Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Rekebisha kidogo heading ni
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana "
Spika kawa mdogo kama piriton!
P
Yani yeye akizani Rais anaweza kuchezewa kama Pasco?

Uspika wa Ndugai unashikiliwa na kadi ya ccm, wakichukuwa kadi yao uspika na ubunge kwishney.

Rais ni jambo lingine kabisa, nadhani leo Humphrey Polepole atakuwa amepata clear msg kwamba wanaokwambia tupo nyuma yako yakikukuta ukigeuka nyuma hutowaona.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
kanuni ile uliyonyamazisha wengine ndio hiyo hiyo inatumika
 
Yaani unaweza andika hiyo habari hata bila kuhudhuria huo mkutano au kumsikiliza ... inajulikana atakachosema, kwa Mwandishi kuhudhuria ni kupoteza tu muda ... pia atakazia kupiga watu mkwara kuheshimu bunge
Kuhudhuria sio kupoteza muda Kaka.
Kunakuwaga na bites kabla ya mkutano halafu lunch ya nguvu baadae kwa watakaokuwa wavumilivu wa kusikiliza na kuandika ujinga Kuna bahasha ya nauli.
 
Yani yeye akizani Rais anaweza kuchezewa kama Pasco?

Uspika wa Ndugai unashikiliwa na kadi ya ccm, wakichukuwa kadi yao uspika na ubunge kwishney.

Rais ni jambo lingine kabisa, nadhani leo Humphrey Polepole atakuwa amepata clear msg kwamba wanaokwambia tupo nyuma yako yakikukuta ukigeuka nyuma hutowaona.
Polepole huyu huyu ?
 
Alichofanya Ndugai ni kumuongezea nguvu Maza.... Wakati huo huo yeye kajimaliza kabisa. Asifikiri watamsamehe kwa hilo pamoja na kujifanya anajibebesha msalaba wake mwenyewe kwa niaba ya wote.

Imagine pamoja na kutukanwa kote kule kashindwa kumuita mtu yeyote kwenye ile kamati yake ya Maadili. Kwa udhaifu aliouonyesha sasa asubiri watakanyompanda mpaka kichwani.

Mbaya zaidi kutubu hadharani kwa design ile, Spika wa Bunge.... Only in Tanzania.
Wewe hujui unachokiandika, baada ya Mungu ni Rais.
 
Back
Top Bottom