mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,338
- 12,471
Spka job Ndugai amesema kuwa wamekwisha mlipa Tundu Lissu ,aliyekuwa mbunge stahiki zake zote
Ameyasema hayo Leo akiwa bungen Dodoma
----
Ameyasema hayo Leo akiwa bungen Dodoma
----
Wakati akitoa mapungufu ya hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kabla ya kuruhusu kuisoma, Spika wa bunge la Tanzania amesema kwamba mojawapo ya mambo yalizungumzwa katika hotuba ya upinzani ni madai ya misharaha ya Lissu, ambapo amedai Mh.Lissu anasitishiwa ubunge alikuwa hadai hata mia.
Wakati akizungumzia kasoro kadhaa za hotuba hio baadhi ya mambo yaliyoandikwa humo ni kunyanyaswa kwa Kiongozi wa Kambi ya upinzani ikiwemo kunyimwa nyumba,gari nk ambapo aliagiza uongozi wa bunge kufuatilia
Baadhi ya kasoro alizoanisha ni makosa ya kimaandishi 'spelling mistakes',kuzungumzia mambo ambayo yeye anasema ni kuingilia Uhuru wa mahakama, kutumia vibaya jina la Raisi nk.
Hata hivyo baada ya kutoa kasoro hizo Spika alisema hotuba hio haitasomwa na mwendo utakuwa ni huohuo iwapo haitakidhi vigezo anavyoona yeye.
Swali: Hivi kwanini Spika anawanyima watanzania fursa ya kupata mawazo na michago mbadala kwa sababu ndogo kama hizo? Je ilishindikana kufanya marekebisho?
Sent from my TECNO K8 using Tapatalk