzi huu wa Ndugai. Kumbukeni wakimmaliza Lissu watakugeukieni na ninyi. Hakuna aliye salama kwa sasa!
#AchaWoga2020
Jamani ndugai hajasema hajui lissu aliko! Ofisi ya spika(bunge) haina taarifa Mbunge wa Singida Mashariki alipo. Tofautisha Ndugai na Ofisi ya Spika(bunge). Ofisi inao utaratibu wake wa kufahamishwa. Na ufahamu kuwa Ndugai hana bunge, bunge ni la Tanzania.
 
good enough ni kuwa hata ccm wenyewe watagawanyika kwa hili... nami napenda iwe kweli ili lisu aanze kupokea pesa za charity ambazo Jiwe na serikali yake wamenyimwa na wataapata taabu sana..
 
Hivi kama wamezuia mshahara na posho, nadhani bado kumvua ubunge tuu

Pia hao viongozi wanaojipangia mishahara minono na posho za kutosha wakitembelea magari yenye viyoyozi na kuishi majumba ya kifalume huku wapiga kula wakirundikiwa kodi, na kuishi maisha ya kuunga unga, Mungu anawaona mwisho wao upo tu

Halafu Kwenye camera unasikia tanasema uchumi umezidi kuimarika,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo aliyefutiwa posho huishi katika nyumba gani?
 
Mkuu lengo lilikua ni kumfunga mdomo nankumrudisha home mzururaji. Nafikiri lengo limetimia
Kama aliweza kwenda mataifa ya nje na kufanyiwa mahojiano na vyombo vya habari anashindwaje kurudi TZ na kufatilia maslahi yake.
 
Kama ndio dhamira yake hiyo ,hiyo Ndugai atakufa yeye na anayemtuma ,Lissu yupo tu hivi hizo risasi zenu 16 halafu mtu akapona hazijawaundisha tu .
 
Ndungai na bunge zima nawapongeza kwa kufuata taratibu na kanuni walizojiwekea.

Haiwezekani mtu anakula posho na mshahara ambao ajaufanyia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimrod Mkono, Ndugai, prof Mwandosya nk nk ni miongoni mwa wabunge wa CCM waliokaa nje ya nchi huku wakilipwa. Na hujanung'unika, iweje nongwa kwa Lissu ???!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika #Bollen_Ngeti

SPIKA NDUGAI ANATAKA LISSU AFE??

KITENDO cha Bunge la Ndugai kumfutia mshahara na posho zingine za kibunge Tundu Lissu ni unyama na ushahidi wa dhahiri kuwa Spika Job Ndugai akibanwa anaweza walau kusaidia kujua waliopanga kumuua kwa mabunduki Lissu September 7, 2017.

Mwanzoni nilijua ni kauli tu za kisiasa lakini kwa Ndugai kuamua kweli kumfutia mshahara Lissu ni jaribio jingine la kutaka kumuua Lissu na safari hii naona wanataka afe kwa njaa na familia yake.

Risasi 16 zilishindikana kumuua Lissu baada ya Mungu kusimamia "show". Jaribio la pili lilikuwa ni kumfutia dhamana ili akamatwe na Interpol aswekwe ndani na magongo yake na majeraha. Hakika angekufa kwa mateso na uchungu. Hili nalo Mungu akaepusha. Mahakama ikakataa. Safari hii naona njia sahihi iliyochaguliwa ni kumfutia mshahara Lissu ili afe kwa njaa, watoto wasiende shule, ndugu tegemezi waathirike. Huku ni kumuua Lissu na ni uthibitisho kuwa nguvu ya kummaliza Lissu ni kubwa mno kiasi kwamba bila Mungu Lissu si kitu!

Ndugai anadai hajui aliko Lissu na anafanya nini huko asikojua. Ndugai akumbushwe tu kwamba Lissu yuko hospitali huko Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risaso 38 na 16 kumuingia mwilini na hivi karibuni amemaliza kufanyiwa upasuaji wa 23. Anasubiri uamuzi wa madaktari kumruhusu kutoka au la!

Lissu ni Mtanzania kama wewe na mimi. Ana ndugu, jamaa na marafiki hata ndani ya Mafikizolo, Chadema, Inzile, Gweregwere, CUF, jeshini, TISS, vyuoni, Magogoni nakadhalika! Tumuombee apone ili awatumikie wananchi wake. Tofauti zetu kisiasa zisitutofautishe hadi kufikia kuuana kwa njaa. Wabunge wote unganeni kumpinga Ndugai, pigeni kelele hadi nchi za mbali kupinga uamuzi huu wa Ndugai. Kumbukeni wakimmaliza Lissu watakugeukieni na ninyi. Hakuna aliye salama kwa sasa!
#AchaWoga2020
Ndugai naye zamu yake ya kusulubiwa inakaribia... haiko mbali!
 
Back
Top Bottom