Spika Ndugai unataka Lissu afe?

Spika Ndugai unataka Lissu afe?

Mambo haya ni ya kusikitisha sana, mwanadamu hata akutendee ubaya gani huna mamlaka ki imani kujaribu kutoa uhai wake au yoyote yanayofanana na hayo.

Mtu anapigania uhai wake wewe unanyima mshahara? vidonda vioze, familia imtenge sababu yupo hoi bin vuu - unataka nini tena??
 
Akujazuia ina maana kapona kwanini asirudi kufanya kazi za kibunge?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi hapa kwetu hakuna mgonjwa aliywahi kuhojiwa na vyombo vya habari?

Kigwangala akiwa Muhimbili hakuhojiwa? Mbona Ndugai hakusema arudi bungeni kwa sababu ameongea na vyombo vya habari?

Mwigulu, hivi karibuni, baada ya ajali, kabla hajapona hakuhojiwa na vyombo vya habari? Tusiwe wendawazimu au tukakokotwa na mashetani bila kujitambua. Tuutambue utu na ubinaramu wetu, tutende kwa kadiri ya hivyo tulivyopewa na Muumba wetu. Wala tusiukatae utu na werevu wetu tukautumikia ujinga na ubaradhuli badala ya hekima iliyoingizwa nafsini mwetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Anaandika #Bollen_Ngeti

SPIKA NDUGAI ANATAKA LISSU AFE??

KITENDO cha Bunge la Ndugai kumfutia mshahara na posho zingine za kibunge Tundu Lissu ni unyama na ushahidi wa dhahiri kuwa Spika Job Ndugai akibanwa anaweza walau kusaidia kujua waliopanga kumuua kwa mabunduki Lissu September 7, 2017.

Mwanzoni nilijua ni kauli tu za kisiasa lakini kwa Ndugai kuamua kweli kumfutia mshahara Lissu ni jaribio jingine la kutaka kumuua Lissu na safari hii naona wanataka afe kwa njaa na familia yake.

Risasi 16 zilishindikana kumuua Lissu baada ya Mungu kusimamia "show". Jaribio la pili lilikuwa ni kumfutia dhamana ili akamatwe na Interpol aswekwe ndani na magongo yake na majeraha. Hakika angekufa kwa mateso na uchungu. Hili nalo Mungu akaepusha. Mahakama ikakataa. Safari hii naona njia sahihi iliyochaguliwa ni kumfutia mshahara Lissu ili afe kwa njaa, watoto wasiende shule, ndugu tegemezi waathirike. Huku ni kumuua Lissu na ni uthibitisho kuwa nguvu ya kummaliza Lissu ni kubwa mno kiasi kwamba bila Mungu Lissu si kitu!

Ndugai anadai hajui aliko Lissu na anafanya nini huko asikojua. Ndugai akumbushwe tu kwamba Lissu yuko hospitali huko Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risaso 38 na 16 kumuingia mwilini na hivi karibuni amemaliza kufanyiwa upasuaji wa 23. Anasubiri uamuzi wa madaktari kumruhusu kutoka au la!

Lissu ni Mtanzania kama wewe na mimi. Ana ndugu, jamaa na marafiki hata ndani ya Mafikizolo, Chadema, Inzile, Gweregwere, CUF, jeshini, TISS, vyuoni, Magogoni nakadhalika! Tumuombee apone ili awatumikie wananchi wake. Tofauti zetu kisiasa zisitutofautishe hadi kufikia kuuana kwa njaa. Wabunge wote unganeni kumpinga Ndugai, pigeni kelele hadi nchi za mbali kupinga uamuzi huu wa Ndugai. Kumbukeni wakimmaliza Lissu watakugeukieni na ninyi. Hakuna aliye salama kwa sasa!
#AchaWoga2020
Lissu aliombea Tanzania inyimwe misaada na kweli haijapata misaada na yeye ndio maana kakosa mshahara kwasababu hatujapata misaada nafikiri tuisome namba wote pamoja na yeye aliyeombea nchi inyimwe misaada. Analia Lia mitandaoni huku alienda kuwaambia mabepari wainyime Tanzania misaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muulize lissu kwasababu ni learned na anajua ila anawadaa wafuasi wake kutafuta sympathy.

Mwanasheria gani ajui taratibu za kufuata katika kudai haki(madai) yake ya posho na mshahara amebaki anaandika nakala ndefu ambazo sio suluhu ya ishu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikuwa na shaka na uduni wa akili yako ila sikufahamu kama una akili duni kiasi hiki
 
Sikuwa na shaka na uduni wa akili yako ila sikufahamu kama una akili duni kiasi hiki
Mwenye akili kubwa Lissu tu na wewe mfuasi wake.

Kama kweli mna akili kubwa malalamiko ya kunyimwa mshahara na posho mnapeleka mitandao ya kijamii badala ya kupeleka barua sehemu uhusika(ofisi za bunge),serious?

Njaa mbaya sana na haina baunsa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka hata Mama yangu hapo enzi za uhai wake kwa bays lolote alikuwa anafananisha na akili za kabila hill....!
 
Nakumbuka hata Mama yangu hapo enzi za uhai wake kwa bays lolote alikuwa anafananisha na akili za kabila hill....!
 
Nakumbuka hata Mama yangu hapo enzi za uhai wake kwa bays lolote alikuwa anafananisha na akili za kabila hill....!
 
Taratibu na kanuni haziangalii sura usipozifuata kufa tu tutakuzika.
imagine wewe ndio ungekuwa mwanafunzi waa kidato cha pili halafu lissu angekuwa ndio baba yako wa kambo anayekulipia ada ili umalize kidato cha nne, ungeanduka utumbo kama huo?.
 
Kufanya kazi na magufuli kutawaharibia cv viongozi wengi sana wanaoendekeza matumbo.
 
Back
Top Bottom